SoC01 Mwanafunzi Bora Chuo Kikuu Mzumbe aliyejiajiri kwa kukusanya na kubeba taka na kufanikiwa

Stories of Change - 2021 Competition

teju

Member
Feb 24, 2015
82
310
Naitwa Teju ni kijana wa kitanzania nilisoma shule ya sekondari Ivumwe Secondary school nilipata ufaulu wa Diraja II (Division Two) na ALevel Mbalizi Secondary school nilipata ufaulu wa Daraja I (Division One) na baadaye nilijiunga chuo kikuu cha Mzumbe Course ya Usimamizi wa Biashara katika Masoko (Business Administration in Marketing Management) na nilibahatika kuwa Best student of 2019 kwa kupata First Class ya juu kabisa kwa mwaka

Wakati nikiwa Chuo kikuu nilikua nilitamani sana siku moja nije niwe Mwalimu wa Chuo kikuu hasa vyuo vikubwa hapa Nchini na nje ya Nchi. Na hii ndi ndoto ambayo vijana wengi hasa wanafunzi wa vyuo vikuu huota na hutamani Siku moja wakimaliza Elimu yao basi watakuja kufanya kazi nzuri tena walizo somea. Mfano Marketing Manager, Bank Officer, Accountant na kadharika, lakini uhalisia ulikua hivi baada ya kumaliza Chuo kikuu.

Nakumbuka ilikuwa tarehe 28/7/2019 baada ya kumaliza mitihani yangu ya mwisho ya muhula wa mwisho, kwanza kabisa Darasa letu kuliandaliwa bonge la Sherehe ya kujipongeza kwa kumaliza chuo kikuu, wakati sherehe ile ikiendelea tulikua tukibadilishana mawazo na kushare Address za makampuni mbalimbali kwenda kuomba kazi maana nilikua nikijua kwa ufaulu ule siwezi kukosa kazi nzuri kwenye ofisi nzuri ya Umma ama Binafsi.

Basi wakati watu wakiendelea kuimba na kucheza Nyimbo mbalimbali zenye kuburudisha na kuashiria furaha imetawala, mimi ilikua tofauti kwani nilikua nikiwaza muda wote ambao nimeutumia shule kuanzia darasa la kwanza hadi Chuo kikuu, lakini pia nilikua najaribu kutafakari baada ya kumaliza chuo nini kitafuata? picha ilikua iki niijia ya nyumbani kijijini kwetu Mamba kisalasi,Kata ya Mamba Tarafa ya Kipembawe wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya.

Ndugu msomaji mimi ni kijana wa kiume nilie zaliwa katika Familia ya kimasikini sana, ya wazazi wakulima wa jembe la mkono wasio na uhakika wa kupata pembejeo za kilimo kwa wakati, na ambao hawana uwezo hata wa kulipa ada ya Shule. Katika safari yangu ya elimu niliweza kubahatika kusomeshwa na watu mbalimbali walio kuwa wanaona na kuthamini jitihada zangu za kusoma kwa bidii na kufauru vizuri.

Basi nilipokuwa nikikumbuka nilivyokua nikenda shule Peku, nikikumbuka wakati nikifukuzwa ada ya shule wazazi wanakuja kumuomba mwalimu mkuu ili walete Mahindi wayathaminishe na fedha ili mimi niendelee na shule, basi Machozi yalianza kunidondoka na hasa nilipo fikilia wakati wa mahafari wazazi wangu watakuwa na furaha sana na pengine wakiamini kuwa sasa kijana wao nimemaliza Chuo kikuu hivyo naenda kupata kazi na angalau wapumzike namimi niweze kuwasaidia Majukumu mengine.

Ndugu msomaji hali ilizidi Kua mbaya baada ya hotuba ya mwalimu wetu mlezi wa darasa, alipo sema "Najua wengi wenu mmesoma kwa bidii na sisi tumewapika na mmepikika vilivyo, ningekuwa na kampuni kubwa ya Masoko ninge ajiri nusu ya darasa lenu maana katika historia ya kufundisha chuo hiki nadhani mwaka huu ndio tumetoa wanafunzi ambao kuanzia wakwanza mpaka wa mwisho wote wameiva " pia aliongeza kwa kusema hali ilivyo kwenye soko la ajira ni mbaya sana, mmemaliza kipindi kihaya ambacho hata chuo hakina bugeti ya kuwabakisha wanafunzi bora kwa ajili ya kuandaa waje wawe waalimu huko baadaye lakini nendeni mkapambane na maisha na usiogope wala msichague kazi kwani mchagua jembe si tukamalizia kwa kusema Mkulimaaaaaa, akashukuru na kuaga.

Maneno yale pamoja na ya wazazi yalinipa ujasiri mkubwa sana, kwa kuwa wakati nikisoma Chuo nilikua nimepanga na kodi ya pango ilikua inaisha tarehe 30/07/2019 basi inabidi nijipe moyo nikasema Mimi ni msomi wacha nipambane elimu hii ni makaratasi tu ila mimi naanza upya. Basi siku iliyo fuata wenzangu walikua wakikata tiketi za mabasi kwaajiri ya kurudi makwao mimi niliamkia kwa baba mwenye nyumba na kumuomba niendelee kubakia pale na namtafutia Kodi ya pango angalau tarehe 15/8/2019 nitamlipa. Mungu mwema mzee yule akakubali na mimi ndio nilipo ingia mtaani rasmi na kuanza kutafuta Fulsa.

Fulsa yangu ya kwanza kuiona ilikua ni kukusanya taka majumbani, maofisini na sehemu za Biashara, na kuzipeleka sehemu rasmi iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kukusanyia taka Basi mwanzoni nilianza kwa aibu sana nilikua nikikodi tololi kwa shiringi 5000 kwa siku alafu napitia mitaani naita MBEBA TAKA ANAPITA hapo ndipo niligundua kunafulsa kwenye eneo hilo watu wakitoa majumbani na kunitia njoo njoo uchukue. Kila aliyepakia taka alinilipa kiwango cha chini 500/= lakini wapo walio Lipia zaidi kwa hiali yao.

Baada ya muda mfupi viongozi wa mitaa wakiwepo Mabalozi hasa balozi Mwampiki waliniita na kanishauri kuwa nipange ratiba ambayo wananchi wataifuata angarau mara moja kwa wiki wawe wanaweka taka kwenye mfuko na kuziweka pembezoni mwa barabara kila jumamosi, na wao wawa hamasishe jamii kulipa shilingi 3000/= kwa mwezi basi nilikubari na hapo ndio kazi ikawa nzuri muamko ulikua mkubwa na mapokeo yakawa mazuri hivyo nilianza kupata kipato ambacho kiukweli niliona Kuna njia mbele nitatoboa, hapo kunavijana wawili ambao huwa wanashinda jalalani/dampo kuokota vitu nikawachukua na kuanza kufanya nao kazi tulianza kukodi gari ndogo kirikuu na baadaye kadri huduma ilivyo kuwa bora ndivyo wananchi maeneo jirani wakawa wanahitaji huduma yetu. Tumeenda hivyo mpaka mwaka huu mwezi wa kwanza niliandika proposal Halimashauri kuomba watupe eneo kubwa na uwe mradi wa kuosaidia jamii na serikali kusafisha mazingira na kuondosha taka Majum
bani, sehemu za biashara na kwenye Taasisi mbalimbali .

Halimashauri walikubali na kuanzia mwezi wa 3/2021 walinisainisha mkataba na sasa natakiwa kukusanya Milioni 12 kwa mwezi
Katika 100% Asilimia 30inabakia Halimashauri kwa ajili ya kuendeshea shughuri za dampo kuu, na asilimia 70 naipata mimi mzabuni hivyo Kwasasa nimeajiri vijana 8 wanao kusanya Fedha mitaani (Ada ya taka) na nawalipa 360,000/= na pia vibarua 4 wakupakia taka kwenye tipa ambao nawalipa @20, 000/= kwa siku na wanafanya kazi siku 15 kwa kila mwezi.

Pia katika kazi hii mwaka jana niliweza kununua kipande cha ardhi cha milioni 6 ambapo nimeweza kuanza ujenzi mwaka huu na Lengo ni kuwa na dhamana isiyo hamishika ili niweze kukopesheka Bank na hatimae niweze kukopa na kununua Gari kubwa Tipa Scania au Howo, Faw au Fuso kwa ajiri ya kubea taka na niachane na magari ya kukodi ambayo natumia gharama kubwa ya uendeshaji wa kazi.

Husia wangu kwa vijana tusidharau kazi, waje wajifunze kwangu kazi zote ni kazi wasichague kazi wakati hawana kazi chagua kazi ukiwa tayali kazini na sio lazima kuajiriwa waweza kujiajiri pia TUKUMBUKE HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA tusiogope kuanza chini.Ahsante nawasilisha
 
Mkuu, hizi shughuli zako unafanyia mkoa gani ili nije nijifunze.
Hongera sana dogo. Hongera kwa uthubutu.

Umeapply properly marketing skills zako kwenye sekta ya uzoaji taka.

La mwisho,please improve your communication skills too.
Hata mimi nimeshangaa uandishi wa mtu aliyemaliza chuo kikuu na kupata gpa ya juu, ok ameeleweka though.
Mimi wa lasaba B nafikiri naweza kuandika kuliko yeye.
 
Wewe ni mtunzi tu mzuri wa stori, ila hakuna cha best student hapo kwa mwandiko huo…. usitake tuamini Mzumbe ni kama The Amazon College tu.

Kwa kuwa lengo ni story of change, idea yako ni nzuri yaani umetisha mwanangu.
Nashukuru kwa ujasiri wa kunikosoa na kunirekebisha kwani kufanya hivyo naamini unayo nia ya dhati kabisa ya kuniboresha niwe Mwandishi bora nimeupokea kwa 🤲🤲
 
Usiishie kusomba tu taka ishia kwenye kuzigeuza taka kuwa fursa mfano zibadili ziwe bidhaa.mfano mbolea,taka za plastic zisage soko lipo kubwa huwezi lijaza kuna mchina anataka tani 300 kwa mwezi za taka za plastic ngumu zilizosagawa ananunua tani moja kwa shilingi milioni moja na laki 2 yupo mwanambaya mkuranga.
Hichi ni kiwanda kimoja tu,au nikulink na wanunuzi wa nje ya nchi wa kununua taka.Nikufunze kutengeneza mbolea organic manure uuze kwenye mashamba ya kilimo hai wanaoexport nje mboga na matunda.Tenganisha taka karatasi na maboksi yupo mnunuzi mkubwa nikulink nae.Zipo mashine za kugeuza taka plastic kuwa vigae tiles, pavers,mbao,nk.Au nikufunze kutengeneza dizeli na petrol,gas kutokana na taka za plastic hii ni fursa dizeli lita 2500 taka unakusanya bure gharama ya kuigeuza dizeli ni shs 100 kwa lita ukiuza lita ya dizeli kwa shs 2000 mfano uza lita 1000 kwa siku tu.Dizel unauza kwenye magari,mitambo,nk.
Fursa ni nyingi sana ukifungua akili.
 
Mkiajiriwa nyie mnaona wenzenu hawana akili kabisaaa..!!
Kama mshahara haukutani mwezi yaani unakusaidia usife njaa Ili ukatumike tena kesho si bora anaeingiza kwa juhudi zake,Mdogo Mdogo akiwa na ndoto kuu ya kufika mbali ndo tasfiri ya anza kwa mikono ukingojea jembe
 
Biashara ya taka inazalisha mabilioni ya dola kwa mwaka kwa wafanyao.
Na jamaa zangu wanaofanya hizi mambo mda mfupi tu wako mbali hakuna aliyewahi akafilisika wengi walizidi kuongeza mashine.Ni ajira ya kudumu pia.
 
Usiishie kusomba tu taka ishia kwenye kuzigeuza taka kuwa fursa mfano zibadili ziwe bidhaa.mfano mbolea,taka za plastic zisage soko lipo kubwa huwezi lijaza kuna mchina anataka tani 300 kwa mwezi za taka za plastic ngumu zilizosagawa ananunua tani moja kwa shilingi milioni moja na laki 2 yupo mwanambaya mkuranga.
Hichi ni kiwanda kimoja tu,au nikulink na wanunuzi wa nje ya nchi wa kununua taka.Nikufunze kutengeneza mbolea organic manure uuze kwenye mashamba ya kilimo hai wanaoexport nje mboga na matunda.Tenganisha taka karatasi na maboksi yupo mnunuzi mkubwa nikulink nae.Zipo mashine za kugeuza taka plastic kuwa vigae tiles, pavers,mbao,nk.Au nikufunze kutengeneza dizeli na petrol,gas kutokana na taka za plastic hii ni fursa dizeli lita 2500 taka unakusanya bure gharama ya kuigeuza dizeli ni shs 100 kwa lita ukiuza lita ya dizeli kwa shs 2000 mfano uza lita 1000 kwa siku tu.Dizel unauza kwenye magari,mitambo,nk.
Fursa ni nyingi sana ukifungua akili.
Nahitaji hili somo
 
Umemaliza vibaya mkuu,UKIFUNGUA AKILI.afungue zaidi ya hapo kivipi??ndo anaanza hata miaka mi3 bado
 
Husia wangu kwa vijana tusidharau kazi, waje wajifunze kwangu kazi zote ni kazi wasichague kazi wakati hawana kazi chagua kazi ukiwa tayali kazini na sio lazima kuajiriwa waweza kujiajiri pia TUKUMBUKE HATA MBUYU ULIANZA KAMA MCHICHA tusiogope kuanza chini.Ahsante nawasilisha
Hongera ndugu teju
Tayari kura yangu kwako
 
Mleta mada kama hujaoa nakupa binti yangu bikra na graduate mwenye GPA nzuri bure.
Hongera sana kijana.!
 
Hongera
Sijui wa kanda ya Ziwa
Unachanganya R NA L
SHUGHULI sio shughuri
Fursa sio fulsa
Kufaulu sio kufauru

Andiko ni zuri ila sijui kwa nini Jamii forum wameruhusu andiko liwe kama story.
 
Back
Top Bottom