Apungua Kilo 58 baada ya kuwekewa puto Hospitali ya Mloganzila

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
WhatsApp Image 2024-02-27 at 20.27.01_4e01e86b.jpg

WhatsApp Image 2024-02-27 at 20.27.01_e53289cf.jpg
Mkazi wa Ngara mkoani Kagera, Charles Mwakameta amepungua Kilo 58 baada ya kuwekewa puto maalum (intragastric ballon) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila na kukaa na puto hilo kwa takribani mwaka mmoja.

Mwakameta amepunguza uzito kutoka Kilo 151 alizokuwanazo kabla ya Februari 20, 2023 alipowekewa puto hadi kufikia Kilo 92.65 alipotolewa puto hilo Februari 26, 2024.

Akielezea kuhusu safari yake ya kupungua uzito Mwakameta amesema ilianza baada ya kumuona msanii Peter Msechu ambaye aliwekewa puto hospitalini hapa na kuona kwamba huduma hii ni ya kweli na ina matokeo mazuri.

“Kipindi nilipokuja kuwekewa puto nilikuwa na kilo 151 lakini mpaka leo nimekuja kutoa puto baada ya mwaka mmoja nina kilo 92.65, watu walikua wakinicheka kutokana na uzito uliokithiri pia ninataka kuwaasa watanzania wenzangu wenye matatizo ya uzito mkubwa kuweka puto kunasaidia kupunguza uzito na wasiogope," amefafanua Mwakameta.

Kufuatia matokeo hayo mazuri ameishauri kufika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila ili kupata huduma ya kuweka puto ambayo imemsaidia na hajapata madhara yoyote zaidi ameweza kubalilisha mfumo wake wa maisha.

Muhimbili Mloganzila ilianzisha huduma ya kupunguza uzito kwa kutumia puto (intragastric balloon) ambapo tangu kuanzishwa kwa huduma hii Novemba 2022 takribani wananchi 158 wamenufaika na huduma hiyo.

Chanzo: Hospitali ya Mloganzila
 
Ni hatua, yabidi fanya mahojiano naye kupata sikia amejihisije kutoka 151 hadi 90's

Ivi muda wa kulala hutakiwi lala kwa tumbo ama?
Hutakiwi kunywa vitu vya moto moto kama chai/mtori/supu etc ama?
 
Kuna yule msanii bonge chawa wa chama flani hivi na yeye aliwekewa hilo dude lakini badala ya kupungua ndo kaongezeka zaidi...
Ningeweka picha yake lakini naogopa!
 
H
Mkazi wa Ngara mkoani Kagera, Charles Mwakameta amepungua Kilo 58 baada ya kuwekewa puto maalum (intragastric ballon) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila na kukaa na puto hilo kwa takribani mwaka mmoja.

Mwakameta amepunguza uzito kutoka Kilo 151 alizokuwanazo kabla ya Februari 20, 2023 alipowekewa puto hadi kufikia Kilo 92.65 alipotolewa puto hilo Februari 26, 2024.

Akielezea kuhusu safari yake ya kupungua uzito Mwakameta amesema ilianza baada ya kumuona msanii Peter Msechu ambaye aliwekewa puto hospitalini hapa na kuona kwamba huduma hii ni ya kweli na ina matokeo mazuri.

“Kipindi nilipokuja kuwekewa puto nilikuwa na kilo 151 lakini mpaka leo nimekuja kutoa puto baada ya mwaka mmoja nina kilo 92.65, watu walikua wakinicheka kutokana na uzito uliokithiri pia ninataka kuwaasa watanzania wenzangu wenye matatizo ya uzito mkubwa kuweka puto kunasaidia kupunguza uzito na wasiogope," amefafanua Mwakameta.

Kufuatia matokeo hayo mazuri ameishauri kufika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila ili kupata huduma ya kuweka puto ambayo imemsaidia na hajapata madhara yoyote zaidi ameweza kubalilisha mfumo wake wa maisha.

Muhimbili Mloganzila ilianzisha huduma ya kupunguza uzito kwa kutumia puto (intragastric balloon) ambapo tangu kuanzishwa kwa huduma hii Novemba 2022 takribani wananchi 158 wamenufaika na huduma hiyo.

Chanzo: Hospitali ya Mloganzila
Kilo 151 ni boda boda ama mtu😊😄
 
Puto kwa ambassador msechu liligoma huenda tumbo lili lidigest pia maana ambassador ilibidi aiwakilishe lakini likagoma likatuacha na maswali
 
Mkazi wa Ngara mkoani Kagera, Charles Mwakameta amepungua Kilo 58 baada ya kuwekewa puto maalum (intragastric ballon) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila na kukaa na puto hilo kwa takribani mwaka mmoja.

Mwakameta amepunguza uzito kutoka Kilo 151 alizokuwanazo kabla ya Februari 20, 2023 alipowekewa puto hadi kufikia Kilo 92.65 alipotolewa puto hilo Februari 26, 2024.

Akielezea kuhusu safari yake ya kupungua uzito Mwakameta amesema ilianza baada ya kumuona msanii Peter Msechu ambaye aliwekewa puto hospitalini hapa na kuona kwamba huduma hii ni ya kweli na ina matokeo mazuri.

“Kipindi nilipokuja kuwekewa puto nilikuwa na kilo 151 lakini mpaka leo nimekuja kutoa puto baada ya mwaka mmoja nina kilo 92.65, watu walikua wakinicheka kutokana na uzito uliokithiri pia ninataka kuwaasa watanzania wenzangu wenye matatizo ya uzito mkubwa kuweka puto kunasaidia kupunguza uzito na wasiogope," amefafanua Mwakameta.

Kufuatia matokeo hayo mazuri ameishauri kufika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila ili kupata huduma ya kuweka puto ambayo imemsaidia na hajapata madhara yoyote zaidi ameweza kubalilisha mfumo wake wa maisha.

Muhimbili Mloganzila ilianzisha huduma ya kupunguza uzito kwa kutumia puto (intragastric balloon) ambapo tangu kuanzishwa kwa huduma hii Novemba 2022 takribani wananchi 158 wamenufaika na huduma hiyo.

Chanzo: Hospitali ya Mloganzila
Kuweka puto gharama zake zikoje? Masharti ya kuishi na hilo puto ni yapi?
 
Back
Top Bottom