Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe wadai kucheleweshewa pesa yao waliyolipa kwa ajili ada kabla ya Serikali kuwaongeza mkopo

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro wanadai kuwa wanakumabana na kizungumkuti katika kudai kurejeshewa pesa yao waliyoilipa kwa ajili ya ada kabla ya Serikali kuwaigizia mkopo wa ada, ambapo wamehoji chuo kinatumia utaratibu gani unaotoa idhini ya kuhodhi pesa hiyo kwa muda huo zaidi ya miezi nane.

Mwanafuzi mmoja wa kitivo cha Sheria chuoni hapo amesema "Kumekuwa na utaratibu wa kuendesha mambo mengi kimabavu na vitisho badala ya kufuata misingi ya sheria. Mpaka sasa kuna madai ya fedha nyingi sana ambazo wanafunzi tunakidai chuo, fedha hizi zinatokana na malipo ya ada ambayo tulilazimika kulipa wakati wa usajiri ambazo hatukulipa makusudi bali tulishinikizwa kutokana na ufinyu wa muda wa usajiri wakati huo tulitumia fedha ya kujikimu ili kulipa ada kabla ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongeza fedha za mkopo kwa wanafunzi"

Ameongeza kuwa "ikumbukwe kwamba mara baada ya Rais kuongeza fedha kwa wanafunzi, wengi wetu tulipata 100% ya mkopo wa ada kwa hiyo kupunguziwa mzigo wa ada, lakini mpaka wakati huo wengi wetu tulitumia fedha za kujikimu kulipa ada na wengine kukopa madeni mitaani au wazazi kujiingiza kwenye mikopo ya kinyonyaji kama "kausha damu" ili tulipe ada."

Andai kuwa "Mara baada ya Serikali kutulipia ada, tuliandika barua kukitaka chuo kuturejeshea fedha hizo zilizolipwa awali ambazo katika mfumo inaonekana ni ''ada iliyozidi" lengo likiwa ni kuweza kusoma tukiwa na fedha ya kujikimu, lakini mpaka leo hatujalipwa."

"Tangu mwezi mei, tulindika barua hizo lakini majibu ya chuo ni kizungumkuti. Wanatofautiana wenyewe kwa wenyewe wanachotueleza, kuna wanoshangaa kwamba kwanini suala hilo halijafanyiwa kazi, wengine walidai kuwa mchakato huo umekamilika tutapewa fedha Mwezi Juni 2023 lakini umepita na hatujapata fedha zetu"

Aidha Mwanafuzi huyo ambaye amewakilisha wenzake kueleza suala hilo ameendelea kueleza juu ya madai hayo kwamba "Hii ni septemba, fedha bado haijalipwa, tarehe 19/9/2023 tulishangazwa na mmoja wetu kupigiwa simu kwamba fedha hatalipwa mpaka 2024 kitu ambacho ni kichekesho."

Amesisitiza kuwa "Pamoja na kusubiri malipo hayo, tunaweka wazi kwamba msimamo wa mara kwa mara wa kuzuia fedha za wanafunzi ni kuminya haki yao ya kiuchumi. Ni unyonyaji na uonevu; pia ni kinyume kabisa na sheria ya vyuo vikuu, sheria za mitihani (Exams By-laws) na Mzumbe Charter kwani hakuna kifungu kinachokitaka chuo kuzuia na kuhodhi fedha za wanafunzi kwa miaka mitatu bila sababu za msingi"

Amedai kwamba wamekuwa wakiandika barua kutaka ufafanuzi wa jambo hilo lakini mpaka sasa barua hizo majibu hazijajibiwa wala kujuzwa kwa maandishi yoyote kile kinachoendelea "Tuaamini kuwa wanashindwa kuzijibu kwa sababu mchakato huo si halali, itakuwa kuna mchezo mchafu unachezwa kwenye pesa zetu"

Aidha Mwanafuzi mwingine ambaye nae amewakilisha wenzake kungumzia swala hilo amedai kuwa kumekuwepo na mazingira yanayoleta mashaka ikiwemo majibu yanayotoka kwa baadhi ya mamlaka za chuo hicho kuwa pesa hizo zitalipwa baada kumaliza muda wao wa masomo.

"Tunapata mashaka na wasiwasi kuna wanaosema kwamba pesa hizi tutazipata mwaka wa mwisho mtu akiwa anamaliza hii sio haki na ni uongo tu, pesa tunayotakiwa kupewa baada ya hapo ni elfu 30,000 ya tahadhari kulingana na taratibu lakini pesa hii ni haki yetu kuipata sasa" ameeleza mwanachuo huyo

Ameongeza kuwa "bodi ya mikopo kwenye mfumo inatambulika imetoa pesa na huko mbeleni tutakuja kuzilipa, hizi ambazo tulikuwa tumelipa kwa sasa zinasoma kama ada iliyozidi kwahiyo ni pesa zetu halali tunatakiwa kurejeshewa kama kwenye vyuo vingine walivyofanya"

Inakadiliwa kuwa wanafunzi wanaodai pesa hiyo sio pungufu ya 500 ikiwa wengi wao wanadai Shilingi laki tano na zaidi.

Pesa hiyo wanadaiwa kuilipa October, November 2022 wakati wa usajili wa mwaka mpya wa masomo ambapo wanafunzi wengine majina yao yalikuwa hayajapitishwa na bodi ya mikopo kulipiwa ada na wengine kuongezewa asilimia ya kulipiwa ada kutoka asilimia za awali huku wengine wanadaiwa kulipa pesa hizo kipindi rufaa zao zikiwa bado azijajibiwa na kuamuru walipiwe ada.

Majibu ya Chuo: Chuo Kikuu cha Mzumbe chakiri Wanafunzi zaidi ya 330 wanadai malipo ya 'refund' chuoni hapo
 
Wawalipe mbona kudai ada wanakomaa!
 
Back
Top Bottom