Mtu mzima aliyekuzidi umri akikukwaza usimtukane, tafuta mtu mzima mwenzake amwambie ajirekebishe

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu vijana watanzania;

Mtu mzima aliyekuzidi umri akikukwaza usimtukane matusi. Mkikutana mkwepe au tafuta mtu mzima mwenzake amwambie ajirekebishe.

Nimeamua kusema hivi kwa maana kwamba, juzi baada ya kutoka katika mizunguko yangu kule Tabata mida kama ya saa moja na nusu jioni nikasema ngoja nipumzike kidogo katika kochi huku nikisubiri saa mbili ifike nitazame taarifa ya habari ya ITV, mara paaaap usingizi ukanipitia.

Nikiwa nimesinzia kwa mbaaaali ninasikia kama watu wanapiga kelele nje. Kutokana na wingi wa zile kelele sikuweza kabisa kuendelea kusinzia, nikasema ngoja nitoke nje nikaangalie kuna nini kinaendelea huko.

Daaah aisee, nilipofika nikakuta kijana wa nyumba ya jirani around 21 years anaporomosha matusi makubwa sana ya nguoni kwa baba mtu mzima umri kama 62 hivi. Huyo baba pia ni jirani tu hapa.

Nilijisikia aibu sana kwa kweli. Nikawa ninajiuliza kimoyomoyo, huyu mtoto anapata wapi ujasiri wa kutoa maneno mazito kama haya kwa huyu baba mtu mzima mwenye watoto 5 na wajukuu 2?

Kesho yake baada ya ule ugomvi kuisha nikajaribu kuwauliza baadhi ya watu niliowakuta katika ule mzozo wa jana yake wakawa wanasema kwamba yule baba mtu mzima huwa anamtaniaga sana yule dogo kwamba yeye atarefuka lini kama wenzake mbona kila siku anazidi kuwa mfupi tu kwenda chini (Tabia mbaya ya kuendekeza masiraha yaliyopitiliza na watoto wadogo)

Inaonekana kuwa kijana alikuwa amechoshwa kabisa na tabia ile ya miaka mingi sasa akaona ni bora amtukane matusi kama yote ili hasira za miaka yote hiyo ziishe.

Mimi nilichokifanya nilimuita yule dogo kisha nikaongea naye kirafiki sana kwa maana huwa wote tunashabikia chama la wana Man UTD.

Niliongea naye kama rafiki tu na kumwambia Mtu mzima aliyekuzidi umri akikukwaza usimtukane matusi.

Mkikutana mkwepe au tafuta mtu mzima mwenzake amwambie kisha yeye ajirekebishe. Je, huu ni ushauri sahihi wa kumpa kijana yule?

Wewe mwana JF ukikwazwa na mtu aliyekuzidi umri huwa unachukua hatua gani?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Sisi vijana na watu wazima tuna fanana tabia wazee wa miaka 20 ijayo cjui wata fananaje ukienda Marekani uki mwangali Trump ndio una pata tafsiri
 
Hakuna vijana wapumbavu dunia hii kama wavuta bangi wa bongo,Hawana maadili kabisa wao hawaoni aibu kumpiga makofi mtu mzima sawa na mzazi wake uku akijisifu atamuongezea dozi siku nyingine.

Ukiona kijana anamtukana mtu mzima bila uwoga jua tatzo lipo kwa mama mlezi,alikuwa hampi kalipio,onyo au viboko kwa makosa ya utovu wa nidhamu kwa watu waliomzidi umri.Ni ngumu kubadilika akiwa ukubwani.
 
Hakuna vijana wapumbavu dunia hii kama wavuta bangi wa bongo,Hawana maadili kabisa wao hawaoni aibu kumpiga makofi mtu mzima sawa na mzazi wake uku akijisifu atamuongezea dozi siku nyingine.
Ukiona kijana anamtukana mtu mzima bila uwoga jua tatzo lipo kwa mama mlezi,alikuwa hampi kalipio,onyo au viboko kwa makosa ya utovu wa nidhamu kwa watu waliomzidi umri.Ni ngumu kubadilika akiwa ukubwani.
Akileta ujinga na utu uzima wake kwny mwendokasi anaweza shikwa hata tako na wahuni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom