Watu wakichoka na wakakata tamaa,wala haitasaidia kupeleka mizinga,hata wakipeleka Rocket launcher,122 mm howrtzer,130 mm,BM,85 mm bado naamini haitasaidia,miaka 1989 niliwahi kuona video halisi sio ya kuigiza ya vita kati ya wapelestina na Israel,wapelestina walikuwa wanakabiliana kwa mawe wakati waisraeli wakitumia silaha za moto,lakini tusisahau ya Afrca Kusini,makaburu walikuwa wanatumia silaha za moto,bado walishindwa na ubaguzi ukaisha na mandela akatoka jela na kuiongoza nchi,lakini pia nimewahi kuona vita ya masaa 6 kati ya wachimbaji wadogo wa almasi hapo maganzo,polisi walianza kurusha risasi za moto lakini raia walikuwa wanatumia silaha za jadi ikiwemo maarufu kwa jina LUTAGO kwa kiswahili wanaita kombeo kama sikosei.
Maoni yangu ni kwamba wakakae na wananchi wafanye mijadala ya wazi,uhuru na serikali i-facilitate mambo yote mpaka waje na resolution ambayo itakuwa ya amani.kwa nini mradi huu ufanyike pasipo ku-implement participatory method?wao wanamtwara walipaswa wajulishwe fursa zao kwenye mradi huu,sio wajulishwe damu zao ni lita ngapi zitamwaga kwa risasi wanazozinunua kwa kodi zao,sio maiti ngapi zitakazokotwa zikiwa zimepigwa risasi na polisi wanalipwa mshahara kutokana na jasho lao kwa kazi ngumu za kilimo na nyinginezo.kwa hili hakika hakutakuwa na suluhu,kwanza nashangaa badala mradi uonekane ni wa wananchi wanataka mradi uwe ni wa seriklai na wawekezaji,je ulinzi wake utakuwaje hata baada ya kujengwa?
YOU people,hasa MACCM think twice