Mtwara kimenuka: Mabomu ya machozi yarindima!

suleym

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
1,960
1,205
Hali mijini hapa ni tete! Mabomu yanarindima mjini hapa kuwatawanya wananchi wanaojiandaa na mkutano mkubwa unaotarajiwa kufanyika mjini hapa kuhusu suala zima la gesi.

Chanzo cha mabomu hayo kupingwa ni baada ya umeme kukatika/kukatwa eneo panapotarajiwa kufanyika mkutano huo uwanja wa mashujaa mjini hapa na baada ya kuona hivyo wananchi wakaamua kuandamana kuelekea Tanesco kujua chanzo cha tatizo hilo la umeme na hali hiyo kupelekea polisi kuanza kuvurumisha mabomu ya machozi.

Ifahamike kwamba kumekuwa na mvua kubwa mjini hapa toka usiku wa leo ambayo inaweza ikawa chanzo cha kukatika kwa umeme huo (huu ni mtazamo wangu) ingawa inaweza ikawa hujuma pia.

Eneo nilipo umeme upo hali hii ya sintofahamu imepelekea huduma muhimu za kijamii kama maduka na soko kufungwa.

updates:
wakuu nimetoka kwenye mkutano umefanyika hapo mashiujaa kiukweli sikuweza kuendelea kuwaletea live kutokana na hali ya mvua pale uwanjani. kifupi mkkutano umehutubiwa na wazungumzaji kadhaa wakiwepo wasanii na wabunge, wasanii walikuwa ni afande sele na kala pina kwa upande wa bunge nimagdalena sakaya, sulemani bungala (bwe.ge) na barwan, wazuinguzaji wengime walikuwa ni katani na mtatiro

wote kwa hakika wamezungumza mengi sana na wote wameungana na wanamtwara katika kuhakikisha rasilimaliya gesi inawanuifaisha watu wa mtwara nakusini kwa ujmla kwa upande wa wasanii hakika afande sele amejitahidi sana kuongea kwa kujenga hoja. pamoja na kuwa nahali ya mvua wananchi hawakuondoka pale uwanjani kwa kweli serikali isipuuze haya madai ya watu wa mtwara kwa mfano kwa jinsi inavyoonekana vijana wako tayari kwa lolote serikalli iache kiburi. katika mkutano huo kumekusanywa saini za watu 26,000 na kuwatuma wabunge kupeleka bungeni madai yao na munge wa lindi mjini ameeleza mara baada ya mkutano huo wa bunge kma madi ya wanantwara na kusini yote watakutana lindi kwa maandamano makubwa yatakayo fanyika tarehe 23 februari mwaka huu hadi kieleweke

lakini pia kulikuwa na jambo la kusikisha, kumetokea ajari pale njia panda ya kuelekea eapot ya mtwara gari lililokuwa linatokea tandahimba likiwa na wananchi limepata ajali na watu watatu kuumia nakupelekwa hosptali ya mkoa ligula na mmoja inaelezwa hali yake sinzuri anatakiwa kupelekwa muhimbili kwa matibabu zaidi, jambo ambalo lilimfanya bwana katani kuumba umati mkubwa uliohudhuria kutoa mchango kuwezesha safari hiyo na wananchi kuitikia jambo hilo ni hayo tu wakuu. picha zitafuata punde.



SAM_0187.JPG SAM_0188.JPG Photo0138.jpg Photo0136.jpg
 
asante mkuu kwa taarifa hizi muhimu, tujuze zaidi kadir mambo yanavyoenda sisi tulioko mbali
 
Hakuna haja ya kuwapiga wenye nchi mabomu! Mara zote nasema suala la gas na wanamtwara litamalizwa na serikali na wanamtwara wenyewe endapo tu serikali ikikumbuka kuwa kuna kitu kiitwacho meza ya mazungumzo. Hatutegemei kusikia siasa au mabomu tena!!
 
Hizi ni salamu tosha kabisa kwa Serikali ya CCM kuwa wananchi sasa wanajua kujitetea hata kama SERIKALI imeshindwa kuwatetea, wananchi sasa wanajua chema na kibaya na wanajua nini wanataka.........chukulia hali hii na 2015 wakati CCM watakapoiba kura nini kitatokea.
 
... Mtwara msilegee. Mkilegea tu gas inachukuliwa. Nanyi anzeni kutumia mabomu ya kwenu.
 
Nguvu hizi zinazotumika ni kiashirio cha ukomo wa kufikiri.Mjadala wa Gesi au Rslimali za taifa kwa ujumla hauwezi kuzimwa kwa nguvu.Dikteta Dhalimu Wa Nigeria General Sani abacha alitumia Nguvu nyingi kuwanyamazisha Akina Ken Saro Wiwa kule Niger Delta akishirikiana na makampuni ya kibepari ya Shelly,CHEVRON,BP n.k katika kuhujumu raslimali ya Mafuta dhidi ya watu wa Ogun lakini mwisho wake haki ilishinda na yeye alikufa vibaya.

Hapa Tanzania watawala wanatuelekeza kufuata njia ya Ken,Daima tutashinda!
 
Viongozi wengi tulionao ...hekima na busara ni sifuri, walivyo wajinga wao wanaaangalia suala la Gesi kama Gesi basi
 
Hii si sawa hata kidogo.

Maskini akikosa chakula, atamla tajiri. CCM kaeni vyema na wananchi, tofauti na hapo jipakeni tu pilipili they are coming for you.
 
Angalieni tu msije mkawa kama Mwangosi(R.I.P).Manake polisi hawatumii akili zao za kuzaliwa!zaidi ya ganja na viroba!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom