Mwana FA: Fainali ya Simba dhidi ya RS Berkane itachezwa Benjamin Mkapa

Mwana FA: Fainali ya Simba dhidi ya RS Berkane itachezwa Benjamin Mkapa

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) amesisitiza kuwa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba SC na RS Berkane itachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Mei 27, 2024 kwa kuwa Serikali imefanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha eneo la kuchezea la uwanja wa Benjamini Mkapa linakuwa sawa ikiwemo kuajiri kwa dharura mkandarasi mwenye uzoefu mkubwa kwenye masuala hayo.

Mwinjuma ametoa kauli hiyo leo Mei 5 2025 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu maswali mbalimbali ya wabunge waliotaka kupata uhakika wa Serikali kukamilisha marekebisho ya eneo la kuchezea kwa wakati ili uwanja huo utumike kwa mchezo huo.

"Niwatoe hofu wapenzi wa mpira wa miguu wakiwemo wapenzi wa Simba SC kuwa mechl ya Fainali ya kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba SC dhidi ya Berkane itachezwa palepale Benjamini Mkapa hakuna mahali inaenda na tukio hili la kihistoria litafanyika mbele ya macho yao wakiwa wanalishuhudia"
View attachment 3325338
SOMETIMES WANASIASA SIO WA KUWAAMINI SANA, WAKISEMA NJE KUNA MVUA TOKA NA WEWE UKAHAKIKSHE

NGOJA TUONE...WENGINE NI MATOMASO
 
Kwa nini kulazimisha kuchezea Taifa. Au kwasababu ndiko wanapologea.
Mbona mchezo wa Yanga walikimbia??? Ile kauli ya Kwa Mkapa hatoki mtu iliishia wapi?? Simba na mbereko yao TFF wana wewesek tu. DHULUMA waliowafanyia YANGA itawatafuna this time around!
 
Wangeipeleka Amani Zanzibar. Pitch ya kwa Mkapa bado haipo vizuri
Mm nashangaa kwann Simba, TFF na Serikali wanang'ang'ania Kwa Mkapa? Hii game ni ya CAF, hii siyo Ligi ya NBC iliyojaa upendeleo na upuuzi mwingi. CAF ndo wenye mchezo fuateni maelekezo ya CAF msfikiri hii mechi ya Simba na Yanga...!!!
 
Mm nashangaa kwann Simba, TFF na Serikali wanang'ang'ania Kwa Mkapa? Hii game ni ya CAF, hii siyo Ligi ya NBC iliyojaa upendeleo na upuuzi mwingi. CAF ndo wenye mchezo fuateni maelekezo ya CAF msfikiri hii mechi ya Simba na Yanga...!!!
Ngoja tusuburi rufaa yao kesho
 
1747499646648.jpg
 
Ngoja tusuburi rufaa yao kesho
Ujue nini? Baba wa Taifa alisema Ukianza kula nyama ya mtu hutaacha na hiyo Dhambi itakutafuna. TFF, BODI YA LIGI wamefanya maamuzi ya kipuuzi sana kuhusu mechi ya Simba na Yanga 8 March,2025.

TFF na Board ya League mpaka sasa hawajatoa maamuzi yoyote badala yake wamepanga tarehe mchezo urudiwe 15 June, bila ya kutoa judgement what really conspired on 8th March, why Simba refused to appear at Ben Mkapa pitch without any no good reason!!!
Hiyo dhambi imewarudia kwa mlango mwingine. TFF na League Board lazima wajitathimini.
 
Back
Top Bottom