Tamko la pamoja la ITV, EATV, Channel 10, Clouds TV kuhusu kutoonekana kwenye ving'amuzi vya Azam, DSTV na Zuku

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,460
29,157
Tukiwa kama Taasisi rasmi na zinazotambulika zenye jukumu la kurusha kwa jamii maudhui kwa njia ya Televisheni, jukumu letu la kwanza limekuwa ni kuhakikisha tunafikisha habari kwa wananchi ambao ndio walaji wakuu wa maudhui tunayozalisha.

Kama vyombo vya habari, nia yetu ni kushuhudia mabadiliko chanya ya kiteknolojia yakiwa baraka kwetu na kuendelea kutupa wepesi wa kuwafikia walengwa wetu (watazamaji na wasikilizaji) katika maeneo tofauti ya nchi yetu.

Sisi kama warusha maudhui yasiyolipiwa kwa takribani wiki moja sasa kumekuwa na sintofahamu juu ya kuzuiwa kurushwa kwa maudhui katika ving’amuzi vya AZAM, DSTV na ZUKU jambo ambalo limeleta usumbufu na mkanganyiko miongoni mwa walaji wetu wa mwisho. Ni kweli kwamba sintofahamu hili haikuanza leo, suala hili lipo toka mwaka 2016 na katika kipindi chote hiki busara zaidi imekuwa ikitumika kuhakikisha kuwa tunapata suluhisho ambalo haliathiri upande wowote (mamlaka, taasisi na wananchi)

Tanzania ilianzisha mchakato wa kuhama kutoka kwenye mfumo wa urushaji matangazo wa Analojia kwenda Dijitali (analogue to digital) mwaka 2006. Baada ya Tanzania kuingia kwenye mfumo huo, utangazaji wa maudhui kupitia miundombinu ya ardhini (DTT) umewezesha kwa aina zote za maudhui yaani ile ya chaneli zenye kutazamwa bila malipo (FTA) na ile ya maudhui ya kulipia (Pay Television). Awali mfumo wa maudhui ya kulipia ulikuwa unapatikana kwenye utangazaji kwa njia ya satellite pekee.

Mchakato huo ulipelekea kuingia kwa watoa huduma mbalimbali nchini ambao walikuwa na majukumu ya kurusha matangazo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na hapa ndipo kampuni kadhaa zilipoanza kuuza ving’amuzi tofauti kwa wananchi bila maelekezo ya kuwa chaneli za FTA zitaonekana kwa baadhi tu ya ving’amuzi ambavyo vimeelezwa kuwa vilishinda zabuni.

Utaratibu wa soko ulichukua nafasi na kuwapa uhuru wananchi kuchagua king’amuzi akipendacho huku akifahamu wazi atakuwa na uwezo wa kuona chaneli zote za ndani pamoja na zile za nje anazotoa muuzaji wa king’amuzi bila kulazimika kuwa na king’amuzi zaidi ya kimoja. Hata hivyo baadhi ya kampuni zilizoshinda zabuni ya kujenga na kusambaza maudhui ya chaneli zisizolipiwa kama STAR TIMES yameendelea kuwa na ving’amuzi vya aina mbili yaani vile vya kulipia (subscription) na vile vya maudhui yasiyolipiwa ambapo chaneli zenye maudhui yasiyolipiwa hupatikana kote.

Uamuzi wa kuziondoa chaneli zenye maudhui yanayotazamwa bila kulipia (FTA) kwenye ving’amuzi vya DSTV, AZAM na ZUKU kunawanyima wananchi haki yao ya msingi na ya kikatiba ya kupata habari kwani mfumo wa DTT kwa mazingira ya sasa bado haujafanikiwa katika sehemu nyingi za nchi yetu hali inayosababisha huduma kuwa chini na ya kiwango duni jambo liliopelekea wananchi wengi kuchagua kujiunga na ving’amuzi vya DSTV, AZAM na ZUKU.

Ni wazi kuwa hatua hii ina madhara makubwa katika soko la utangazaji nchini kama tunavyoanisha hapa chini.

1.USHINDANI WA KIBIASHARA
Kama inavyoeleweka soko la Televisheni kwa nchi za Afrika ya Mashariki ni moja. Kuziondoa chaneli za Tanzania katika vingamuzi vya DSTV, AZAM na ZUKU wakati Televisheni/Chaneli za kutoka nchi nyingine ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki zinaendelea kuonekana hapa Tanzania kuna athari KUBWA SANA kibiashara na KIUCHUMI.

Hi ni kwa sababu mawakala walio wengi wa MATANGAZO YA BIASHARA, wanafanya kazi zao katika nchi zote ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kwa Televisheni za hapa kwetu kutoonekana katika vingamuzi tajwa hapo juu kutawafanya wasite kutupatia matangazo ya biashara kwani ni dhahiri kuwa Televisheni zetu zitakuwa NA WIGO MDOGO sana wa kuifikia hadhira ukilinganisha na
Televisheni nyingine za Afrika Mashariki ambazo kwa namna kubwa zinatoa maudhui yanayokaribiana na chaneli za Tanzania. Kwa kiasi kikubwa hili litayumbisha na kufanya chaneli zetu zishindwe kumudu gharama za uendeshaji jambo litakalopelekea athari kubwa sana za kiuchumi na kuathiri ajira za wafanyakazi na mapato ya kodi zinazolipwa kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Sintofahamu hii imesababisha kusimama kwa kampeni kubwa ya kitaifa ya “URITHI FESTIVAL” ambayo ilitakiwa kuanza mapema mwezi huu kutokana na kutopatikana kwa chaneli za kitanzania katika baadhi ya ving’amuzi vyenye watumiaji wengi kama AZAM, DSTV na ZUKU kwani zaidi ya robo tatu ya walengwa wa kampeni hii hawatofikiwa.

2.ATHARI KWA MAUDHUI YA KITANZANIA

Uamuzi huu utasababisha watanzania kutopata maudhui waliyoyazoea ya kitanzania kupitia vipindi vilivyotayarishwa hapa nyumbani hususan taarifa za habari, vipindi vya elimu, mambo ya kijamii, burudani, kazi zinazofanywa na viongozi kuhusiana na maendeleo na mustakabali ya nchi yet una badala yake watakuwa wanapokea maudhui ya kutoka nchi zingine ambazo zinaonekana kwenye ving’amuzi vyote

Hali kadhalika kama Taifa tutakuwa tumekubali kulisha vizazi vyetu tamaduni za wenzetu jambo ambalo linaweza likaathiri mila na tamaduni za Tanzania kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

3. JUHUDI ZA KUJENGA UCHUMI WA KATI

Moja ya jambo kuu la msingi la Serikali hii ya awamu ya Tano ni namna ambavyo Rais Dkt. John Pombe Magufuli amekuwa mstari wa mbele kuwezesha mazingira ya kujenga uchumi wa kati.

Sekta hii ya utangazaji, imetoa fursa ya kutengeneza kiwanda cha kipekee cha watengeneza maudhui (Production Houses). Hawa jukumu lao kuu ni kutengeneza vipindi tofauti ambapo sisi tunaorusha maudhui hayo, aidha tunanunua kutoka kwao au tunagawana mapato ya udhamini. Vipindi vya aina hii vinatakiwa kuwa vingi na viweze kuwafikia Watanzania wote na sio sehemu tu ya wananchi.

Moja ya msingi mkuu ya wanaopewa leseni ni kuhakikisha wanafika sehemu kubwa ya nchi. Kwenye vikao rasmi kati yetu na TCRA, wote kwa pamoja tulikubaliana kuna maeneno hayafikiwi na busara ilitumika kwa muda wote huu kuendelea kuwapa Watanzania haki yao ya kupata habari. Kupungua kwa watazamaji wetu kwa kiasi kikubwa kutaathiri mapato yetu na hivyo kiwanda kipya cha utengenezaji wa maudhui haitakuwa ajabu kikipotea.

Changamoto hii kubwa ndio ilitufanya sisi kutafuta namna ya kupanua wigo wetu ili kuwafikia wananchi katika maeneo ambao walikuwa hawapati taarifa.

4. WITO WETU

Tunafahamu kuwa uamuzi huu umetokana na Sheria ambayo ipo kihalali lakini kama tulivyoeleza hapo uwepo wa Chaneli zetu kwenye ving’amuzi hivyo bado ni muhimu kwa kuzingatia namna na ukubwa ambao ving’amuzi hivi vimesambaa ingawa pia tunafahamu chaneli zetu zitaendelea kuwepo kwenye ving’amuzi vilivyoainishwa kisheria.

Suala la ununuzi wa ving’amuzi vipya kwa wale waliokuwa wanatumia ving’amuzi vya AZAM, ZUKU na DSTV ili waweze kupata chaneli zetu za ndani linaweza kuchukua muda mrefu au kutofanyika kabisa kutokana na hali ya uchumi wa baadhi ya watazamaji wetu ambao wengi wana kipato cha chini na kati.

Kwa mara nyingine wananchi watalazimika kubeba mzigo wa gharama za kununua ving’amuzi ambavyo vitawapa mahitaji ya chaneli mbalimbali. Katika mazingira ya wananchi wa kawaida tunaowahudumia kununua king’amuzi zaidi ya kimoja ni mzigo, ambao bado tunahitaji busara na kuwaandaa kuingia katika hizo gharama.

Kimsingi tunaamini sheria hutungwa lakini ikibainika kuwepo kwa mapungufu, sheria hiyo huangaliwa upya na kufanyiwa marekebisho.

Tunaamini huu ni muda muafaka wa kufanya marekebisho ya vipengele vya sheria hii ambavyo haviendani na hali ya sasa lakini wakati michakato ya urekebishaji ikiendelea tunapaswa kuzingatia kwamba WATANZANIA wanaomiliki ving’amuzi vya ZUKU, DSTV na AZAM wanapaswa na wanayo haki ya kuendelea kuona chaneli zetu za kitanzania zenye maudhui yanayotazamwa bila kulipia (FTA) na tunaamini kuwa, kama ambavyo tumekuwa tukiongozwa na BUSARA katika kutafuta suluhisho juu ya jambo hili toka mwaka 2016 ndivyo hivyo busara itatumika tena kwa wakati huu .

TAMKO HILI LA PAMOJA LIMETOLEWA NA ITV, CLOUDS TV, CHANNEL 10 NA EAST AFRICA TELEVISION.
https://web.facebook.com/CloudsFmRa...1826.161194720590621/1967307509979324/?type=3
 
kile kipindi clouds imevamiwa ni chanel gani ilikiuka makubaliano ya kutomrusha bwana yule, leo wameungana tena
 
Taarifa ya pamoja kwa wananchi
IMG-20180810-WA0064.jpg
FB_IMG_1533929495148.jpg
FB_IMG_1533929499448.jpg
FB_IMG_1533929503179.jpg
FB_IMG_1533929507248.jpg
 

Attachments

  • FB_IMG_1533929507248.jpg
    FB_IMG_1533929507248.jpg
    28.3 KB · Views: 136
  • FB_IMG_1533929507248.jpg
    FB_IMG_1533929507248.jpg
    28.3 KB · Views: 137
Jamaa kingamuzi cha azam kinaonyesha Access deniedtoka jana tatizo nini?
 
Ukiipitia taarifa hii utagundua kuna mambo mengi ndani yake. Kwanza TCRA kwa malengo ya uundwaji wake ni Mamlaka ya Udhibiti kama zilivyo mamlaka zingine nyiingi zilizoundwa kwa malengo na muundo huo katika nchi yetu, kwa kimombo huitwa REGULATORY AUTHORITIES. Malengo ya wazi na yanayoonekana(mkolezo umesisitizwa) ya Mamlaka hizi iwe ni katika mambo ya Vyakula na Dawa, Bima, Usafirishaji, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, Nishati na kadhalika hua ni kuhakikisha sheria , kanuni na taratibu katika sekta husika zinafuatwa

Ni mtazamo na maoni yangu ya muda mreefu sana kwamba majukumu na madhumuni yaliyofichika ya Mamlaka hizi ni vyombo vya kimabavu vya dola kama ilivyo polisi ambapo vinawajibu wa kudhibiti mwenendo wa sekta husika ziendane na kufuata siasa za nchi za wakati husika

Kwenye taarifa yao ya pamoja hapo juu vyombo vya habari vilivyolalamika vimeorodhesha athari hasi za kiuchumi na kijamii kwa nchi zitakazoletwa na katazo hili la TCRA kwa jina la kufuata sheria kana kwamba TCRA hawajui kitu hicho! Taarifa inatukumbusha kua ajira za wafanyakazi zitaathirika lakini hata itaathiri hata mapato ya Serikali INAYOONGOZWA NA DR JOHN POMBE MAGUFULI.

Kwa maoni yangu taarifa kutukumbusha kwamba serikali hii inaongozwa na nani ni lugha ya kimkakati kwa kua wameelewa muelekeo wa serikali ya awamu ya tano vinginevyo hapakua na haja ya kutaja jina la Mheshimiwa Rais maana dunia nzima inaelewa serikali hii ianongozwa na nani.Ninavyoona tunarudi kwa kasi kuelekea mfumo wa chama kimoja hata kama sio kisheria au kimuundo bali kiuhalisia

Japo sera za nchi hazisemi hivyo lakini matamko na matendo ya Mamlaka mbalimbali za nchi yanatuelekeza kwenye siasa ya Ujamaa(katiba yetu bado inatambua hivyo) ambapo Uchumi unatumikia Siasa na si kinyume chake. Jambo lolote kwanza linapimwa kwa maslahi ya kisiasa ya walio madarakani wakati huo bila kuangalia athari za kiuchumi na kijamii, maana kama ilivyosema taarifa ya watoa huduma kama ni sheria basi ingeweza kurekebishwa bila kuathiri maslahi ya upatikanaji wa habari kwa mamilioni ya Watanzania

Ni kweli sheria hii ipo kihalali lakini kwa maoni yangu kama ilivyo sasa hivi ni sheria mbaya(bad law), na kama kweli haijawekwa hivyo ili kutimiza lengo na jukumu lililojificha la TCRA kudhibiti vyombo vya habari ili viogope na vifuate muelekeo unaotakiwa na wanasiasa basi na tuifute
 
Back
Top Bottom