Mtu mzima aliyekuzidi umri akikukwaza usimtukane, tafuta mtu mzima mwenzake amwambie ajirekebishe

madaraja,barabara, umeme nk yanarahisisha maisha kwa kupunguza gharama za usafiri Kwahiyo October tunampigia kura Magufuli kwa 98% Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania.
Unakera brother. Haina haja ya kutumia accounts mbili kwenye uzi mmoja.

Uzi wako umekuwa wa kipumbavu kwa sababu hauna akili wewe na huyo magufuli wako.

Kama unampenda sana kampe tigo badala ya kuleta uzi halafu unajijibu hovyo hovyo kwa multiple accounts!
 
Acha kunifananisha mimi na watu wa ajabu ajabu. Njoo ccm basi
 
Kumbuka hata Wajinga nao huzeeka.
Kumkwepa anayekukwaza ni kuendekeza unafiki.
Kumtukana ni kujidhalilisha mwenyewe pia.
Ila kumchana live Mzee jiheshimu ni jambo sahihi zaidi.
 
Vita ni Vita ukiwa uwanja wa mapambano na unahisi kuzidiwa na adui ni kufwatua tu bila kujali madhara
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu vijana watanzania;

Mtu mzima aliyekuzidi umri akikukwaza usimtukane matusi. Mkikutana mkwepe au tafuta mtu mzima mwenzake amwambie ajirekebishe.

Nimeamua kusema hivi kwa maana kwamba, juzi baada ya kutoka katika mizunguko yangu kule Tabata mida kama ya saa moja na nusu jioni nikasema ngoja nipumzike kidogo katika kochi huku nikisubiri saa mbili ifike nitazame taarifa ya habari ya ITV, mara paaaap usingizi ukanipitia.

Nikiwa nimesinzia kwa mbaaaali ninasikia kama watu wanapiga kelele nje. Kutokana na wingi wa zile kelele sikuweza kabisa kuendelea kusinzia, nikasema ngoja nitoke nje nikaangalie kuna nini kinaendelea huko.

Daaah aisee, nilipofika nikakuta kijana wa nyumba ya jirani around 21 years anaporomosha matusi makubwa sana ya nguoni kwa baba mtu mzima umri kama 62 hivi. Huyo baba pia ni jirani tu hapa.

Nilijisikia aibu sana kwa kweli. Nikawa ninajiuliza kimoyomoyo, huyu mtoto anapata wapi ujasiri wa kutoa maneno mazito kama haya kwa huyu baba mtu mzima mwenye watoto 5 na wajukuu 2?

Kesho yake baada ya ule ugomvi kuisha nikajaribu kuwauliza baadhi ya watu niliowakuta katika ule mzozo wa jana yake wakawa wanasema kwamba yule baba mtu mzima huwa anamtaniaga sana yule dogo kwamba yeye atarefuka lini kama wenzake mbona kila siku anazidi kuwa mfupi tu kwenda chini (Tabia mbaya ya kuendekeza masiraha yaliyopitiliza na watoto wadogo)

Inaonekana kuwa kijana alikuwa amechoshwa kabisa na tabia ile ya miaka mingi sasa akaona ni bora amtukane matusi kama yote ili hasira za miaka yote hiyo ziishe.

Mimi nilichokifanya nilimuita yule dogo kisha nikaongea naye kirafiki sana kwa maana huwa wote tunashabikia chama la wana Man UTD.

Niliongea naye kama rafiki tu na kumwambia Mtu mzima aliyekuzidi umri akikukwaza usimtukane matusi.

Mkikutana mkwepe au tafuta mtu mzima mwenzake amwambie kisha yeye ajirekebishe. Je, huu ni ushauri sahihi wa kumpa kijana yule?

Wewe mwana JF ukikwazwa na mtu aliyekuzidi umri huwa unachukua hatua gani?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
utan mbaya
 
Ngoja kwanza, wewe ni rika moja na yupi kati ya wagomvi hao?

Huenda huyo unayemuita Mzee hapa wala hakukwazika na matusi hayo, wamezoeana ni utani wao miaka na miaka.
 
Nilichoelewa hapo ni kuwa ulilala huko huko Tabata, tena sebleni kwenye kochi... kesho yake ukapata kufuatilia utani wa watu.
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Ndugu zangu vijana watanzania;

Mtu mzima aliyekuzidi umri akikukwaza usimtukane matusi. Mkikutana mkwepe au tafuta mtu mzima mwenzake amwambie ajirekebishe.

Nimeamua kusema hivi kwa maana kwamba, juzi baada ya kutoka katika mizunguko yangu kule Tabata mida kama ya saa moja na nusu jioni nikasema ngoja nipumzike kidogo katika kochi huku nikisubiri saa mbili ifike nitazame taarifa ya habari ya ITV, mara paaaap usingizi ukanipitia.

Nikiwa nimesinzia kwa mbaaaali ninasikia kama watu wanapiga kelele nje. Kutokana na wingi wa zile kelele sikuweza kabisa kuendelea kusinzia, nikasema ngoja nitoke nje nikaangalie kuna nini kinaendelea huko.

Daaah aisee, nilipofika nikakuta kijana wa nyumba ya jirani around 21 years anaporomosha matusi makubwa sana ya nguoni kwa baba mtu mzima umri kama 62 hivi. Huyo baba pia ni jirani tu hapa.

Nilijisikia aibu sana kwa kweli. Nikawa ninajiuliza kimoyomoyo, huyu mtoto anapata wapi ujasiri wa kutoa maneno mazito kama haya kwa huyu baba mtu mzima mwenye watoto 5 na wajukuu 2?

Kesho yake baada ya ule ugomvi kuisha nikajaribu kuwauliza baadhi ya watu niliowakuta katika ule mzozo wa jana yake wakawa wanasema kwamba yule baba mtu mzima huwa anamtaniaga sana yule dogo kwamba yeye atarefuka lini kama wenzake mbona kila siku anazidi kuwa mfupi tu kwenda chini (Tabia mbaya ya kuendekeza masiraha yaliyopitiliza na watoto wadogo)

Inaonekana kuwa kijana alikuwa amechoshwa kabisa na tabia ile ya miaka mingi sasa akaona ni bora amtukane matusi kama yote ili hasira za miaka yote hiyo ziishe.

Mimi nilichokifanya nilimuita yule dogo kisha nikaongea naye kirafiki sana kwa maana huwa wote tunashabikia chama la wana Man UTD.

Niliongea naye kama rafiki tu na kumwambia Mtu mzima aliyekuzidi umri akikukwaza usimtukane matusi.

Mkikutana mkwepe au tafuta mtu mzima mwenzake amwambie kisha yeye ajirekebishe. Je, huu ni ushauri sahihi wa kumpa kijana yule?

Wewe mwana JF ukikwazwa na mtu aliyekuzidi umri huwa unachukua hatua gani?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
wazo jema
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom