Story of Change Mwanafunzi Bora Chuo Kikuu Mzumbe aliyejiajiri kwa kukusanya na kubeba taka na kufanikiwa

teju

Member
Feb 24, 2015
79
150
Naitwa Teju nikijana wa kitanzania nilisoma shule ya sekondari Ivumwe Secondary school nilipata ufaulu wa Diraja II (Division Two) na ALevel Mbalizi Secondary school nilipata ufaulu wa Daraja I (Division One) na baadaye nilijiunga chuo kikuu cha Mzumbe Corse ya Usimamizi wa Biashara katika Masoko (Business Administration in Marketing Management) na nilibahatika kuwa Best student of 2019 kwa kupata First Class ya juu kabisa kwa mwaka

Wakati nikiwa Chuo kikuu nilikua nilitamani sana siku moja nije niwe Mwalimu wa Chuo kikuu hasa vyuo vikubwa hapa Nchini na nje ya Nchi. Na hii ndi ndoto ambayo vijana wengi hasa wanafunzi wa vyuo vikuu huota na hutamani Siku moja wakimaliza Elimu yao basi watakuja kufanya kazi nzuri tena walizo somea. Mfano Marketing Manager, Bank Officer, Accountant na kadharika, lakini uhalisia ulikua hivi baada ya kumaliza Chuo kikuu.

Nakumbuka ilikua tarehe 28/7/2019 baada ya kumaliza mitihani yangu ya mwisho ya muhula wa mwisho, kwanza kabisa Darasa letu kuliandaliwa bonge la Sherehe ya kujipongeza kwa kumaliza chuo kikuu, wakati sherehe ile ikiendelea tulikua tukibadilishana mawazo na kushare Address za makampuni mbalimbali kwenda kuomba kazi maana nilikua nikijua kwa ufaulu ule siwezi kukosa kazi nzuri kwenye ofisi nzuri ya Umma ama Binafsi.

Basi wakati watu wakiendelea kuimba na kucheza Nyimbo mbalimbali zenye kuburudisha na kuashiria furaha imetawala, mimi ilikua tofauti kwani nilikua nikiwaza muda wote ambao nimeutumia shule kuanzia darasa la kwanza hadi Chuo kikuu, lakini pia nilikua najaribu kutafakari baada ya kumaliza chuo nini kitafuata? picha ilikua iki niijia ya nyumbani kijijini kwetu Mamba kisalasi,Kata ya Mamba Tarafa ya Kipembawe wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.

Ndugu msomaji mimi nikijana wa kiume nilie zaliwa katika Familia ya kimasikini sana, ya wazazi wakulima wa jembe la mkono wasio na uhakika wa kupata pembejeo za kilimo kwa wakati, na ambao hawana uwezo hata wa kulipa ada ya Shule. Katika safari yangu ya elimu niliweza kubahatika kusomeshwa na watu mbalimbali walio kuwa wanaona na kuthamini jitihada zangu za kusoma kwa bidii na kufauru vizuri. Basi nilipo kua nikikumbuka nilivyokua nikenda shule Peku, nikikumbuka wakati nikifukuzwa ada ya shule wazazi wanakuja kumuomba mwalimu mkuu ili walete Mahindi wayathaminishe na fedha ili mimi niendelee na shule, basi Machozi yalianza kunidondoka na hasa nilipo fikilia wakati wa mahafari wazazi wangu watakuwa na furaha sana na pengine wakiamini kuwa sasa kijana wao nimemaliza Chuo kikuu hivyo naenda kupata kazi na angalau wapumzike namimi niweze kuwasaidia Majukumu mengine.

Ndugu msomaji hali ilizidi Kua mbaya baada ya hotuba ya mwalimu wetu mlezi wa darasa, alipo sema "Najua wengi wenu mmesoma kwa bidii na sisi tumewapika na mmepikika vilivyo, ningekuwa na kampuni kubwa ya Masoko ninge ajiri nusu ya darasa lenu maana katika historia ya kufundisha chuo hiki nadhani mwaka huu ndio tumetoa wanafunzi ambao kuanzia wakwanza mpaka wa mwisho wote wameiva " pia aliongeza kwa kusema hali ilivyo kwenye soko la ajira ni mbaya sana, mmemaliza kipindi kihaya ambacho hata chuo hakina bugeti ya kuwabakisha wanafunzi bora kwa ajili ya kuandaa waje wawe waalimu huko baadaye lakini nendeni mkapambane na maisha na usiogope wala msichague kazi kwani mchagua jembe si..... tukamalizia kwa kusema Mkulimaaaaaa, akashukuru na kuaga.

Maneno yale pamoja na ya wazazi yalinipa ujasiri mkubwa sana, kwa kuwa wakati nikisoma Chuo nilikua nimepanga na kodi ya pango ilikua inaisha tarehe 30/07/2019 basi inabidi nijipe moyo nikasema Mimi ni msomi wacha nipambane elimu hii ni makaratasi tu ila mimi naanza upya. Basi siku iliyo fuata wenzangu walikua wakikata tiketi za mabasi kwaajiri ya kurudi makwao mimi niliamkia kwa baba mwenye nyumba na kumuomba niendelee kubakia pale na namtafutia Kodi ya pango angalau tarehe 15/8/2019 nitamlipa. Mungu mwema mzee yule akakubali na mimi ndio nilipo ingia mtaani rasmi na kuanza kutafuta Fulsa.

Fulsa yangu ya kwanza kuiona ilikua ni kukusanya taka majumbani, maofisini na sehemu za Biashara, na kuzipeleka sehemu rasmi iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kukusanyia taka Basi mwanzoni nilianza kwa aibu sana nilikua nikikodi tololi kwa shiringi 5000 kwa siku alafu napitia mitaani naita MBEBA TAKA ANAPITA hapo ndipo niligundua kunafulsa kwenye eneo hilo watu wakitoa majumbani na kunitia njoo njoo uchukue. Kila alie pakia taka alinilipa kiwango cha chini 500/= lakini wapo walio Lipia zaidi kwa hiali yao. Baada ya muda mfupi viongozi wa mitaa wakiwepo Mabalozi hasa balozi Mwampiki waliniita na kanishauri kuwa nipange ratiba ambayo wananchi wataifuata angarau mara moja kwa wiki wawe wanaweka taka kwenye mfuko na kuziweka pembezoni mwa barabara kila jumamosi, na wao wawa hamasishe jamii kulipa shilingi 3000/= kwa mwezi basi nilikubari na hapo ndio kazi ikawa nzuri muamko ulikua mkubwa na mapokeo yakawa mazuri hivyo nilianza kupata kipato ambacho kiukweli niliona Kuna njia mbele nitatoboa, hapo kunavijana wawili ambao huwa wanashinda jalalani/dampo kuokota vitu nikawachukua na kuanza kufanya nao kazi tulianza kukodi gari ndogo kirikuu na baadaye kadri huduma ilivyo kuwa bora ndivyo wananchi maeneo jirani wakawa wanahitaji huduma yetu. Tumeenda hivyo mpaka mwaka huu mwezi wa kwanza niliandika proposal Halimashauri kuomba watupe eneo kubwa na uwe mradi wa kuosaidia jamii na serikali kusafisha mazingira na kuondosha taka Majum
bani, sehemu za biashara na kwenye Taasisi mbalimbali .

Halimashauri walikubali na kuanzia mwezi wa 3/2021 walinisainisha mkataba na sasa natakiwa kukusanya Milioni 12 kwa mwezi
Katika 100% Asilimia 30inabakia Halimashauri kwa ajili ya kuendeshea shughuri za dampo kuu, na asilimia 70 naipata mimi mzabuni hivyo Kwasasa nimeajiri vijana 8 wanao kusanya Fedha mitaani (Ada ya taka) na nawalipa 360,000/= na pia vibarua 4 wakupakia taka kwenye tipa ambao nawalipa @20, 000/= kwa siku na wanafanya kazi siku 15 kwa kila mwezi.

Pia katika kazi hii mwaka jana niliweza kununua kipande cha ardhi cha milioni 6 ambapo nimeweza kuanza ujenzi mwaka huu na Lengo ni kuwa na dhamana isiyo hamishika ili niweze kukopesheka Bank na hatimae niweze kukopa na kununua Gari kubwa Tipa Scania au Howo, Faw au Fuso kwa ajiri ya kubea taka na niachane na magari ya kukodi ambayo natumia gharama kubwa ya uendeshaji wa kazi.

Husia wangu kwa vijana tusidharau kazi, waje wajifunze kwangu kazi zote ni kazi wasichague kazi wakati hawana kazi chagua kazi ukiwa tayali kazini na sio lazima kuajiriwa waweza kujiajiri pia TUKUMBUKE HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA tusiogope kuanza chini.Ahsante nawasilisha
 
Upvote 237

Born1703

JF-Expert Member
May 17, 2020
597
1,000
Mkuu, sijakuelewa vyema, Ulisoma Mzumbe na hiyo ipo Morogoro na hapo hapo kabla hujarudisha chumba ulichokuwa umepanga ukiwa chuoni ukamuomba Mzee mwenye nyumba ukae zaidi ili ukataharike, vipi hiyo nyumba ipo mbeya au ipo Moro??--- hapo sijakuelewa mkuu.
Mbeya mzumbe ipo
 

Jovin Jr

New Member
Jul 22, 2021
1
20
Miaka ya nyuma mwanafunzi akifanya vizuri haachwi azurule mitaani lakini nowadays nibora mtoto umpeleke VETA na umsaidie vifaa ajiajiri
 

Mohamed H

New Member
Jul 22, 2021
1
20
Naimani kwa uzi huu utashinda ila ukishinda hiyo 5M hakikisha unatafuta ma power tools then unafungua local small industries and then uwaunganishe vijana wenye ndoto na wapambanaji kama wewe
 

timothmakata

New Member
Jul 22, 2021
1
20
Halmashauri nyingi huwa wanasumbua kulipa fedha vip kwa huko hiyo sio changamoto? hasa kwako na wazabuni wengine?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom