Mr Lukwaro
JF-Expert Member
- Jun 3, 2023
- 357
- 621
Mifumo ya elimu Chuo Kikuu bado inaendeleza elimu ya kukariri kile mwalimu anachosema na sio kumuandaa kijana kujiajiri baada ya kumaliza Chuo kikuu.
In fact, Soko la Ajira limesha dorora, Soko limejaa wateja wengi kuliko wanunuzi. Watu wa Uchumi mtuambie hii inaashiria nini.🤷
Wadau badilisheni sera na mguse sehemu za Msingi. Kupunguza Elimu ya Msingi kuwa Darasa la sita bado haiwezi kuwa Best solution la Tatizo hili la Ajira.
Yaani mnaendelea kupiga Booster mazao yakuwe haraka, wakati wanunuzi hakuna. Mnaatuumiza Wakulima.
Sasa tengenezeni sera ya elimu inayogusa Soko moja kwa Moja. Itengenezeni bidhaa ijiuze yenyewe.
Vigezo vya GPA kwa baadhi ya Kozi visiwe kipaumbele , Tamko la 3.8 kuwa ndo GPA ya Ajira halina ukweli, Mana hata wakipata izo 3.8 GPA wakiwaomba kazi hamto waajiri..!!