Mvua na dishi la Dstv kusumbua

Mvua na dishi la Dstv kusumbua

Sasa huku Arusha ndio kiboko mvua ikifunga wingu la maana inakata dstv, sasa na tanesco nao huwa wanajiongeza mvua ikianza tu umeme unakata hapa toka saa kumi na mbili no umeme acha tu
Dstv kama tanesco hawapatani na mvua ila afadhsli tanesco ikikata luku inasimama, dstv ikikata salio linaliwa tu.
 
Kama tatizo lingekuwa dish set up basi dstv wasingeweka 'due to bad weather' kwenye notification wangeweka check your dish and connection
Ni mvua mbona ukiwapigia wanakwambia ikiwa na upepo ndiyo sana na wenyewe husema hali ya hewa
 
Kuna mtu kafunga dish la 8ft,(ungo mkubwa sana) kanunua decoder ya DStv ila tatizo la kukatika kwa matangazo kipindi cha mvua liko pale pale.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ni shida yaani na wenyewe wanawatengenezea mafundi wao ulaji na ajira
 
Ni mvua mbona ukiwapigia wanakwambia ikiwa na upepo ndiyo sana na wenyewe husema hali ya hewa
Ndio nawashangaa hawa mafundi wa hapa jf wanaojidai za kwao ni weather proof!
 
Ndio nawashangaa hawa mafundi wa hapa jf wanaojidai za kwao ni weather proof!
Yaani acha mie huwa nawapigia tunaongea kuna wakati channel zinazopotea hunielekeza, mafundi wapo humu kazi kweli, hivyo sijui vidude gani mie vyote vipo
 
Mara nyingi mvua ikinyesha DSTV matangazo yanakatika. Kwa mwezi huu wa nne na masika hizi si ajabu mvua ikanyesha wiki nzima au mara tano kwa wiki na hapo hutaona matangazo ya DSTV.

Je hapo si sawa na mtu unalipia huduma na huipati? Afadhali Tanesco umeme ukikatika LUKU haisomi kwahio huliwi pesa bure. Mfano leo kuanzia mchana huku nilipo mvus inanyesha mwendo ni on off kwenye DSTV.

Kuna njia yoyote DSTV mnaweza kufidia siku ambazo matangazo yanakatika kwasababu ya mvua?
Cc TCRAView attachment 738366
Tafuta fundi mzuri aongeze signal kwenye dish hilo tatizo hutaliona,kukatika huko kunasababishwa hupati signal za kutosha,ikitokea wingu au mvua inakata signal hizo chache unazopata
 
Watu wengi mnajibu as if ni isolated case. Sehemu nyingi mvua ikinyesha DSTV inakata. Kwenye baa,hotel na majumbani. Ina maana hao wote dishes zao zimefungwa vibaya? Na wafungaji na wauzaji wa hizo dishes ni dstv na mafundi wao. Sio kwamba watu wanaokota tu dish na kujifungia dstv
Basi kama unavyosema ni hivyo basi mimi nina bahati nzuri na dstv maana nilifunga dstv na azam nina karibia mwaka sasa azam ndio huwa inanisumbua ila dstv hata siku moja,
 
Tafuta fundi mzuri aongeze signal kwenye dish hilo tatizo hutaliona,kukatika huko kunasababishwa hupati signal za kutosha,ikitokea wingu au mvua inakata signal hizo chache unazopata
Nyinyi watu mnachekesha. Ikiwa na tatizo la signal hausubiri mvua kuanza kusumbua, tena S3 ndio ya kwanza kuanza kukata. DSTV wenyewe wanajua nini kinatokea mvua ikinyesha.
 
Hivi ni channel ipi huwa inaonyesha wwe sana, maana mimi huwa naangalia s8, s9 ,s10 , kuna nyingine zaidi ya hizo. Hapa nasubiria wrestlemania s8
Huwa siangalii hio WWE hivyo hata sijui inaoneshwa,channel ipi
 
IMG_5988.JPG
Mm ndo Nipo naicheki Live hapa ipo poa sana
 
Seriously digital technology imeshindwa kupambana na mvua?
Mbona kwenye process japo changamoto ya Mvua ni Kubwa sana kwa dish zote zilizo above KU Band, Yale madishi makubwa hayana shida mana frequency range yake band ni Kubwa hio Hali ya hewa kama mvua haiathiri sana strength of signal
 
Mkuu hapo tatizo sio mitambo ya DSTV bali satellite dish yako.

Wakati kwako inasumbua sehemu nyingine ipo safi kwa maana wao mitambo yao ipo vizuri.

Suluhisho la tatizo hilo ni cable ingawa ni technology ya zamani.
Jamaa yuko sahihi Mkuu sio tatizo la dish bali ni Changamoto hii huwakumba wateja karibu wote wa dish ndogo izi Za KU band panapokuwa na mvua
 
Wavivu tuu hao, hiyo ni fursa kwa mafundi na watu wa IT kutatua tatizo hilo na wachaji bei ya marekebisho mradi tuu isiwe inajirudia rudia.

Yaani akishakusetia dish na kulikaza hata I've kimbunga wee unakula burudani tuu.
Tatizo sio dishi kuyumba tatizo ni Frequency zinazotumwa na Transponder Juu huko kuja chini Ni ndogo sana yani zina short wave length Ila high frequency ivo kupelekea even matone ya maji Kuzipata izo waves na kuzipindisha au kuzitoa kwenye line of sight
 
The funny thing ni kuwa huu ungo sijaokota tu nikafunga. Nimenunua dstv wao wakaja kunifungia sasa ukisema tatizo ni ungo wangu unanishangaza.
Sasa dstv hawakujua juu ya hili tatizo wakatufungia huo ungo unaosema wewe? Kwanini hawafanyi hivyo?
Jamaa kakushauri technically sana ivo vidishi vidogo bado ni Changamoto sasa unafikiri dstv watakuambia kuwa wakati wa hali mbaya ya hewa uta loose signal???
 
Mara nyingi mvua ikinyesha DSTV matangazo yanakatika. Kwa mwezi huu wa nne na masika hizi si ajabu mvua ikanyesha wiki nzima au mara tano kwa wiki na hapo hutaona matangazo ya DSTV.

Je hapo si sawa na mtu unalipia huduma na huipati? Afadhali Tanesco umeme ukikatika LUKU haisomi kwahio huliwi pesa bure. Mfano leo kuanzia mchana huku nilipo mvus inanyesha mwendo ni on off kwenye DSTV.

Kuna njia yoyote DSTV mnaweza kufidia siku ambazo matangazo yanakatika kwasababu ya mvua?
Cc TCRAView attachment 738366

Solution hapo ni cable tu.

Swali ni je, cable services zipo bongo??
 
Ni hivi, satellite dish nyingi zinazotumia LNB za Ku-band zinakuwab na matatizo hasa kukiwa na hali ya hewa mbaya, mvua nyingi, mawingu mengi. Tofauti na LNB za C-band ambazo zipo stable sana na signal strength inakuwa vizuri tu wakati wa mvua.
Umeniacha
 
Back
Top Bottom