Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimekuwa kwenye wakati mgumu kwa muda sasa.

Nimeolewa na Nina miaka miwili kwenye ndoa lakn sikuwa tayari kuzaa kwakuwa tulikubaliana mpaka nimalizie masomo yangu ya masters ambayo natarajia kumaliza mwaka huu.

Tumekuwa tunaishi vizuri tu na mume wangu nikimtii na kuwajibika kwa majukumu yangu yote kama mke kwa mumewe pamoja kuwa Ninafanya kazi na kusoma pia.

Mimi ni muajiriwa lkn mume wangu wangu ni mfanyabiashara kariakoo.

Nina mdogo wangu ambaye aligraduate mwaka jana akaomba akae kwangu wakati anatafuta kazi, sikuona shida nikamkubalia.

Tangu aje tumekuwa tukiishi vizuri tena kwa amani.

Kama Dada nilijitahidi kumtengea mdogo wangu bajeti yake toka kwenye mshahara wangu kwa kila mwenzi iliaweze kumudu kufuatilia mambo yake kirahisi.

Baada yakuwa nae kwa miaezi mitano nikaanza kuona mabadiriko kadhaa.
Akawa karibu na mume wangu sana, sikujali nikajua ni ushemeji tu.

Siku moja nilirudi nyumbani mapema sikukuta mtu.

Nikaendelea na maandalizi ya chakula cha jioni, nikiwa jikoni nikasikia sauti ya mume wangu na mdogo wangu wanabishana.

Niliposogea dirishani nisikilize vizuri huku nikichungulia nje nikaona dogo analia na mume wangu anambembeleza huku akimfuta machozi.

Nikatulia nione nini kinaendelea, nikasikia mume wangu anamwambia itabidi tuitoe maana Dada yako akijua wote tutakuwa nawakati mgumu..

Nikachukua simu yangu nikawa nawarekodi, baada ya muda wakaingia ndani nami nikajifanya sijui chchte.

Sikuwauliza chchte nikijipa muda wa kufanya utafiti zaidi.

Baada ya wiki, mdogo wangu akaniambia kuwa ana shida na Mimi.

Nikamsikiliza akaniambia kuwa ana mimba..

Sikuhamaki wala kuonyesha kama najua chchte, nilimuulize nani muhusika akajibu hajui.

Nikamwambia kama hujui sina namna ya kukusaidia siku ukijua utaniambia nijue jinsi ya kukusaidia.

Akaanza kulia na kunipigia magoti huku akisema nisamehe Dada, nikamwambia wala hujanikosea.

Nikamwambia wewe ni mtu mzima umeamua kuzaa kunashida gani?

Baba wa mtoto naamini yupo kwahiyo sikuhukumu.

Akasema, kuna jambo nataka nikwambie..
Niikamwambie aniambie..
Akasema lakini naomba unisamehe, shemeji ndo amenipa mimba.

Kwakweli niliumia sana, nikamuuliza wana muda gani tangu waanze mahusiano akajibu ni miezi minne sikujibu neno, nikaendelea na shughuli zangu.

Mume wangu alikuwa matembezi, aliporudi nikawaita wote wawili, nikamwambie Dogo aseme alichoniambia mbele ya shemeji yake.

Akasema tena ana mimba ya shemeji yake..mume wangu kusikia vile akataka kuwa mkali..

Nikamwambia hana haja ya kufoka, nikanyamaza sikusema wala kulaumu chchte.

Nikaamua kuwaita wazazi wangu na wake pia bila wao kujua,

Walipo kuja nikawambie Mimi ndiye niliyewaita lkn mume wangu na mdogo wangu ndiyo wanachakuwaambia.

Walipoulizwa wanasemaje dogo akaeleza kuwa anamimba ya shemeji yake..

Mume wangu alipoulizwa kwa unyonge sana alikubali. Wazazi wakaniuliza Nina maamuzi gani?
Nikawajibu nimeamua kumuachia mume mdogo wangu.

Wazazi wakanisihi nimsamehe na tuendelea na maisha ya ndoa..na dogo arudi kwa wazazi.

Niliwakatalia nakuwambia kuwa nisingeweza kuvumilia ndoa ya aina Ile..nikamwambia wasijipotezee muda wao kuniambia cha kufanya niliwaita waje wasikie uchafu niliofanyiwa then baada ya hapo mimi ndo nitoe maamuzi
Nilisisitiza maamuzi yangu nikutoendelea na ndoa tena.

Waliniambia nisichukue uamuzi bila kutafakari wakanipa wiki tatu za kufikiria Leo hii ni siku ya nane tangu nipewe muda wa kutafakari..

Niliwaomba niwe mbali na watuhumiwa wangu kipindi cha kutafakari.

Nikawasihisi watuhumiwa wao ndo wanipishe nyumbani kwangu, maana tunapoishi ni kwangu.

Wameondoka na sijui walipo kwenda.

Binafsi sijisikii kuendelea kuishi na huyu mwanaume ingawa kweli tumeshafunga ndoa lkn siwezi kuwa na raha ya ndoa ktk mazingira kama haya.

Najiuliza heshima yangu iko wapi?

Jamii inanionaje?

Na mtoto atayezaliwa ntamuonaje?

Naona dhambi hii ni kubwa sana siwezi kuibeba.

Wadau naomba msaada maamuzi niliyochukua naweza kuwa sahihi? Nisaidie plz.

Naomba plz sihitaji matusi wala mizaha nahitaji ushauri na faraja.

Naamini ktk wingi wamashauri hapakosi hekima.
ayo ni majaribu! hebu nenda urudi kwa mumeo! utalipwa na Mungu katika kusamehe jambo zito namna hiyo!
 
Unadhan ni rahisi hivyo? By the way ndoa ni ya thamani kama itathamini na wahusika wote ikiwa ni pamoja na kutunza maagano,vingenevyo inakuwa ni ndoano
Upo sahihi, songa mbele na mipango yako, acha hiyo mizinzi iendelee kuzinzika
 
Wewe Gojaga Nize acha kupotosha maandiko, Yesu na Stefano walifanya vile kutetea imani na wala si kuitetea dhambi. Sote tumemshauri asamehe na asiwe na kinyongo nao lakn asikubali tena kuendelea na maisha ya ndoa ya maigizo, achane nao aendelee na ratiba zake, biblia imehalalisha kutenga pale inapotokea uasherati je kilichofanywa na mume wa leah2 si zaidi ya uasherati? Huyo mume wa leah2 na namuona kama kahaba na Malaya tu ni wa kukimbia kama ukoma. Leah Dada angu huo ukurasa ufunge na anza upya, usilie tena zinatosha sasa ni wakati wa kujifuta machozi na kuchukua hatua.
Leo ni jumapili nenda kanisani tena ukiwa umechangamka kbsa.

Habari za ndoa mpya Bw Moniccca. Kama umesoma vizuri nilichoshauri no kwamba, nataka kwanza asamehe kwa dhati kutoka ndani ya moyo wake. Na hill jambo la kusamehe hawezi kusamehe hivihivi bila kumhusisha Mungu.

Akishasamehe, then yeye mwenyewe atapima kichwani mwake.

Moniccca siku zote kufanya maamuzi wakati unatatizo huwa sio best solution. She needs to have more time and I am insisting hiyo time isiwe time ya kuwaza na kuwazua iwe in time ya kushirikisha Mungu hilo jambo.

Ndoa haikufungwa sebuleni ilifungwa kanisani na mungu alihusishwa iweje Leo unatoa conclusion kana kwamba we ndo uliyewaunganisha?

Sitetei uovu Ila nataka asamehe kwanza!!
 
Mianaume mingine mi binafsi na inawivu sana,haipendi kuona wake zao wapo juu, et ulikataa kuzaa utazan wakati wankubalia ilikuwepo! Vipi kama leah2 angepewa mimba na shemeji yake? Mngemshauri huyo mwanaume kuendelea na mkewe! Acheni upoyoyo,.
 
Umefanya uamuzi sahihi, hakuna haja ya kuendelea Na ndoa hiyo.!
 
Habari za ndoa mpya Bw Moniccca. Kama umesoma vizuri nilichoshauri no kwamba, nataka kwanza asamehe kwa dhati kutoka ndani ya moyo wake. Na hill jambo la kusamehe hawezi kusamehe hivihivi bila kumhusisha Mungu.

Akishasamehe, then yeye mwenyewe atapima kichwani mwake.

Moniccca siku zote kufanya maamuzi wakati unatatizo huwa sio best solution. She needs to have more time and I am insisting hiyo time isiwe time ya kuwaza na kuwazua iwe in time ya kushirikisha Mungu hilo jambo.

Ndoa haikufungwa sebuleni ilifungwa kanisani na mungu alihusishwa iweje Leo unatoa conclusion kana kwamba we ndo uliyewaunganisha?

Sitetei uovu Ila nataka asamehe kwanza!!
Njema Gojaga Nize, ni kusahihishe, Mimi si bw. Moniccca, mim ni bi moniccca. Ila nyie wanaume wabinafsi sana
 
Aisee haya ndio matatizo ya wasomi et nilikataa kuzaa mpaka niwe na mastars imagen mwanaume akusubili umalize masomo ndo umzalie wakati amesha kuoa umpe anachotaka sasa we endelea na PhD yy akae na mke wake walee familia yao
Una matatizo makubwa ya ufahamu na ubinafsi, muuendekeza mfumo dume, halafu inaonekana una roho mbaya.
 
kaka alitaka asome kwanza ndio azae ndoa ya nini?? angesoma hadi akamaliza madarasa yote kisha arudi kwenye ndoa ili akikaa ajue ni kugegedwa na kuzaa, minyodo ya kusoma imemtumbukia nyongo.
Nakuona ktk level ya juu ya ujinga wako
 
Kama ndani ya moyo wako bado kuna hisia za upendo kwa mumeo msamehe...utaumia zaidi wakati utakapo achana naye halafu akamuoa mdogo wako utaumia zaidi...ni ushauri ila maamuzi unayo ww sbb unamjua zaidi mumeo na maisha yenu...ila pole sana inauma
 
Kama haufanyi kazi Global Publishers.. Basi utakuja kushtuka kwenda kuomba ajira while it's too late....
 
Mimi nawalaumu wote nikianza na wewe kwa kiasi kikubwa ndo umesababisha, kwanza maamuzi yako ya kuzaa mpaka umalize masters sidhani kama yaridhiwa na mume wako yawezekana uliforce kutokana na uwezo wako wa kipato maana hata nyumba umesema ni yako maana yake mume aliish kwako na sio kwenu, pili kazi ili kufanya uwe bize pengine usijal mambo mengine hasa ya kimapenz ndio maana hata ulipogundua ukaribu uliopo kati ya mumeo na mdogo wako wala haukushituka ili hali ukijuaa mdogo wako ni mtu mzima, tatu hata katika uombaj wa msamaha sijasikia ukisema mume ameomba msamaha inaonyesha amekubali tu kwakuwa familia zote zimekutana,

Mtazamo wangu ni vema familia ikakubaliana hiyo mimba itolewe ili kuleta jamani pande zote mbili hata kama utaachana naye kwa sababu kama mtoto atazaliwa mahusiano yao yataendelea kwako itakuumiza sana kuliko hata unavyoumia saiz, usiruhusu wakaoana et umemuachia kumbuka huyo mdogo wako ni ndugu yako bado hilo suala litakutafuna hasa ukifikiria mwanaume haonyeshi kujutiaa hilo suala
 
Iikuwa imebaki kidogo nikupe like,ila hapo uliposhauri familiya ikubaliane mimba itolewe imesababisha uikose like yangu mkuu.
 
Hapa sasa ndipo nafasi ya "dr chris mauki" inapotamalaki,haise dada yangu naomba umwone huyo mtaalamu wa masuala ya kisaikolojia atakusaidia sana
 
Sikumbuki vizuri na siwezi kukinukuu kwa usahihi hicho kifungu kutoka kwenye Biblia Takatifu. Ni jambo moja tu linaloweza kufanya ndoa kuvunjika nalo ni UASHERATI. Hivyo maamuzi zaid unayo wewe
 
Back
Top Bottom