Muhimbili kuanza kutoa huduma ya kuvuna mayai kwa Wanawake na kuwasaidia kuyahifadhi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inatarajiwa mwanzoni mwa mwaka 2024 kuanza kutoa huduma ya kibingwa kwa kuvuna mayai ya Wanawake na kuyahifadhi kwa ajili ya matumizi ya madae endapo wahusika watayataka.

Akizungumzia huduma hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali Hiyo, Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa wanatarajia kuanza kutoa huduma hiyo ya kibingwa ikitambulika zaidi kama 'In vitro fertilization (IVF) baada ya kubaini kuwepo kwa changamoto ya uzazi kwenye siku za hivi karibuni inayotokana na sababu mbalimbali.

Amesema kuwa katika huduma hiyo Wanawake ambao hawajazidi miaka 30 wanaweza kuvuna mayai yao na kuyahifadhi na badae wakiwa wanahitaji kubeba ujauzito wanapatiwa mayai yao kwa ajili hilo.

"Wengi tunajua kwa miaka ya hivi karibuni tatizo kubwa la Watu kupata ujauzito au kushika ujauzito na safari zimekuwa nyingi kwenda nje gharama zimekuwa kubwa, kwahiyo kupitia Serikali tukafikiria kwamba tufanye uwekezaji mkubwa... katika moja ya huduma ni utunzaji wa mayai ya wakina Dada ambao hawako tayari kupata ujauzito kwa sasa kwa sababu moja au nyingine"

"Kwahiyo yale mayai tutaweza kuyavuna na kuyatunza kadri ya muda yeye Dada atakapokuwa tayari"ameeleza Prof.Janabi

Amesema kuwa vifaa vinavyotarajiwa kutumika kwa ajili ya kutoa huduma hizo za kibobezi tayari vimenunuliwa, ambapo amedai kuwa kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kukamilisha ujenzi wa jengo maalumu litakalotumika.

"Vifaa ni gharama kubwa tumeweza kubana mapato ya ndani kwa kujikusanya na vile vifaa tumenunua kwa Bilioni 1.1"amesema Prof. Janabi

Ameongeza kuwa "Hii ni hospitali ya Taifa tunatakiwa kufanya vitu vya kibobezi kweli kweli tofauti na hospitali za Wilaya, hospitali za Kanda, kwahiyo hiki ndicho tutakifanya kwenye huduma zetu bobezi ambazo zitaanza mwakani"

Aidha Daktari Bingwa wa magonjwa ya Kike na uzazi,Martrida Machael Ngalina ambaye Mkuu wa kitengo cha kuwasaidia watu kupata uzazi kwa njia mbalimbali amesema kuwa maandalizi ya kuanza kutoa huduma hiyo yapo mbioni kukamilika ikiwemo vifaa vinavyotajika, kuwapatia utaalamu wataalamu ambao watatoa huduma hiyo na kuwa mwakani huduma hiyo itaanza kutolewa

Amesema kuwa kwa Taifa hakuna tafiti za moja kwa moja ambazo zipo wazi kuhusu changamoto za uzazi lakini amedai kuwa tatizo hilo lipo kwa wingi licha ya kuwa suala hilo watu wengi hawapendi kuliweka wazi.

"Kwa hapa Muhimbili tukikaa kiliniki pale kati wagonjwa 10 wanaokuja mmoja au wawili wana l matatizo ya uzazi kuna siku unaweza kudhani kama wameitana unakuta watu tisa kati ya 10 wana matatizo ya uzazi, kwahiyo tumekuwa tukijaribu kuanza kuweka takwimu, vilevile kujua jinsi ya kuwang'amua maana mwingine anakuja kwako asemi kama anatafuta mtoto anaongea pembeni kwamba Daktari naumwa mgongo, unatakiwa kujiongeza kujua kuwa shida yake anataka mtoto, lakini tatizo lipo kubwa"

Akifafanua huduma hiyo itakavyofanyika kitalaamu amesema "Hii dhana ya kuhifadhi mayai imekuwepo kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wanaopata kansa au wagonjwa ambao hawataki kuzaa sasa hivi wanataka kuzaa badae maana kuna wengine wangependa wasome kwanza wamalize hivyo wanataka ubora wa mayai yao akiwa na miaka 25 ubaki hivyo hivyo hata akiwa na miaka 45 awe na ubora wa mayai"

"Kwahiyo wakati wowote ukiwa ndani ya miaka 35 unaweza kwenda kuvuna mayai na unaweza kuambiwa yana ubora kiasi gani"

Ameeleza namna mayai hayo yatakavyovunwa na kuhifadhiwa "Shughuli ya kuhfadhi mayai tunao utaalamu wa kuhifadhi kwa njia mbili unaweza kuhifadhi kwenye mwili wako mfano tunaweza kuweka kwenye mkono sehemu ambapo yai litakuwa salama harafu badae ukaja kutoa kwa ajili ya ujauzito, nyingine ni kuhifadhi kwenye vifaa vyetu"

Amesema kuna njia mbalimbali zinaweza kutumika kuvuna mbegu hiyo ya Mwanamke, kwa kumsisimua au au kutumia mionzi au upasuaji mdogo ili kuvuna yai hilo.

Aidha Daktari huyo ameeleza kuwa Wanawake kadri umri unavyoenda ndivyo wanakuwa kwenye hatari ya kupoteza mayai yanayowawezesha kupata ujauzito ni tofauti na ilivyo kwa wanaume, lakini amedai kuwa hata mbegu hiyo ikihifadhiwa Mwanamke anaweza kuichukua akiwa ameshafikisha miaka 45 na akapata mtoto.

Kuhusu utaratibu utakaotumika Prof. Janabi amesema kuwa wataweka utaratibu ambao watakaohitaji huduma hiyo watakuwa wanachangia.
 
Wanataka kuvuna ya wasichana tu, wanasema ya watu wazima yamekomaa hayana ubora. Msichana anaweza kuvunwa mayai ila akitaka kuzaa atazaa kwa wakati anaotuka mwenyewe!
 
Vipi na kwa wanaume lini wataanza kuvuna mbegu zao? Bila shaka hapo napo watataka kuvuna mbegu za wavulana, huenda wakasema mbegu za watu wazima hazina ubora kama kwa wanawake wakubwa wanavyosema mayai yao hayana ubora ukilinganisha na mayai ya wasichana!
 
yan njia ya mojawapo ni kumsisimua 😂😂😂😂 huyu professa akae chini atulie alisema ukiona unawashwa mwili ni dalili ya ugonjwa figo mara hii hivi yeye anajiona alivyo lakini? mara watoto kuzaliwa kuanzia kg4 ni wagonjwa jamani huyu baba mimi sjasoma udokta lakini namuona kama ana tatizo kichwani
 
Back
Top Bottom