Mkuu wa Mkoa wa Dar Paul Makonda na Mjasiriamali Carol Ndosi, wana bifu la kimya kimya?

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,055
Jibu la RC wa Dar, Paul Makonda kwa Mjasiriamali na Mdau wa Maendeleo, Carol Ndosi leo kupitia ukurusa wa Twitter baada ya kumuandikia barua linasema mengi.

Inavyoonekana, kuna mgongano wa kimaslahi kati ya Mjasiriamali huyo na Gavana wa Jiji la Biashara asiyekaukiwa headlines, Paul Makonda.

Nini tatizo? Kwa takribani miaka miwili sasa, Carol hafanyi tamasha lake la Nyamachoma kama ilivyozoelekea jijini humo. Na, amewahi kunukuliwa akilalamika kwamba mamlaka zinambania kwa sababu ambazo wengine wenye matamasha wanaruhusiwa kufanya. Double standards?

Sasa, baada ya kimya ama pengine jitihada za kimya kimya, naona Carol ameamua kumuandikia barua ya wazi kwa RC Makonda na kuiweka mitandaoni;

Carol Ndosi alimuandikia barua Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda.

Barua ya Wazi kwako Mheshimiwa Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Salaam Kaka.

Ni matumaini kuwa ni mzima wa afya na unaendelea kulitumikia taifa. Naomba niwasilishe barua hii, nikitambua wazi kuwa inawezekana kabisa usijibu, au jibu likatufedhehesha zaidi nafsi zetu. Nimefunga na kusali leo kuomba hata kama ni kulisemea hili, basi iwe kwenye maneno ambayo hayatopokelewa kama shambulizi na wala lisije kuendeleza mlolongo wa visasi kama wengi wamekua wakiniaminisha. After all, mimi ni mkazi wa mkoa wako, if anything that should count for something. Allow me to tell like it is, as I believe I always do.

Naamini ni haki yangu kama Mtanzania kusema pale ninapoona sijatendewa haki, na si mimi tu, naandika kwa niaba ya wafanyakazi 33 wa Nyama Choma Festival na watoa huduma, wafanyabiashara na washiriki wote zaidi ya 200 waliokua wanategemea kwa kiasi kikubwa tamasha hili lililokua linafanyika mara 3 kwa mwaka mkoani kwako.

Ni siku nyingi tangu ofisi yako imesikia kutoka kwetu, yaani Waandaji wa Tamasha la Nyama Choma Festival, tangu tulivyokuja mwanzoni mwa mwaka huu (March 2018) na kusisitiziwa na ofisi yako tukufu kuwa bado uamuzi ni ule ule kuhusu matumizi ya Leaders Grounds.

Rejea tamko lako la tarehe 24.11.2017 ambapo ulitangaza kupiga marufuku matukio yanayoenda zaidi ya saa 12 jioni kufanyika viwanja vya Leaders Club. Ulisisitiza kuwa ulitoa ruhusa maalum kwa watayarishaji wa Tamasha la Fiesta kwa sababu maalum lakini ulisema na nanukuu ‘ni haki ya watu kwenye makazi hayo kulala’. Ulitoa rai kuwa ni kutokana na makazi ya watu na ubalozi kwenye eneo.


Tamko hili lilitolewa wiki moja kabla ya tarehe iliyopangwa na kutangazwa kufanyika tamasha letu la nyama choma festival. Tulipatwa na mshtuko mkubwa sana ukizingatia kuna fedha nyingi sana ambazo tayari tulikua tumeshaingia gharama kwenye maandalizi na zisingeweza kurejeshwa.

Rejea barua yetu tuliyokuandikia Desemba 2017 kuomba kama inawezekana na sisi kupewa kibali maalum, kwa masharti kama waliyopewa wenzetu wa Fiesta ya mwisho saa 6 Usiku (ingawa waliruhusiwa kupiga mziki hadi asubuhi). Nikukumbushe tu pia, tamasha letu halina tofauti sana na hilo la wenzetu waliloruhusiwa kwani letu pia huambatanisha burudani ya muziki ingawa main concept ni Nyama Choma za kila aina na biashara mbali mbali.



1*ljwPYI_mxxpgd7L43XND4g.jpeg

Tulifuatilia jibu wiki nzima ofisini kwako huku tukiwataarifu wateja wetu kuwa inabidi tuahirishe tamasha hadi pale ambapo tungepata mbadala. Majibu tuliyopewa sihitaji kukumbusha kwani naamini utakua unayakumbuka fika.

Nilipoona jitihada hizi hazijibiwi, ilibidi niombe msaada kwa kila ninayemfahamu aliye karibu na wewe atoe appeal on my behalf. Hili pia liligonga mwamba. Kwanza mmoja alinijibu kuwa hata hunifahamu. Naomba nikukumbushe mimi ni yule yule Carol tuliyokua tuna mawasiliano ya salaam, na pia ni yule yule niliyokuhoji kwenye kipindi cha siasa za siasa one on one wakati ukiwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni kwa lisaa lizima. Pia ni yule yule anayehusika na kutayarisha hili tamasha ambalo ulihudhuria 5 Desemba 2017 kama picha inavyoonyesha hapa



1*9saOmkKDKENy0Rw6FbdJsQ.jpeg

Hili tamasha la 5 Desemba lililofanyika Leaders lilikua la huzuni pia kwani wakati wa tamasha tulimpoteza mshiriki wetu, mhudhuriaji na supporter mkubwa sana wa tamasha letu, alikua kama mama yetu pia. Rest in Peace Mama Mzungu. Wakati tunashirkiana na kikosi cha polisi kutoa mwili na kuupeleka Muhimbili ulikuwepo na ulikua unasisitizia kama kuna lolote nahitaji kama msaada nikwambie. Sijui kama haya matukio ni kumbukizi tosha, mimi ni yule yule.
Nilijibiwa vitu tofauti,kuna wengine walisema kabisa ‘Carol, hapa pagumu sana’.Wengi walikuwa wananiuliza ‘kwani umemkosea nini’. Kitu ambacho hakikua kwenye kumbukumbu yangu kabisa kwani hata tuhuma zozote zilizokua zinasemwa juu yako hata kipindi kile cha ‘identity crisis’ sikuwahi kutia neno. Nilijihoji sana na kuwauliza wote niliokua nao karibu kama wana kumbukumbu yoyote. Mmoja alinijibu hivi…


1*0UgL2cVEGAY1JuE0rWH40A.jpeg



1*oR_ww-fmuE1o1_0QJmVFqQ.jpeg

Mwisho, nilipigwa simu saa 2 usiku, bahati mbaya nilikua nimeshalala kutokana na kusumbuliwa sana na Pressure wiki hiyo lakini asubuhi nilikutana na Ujumbe huu .



1*B-A6kR01nAE04ObZXStong.jpeg

Nilipo mpigia simu Kaka yangu Lemutuz, kwanza alinitaarifu na ‘kunikanya’ kama Kaka. Alisema kuwa Umeniruhusu kwenda kufanya Tanganyika Packers na nifanye taratibu za kibali. Huwezi kuniruhusu kufanya Leaders kwani umeshatoa tamko na kama kiongozi ukitengua utaonekana hauna msimamo. Nilimshukuru kwa taarifa na kumwambia nitaanza taratibu za kupata uwanja wa Tanganyika Packers.

Hata hivyo kama wengine, nilimuuliza kama anafahamu kama nimewahi kukukosea, kwani hata nilivyoenda ofisini kwako sikuruhusiwa kukuona, jambo lililo si la kawaida ukizingatia utayari wa kiongozi wetu wa mkoa kuonana na wananchi wake kila siku.

Nilihoji ili kama ni kosa, niombe msamaha kwani mimi ni binadamu na si timilifu. Kaka Lemutuz alisema yeye hafahamu na akasema pia ‘kwanza amesema hata hakufahamu na wewe umekua caught kwenye cross fire tu’, nikamkumbusha hilo tamasha la 5 Desemba 2017 kwani walikua wote, na nilivyoenda kuwasabahi na kuwakaribisha kwenye tamasha walikua wamesimama wote. Akasema ‘anyway, inabidi uangalie sana unachoongea, you look like you are anti-government, mimi nakufollow twitter naona unavyoongea, am just telling you to be wise’.

Nilimshukuru kwa ushauri na kumwambia nitamtaarifu taratibu zinaendaje kupapata Tanganyika Packers. Hili pia lilikua na changamoto, na hadi tarehe 8 Desemba asubuhi, siku moja kabla ya tamasha kufanyika Tanganyika Packers tulikua hatujapewa kibali. Hatimaye kilitolewa na tukaendelea na tamasha. Halikua zuri kabisa. Rejea ‘Barua kwako Mjasiriamali unayeanza’ ambayo nilielezea changamoto tulizokutana nazo.

Barua kwako Mjasiriamali Unayeanza.

Salaam kwako, ni matumaini yangu kuwa Mwaka 2017 unaumaliza kwa kushukuru Mungu kwanza kwa uhai na afya uliyo nayo wewe, na uwapendao. Ni wengi walitarajia kufika, lakini mipango ya Mungu haina makosa.

Nitaongea kama ninavyoongeaga na vijana wengi tukikutana kubadilishana mawazo..Nitaongea kama Sister Carol.

2017 umekua ni mwaka ambao personally nimesikia vilio vingi sana katika fani yangu ya ujasiriamali. Ingawa wengine wameweza kutafuta upenyo wa kubadilisha ‘challenge into opportunity’, wengi wameishia kufunga biashara, kubadilisha biashara, kurudi kuajiriwa kwa wale waliokua wamejiajiri na wengine kukata tamaa kabisa ya maisha.

Mzunguko wa fedha haupo kama ulivyo kua miaka 2 iliyopita, na kwa wasomi ni kitu kinachoeleweka kabisa lazima nchi ipitie mtikisiko kukiwa na major reforms kwenye sekta za biashara na uchumi. Nilisoma mwezi wa 9 au 10 kuwa zaidi ya biashara 7000 zimefungwa ndani ya mwaka mmoja. Nilijiuliza sana ‘what became of all those who depended on these businesses all the way down to the value chain?’.

Nilijifunza siku nyingi kuwa ukitaka biashara iwe sustainable, uongeze value kwa kushirikisha watu wengi zaidi kwenye chain. Kwa mfano, kwenye biashara ya matamasha ambayo wengi ndio mnanifahamu kupitia Nyama Choma Festival, tunajivunia kuwa sio tu ni biashara lakini tumeweza kuunganisha supply chain kutoka kwa mfugaji, mkulima, wauza nyanya na tangawizi sokoni, wafanya usafi, watu wa maturubai, viti, meza, vyombo vya usalama, vya afya..the list goes on.

Ndio maana jukumu la kuendesha hili tamasha ni kubwa mno na tunaamini kwa miaka 6 hatujaweza wenyewe bali kwa kudra za mwenyezi Mungu na neema zake pamoja na support kutoka kwa wananchi na wadau wetu.

Nakuandikia wewe mjasiriamali leo, ambae ulianza kama mimi, kwa juhudi na bidiii na mtaji wako MWENYEWE, no offence kwa wale ambao wamekua spoon fed, tena kuna ambao nawafahamu ‘wameboostiwa’ lakini mafanikio yao ni kutokana na juhudi walizoweka baada ya ‘kuboostiwa’. But I honestly have issues with arrogant condescending pompous people who did not knock down their own doors.

Nataka nikusisitizie kuwa haijalishi mara ngapi utaanguka, au nani alianza safari na wewe akakuacha au umepoteza mali ngapi, cha msingi ni nafsi yako inakwambia nini kuhusu dhamira yako. Dhamira yangu ni kufanya kazi kwa bidii, kuleta maendeleo kwa wanaonitegemea na wanaonizunguka. Huwa najitahidi kama nina furaha, basi wanaonizunguka wawe hivyo pia. This pushes me everyday, together with what I believe is my purpose, which is to aspire to inspire.

Sasa nikueleze tu tuliyopitia sisi kama Nyama Choma Festival mwaka huu, ujaribu kuona kama unaweza kupata inspiration au motivation kutokana na hili. Kujenga brand si jambo dogo, tumejitahidi, 7 years in 2018 ; we are beyond grateful for the run that we have had. We have seen the best and the worst. Kama nilivyosema, miaka 2 kidogo kama nchi (false modesty) tumetikisika kwenye mzunguko wa fedha, hata wadhamini nao mtikisiko umewaathiri. Haya makampuni ya bia na telecomms ambao ni big spenders kwenye sponsorship wamecut down sana marketing budgets zao.

So kwa mfano, TNCF ilikua inaendeshwa kwa 65% ya sponsorship fee na 35% ya makusanyo toka kwenye kiingilio getini. 2016/17 imekua ikiendeshwa na operating capital ya kampuni, na mwenye tamasha pamoja na 25% sponsorship fee na chochote kinachopatikana getini.

Kwa wachumi mtakua mmeelewa kabisa ilihitaji turnout kubwa kuwa na turnover kubwa. Haisadii pia kama brand umeijenga kwa standard fulani kwahiyo scaling back itaathiri quality of the event. 2016 kwanza tukasema kwasababu hali sio nzuri, tunapunguza Dar editions from 4 to 3 maana purchasing power ya watu pia imeshuka..ma-buckets na ma-ndafu hayanunuliwi kama yalivyokua yananunuliwa 2015.

Anyways, tulipitia changamoto nyingine ya crack down ya mamlaka ya kodi, si kwetu bali kwa washiriki wetu. Wengi wa washiriki wetu ni wajasiriamali wadogo au ndio wanajaribu, chochote wanachokipata pale ndio kinampa nguvu ya kwenda kufanya kikubwa zaidi. Utekelezaji wa makusanyo ikabidi wajasiriamali na wafanyabiashara wote nyama choma kuwa na mashine za EFD, failure of which walichukuliwa hatua kwa kupigwa fine. Hii iliwanyong’onyeza wajasiriamali wengi na tukapoteza wachoma nyama na washiriki wetu mashuhuri katika kushiriki tena kwa kuogopa fine maana ilikua sio kukosa mashine tu, hata kama unayo, umejisahau kutoa wakakukuta hata kwa mteja mmoja ilikua ni fine not less than 2.5 Mil TZS. Iliwaathiri pia sponsors ambao walikua wakishiriki wanauza na bidhaa zao pia so guaranteed return on investment.

So 2017 tukabadilisha ratiba na kufanya tamasha la kwanza Dar es Salaam 29th April..siku mvua KUBWA sana iliponyesha in years. Ile mvua ilikua historical, na Leaders Grounds bahati mbaya tulikua hatujashuhudia mvua ikinyesha kama maji yakijaa panakuwaje. It was horrible. Palifurika! First event of the year in Dar,( shimo lenu la hela) and this happens.

On top of that media partner wa kipindi hicho alituangusha ilikua tufanye media campaign kabambe lakini hadi Jumatano kabla ya event bado tulikua tunatafutana na MOU…labda promo zaidi ingesaidia.We were devastated. Not just because sisi kama sisi tulipata hasara ya 68 Mil+ ( mind you hamna sponsorship funds tunabeba budget wenyewe hapo na mdhamini mmoja mkubwa), but sababu hamna kitu huwa kinatuumiza kama mabanda ya nyama choma yakibaki na chakula. Kwetu sisi hapo ndio tunaona tumeshindwa kudeliver, even if the rain was out of our hands contrary to what people used to say about us eti tunastopisha mvua..smh.

Anyways, dusted ourselves off, head held high and marched on….so fast forward the next event in Dar..again ndio shimo letu hili. Tumepiga loss in April, we have 3 events to do before the Dar one..tulifanya..ila kwa mbinde. Ikaja ya Dar ya August, it wasn’t bad but it wasn’t good either, ndio sheria ya matamasha ilikua imeanza kutekelezwa, ikabidi tuzime mziki saa 7…tofauti na saa 8 au 9 tuliyokua tunaendaga.

Tukapiga moyo konde na kusema let's keep pushing, na tuwaze namna gani tunaweza endelea kwenye fani aidha kwa kuscale back au kucome up na njia nyingine ya kuwafikia wateja wetu. Tabata BBQ Fever was born, tukasema sasa tunafanya nyama choma kwenye vitongoji. Tukafanya matayarisho yetu ya Tabata, ingawa tulitapeliwa uwanja at first (si kwa hela), watu tuliokua tunaongea nao kumbe sio wamiliki na baada ya mmiliki kujua kidogo ikawa problem..lol..anyway tuliisort tukafanya set up Friday, Saturday event.

Come Saturday, event is ongoing..tukafuatwa tuzime mziki na kusambaratisha wanachi saa 4 usiku. Kibali chetu kilisema Saa 6 usiku ndio mwisho. Hapo tukawa tumeingia loss ingine, because kwa wale kwenye event business 2 hours is a lot and can give you 10 Mil Tzs easily. So hadi hapo ikawa ni loss after loss.

Bado tukaendelea kupiga moyo konde, tukapambana na za mkoani, Mwanza, Arusha, Dodoma huku tunaendelea kurecover loss na tuko na sponsor wetu yule yule mmoja maskini hajawahi kututupa #TeamGreen. Tukawa tunajipa matumaini Dar 2nd of December walau tutapumua. Uwanja wa Leaders ukapigwa marufuku one week before our event, with non refundable expenses amounting to 23 Mil TZS. Tulitoa tamko na kuwafahamisha wateja wetu, tukaomba sana ushirikiano kutoka kwa washiriki na wahudhuriaji maana kama nilivyosema, nyama choma sio ya waandaji tu, kuna wengi mno wanaotegemea jukwaa hili na ndio maana ilibidi tuappeal to the masses to save this.

Tanganyika packers was the only option lakini kama ilivyo desturi ya Watanzania, huwapeleki tu venue mpya, we saw this tulivyohamishwa toka UDSM to Leaders the first time. Tukajitahidi kufanya matayarisho lakini siku ya siku, masupppliers kutoka wenye mabati, mobile toilets, tents walituangusha MNO.

Washiriki wetu walijaribu kupambana na MVUA kubwa tu na hata baada ya kunyeshewa mkaa na nyama waliamka tena mvua ilivyokata na kuendelea. Kuna wateja walikuja mvua inanyesha wanatembea kwenye mvua kuja kutusupport. Kuna wajasiriamali wadogo walifanya wawezalo kutokana na mazingira ili biashara iendelee.

9 Dec jambo la msingi nililo kuwa najiambia ni ‘ I just want this night to end’. Everything was just going WRONG. Mziki ukazimwa na DJ aliyekua anatake over sababu aliingia kwenye mfarakano na walinzi katika kujitambulisha wakakosana lugha. IT WAS A HORRIBLE DAY. So another loss incurred, brand suffered. Kesho yake bado uamke uwaze ‘what is the next step?’.

Nimetumia wiki moja kukaa na kupanga tena mawazo na ARI maana yataka ARI kuendelea. Bado naendelea kujipanga na team, lakini ninalofahamu ni QUITTING is NOT an option. Leo nimeamka, mdhamini wetu #TeamGreen amepledge tena for 2018, lakini yabidi kukaa chini na re-strategize. At least thats good news and we are hopeful. I want to insist on these things, choose your partners wisely..kuna ambao tuliwategemea lakini wametuangusha vibaya mno. Some support systems are just there for material things and when you have something, We are not friend-less for no reason. You might have better luck than some of us. If you are a woman, Some support systems because of their sexism and male chauvinistic behaviours will turn on you when you don’t agree with their shenanigans or do not accept defeat..they will even go to the length of tarnishing your brand and when they fail claim you did not ‘appreciate’ them hence the retaliation. The other is resilience to keep going..kama hujazungukwa na ambao wanakwambia ‘unaweza’ inabidi ujiambie mwenyewe.

Some will just want to watch you drown because you were a good swimmer, so ‘kama alikua anajua kuogelea mbona leo anazama’ kind of mentality.

This happened to us 6 years down the line, and we were broken. You will fall, you will rise but you cannot STOP. Kama wewe unasoma hii sasa hivi na ulikua ndio kwanza unaanza au umekutana na misuko suko please, first know your purpose. My purpose is to use what I have to uplift others, and because of that I keep going…no matter what you throw at me, I will stand up and keep walking. GOD gave me a bullet proof vest that only HE can penetrate. Find your purpose and let it drive you! let it be the reason for you to keep going everyday no matter what.

Sympathy? why not for those filled with compassion and empathy will reciprocate. Only the evil spirited will mock. Tunaonewa? Hell YES! Walk in our shoes and tell us that is not true. It doesn’t stop us though! We keep pushing! Against all odds! Nilienda kuappeal decision ya leaders nikawa rejected na kuishia kuzimia mbele za watu..did I stop? No! Niliomba nionewe huruma? NDIO! Sababu this is bigger than me…way bigger.

I take my failures in what I do seriously because if I fail..Aunt Asia na Muhsin wa mabati amefeli, if I fail, Imani wa tents amefeli, If I fail, Abraham wa sound system amefeli, if I fail, G4S, JKT SUMA, POLICE wamefeli, if I fail, Aggreko amefeli, if I fail, Mabanda ya Nyama Zaidi ya 10 na wafanyakazi sio chini ya 7 wanaotegemea kipato hicho wamefeli, if I fail wote waliowauzia chochote hawa mabanda na hawakumaliziwa hela zao wamefeli, if I fail, watoa huduma wote wamefeli, if I fail, mamlaka ya kodi imefeli, if I fail my team imefeli, if I fail my family, my two beautiful daughters wamefeli, if I fail, my country has failed. I CANNOT AFFORD TO FAIL, and when I do, I CANNOT NOT TRY AGAIN. That is my purpose. All the best with yours!


Mhe. Paul Makonda, naandika hii barua kwa kuwa nimetaarifiwa kuwa sasa viwanja vya leaders vinatumika tena, na utenguzi wa tamko umefanya wewe mwenyewe. Ni mwaka mzima sisi kama waandaji tumesitisha shughuli zetu za tamasha kwani ingawa tunafanya mikoa mingine, Dar es Salaam ndio ilikuwa inatuwezesha na kutupa mtaji wa kwenda huko kwingine.

Nilivyosikia tangazo la kwanza la wenzetu,wakitangaza kuwa tamasha lao linafanyika pale pale Leaders nilipata mchanganyiko wa hisia. Kwanza nilifurahi maana nilisema hatimaye, na kama wenzetu wameruhusiwa basi na sisi tutaruhusiwa. Lakini mara baada ya hapo nikapatwa na fedheha, nilipowakumbuka vijana wangu wote na watoa huduma waliokua wanatutegemea, kuwa wamekosa kipato kwa mwaka mzima.

Ni haki yangu kuuliza na kupewa sababu ambazo zimepeleka utenguzi huu na kama kuna mabadiliko yoyote ya sababu ulizotupa uliposema Leaders Grounds Hapafai. Ni ngumu kutokuamini utenguzi umefanyika coincidentally wakati wenzetu wamepanga tamasha lao. Ubinadamu unanifanya nihoji Je sisi la kwetu halina thamani au mchango wowote? Wao hawapigi mziki? makazi ya watu yamehamishwa Leaders sasa? Nawaelewesha vipi wenzangu kuwa haikua personal vendetta, au mimi ndio nilishindwa ‘kuget through’. Kama ni kunyanyua vipaji hata sisi tunanyanyua, kama ni kodi hata sisi tunalipa, na sio sisi tu, wote wanaoshiriki kwenye mnyororo wa thamani wa tamasha hili. Kama ni ajira na fursa, hata sisi tunatoa kupitia tamasha hili. Kwanini ilibidi tuteseke mwaka mzima kama mazingira hayajabadilika?

Nimeambiwa hata mimi nikitaka kufanya sasa naruhusiwa..bahati mbaya tumechelewa sana kwani wadhamini wengi wameshafunga vitabu vyao na bila ya wao hatutaweza kufanikisha.

Nimesali sana kuwa tuweze kuendelea mwaka 2019 na hii ruhusa bado iwepo na tuweze kufanya tamasha kwa amani na kurudisha chanzo kingine cha ajira na vipato kwa mamia ya watu.

Yangu yalikua haya machache, na kama nilivyojihami, sitarajii jibu. Langu lilikua kukueleza tu jinsi ambavyo tuliathirika na tamko lako, na hisia zetu baada ya utenguzi mwaka huu. Pia kukusihi tu kuwa ingawa tunaweza kupishana mitazamo na mawazo, tunajitahidi sana kupitia nyanja mbali mbali kusukuma gurudumu la maendeleo nchini kwetu. Mimi kama Mtanzania najivunia sana nchi yangu and I remain loyal to my purpose which is to contribute to this country’s development. Mimi sio ADUI. Ni mwananchi mwenzako, ni Mama, ni mtoto, ni dada and most importantly, ni BINADAMU.

Naomba Bwana Yesu, Malaika wake na Roho Mtakatifu wakaseme na wewe, wakuonyeshe uchungu tuliopitia. Mwisho nikutakie uongozi mwema wa Mkoa wetu wa Dar, na ushiriki mwema kwenye tamasha linalokuja, natumai na sisi tukikukaribisha mwakani Insh’allah, utajumuika na sisi na kutuunga mkono kama wenzetu.

Namalizia na bandiko kutoka kwa Operations Manager wa Nyama Choma Festival- labda maneno yake pia yataleta mwanga zaidi kwenye hili.






Jibu la Makonda;

Nasikia kuna barua. Barua andika kwa Ofisi ya Mkuu wa mkoa. Humu mitandaoni ofisi haina anwani.
1542952415894.png



Swali la Msingi: Kama malalamiko ya Carol ni valid; kuna sababu zipi za msingi zinazomfanya RC Makonda 'kumbania' Mjasiriamali huyu?!
 
Me sijui. Ndio maana nikasema kama malalamiko yake ni valid.. Why ambanie? Nini kinaleta mzozo kati yao?
Halafu ningeshauri usome hoja za Carol kwanza.. Naona kama umekuja kujibu mbio mbio sijui umesoma saa ngapi..

Nami nakushauri kiungwana: uwe unasoma na kuelewa ulichokisoma.

Mimi sijajibu. Sijatoa kauli.

Nimeuliza swali na alama ya kuuliza nikaiweka mwishoni mwa swali langu.
 
Jibu la RC wa Dar, Paul Makonda kwa Mjasiriamali na Mdau wa Maendeleo, Carol Ndosi leo kupitia ukurusa wa Twitter baada ya kumuandikia barua linasema mengi.

Inavyoonekana, kuna mgongano wa kimaslahi kati ya Mjasiriamali huyo na Gavana wa Jiji la Biashara asiyekaukiwa headlines, Paul Makonda.

Nini tatizo? Kwa takribani miaka miwili sasa, Carol hafanyi tamasha lake la Nyamachoma kama ilivyozoelekea jijini humo. Na, amewahi kunukuliwa akilalamika kwamba mamlaka zinambania kwa sababu ambazo wengine wenye matamasha wanaruhusiwa kufanya. Double standards?

Sasa, baada ya kimya ama pengine jitihada za kimya kimya, naona Carol ameamua kumuandikia barua ya wazi kwa RC Makonda na kuiweka mitandaoni;




Jibu la Makonda;



Swali la Msingi: Kama malalamiko ya Carol ni valid; kuna sababu zipi za msingi zinazomfanya RC Makonda 'kumbania' Mjasiriamali huyu?!

Carol Ndosi amefanya quotes za kufa mtu
 
Nami nakushauri kiungwana: uwe unasoma na kuelewa ulichokisoma.

Mimi sijajibu. Sijatoa kauli.

Nimeuliza swali na alama ya kuuliza nikaiweka mwishoni mwa swali langu.

It never gets old with you, does it? Ligi, ujuaji, kuhamisha mijadala etc..

Hukuuliza kwa kutaka kujua.. Uliuliza ili tuanze kubishana. Ndivyo ulivyo!
 
Swali la Msingi: Kama malalamiko ya Carol ni valid; kuna sababu zipi za msingi zinazomfanya RC Makonda 'kumbania' Mjasiriamali huyu?!
Nawe huna uhakika kama ni valid
Huyo Ndosi kwani haijui ofisi ya RC ilipo au anatafuta umaarufu tu
 
Back
Top Bottom