Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Pole sana,ila endelea na mume wako ,mdogo wako aendelee na maisha yake na mtoto akizaliwa atalelewa na mme wako.Akishakuwa mkubwa ataunganishwa na watoto wako utakaobarikiwa.
Ukimuacha mme wako amuoe mdogo wako ,utaumia maisha yako yote kwa kuporwa mme na mdogo wako na utakubali awe shemeji yako?
 
Leah Leah Leah leahLeah Leah, Mwenyezi Mungu akutangulie
Tuwasiliane
blessings
 
Dah.
Hapo kuna mambo mawili inabidi yawekwe sawa.
  • Achana na huyo mume, kwa maana ya kuvunja ndoa, ukikubali kuendelea naye utapata majuto maisha yako yote na aibu ya milele mpaka unaenda kaburini, hilo ni donda zito sana katika maisha yako, huwezi kulibeba.
  • Pili hakikisha pia hata mdogo wako haolewi na jamaa, maana pia akiolewa bado itakuwa ni pigo kubwa sana kwako na maumivu yake huwezi kuyabeba pia, kifupi huyo jamaa na mdogo wako inabidi watengane kabisa tena kwa makubaliano maalumu ustawi wa jamii au polisi, mdogo wako kwa kukuingilia ndoa yako inabidi achague moja either aendelee na undugu na wewe kwa kuachana na jamaa au aendelee na jamaa kwa kuendelea na wewe.
Tatizo litakuja kwa mtoto atakayezaliwa, inabidi muweke makubaliano ya namna mtoto atakayezaliwa atalewewa na nani. Kama ni mama pekee baba asithubutu kuja hata kumjulia hali, kama ni baba pekee mama yake amkabidhi kwa baba yake na asahau kabisa kama aliwahi kuzaa.

Kinyume cha hapo hio ni aibu ya familia na audui mkubwa sana baina yenu ninyi wawili, mtu na dada yake[/QU
Mhhhh
 
Mie sijaona tatizo hapo...
Mtoto ni baraka toka kwa Mungu.
 
Siku zote usitoe maamuzi ukiwa aidha na hasira au furaha sana.....!
 
Duh! Pole sana dada. Huu ni mtihani kweli kweli. Hatua zote ulizochukua ni hatua za maturity person. Hongera maana wengi wetu tungekosea mpaka sasa. Mungu akusaidie uvuke salama. Uamuzi ulioutaja kuwa umechukua naona ndio sahihi. Sio rahisi kuwa na a sustainable marriage hapo. You will end up with guilty. Wasamehe tu na Mungu akusaidie, but usiendelee nayo.
 
Nakuomba leeeeehhh usitoe mimba yangu

Pole Leah...Kina Leah wanakuwaga wapole na wanyenyekevu....Nakuonea huruma

Mdogo wako Rachel hajakosea

Kasome Biblia ujue Rachel na Leah walikuwa na mahusiano gani....Na nini kilitokea Pale Yakobo alipotaka kuoa.

Lakini nisikilize Leah;

Kosa limeshatokea,Msamehe Mume wako,Tunza ndoa yako...kama kuna makosa ulifanya mwanzo usiyarudie.....Mtoto atakayezaliwa atakuwa wa kwako..kwa sababu ni wa mdogo wako.....

Option pekee itakayokupa Amani ni kusamehe...La sivyo itakutesa sana maishani kwako

Msamehe Mumeo...Wanaume tuko wajinga sometimes......Pia mdogo wako amefanya ujinga sana......

Nakuomba sana Leah...sawa mama eeeeehhhh
 
a1aa306b019b48743039a0b1f6909068.jpg

Huu ushauri ni rahisi sana kuutoa kama Jambo halijakufika eti Yule mtoto aje Hapo seriously? Wanaume bana.
Mm ya mtoto kurudi? Hujavaa viatu vya mhusika.
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.

Hebu ninaomba uje PM urgently with me, promiseful nitakusaidia kwa hakika.
 
Kwanza Pole sana shemeji, kiuhalisia umeshiriki kuhakikisha shetani anaimiliki familia yako, wanaume wengi na jamii kwa ujumla baada ya ndoa wanategemea kupata watoto, hayo unayosema ulimshirikisha? je aliafiki? tabia za mdogo wako je?
Masomo ungeweza kuendelea nayo baada ya kuzaa au ulikuwa na malengo yako binafsi? Anyway pole sana,, ndoa ni ya watu wawili tuu....wewe ndie muamuzi....sikushauri kuendelea na huyo mlume,, keshazaa na mdogo wako ni shemeji yako huyo...
 
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
Achana na mtu anayepandilia kama mbuzi wa shehe mtaani! Lakini ulistahili uwe umeshamfahamu mumeo. Tatizo la wasomi wengi ni kuigiza maisha na kujikuta una overlook natural behaviour. Binti wa 20s na mumeo, eti wataniane tuuu! NO!
Achana naye, tutakutana mitaani kwa mengine, kuliko kulizwa na unayemwamini.
 
pole kwa yote yaliyokupata. lakini kumbuka ndoa sio mchezo. samehe saba mara sabini. hapo ni wewe wa kuamua kulinda ndoa yako ama kubomoa.
 
Sasa roho inakuuma nini?huyu si ndugu yako lakini?na huyo mtoto utakua mama yake mkubwa.
 
Yaani hiyo picha ni chafuu naona Kama haibebeki, nachoona ni bora umsamehe mdogo wako na kuwa nae karibu nakumpenda tuu hata ikibidi umsaidie, ila futeni uhusiano na huyo mwanaume asiendelee na mdogo wako wala na wewe maana hakuna mtoto Kati yako na yeye, huyo mume wako mumfute kwenye familia yenu huyo mtoto wa mdogo wako atakaezaliwa usimchukie mumlee na mumpende huyo mwanaume ndio mumtenge ila mtoto wake msimnyime na awe guru kumuhudumia ikiwa atataka.
 
Kwanza pole,pili mdogo wako hana tofauti na hawara(samahani kwa kutumia neno hili kwa mdogo wako),na wanasema hawara ni shimo refu lenye kiza ukivutwa humo kutoka ni shida maana huoni,what am trying to say ni kwamba kamwe usimwachie nyumba yako hawara au mchepuko cjui,komaa na ndoa yako.Matatizo ya hapa na pale hutokea japo hili zito kulibeba.Kwanini umwachie mdogo ako mumeo?,kaa chini tafakari kwanza kwanini unaondoka?,ukishaondoka utakua umefaidika nini(maana kinyongo bado utakua nacho kwa mdogo wako),inawezekana pia na wewe ukawa umechangia kwa namna moja au nyengine.Japo kikanisa ndo hii inavunjwa bila ubishi ila inahitaji maamuzi magumu.Akili ya kuambiwa changanya na yako halafu ndo ufanye maamuzi.
 
Back
Top Bottom