muda mwingine yatupasa kujiuliza hivi tunaposhauri tunashauri ili kuponya mtu, ama tunashauri kishabiki ili kuumiza watu. tukiamua kuwa mahakimu basi je siye tu wasafi zaid na sana kuliko huyu mume wa
leah2 ama nikutaka tu tuonekane kwa miandiko yetu kwamba tuko sawa ilihali mioyoni mwetu hatuko hivi.
Biblia inasema hivi ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo, na tuna kitabu cha yoshua bin sira kikasema usitie chumvi kwa jambo lolote iwe kwa heri ama shari na wala usipate kuitwa adui badala ya mpatanish.
Mwimba zaburi alisema heri wapatanish maana wao watamwona Bwana.
nimesema hayo yote nikiwa na lengo moja tu simaanish mimi ni mpatanish ila naangalia je ni jamii gani ambayo sisi tunataka kuijenga. Hivi tunataka kuwa na jamii yenye visasi na vinyongo ama jamii yenye kuheshimiana na kuchukuliana mizigo? ikiwa Kristo alisamehe na kutuchukulia mizigo kila leo iweje sisi tusimame kifua mbele tuone huu mzigo wa mume wa
leah2 ni mkubwa sana hauchukuliki?
Je umewaza hatma ya mpasuko wa kifamilia ambao utatokea kwa akina
leah2? je umejiuliza vipi familia ya mume wa
leah2 itamchukuliaje mtoto atakayezaliwa? unaonaje kama
leah2 akiweza kuyatatua kwa namna ambayo hata yeye mwenyewe haitampa mzigo nafsini na siku moja atajikuta kuwa na amani maisha yake yote kwa uamuzi huo?