Muhimbili waanza kutoa huduma kupunguza uzito, watatu wenye kilo 100+ wamepata huduma kwa Sh milioni 3.5 hadi 4

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila,iliyopo jijini Dar es Salaam, imeanza kutoa huduma ya kupunguza uzito uliokithiri, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.

Hadi sasa watu watatu wenye uzito zaidi ya kilogramu 100 wamepata huduma hiyo inayogharimu kiasi cha Sh milioni 3.5 hadi Sh milioni 4.

Akizungumza na waandishi wa Habari Leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof Mohammed Janabi, alisema hawatoi huduma hiyo kwa sababu ya urembo bali wanalenga kusaidia watu.

“Hii ni operesheni yetu ya tatu leo na siku ya leo tumewafanyia watu wawili hawa wote ni kilo 100 kwenda juu, wa kwanza kilo 160 na wengine kilo 105, hawajafanya kwa sababu ya urembo.

“Wiki moja iliyopita tulifungua kliniki ya mafuta tunawakaribisha hospitali zingine ziweze kuleta wagonjwa wake kupata huduma,”amesisitiza Prof Janabi.

Amesema utoaji huduma hiyo utahusisha tumboni kupitia mdomo hali itakayopunguza kiwango cha chakula kwa muhusuka.

“Tutaweka kwa miezi nane, tutaingiza kupitia mdomo hadi kwenye tumbo hakuna upasuaji tutatumia mitambo ifike mahali pake tutajaza dawa linapunguza ukubwa wa tumbo ukila kidogo utashiba hivyo tunategemea uzito utapungua.

Prof Janabi ameeleza kuwa faida kubwa ni kusaidia kukukinga na magonjwa ya kisukari, kiharusi, moyo, kushindwa kupumua.

Amebainisha kuwa matibabu yatakayotolewa ni siri ya mgonjwa, ambapo pia matibabu hayo huchuku siku mbili tu.

“Siku ya kwanza unaweza kusikia kama unavidonda vya tumbo, lakini baada ya muda utaendelea kawaida, hospitali hatukaribishi watu lakini tunawaomba wale wenye uzito mkubwa wafike kliniki, tuna kliniki ya siku mbili hapa Mloganzila na siku mbili Muhimbili Upanga,” amesisitiza.

Pamoja na hayo amesema pindi mgonjwa anapopatiwa huduma hiyo na kupungua atapata usaidizi wa mtaalamu wa lishe, ili asiongeze tena kiwango cha kula na uzito kuongezeka tena.

“Kabla ya kumuhudumia tutapima vitu vingine vyote ndo utakuja kupata huduma, faida kubwa ni kitu ambacho baada ya miezi nane tutatoa na hali ya kula kidogo itaendelea na akirudi tabia ya mwanzo anaweza kuwekewa mara nyingine hivyo ni vyema kuweka kiasi,” amesema.

Amesema mfumo wa Bima ya afya bado haujaanza kutumika hata hivyo watu wafanye mazoezi, wale mlo unaotakiwa.

“Na matatizo mengine ni ya kurithi ukiwa na mtoto ana uzito mkubwa mleteni wakati mwingine unaweza kukuta mtoto amezaliwa na kilo nne watu wakaona ni kitu sahihi kumbe sio kweli,” amesema.

Amesema gharama ya huduma hiyo kwa India ni Sh milioni 15 hadi Sh milioni 20 na Ulaya ni kuanzia Sh milioni 30 kwenda juu.

Amesema mwaka 2023 kwa kipindi cha Januari wanatarajia kuwahudumia wagonjwa 12 kwa gharama ya Sh milioni 3.5 hadi Sh milioni 4.

“Hii ni sehemu ya utalii tiba, hivyo nchi za jirani tunatoa huduma hizi waje kupata huduma ni tiba salama kama tunavyopandikiza figo, uloto na zingine wakitaka kupata huduma hapa ni rahisi,”ameeleza Prof Janabi.

Chanzo: Habari Leo
 
wapo vijana wengi walipokuwa shule (primary/secondary/vyuoni) walikuwa vimbao mbaoooo hahaaaaa

leo hiii wapo na biashara na kazi zaoo ukiwakuta full mshangaooo ....yaanii we acha tuuu... wanakwambia wanahangaika rejea umbao mbaooo hawaweziii
 
Tiketi ya KIFO
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imezindua huduma mpya ya kuweka puto maalumu kwenye tumbo la chakula kwa watu wenye uzito uliopitiliza (intragastic ballon) ambayo itasaidia kupunguza nafasi kwenye tumbo la chakula hivyo kusababisha mtu kula kidogo jambo ambalo litapelekea kupungua uzito.

Akizindua huduma hiyo leo Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema, Mloganzila ndio Hospitali ya kwanza ya umma Tanzania kutoa huduma hiyo hivyo amewapongeza wataalamu kwa kufanikisha jambo hilo” amesema Prof. Janabi
BA9FE061-DAF5-44F2-ACA0-D89F3A64EF8F.jpeg

“Hadi leo tumefanya kwa watu 3 na kuna zaidi ya watu 12 ambao wanahitaji huduma hiyo, wanaotakiwa kupatiwa huduma hii ni wale wenye uzito uliopitiliza ambao ni kuanzia kilo 100.

Kuhusu gharama za huduma hiyo , Prof. Janabi amefafanua kwamba kwa Mloganzila inagharimu TZS 3.5 Mil hadi TZS 4 Mil wakati nje ya nchi ni zaidi ya TZS 15 Mil.
BAC2ECE4-9463-45C5-9462-F563ECCF347D.jpeg

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji, Dkt. Eric Muhumba amesema huduma ya kuweka puto hufanyika kwa dakika 20 ambapo hufanyika kwa kutumia mashine ya Endoscopia (Endoscopy Mashine) hivyo haihusishi upasuaji wa aina yoyote.

Dkt. Eric ameongeza kuwa puto likishawekwa tumboni hukaa kwa muda kati ya miezi sita hadi nane ndipo hutolewa na baada ya hapo mtu huyo atakuwa ameshajenga utamaduni wa kula kidogo hivyo atakuwa amepuguza uzito wa kutosha.

Pia Dkt. Eric ameishauri jamii kufanya mazoezi na kula chakula kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu wa lishe ili kuwa na afya bora na kuepuka kupata uzito uliopitiliza ambao unasababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo kisukari, magonjwa ya moyo na kiharusi.
5BB50290-8922-4AC3-B3CD-1FC80980F6A8.jpeg

Naye, Mjumbe wa Kamati ya Utalii Tiba (Medical Tourism) Bw. AbdulMarik Mollel ameipongeza MNH-Mloganzila kwa kuzindua huduma hiyo ambayo itafungua milango kwa watu kutoka nchi jirani kuifuata kwa kuwa ni salama na gharama zake ni nafuu hivyo kusaidia kuitangaza Tanzania.
 
Yule punjabi aliyesema kipindi kile ana puto tumboni kumbe inawezekana kweli aliwekewa aisee nilidhani nimeona matibabu kumbe bado
 
Back
Top Bottom