Kisa cha kweli: Niliacha kazi nikajiunga masters ili nimsomeshe mdogo wangu chuo

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,750
8,959
Kisa cha kweli: Niliacha kazi nikajiunga masters ili nimsomeshe mdogo wangu chuo
Hiki ni kisa cha kweli ilinitokea mara tu baada ya kupata kazi katika Shirika fulani hapa nchini.

Tangu zamani ndoto yangu kubwa ilikua ni kusoma nje ya nchi kwa scholarship. Mara tu baada ya kuhitimu masomo yangu ya shahada nilibahatika kuajiriwa kwenye shirika X ijapokuwa mshahara niliopewa ulikua mkubwa ila haukuweza kutosha kulipia karo ya mdogo wangu aliyekuwa akisomea astashahada katika chuo fulani jijini X.

Wakati nikiwa nafanya kazi katika shirika lile nilizoea kutumia simu yangu kuingia mtandaoni kufuatilia fursa mbalimbali za scholarship nje ya nchi. Ndipo siku moja nilikutana na tangazo la scholarship linalotoa ufadhili kusomea masters nchi X. Nilifurahishwa na kiwango cha pesa ya kujikimu iliyotajwa katika tangazo lile. Walikua wanatoa pesa ya kujikimu ya 1.5M kwa mwezi ukiachana na ada, bima na pesa ya malazi.

Hakika nilipopiga hesabu niligundua hiyo pesa ingeweza kuniokoa nikaweza kumsomesha mdogo wangu mpaka chuo kikuu. Basi usiku uleule wa mwezi wa 11 nilianza kufanya maombi ya scholarship, nilihakikisha natumia muda wangu ambao sina kazi ofisini na muda wa baada kazi kufanya maombi ya scholarship.

Mpaka kufikia mwezi wa pili nilikua nimeshamaliza kufanya maombi yote. Nikawa nasubiri majibu ya scholarship yatoke. Mwezi wa saba nilipigiwa simu kwamba nimefanikiwa kupata scholarship na hivyo kabla ya mwezi wa tisa nilitakiwa niwe nimeripoti chuoni nchi X.

Hakika sikuamini kama kweli muda umewadia wa kwenda ng'ambo lakini muda wote niliwaza jinsi nitakavyokwenda kutumia hiyo 1.5M kumsomesha mdogo wangu. Hivyo hata sikujiuliza sana, nilikwenda kwa mkurugenzi wa shule nikamweleza kwamba nimepata ufadhili wa kwenda kusoma nje na nitarejea baada ya miaka X.

Mkurugenzi alikubali kwa moyo wote. Basi mwezi wa nane tarehe za katikati nikaenda ubalozi wa nchi X jijini Dar es Salaam, nikaanza kufanya mchakato wa kupata VISA, nikafanikiwa nilihakikisha natumia fedha nilizo save kulipia maana nilijua zitaenda kurudi.

Muda wa safari ulipowadia nilipanda ndege na kuvuka ng'ambo, mara baada ya kufika siku zilizidi kwenda mpaka ilipofika siku niliyoanza kulipwa pesa zangu za scholarship kila mwezi. Pesa zililipwa bila kucheleweshwa wala usumbufu wowote tena bila makato. Lakini cha kushangaza hata bank walikua hawakati hata senti.

Nilihakikisha natumia hiyo fursa kusave hela zangu ili niweze kulipa ada ya kumsomesha mdogo wangu. Mbali na ada ya chuo, kila mwezi nilimpatia boom la laki moja na kumi ili aweze kujikimu lakini pia nilimpatia pesa ya malazi shilingi laki mbili na ishirini kwa mwaka. Ada yake ilikua ni milioni moja na laki mbili japo ilikua inaongezeka kila mwaka. Kiukweli nilipokuwa kazini nilishindwa kusave hata pesa nyingi lakini kule nilifanikiwa kusave pesa nyingi tu.

Katika kile chuo mdogo wangu alisoma kwa muda wa miaka mitatu yaani astashahada mwaka mmoja na stashahada miaka miwili. Nikamwombea shahada akafanikiwa kuchaguliwa kwa mkopo wa loan board. Hivi sasa ndio yupo mwaka watatu chuo X anamalizia shahada yake.

Nilipokuwa nje ya nchi nilijifunza mambo makuu mawili ambayo napenda kuyaongelea hapa.
1. Sio kila mtu anayesoma master's lengo lake ni kuongeza elimu tu rahasha wengine wanasoma master's kwaajili ya kutafuta pesa. Mtu anayesoma masters kwa scholarship mfano nchi niliyokwenda analipwa fedha ambayo inazidi hata mshahara wa mtu anayefanya kazi wizarani. Kwanza uzuri wa ile pesa haina makato hata kidogo unaipokea kama ilivyo.

2. Pili nilipokua kule nilikutana wafanyakazi wanaofanya kazi taasisi kubwa tu hapa Tanzania. Wamefanikiwa kujenga nyumba mara baada ya kupata scholarships.

Naomba niishie kwakusema kwamba watanzania wanafursa nyingi sana za scholarship za kusomea nje ya nchi lakini wengi wao huzidharau hizo fursa. Watu kutoka nchi za afrika magharibi ndio wamekua kinara wa kuchukua hizo fursa. Wamejazana US, UK, CHINA, GERMAN, AUSTRALIA n.k.
 
Nilijiunga na masomo ya uzamili ili nimsomeshe mdogo wangu chuo. Hiki ni kisa cha kweli kilichonitokea mara tu baada ya kupata kazi katika Shirika fulani hapa nchini.

Tangu zamani, ndoto yangu kubwa ilikuwa ni kusoma nje ya nchi kwa scholarship. Mara tu baada ya kuhitimu masomo yangu ya shahada, nilibahatika kuajiriwa kwenye shirika X. Ingawa mshahara niliopewa ulikuwa mkubwa, haukuweza kutosha kulipia karo ya mdogo wangu aliyekuwa akisomea astashahada katika chuo fulani jijini X.

Wakati nikiwa kazini, nilizoea kutumia simu yangu kuingia mtandaoni kufuatilia fursa mbalimbali za scholarship nje ya nchi. Siku moja, nilikutana na tangazo la scholarship linalotoa ufadhili kusomea masters nchi X. Nilifurahishwa na kiwango cha pesa ya kujikimu iliyotajwa katika tangazo hilo. Walikuwa wanatoa pesa ya kujikimu ya 1.5M kwa mwezi, ukiachana na ada, bima na pesa ya malazi.

Hakika, nilipopiga hesabu, niligundua hiyo pesa ingeweza kuniokoa nimsomeshe mdogo wangu mpaka chuo kikuu. Basi, usiku uleule wa mwezi wa 11, nilianza kufanya maombi ya scholarship, nikahakikisha natumia muda wangu ambao sina kazi ofisini na muda wa baada ya kazi kufanya maombi ya scholarship.

Mpaka kufikia mwezi wa pili, nilikuwa nimeshamaliza kufanya maombi yote. Nikawa nasubiri majibu ya scholarship yatoke. Mwezi wa saba, nilipigiwa simu kwamba nimefanikiwa kupata scholarship, na hivyo kabla ya mwezi wa tisa, nilitakiwa niwe nimeripoti chuoni nchi X.

Hakika, sikuamini kama kweli muda umewadia wa kwenda ng'ambo, lakini muda wote niliwaza jinsi nitakavyotumia hiyo 1.5M kumsomesha mdogo wangu. Hivyo, hata sikujiuliza sana, nilikwenda kwa mkurugenzi wa shirika nikamweleza kwamba nimepata ufadhili wa kwenda kusoma nje na nitarejea baada ya miaka X.

Mkurugenzi alikubali kwa moyo wote. Basi, mwezi wa nane tarehe za katikati, nikaenda ubalozi wa nchi X jijini Dar es Salaam, nikaanza kufanya mchakato wa kupata VISA, nikafanikiwa, nilihakikisha natumia fedha nilizosave kulipia maana nilijua zitaenda kurudi.

Muda wa safari ulipowadia, nilipanda ndege na kuvuka ng'ambo, mara baada ya kufika, siku zilizidi kwenda mpaka ilipofika siku niliyoanza kulipwa pesa zangu za scholarship kila mwezi. Pesa zililipwa bila kucheleweshwa wala usumbufu wowote tena bila makato. Lakini cha kushangaza, hata benki hawakukata hata senti.

Nilihakikisha natumia hiyo fursa kusave hela zangu ili niweze kulipa ada ya kumsomesha mdogo wangu. Mbali na ada ya chuo, kila mwezi nilimpatia boom la laki moja na kumi ili aweze kujikimu, lakini pia nilimpatia pesa ya malazi shilingi laki mbili na ishirini kwa mwaka. Ada yake ilikuwa ni milioni moja na laki mbili, ingawa iliongezeka kila mwaka. Kiukweli, nilipokuwa kazini, nilishindwa kusave hata pesa nyingi, lakini pale nilifanikiwa kusave pesa nyingi tu.

Katika kile chuo, mdogo wangu alisoma kwa miaka mitatu, yaani astashahada mwaka mmoja na stashahada miaka miwili. Nikamwombea shahada akafanikiwa kuchaguliwa kwa mkopo wa loan board. Hivi sasa, yupo mwaka wa tatu chuo X anamalizia shahada yake.

Nilipokuwa nje ya nchi, nilijifunza mambo makuu mawili ambayo napenda kuyaongelea hapa:

1. Sio kila mtu anayesoma master's lengo lake ni kuongeza elimu tu; wengine wanasoma master's kwa ajili ya kutafuta pesa. Mtu anayesoma masters kwa scholarship, kama nchi niliyokwenda, analipwa fedha ambayo inazidi hata mshahara wa mtu anayefanya kazi wizarani. Uzuri wa ile pesa ni kwamba haina makato hata kidogo, unapokea kama ilivyo.

2. Pili, nilipokuwa kule, nilikutana na wafanyakazi wanaofanya kazi taasisi kubwa hapa Tanzania. Wamefanikiwa kujenga nyumba mara baada ya kupata scholarships.

Naomba niishie kwa kusema kwamba Watanzania wanafursa nyingi sana za scholarship za kusomea nje ya nchi, lakini wengi wao huzidharau hizo fursa. Watu kutoka nchi za Afrika Magharibi ndio wamekuwa kinara wa kuchukua hizo fursa. Wamejazana US, UK, China, Germany, Australia, n.k.

Scholarship zote hizi hapa ndugu zangu usiogope kuapply ni bure. Tumia bando lako anza sasa:
 
Nilijiunga masters ili nimsomeshe mdogo wangu chuo. Hiki ni kisa cha kweli ilinitokea mara tu baada ya kupata kazi katika Shirika fulani hapa nchini.

Tangu zamani ndoto yangu kubwa ilikua ni kusoma nje ya nchi kwa scholarship. Mara tu baada ya kuhitimu masomo yangu ya shahada nilibahatika kuajiriwa kwenye shirika X ijapokuwa mshahara niliopewa ulikua mkubwa ila haukuweza kutosha kulipia karo ya mdogo wangu aliyekuwa akisomea astashahada katika chuo fulani jijini X.

Wakati nikiwa nafanya kazi katika shirika lile nilizoea kutumia simu yangu kuingia mtandaoni kufuatilia fursa mbalimbali za scholarship nje ya nchi. Ndipo siku moja nilikutana na tangazo la scholarship linalotoa ufadhili kusomea masters nchi X. Nilifurahishwa na kiwango cha pesa ya kujikimu iliyotajwa katika tangazo lile. Walikua wanatoa pesa ya kujikimu ya 1.5M kwa mwezi ukiachana na ada, bima na pesa ya malazi.

Hakika nilipopiga hesabu niligundua hiyo pesa ingeweza kuniokoa nikaweza kumsomesha mdogo wangu mpaka chuo kikuu. Basi usiku uleule wa mwezi wa 11 nilianza kufanya maombi ya scholarship, nilihakikisha natumia muda wangu ambao sina kazi ofisini na muda wa baada kazi kufanya maombi ya scholarship.

Mpaka kufikia mwezi wa pili nilikua nimeshamaliza kufanya maombi yote. Nikawa nasubiri majibu ya scholarship yatoke. Mwezi wa saba nilipigiwa simu kwamba nimefanikiwa kupata scholarship na hivyo kabla ya mwezi wa tisa nilitakiwa niwe nimeripoti chuoni nchi X.

Hakika sikuamini kama kweli muda umewadia wa kwenda ng'ambo lakini muda wote niliwaza jinsi nitakavyokwenda kutumia hiyo 1.5M kumsomesha mdogo wangu. Hivyo hata sikujiuliza sana, nilikwenda kwa mkurugenzi wa shule nikamweleza kwamba nimepata ufadhili wa kwenda kusoma nje na nitarejea baada ya miaka X.

Mkurugenzi alikubali kwa moyo wote. Basi mwezi wa nane tarehe za katikati nikaenda ubalozi wa nchi X jijini Dar es Salaam, nikaanza kufanya mchakato wa kupata VISA, nikafanikiwa nilihakikisha natumia fedha nilizo save kulipia maana nilijua zitaenda kurudi.

Muda wa safari ulipowadia nilipanda ndege na kuvuka ng'ambo, mara baada ya kufika siku zilizidi kwenda mpaka ilipofika siku niliyoanza kulipwa pesa zangu za scholarship kila mwezi. Pesa zililipwa bila kucheleweshwa wala usumbufu wowote tena bila makato. Lakini cha kushangaza hata bank walikua hawakati hata senti.

Nilihakikisha natumia hiyo fursa kusave hela zangu ili niweze kulipa ada ya kumsomesha mdogo wangu. Mbali na ada ya chuo, kila mwezi nilimpatia boom la laki moja na kumi ili aweze kujikimu lakini pia nilimpatia pesa ya malazi shilingi laki mbili na ishirini kwa mwaka. Ada yake ilikua ni milioni moja na laki mbili japo ilikua inaongezeka kila mwaka. Kiukweli nilipokuwa kazini nilishindwa kusave hata pesa nyingi lakini kule nilifanikiwa kusave pesa nyingi tu.

Katika kile chuo mdogo wangu alisoma kwa muda wa miaka mitatu yaani astashahada mwaka mmoja na stashahada miaka miwili. Nikamwombea shahada akafanikiwa kuchaguliwa kwa mkopo wa loan board. Hivi sasa ndio yupo mwaka watatu chuo X anamalizia shahada yake.

Nilipokuwa nje ya nchi nilijifunza mambo makuu mawili ambayo napenda kuyaongelea hapa.
1. Sio kila mtu anayesoma master's lengo lake ni kuongeza elimu tu rahasha wengine wanasoma master's kwaajili ya kutafuta pesa. Mtu anayesoma masters kwa scholarship mfano nchi niliyokwenda analipwa fedha ambayo inazidi hata mshahara wa mtu anayefanya kazi wizarani. Kwanza uzuri wa ile pesa haina makato hata kidogo unaipokea kama ilivyo.

2. Pili nilipokua kule nilikutana wafanyakazi wanaofanya kazi taasisi kubwa tu hapa Tanzania. Wamefanikiwa kujenga nyumba mara baada ya kupata scholarships.

Naomba niishie kwakusema kwamba watanzania wanafursa nyingi sana za scholarship za kusomea nje ya nchi lakini wengi wao huzidharau hizo fursa. Watu kutoka nchi za afrika magharibi ndio wamekua kinara wa kuchukua hizo fursa. Wamejazana US, UK, CHINA, GERMAN, AUSTRALIA n.k.
1.5m ndo unaona hela kubwa eti inazifi mfanyakazi wa wizara, mkuu uandishi wako sio wa mtu aliyesoma masters,
 
Ingependeza ukaweka wazi kuwa kilikuwa chuo fulani katika nchi fulani na mchakato wake wa hizo scholarship unafanyika hivi na hivi .
Lengo ili kusaidia wadogo zetu walio vyioni wenye ndoto kama zako za kisomea masters nje ya nchi .

Lakini ulivyofanya wew umepelekea uzi uonekane hauna maana kabisa maana hakuna cha kujifunza ndani ya ulichoandika hao watu wa west Africa wangefanyiana kama ulivyofanya wewr humu sidhani kama wangejazana hizo nchi za U.K , U S A na AUSTRALIA.
 
Shukrani sana kwa ushauri mkuu
 
Back
Top Bottom