Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

...japo inawezekana sana, Leah alitumia nguvu bila maridhiano kwa kutaka kusoma kwanza ndipo abebe ujauzito, and that didn't go down very well with he hubby. Haya mambo yanahitaji maridhiano na makubaliano ya kweli, uwazi na kuwa na busara. Kwa sisi tulio ndani ya ndoa, mkishaoana tu, mara nyingi na wengi wetu tunahitaji kuanza kuwa na familia(watoto), hivyo kama Leah alifanya yote bila maridhiano na maelewano, part of the fault should be hers.

Hata hivyo, mbona wengi wanabeba ujauzito na bado wanachukua masters degree, PhD etc? Najua degree ya kwanza ndio kidogo ina shida, lakini hizi zingine mtu unaweza kusoma na kubeba mimba/kulea. Alikubali kuolewa, akubali kuwa mama, hamna namna.
Unahakika kwamba nililazimisha kutuzaa? Maelezo yangu tank Irish Elena, acheni kutetea uovu, kama unauhakika na hili emu nithibitishie..maana unoangea as if wakati tunakubaliana na wewe ulikuwepo..isitoshe kama huna cha kuchangia ni vyema ukanyamaza. By the way naijua thamani ya ndoa wala nisingependa ifikie hapa ilipofika Ila sina jinsi im ready to let it go.
 
Ungekuwa mtihani 85 per cent wangefeli wanacomment nje ya maelezo yaliyotolewa huyu dada hajasema kusoma masters kulikuwa tatizo kwenye ndoa take, kuzaaa baada ya kumaliza walikubalianan, mumeo Hakuwa na shida ya mtoto ndo maana alitaka shemeji akatoe kabla ya kujulikanaa tendeni haki kabla hamjatoa ushauri vyaaa viatu vyake kwanza ndo uccoment
Asante kwa kunielewa, watu humu.
 
Upo tayali kuiacha ndoa ivunjike na umeshaamua hilo,sasa sijui unaomba ushauli wa nini?.
 
Ngongo umesema kweli kabisa lakin naomba nikuulize maswali haya

a) kipi kitamuua zaid huyu dada kuitwa mtaliki kwa mwanaume alozaa na mdogo wake ama kuitwa mama alolea mtoto wa mdogo wake kwa mume wake?

b)je akitaliki ndipo atakapo pata amani zaid kuliko kulitatua kosa akiwemo ndani bila kutaliki?

c) Hivi kosa ni kuzini na mdogo je akizini na watu usowajua huna uhakika na maisha yao na penyewe kosa hili ni dogo?

d) Hivi kama angepata wazo la kutuliza akili akakaa na mdogo wake akajifungua kisha akamwambia mumewe nakubali kubeba aibu yako ili kuokoa ndoa hii, mpe mdogo wangu mtaji akaanze maisha na mimi nitamlea mtoto huyu kama mwanangu. angepungukiwa nini? je anadhan mwisho wa siku asingepata credit na amani kwa kufanya hivyo?

tusikuze jambo kwa kuweka hisia manake huku hakutatusaidia kujenga jamii yenye heshima, na uadilifu. tunaweza kumsaidia huyu dada kwa kumuonyesha kuwa bado anaweza kusimama kwa ujasiri akatatua matatizo na mwisho wa siku akawa mshindi. sikubaliani na tabia ya sisi watu kumuonyesha kwamba hiyo ndoa ndo imeshakuwa jipu, na kwamba hana la kupata hapo, akatafute amanim kwingine. jiulize iyo amani ataipata kwa mtu yupi ambaye hata mcheat?
Duuh! I see!!? Yaani moyo huo sijajaliwa kbsa angekuwa yeye ni Mungu wangu ningefanya lkn kwakuwa ni mwanadamu kama mim isee hiyo haiwezi tokea, yaani nijishushe mpaka anikanyage! Kumbuka na mim Nina thamani tena kubwa siwezi kabsa kufanya hayo unayoeleza best.
 
kaika hili mwanaume mwenzetu amechemsha.inahitaji ushauri wa makini mno,nadhani unapitia kipindi kigumu sana.
 
Pole sana dada, binafisi nakuomba umsamehe mdogo wako Kwa sababu umesema uliwasikia wakibishana na mumeo akimtaka waitoe hiyo mimba ni dhahiri huyu bwana ampendi mdogo wako ama anatamaa tu na tamaa zake zimevuka kiwango na hana utu kwako na kwa mdogo wako, kitendo cha mdogo wako kuamua kusema ukweli mbele yako ni dhahiri aliona ni kiasi gani alikukosea maana alikuwa na nafasi ya kuitoa hiyo mimba ama kumsingizia mwanaume mwingine kama wadada wengi wanavyofanya.

Kwa sbabu ujazaa na huyu bwana unaweza kutumia muda huo uliopewa kutafakari yafuatayo.

(1) je utapata mwanaume ambaye hataweza kukumbusha maumivu ya aina hii? Kwa maana ya kukufanyia kitu kitachokukumbusha ili tukio?

(2) je moyo wako unahisi uko radhi kumuacha huyo bwana kiasi cha kutokukwaza katika maisha yako? Yaani hautajuta siku utakapokuja kukutana na mwanaume ambaye pengine hatakuwa kama huyu unayetaka kumuacha leo?

(3)Je nikosa kiasi gani ili la mumeo kutia mimba mdogo wako? Je hakuna watu waliolewa na mume mmoja mtu na mdogo wake? Hoja hapa kama unampenda hii si sbabu ya kumuacha kwa sbabu wanaume wote tuna tabia izi tofauti ni nafasi ya kuipata kufanya icho kitu.

(4) Je wewe ukuwa kumsaliti mumeo? Si lazima uwe ulifanya yaan ile hali ya kuhisi unataka kutoka na mtu anayekutongoza ama mko kwenye harakati izo, kama uliwai ni dhahiri kosa la huyu ni mimba na umepata bahati ya kujua.

(5) soma bible mie siyo mtaalam sana lakini nakumbuka aliyezaa na kijakazi wake utakuwa unamjua na kijakazi ni mfanyakazi wa ndani house girl. Maisha yaliendelea.

Wanaume wanaolala na mashemeji zao ni wengi sana. Tatizo atupendi kuwa wakweli.

Binafisi kwa matukio ambayo ninayaona yanaendelea kwenye jamii yetu ilo lako naliona dogo sana, kila mtu akisema matukio yake amabayo yameishamkumba ndani ya ndoa unaweza kujiona wewe hauna tatizo.

Uamzi ni wako
Moyo wako kama unaridhia unaweza kuendelea na msimamo wako lakini kama unaona kuna kale karoho kidogo ka kupenda wasamehe maisha yaendelee.
Nimekuelewa nikujibu tu kifupi, sina tabia za ajabu na huwa siziyngi mkono hata kidogo..sijawahi hata kuwaza kuisariti ndoa yangu ingawa wapo waliojaribu kunifuata kujaribu kunishawishi...
Kwa hii tendo nililotendewa upendo juu ya mume wangu umekwisha kabsa mdogo wangu pia..siwezi kuishi na mtu ambaye amenifanya nipoteze upendo nae
 
Unahakika kwamba nililazimisha kutuzaa? Maelezo yangu tank Irish Elena, acheni kutetea uovu, kama unauhakika na hili emu nithibitishie..maana unoangea as if wakati tunakubaliana na wewe ulikuwepo..isitoshe kama huna cha kuchangia ni vyema ukanyamaza. By the way naijua thamani ya ndoa wala nisingependa ifikie hapa ilipofika Ila sina jinsi im ready to let it go.
Leah, sijaandika kukufurahisha, lakini pia usilete mada ukadhani kila mtu ataongea yanayokupendeza. Ndio maana ikaitwa hoja, tunaijadili kila mtu anavyodhani ndivyo. Hakuna sympathy hapa, kama umekosea lazima tu uambiwe.

Lakini hii ni hadithi ya upande mmoja, hatujui huyo bwana wako angepewa nafasi angesemaje kuhusu ninyi wawili. Ukweli unaujua wewe na yeye. Bado haibadilishi ukweli kuwa amezini na mdogo wako, na huo ni uchafu. Mengine mnayajua wawili, na uamuzi unao wewe.
 
ishu hapa siyo kutafuta mwanaume mwingine, ishu hapa ni kuangalia ni wapi alipo Angukia.

Maana wanaume wote tupo sawa usipo jua jinsi ya kumcare mume wako. Mambo yatakuwa yale yale.
kwa hiyo MUME kumzalisha SHEMEJI yake ni halali simply becoz Leah 2 kashindwa 'kumcare' mumewe au unatetea nn mkuu? fafanua vzr.
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Listen to your heart. Huyo mume hakufai.period.
Kila step unayochukua ni sahii kabisa.
 
Mkuu hizi ndoa zina mambo mengi sana na majaribu kibao unaweza ukatoka mbio mwanzoni kabisa. Dada angalia ndoa yako huyo mdogo wako ni mharibifu na mume wako ameingiliwa na roho ya uzinzi. Chakufanya hakikisha ndoa yako haivunjiki na muondoe huyo dogo hapo home kwako. Jaribu kuwa mke wa kawaida na utafute watoto wako mwenyewe. Good luck!
mkuu ndoa haivunjikije wakati mume KAIVUNJA kwa kumzalisha shemeji yake? hebu fafanua huko kutovunjika unamaanisha nini. wewe unaona hapa kuna NDOA wakati ilishavunjwa?
 
Aisee pole sana. Kuna misala mingine ni mikubwa zaidi ya hii katika maisha. Ukiona jambo limetokea kwako usidhani ni jipya katika ardhi hii. Natambua unaumia kiasi gani na kwa namna kubwa umeamua kusogea pembeni kwahiyo wadau labda wakushawishi vinginevyo.
Huyo mumeo kakukosea. Hakuna shaka katika hili. Ndugu yako na yeye anajua anachofanya na dhamira yake baada ya kutokea kosa na kukataa kutoa huo ujauzito, ina maana dhamira yake ipo wazi. Angekubali kutoa hiyo mimba yasingekufikia. Lakini ndio hivyo Mungu naye kawaumbua.
Bahati kubwa ni kwamba hamna watoto, maamuzi ya kuondoka yanakuwa rahisi. Lakini tatizo jingine, hujui unakoenda au utakapofanikiwa kwenda patakuwaje. Hii inaweza kukufanya utafakari.
Uhakika unapotea zaidi kwa kutoweza kumtathmini mwanaume huyu, je, anajuta kiukweli na hatorudia?
Mie kimtazamo wangu na mapungufu hayo niliyoandika, huwa nina amini kwenye kusamehe na kuweka mambo sawa ili maisha yasonge mbele. Ninakushauri dada yangu, rudisha moyo nyuma, hao umeshawadhalilisha na wamedhalilika vya kutosha. Katika mazingira hayo, mrudie mume wako na huyo kiumbe atakayezaliwa, asikae kwa mumeo (yaani kwako) au hata kwa mama yake, (ikibidi wazazi wenu ndio wamlee mtoto huyo.
Rudisha moyo, kwenye maisha kuna misukosuko, natumai hayatajirudia tena. Pole sana
 
Leah, sijaandika kukufurahisha, lakini pia usilete mada ukadhani kila mtu ataongea yanayokupendeza. Ndio maana ikaitwa hoja, tunaijadili kila mtu anavyodhani ndivyo. Hakuna sympathy hapa, kama umekosea lazima tu uambiwe.

Lakini hii ni hadithi ya upande mmoja, hatujui huyo bwana wako angepewa nafasi angesemaje kuhusu ninyi wawili. Ukweli unaujua wewe na yeye. Bado haibadilishi ukweli kuwa amezini na mdogo wako, na huo ni uchafu. Mengine mnayajua wawili, na uamuzi unao wewe.
Namim sikupost humu ili kufurahishwa wala kuhurumiwa na wewe na pia sikuandika ili wewe upotoshe, sema unachokijua, kueleza yale usiyajua ndiyo kimenifanya nikujibu, kama unataka kujua upande pili ataeleza nini, basi ungeendelea kungoja mpaka atakapo kuwa tayari kueleza ndipo ujibu maana ninahakika kuwa Hana ujanja wa kukaa zaidi ya siku moja hajaingia jf, inamaana thread imeisoma kukaa kwake kimyaa kunaonesha hana cha kusema wala kujitetea, ni hayo tu mkuu
 
Hapa isidanganyike na lolote dada ndoa isiwe sababu ya kuzalilishwa wewe na mdogo wako,kwa hiyo unataka mzalishwe wote wawili?,achana nae mwachie dogo,kwa kuusiana na nyie peke yake inatosha usimpe tena nafasi ya kuwazalisha tena kaa mae mbali kama ukoma,shemeki unamgonga tu kama kaa sawa unasepa zako aah sasa wamejiachia mpaka kaigoti mmh,jifunze kusahau tafuta mwingine akupe faraja.
 
Mianaume mingine mi binafsi na inawivu sana,haipendi kuona wake zao wapo juu, et ulikataa kuzaa utazan wakati wankubalia ilikuwepo! Vipi kama leah2 angepewa mimba na shemeji yake? Mngemshauri huyo mwanaume kuendelea na mkewe! Acheni upoyoyo,.
Duh hivi we Monnica hata mme wako mpya wa majuzi kati nae unamsemea kwa lugha hii hii isiyo na staha ! !! Kama ni hivyo basi hongera kwa kuokota "Bushoke"
 
Mkuu hakuna haja ya kuanza kutumia maneno ya kuudhi. Kila mtu ametoa mawazo kwa jinsi anavyoona na haina maana tunashabikia uzinzi au kumtetea huyo aliyemkosea mke wake. Ninazungumzia kusamehe. Unafikiri bila msamaha kungekuwa ndoa? kila mtu mapungufu yake and then utaachana na watu wangapi kama s
 
Wote wanaosema chanzo ni mwanamke ni malaya wa mtindo huo na wameuhalalisha uzinzi wa mwenzao,hakunyimwa tendo la ndoa!hata angetaka mtoto angesema kilichomfanya alale na mdogo wa mwenzie ni mtoto?mbona mimba ilipoingia alishauri watoe?alikua hajui kama atasababisha mimba?kwa umri wake angekua mwenzie ndo anamimba ya mdogo ake angejiskiaje?geuzia kwako tuseme mkeo anamimba ya kaka yako au mdogo wako!
Vitu vingine sio kwasababu jukwaa ni huru ndo unambwela tu,tumia kichwa kufikiria sio makalio maana hata wewe yanaweza kukukuta.
Kama unaaleji na mwanamke msomi wewe ni mzembe na muoga na hupendi maendeleo kwanza unawasiwasi na uanaume wako[emoji57]
Yawezekana ni kweli hakunyimwa unyumba lakini elewa kulikuwa na sharti la kukwepa mimba mpaka amalize masters, hivyo unyumba haukuwa free kwani pengine jamaa alilazimika au kulazimishwa kutumia kondom mara nyingi kuliko kawaida. Sasa kwa shemeji ilikuwa free sex bila vikwazo vya "kiuchumi" Ni ubatili kutumia kondom kwa mke wangu halali tena eti mwanzo mwanzo wa ndoa, aaaaagh!!!
 
Xambi unaupungufu wa kufifikili iv ata wewe usikie kuna mtakuja mmoja anawachezea dada zako utafurahi?,tena uyo mtu pumba......kabisa,tena afai duniani ata mbinguni,
 
Unahakika kwamba nililazimisha kutuzaa? Maelezo yangu tank Irish Elena, acheni kutetea uovu, kama unauhakika na hili emu nithibitishie..maana unoangea as if wakati tunakubaliana na wewe ulikuwepo..isitoshe kama huna cha kuchangia ni vyema ukanyamaza. By the way naijua thamani ya ndoa wala nisingependa ifikie hapa ilipofika Ila sina jinsi im ready to let it go.
Wewe dada vipi! !? Yaani yeyote aliye kinyume na maamuzi uliyokwisha chukua basi huyo akae kimya hana cha kuchangia! !? Kuna mtu kasema unatuhadaa tu kwani umeshafanya uamuzi wa kufukuza huyo mme kwenye nyumba yako, unachotafuta hapa nikujua wangapi wanakuunga mkono. Ni hatari sana mwanaume kuhamia nyumba aliyojenga mwanamke.
 
Nimekuelewa nikujibu tu kifupi, sina tabia za ajabu na huwa siziyngi mkono hata kidogo..sijawahi hata kuwaza kuisariti ndoa yangu ingawa wapo waliojaribu kunifuata kujaribu kunishawishi...
Kwa hii tendo nililotendewa upendo juu ya mume wangu umekwisha kabsa mdogo wangu pia..siwezi kuishi na mtu ambaye amenifanya nipoteze upendo nae
OK achane nae utapata mwingine akupendae au amua kuishi peke yako mpaka mwisho wa maisha yako, jipende mweyewe kwa dhati.
 
Back
Top Bottom