Mwana FA: Fainali ya Simba dhidi ya RS Berkane itachezwa Benjamin Mkapa

Mwana FA: Fainali ya Simba dhidi ya RS Berkane itachezwa Benjamin Mkapa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,308
Reaction score
18,482
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Hamis Mwinjuma (Mwana FA) amesisitiza kuwa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba SC na RS Berkane itachezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Mei 27, 2024 kwa kuwa Serikali imefanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha eneo la kuchezea la uwanja wa Benjamini Mkapa linakuwa sawa ikiwemo kuajiri kwa dharura mkandarasi mwenye uzoefu mkubwa kwenye masuala hayo.

Mwinjuma ametoa kauli hiyo leo Mei 5 2025 Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu maswali mbalimbali ya wabunge waliotaka kupata uhakika wa Serikali kukamilisha marekebisho ya eneo la kuchezea kwa wakati ili uwanja huo utumike kwa mchezo huo.

"Niwatoe hofu wapenzi wa mpira wa miguu wakiwemo wapenzi wa Simba SC kuwa mechl ya Fainali ya kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba SC dhidi ya Berkane itachezwa palepale Benjamini Mkapa hakuna mahali inaenda na tukio hili la kihistoria litafanyika mbele ya macho yao wakiwa wanalishuhudia"

 
Back
Top Bottom