Mwali: Mmiliki wa DOWANS ni huyu!

Status
Not open for further replies.
Kichekesho ni kwamba tulifikiria kutaifisha mitambo ya Dowans (as an option) bila kufahamu kwamba mitambo hiyo imewekwa kama dhamana kwa mikopo waliyochota benki..Fedha ambazo haijulikani zimetumika au zimekwenda wapi..
Sasa wanabodi pigeni mahesabu kwanza hela wanazochota toka kwetu kisha jumlisha na zile walizochota benki......
Ehhh Mungu weee tumeliwa vibaya jamani!

Bob yaani nimecheka saaaaana leo....na afadhali kesho ni Ijumaa......hivi unakumbuka kuna MEMBER mmoja hapa JF alishawahi kutoa mfano wa biashara ya "Nyani"........yaani sasa naona tutabaki na manyani mikononi.........na tatizo la nyani kulamahindi linabaki pale pale..........na pesa zimeshaishia.........lol
 
Huyu Advocate Ringo Tenga, mbona anaachwa tu wala hapewi msukosuko kuulizwa who is behind Dowans?

Lakin hii ndiyo imekuwa style ya tassisi zetu za kipelelezi ambazo nazo zinaendeshwa na mafisadi -- kwa maana ya wanazoziongoza. Kwa mfano Hosea alishindwa kabisa kum-confront Kimei na kumuuliza yale mabilioni ya Kagoda yaliyolipwa cash over the counter kutoka matawi ya benki yake yalilipwa kwa nani?

Kampuni la Dr. Ringo Tenga hailitwi Ringo & Associates... Linaitwa Law Associates... na Ofisi zake haziko peugeot house, upanga road....

Ofisi za Law Associates ziko Azikiwe Road, CRDB building, Law Associated ni hawa hapa

Masahihisho tu... musiache kuchukia watu bila sababu
 
Huyu Advocate Ringo Tenga, mbona anaachwa tu wala hapewi msukosuko kuulizwa who is behind Dowans?
Lakin hii ndiyo imekuwa style ya tassisi zetu za kipelelezi ambazo nazo zinaendeshwa na mafisadi -- kwa maana ya wanazoziongoza. Kwa mfano Hosea alishindwa kabisa kum-confront Kimei na kumuuliza yale mabilioni ya Kagoda yaliyolipwa cash over the counter kutoka matawi ya benki yake yalilipwa kwa nani?

Dr. Tenga alikuwa mmoja wa wanamageuzi wa awali walioanzisha NCCR. Lakini kama ilivyokuwa kwa Dr. Lamwai, walipoonjeshwa asali ya CCM, wakaachana na kupigania Demokrasia na wakajiozesha kwa mafisadi.

Sina shaka Dr. Tenga hivi sasa naye ni mCCM.
 
As wrote in another post... Dr. Tenga was not involved in this deal!!!!
 
As wrote in another post... Dr. Tenga was not involved in this deal!!!!

Ringo & Associates walihusika na Dowans sawa lakini waliohusika na Kagoda ni Law Associates ya Dr. Ringo Tenga. Ni huyu huyu aliyemtetea Ukiwaona Ditopile Mzuzuri na bila shaka huyu huyu anayehusishwa na Benki Kuu. Hivyo wote kwa namna moja ama nyingine watakuwa wanajua sura halisi za huyo FISADI.
 
Chonde chonde jamani uchaguzi unakaribia, wapinzani jengeni vyama mpaka vijijini ili watanzania wakombolewe na CHAMA KWANZA....
DOWANS na takataka nyinginezo ni mwanzo wa utungu ila mwisho haujawadia. mtakapoona chukizo la kifisadi linataka kutamalaki nchi mjue mwisho ndo unawadia..
 
Wakuu, bado naendelea kutafuta article ya Tanzania Daima ya leo - Jumapili ambapo wameweka majibu ya mmiliki wa Dowans Tanzania Ltd anayeadiwa kuwa bilionea wa Oman na brigadia mstaafu wa Oman. Naomba mtu aiweke hapa, ingawa hakuna cha maana
Lakini pia naomba mwenye subscription ya African Intelligence- the Indian Ocean newsletter atuwekee hapa article niliyoiona katika website yao... nimepata tu ndondoo maana inahitaji subscription
THE INDIAN OCEAN NEWSLETTER - 08/11/2008
TANZANIA
Dowans Tanzania Ltd
An electricity generating company, part of Dowans Holding owned by the Aladawi family of Dubai and Oman, wants to pull down the shutters

Nadhani tukiunganisha na ile article ya Tanzania Daima, the picture gets more interesting....
 
Last edited:
Kwanini walikuwa wanaficha ficha all the time? Huu wizi mtupu. Kampuni ni ya Rostam na ana marafiki wengi tu uarabuni na persia...Si ilisemekana alimwuzia Manji?
Hizi siasa za kujaribisha jaribisha na huku muda unapotea hazina mpango....Wanapiga domo hadi muda ufike wawakamate wananchi pabaya kwa madai ya "Si Tuliwaambia?" No wonder kuna leadership vaccum ya kutisha...JK keshawapa nafasi za kutosha waache kuwadhalilisha wananchi na yeye mwenyewe kuwa kama puppet.
 
Part of which Dowans Holding? Je kuna wale watatu, Suleiman Mohd Yahya Al Adaw, Puthan N.C. Menon and Abbas Ibrahim Al Yousef tuliambiwa nao ni owners wa Dowans Holding SA ambayo ni United Arab Emirates. Du mwaka huu kweli tutapata majine mengi. Haya, tunaomba kuwasilisha majina mengine jameni.
 
Last edited:
huyu Aladawi amekiri kwamba ameltwa nchini na Rostam...na amedai Dowans Tz Ltd ni sehemu ya Dowans HOldings ya South Africa. Pia amedai kuwa Dowans Tz Ltd hawana deni lolote la benki na kwamba wamesingiziwa na kuchafuliwa jina. Ndo maana nimeomba ushirikiano wa wanaJF maana hii connection ya Oman pia inanitia shaka hasa ukizingatia connection ya Oman na Tanzania in particular Zanzibar.
 
Is Aladawi = Suleiman Mohd Yahya Al Adaw ?

Kumradhi article sina hapa lakini niemjaribu kufanya utafiti via internet na inaonekana ya kuwa familia hii huandika majina yao Aladawi au Al Adaw, na kuna ndugu wanafanya biashara mbalimbali....
 
Kumradhi article sina hapa lakini niemjaribu kufanya utafiti via internet na inaonekana ya kuwa familia hii huandika majina yao Aladawi au Al Adaw, na kuna ndugu wanafanya biashara mbalimbali....

Hakuna utata... mwali keshaanza kutolewa.. angalia nyaraka za BRELA... kuna breaking news..
 
huyu Aladawi amekiri kwamba ameltwa nchini na Rostam...na amedai Dowans Tz Ltd ni sehemu ya Dowans HOldings ya South Africa. Pia amedai kuwa Dowans Tz Ltd hawana deni lolote la benki na kwamba wamesingiziwa na kuchafuliwa jina. Ndo maana nimeomba ushirikiano wa wanaJF maana hii connection ya Oman pia inanitia shaka hasa ukizingatia connection ya Oman na Tanzania in particular Zanzibar.

Kama kweli mmiliki wa Dowans kakiri Dowans hawadaiwi na mabenki naona kuna mchezo mchafu hapo.Mabenki yakae mkao wa kuumia.Ina mmana hizo pesa hakukopa Dowans lakini mali zake ziliwekwa Rehani.Ni nani huyo aliyekopa kwa kutumia mitambo ya Dowans? Na pesa hizo alizokopa alipeleka wapi? Nasikia harufu kali ya money laundering hapa.Mabenki ikiwemo benki kuu wachunguze hapo hizo pesa ambazo mwenye kampuni hazijui zilikopa na vishoka au matapeli? Na walizipeleka wapi kufanya nini.Na je mabenki yaweza zipata kulipwa madeni yao.Wataalamu wa mabenki kazi kwenu.Kama nlikopesha matapeli wakawaletea hati feki mtajijua au kama mliweka rehani mitambo ya watu bila ridhaa ya wenyewe napo mtajijua.

Pili kama mwenye kampuni hajui kuwa kampuni yake inadaiwa chochote na mabenki basi mabenki yaliyokopesha maruhuni Dowans au kumdhamini yajiandae kulia kilio cha mbwa kwenye mahakama za kimataifa na kumlipa mmiliki mabilioni ya dola kama walikopesha kizembe zembe.

Ushauri wa bure kwa vyombo vya fedha vichunge huyu mdudu anaitwa Dowans na kama wana akaunti na madai naye wawahi mapema kumbana mwizi wao wa ndani ya nchi aliyekopa hizo pesa kabla hazijaota mabawa zikayeyuka na wao wakabaki na mitambo mitumba iliyooza na kujaa kutu ya Dowans ambayo hawawezi muuzia yeyote.Ni vizuri recovery measures zianze haraka na mwabane wamiliki wote wawe ndani au nje ya nchi.Fanyeni upesi time is running out.
 
Taarifa zaidi zimepatikana kuhusu huyu mwarabu wa Oman na inaonekana ni mwongo kwani alichukua mwenyewe mkopo! Taarifa zaidi This Day ya leo
THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

NEW evidence has emerged about the state of indebtedness of the controversial Dowans Tanzania Limited company, which came close to selling its second-hand 100-megawatt turbines to the state-owned Tanzania Electric Supply Company (TANESCO).

Official company documents show that the listed shareholder of Dowans Tanzania Ltd, Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, signed legal papers with Barclays Bank Tanzania Limited acknowledging a debt of $20m.

The 56-year-old Al Adawi, a citizen of the Sultanate of Oman, surfaced for the first time over the weekend to tell a local Kiswahili newspaper that Dowans Tanzania is not in debt.

Introducing himself as the controlling shareholder of Dowans, he is quoted to have claimed that the reports suggesting that the company received loans from various commercial banks amounting to $75m (over 100bn/-) were false.

However, documents seen by THISDAY confirm that Al Adawi himself signed documents acknowledging a $20m debt from Barclays Bank Tanzania Ltd.

Other official company documents also show that Dowans received further substantial loans from Barclays Bank Mauritius and Stanbic Bank Tanzania Limited.

According to the documents dating back to 2007, Dowans Tanzania Ltd signed a debenture instrument with Stanbic Bank for another loan of $20m.

Two Stanbic Bank employees - Helen Makanza and Jeff Daly - are understood to have been involved in handling the debenture with Dowans.

However, in another development, Stanbic Bank has now declared that Dowans was not indebted to the financial institution.

’’Our records show that the said company (Dowans) is not indebted to our bank,’’ said a letter from Stanbic Bank sent to THISDAY late last week.

According to THISDAY findings, the company surrendered all its assets - including turbines, motor vehicles and machinery spare parts - as security for obtaining the massive bank loans.

Legal documents confirm that the five second-hand turbines now lying idle at Ubungo in Dar es Salaam were part and parcel of the collateral.

The turbines as described in the documents are four trailer-mounted General Electric (GE) TM-2500 gas turbine power generator sets, plus one LM-6000 PD turbine also manufactured by GE.

Each of the mobile TM-2500 power generator sets produces around 20MW of electricity, while the larger LM-6000 PD set is capable of producing up to 48 megawatts.

The Dowans company inventory list submitted to its lenders also includes two step-up transformers for outdoor installation, plus various spare parts for the electrical equipment.

The documents show that Dowans Tanzania Ltd pledged all these assets, both movable and immovable, to secure the hefty loans.

The certificates of indebtedness signed by Dowans show that the company gave up to the banks its rights to ’’all entitlements which it may at any time and from time to time have to the payment of any money.’’

Hongera This Day kwa kazi nzuri na chondechonde Tanzania Daima, msije mkatumika na mafisadi kuwasafishia njia!
 
Kuanzia leo tutaanza kufunua na kuunganisha vipande vipande vya Dowans. Jumamosi iliyopita (tarehe 7 Machi, 2009) tulipata nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Brig. Gen. Al-Adawi mtu ambaye jina lake, na anuani vinaonekana kwenye nyaraka za BRELA kuwa ndiye mmiliki wa kampuni iliyoko kwenye songombingo ya tuhuma za ufisadi ya Dowans. Jumamosi hii iliyopita pia tulipata nafasi ya kuzungumza tena na Brigedia huyo baada ya kugundua kuwa ametuongopea. Kati ya mahojiano ya Jumamosi ile na Jumamosi hii kulifanyika kikao huko Dubai Jumapili ya tarehe 8 Machi, baada ya mahojiano yetu na maamuzi mbalimbali yakachukuliwa.

Leo katika kuifunua Dowans tunaanza na wamiliki tu halafu habari zaidi ya nini kimejiri inakuja wiki hii katika kile tunachokiita "kumfunua Mwali". Kwa vile Waziri Ngeleja amesema anataka mjadala huu wa Dowans ufungwe, tumedhamiria kuhakikisha kuwa tunaufunga kwa namna yetu wenyewe.

Sehemu zote mbili za mahojiano na Gen. Al-Adawi zitarushwa katikati ya wiki hii kupitia mwanakijiji.com na bongoradio.com... USIKOSE KUONGEZEWA MASWALI KWENYE MAJIBU UNAYOFIKIRI UTAYAPATA

Hivyo sasa angalia nyaraka kisha subiri habari....

i268_dowansadawy.jpg

dowans_adadawy_2_phixr.jpg

NB:*
  • Habari ya kuifunua Dowans inatarajiwa kutoka kwenye Cheche na kwenye Magazeti mengine ya kila wiki.
  • Kikwete mwenyewe ni sehemu ya ujio wa kampuni ya Dowans...!!
  • Mahojiano na Al-Adawi yatarushwa pia katikati ya wiki inshallah!
  • Tutaonesha pia jinsi gani Rostam Aziz aliwadanganya watanzania kuwa hakuhusika na suala la ujio wa Dowans na kudai kuwa yeye ni "mkandarasi tu" aliyeomba kazi na "kuambiwa kuacha anuani" yake...

Na mambo mengine ambayo yatakufungua macho kuthibitisha kile unachoweza kuwa umefikiria.. Dowans
 
Kuanzia leo tutaanza kufunua na kuunganisha vipande vipande vya Dowans. Jumamosi iliyopita (tarehe 7 Machi, 2009) tulipata nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Brig. Gen. Al-Adawi mtu ambaye jina lake, na anuani vinaonekana kwenye nyaraka za BRELA kuwa ndiye mmiliki wa kampuni iliyoko kwenye songombingo ya tuhuma za ufisadi ya Dowans. Jumamosi hii iliyopita pia tulipata nafasi ya kuzungumza tena na Brigedia huyo baada ya kugundua kuwa ametuongopea. Kati ya mahojiano ya Jumamosi ile na Jumamosi hii kulifanyika kikao huko Dubai Jumapili ya tarehe 8 Machi, baada ya mahojiano yetu na maamuzi mbalimbali yakachukuliwa.

Leo katika kuifunua Dowans tunaanza na wamiliki tu halafu habari zaidi ya nini kimejiri inakuja wiki hii katika kile tunachokiita "kumfunua Mwali". Kwa vile Waziri Ngeleja amesema anataka mjadala huu wa Dowans ufungwe, tumedhamiria kuhakikisha kuwa tunaufunga kwa namna yetu wenyewe.

Twasubiri kwa hamu kubwa mkuu, tunakuaminia
 
- Mzee Mwanakijiji

- Mola akujaze nguvu and Aluta Continua

- Tunasubiri Cheche/MwanaHalisi kwa shauku kubwa sana
 
Poa MM,

Kama mkurungenzi wa Dowans ni huyu mwarabu (Al Adawi) kwa nini siku zote wanashindwa kumtaja? Au jina lake ni kama la Mungu kwa hiyo tunazuiwa kulitaja taja jina la Bwana Mungu wetu?

Nasubiri kumwona mwali mwenyewe. Naona hapa umetoa ngoma nje zipate jua ili shughuli inoge.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom