Mzazi fanya yafuatayo mtoto akishakuwa mtu mzima tujenge familia bora

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,678
Wengi tumezaliwa katika mazingira flani ambayo mzazi sio mtu wa karibu saaana zaidi ya kuheshimiana Kama baba na mtoto tu.

Nilipokuwa nasoma nilipanga nje na rafiki yangu mmoja yeye alikua anampigia simu mzee wake wanaongea masaa hata matatu hadi manne, Mimi inaweza pita miezi hata 3 au 4 bila ya kuongea na mzazi, na akiona simu anajua huyu jamaa anataka hela tu.

Wazazi wengi wamekua wakiingilia maisha ya watoto wao hata wakifikisha umri Mkubwa, imagine unakaa kwako lakini mzazi anataka kukupangia uishije kwenye maisha yako nyumbani kwako, nilishatoa mfano humu Mimi sikuwahi kumiliki baiskeli zaidi ya kudoea kwa majirani lakini Mimi nimemnunulia mtoto wangu yeye anapiga kelele na kunigombeza napoteza hela tena kwa hasira Sana.

Unakuta wazazi wanampangia mtoto wao kuhusu mwanamke wa kuoa wanataka mwanamke/mwanaume wa aina fulani au kabila Fulani, utasikia usije ukaoa mwanamke ambae hana kazi na mambo mengine mengimengi. utasikia wewe umesoma na unaoa mwanamke ambae hajasoma utadhani kwenye ndoa tunaenda kukariri definition na importance,ndio maana vijana siku hizi wanaoana kwanza huko baada ya miaka washazaa na mtoto ndio anaenda kumtambulisha mchumba wake kwa mzazi maana endapo angempeleka kipindi hawajazaa pamoja lazima mzazi angezingua tu utasikia mbona mfupi saana, mbona ana kipara ni kabila gani hilo?

Mzazi mtoto wako akishafikisha umri mkubwa fanya kushauri tu usimuingilie kwenye maamuzi na mambo yake mengine mtaishia kugombana tu na watoto.

Wazazi watoto wakiwa wadogo hata Kama wakikosea tujitahidi tutumie lugha za staa maana kuna maneno ambayo yanakaa kichwani mpaka ukiwa mtu mzima unakua unayakumbuka, mfano nilipokua mdogo mzazi alikua anapenda kunambia nikikosea "bora ningezaa watoto wachache watoto wengine ni hasara tu 😁😁" na matusi mengine ambayo mpaka sasa nayakumbuka bayana.

Wazazi tujiepushe kua wabinafsi yani tuwashilikishe kwenye mambo ya Miradi (tokea wako wadogo) wakiwa watu wazima mtoto anajua nini cha kufanya, tuna wimbi kubwa la graduate wanalalamika hawana mitaji but na hakika ukichukua graduate mia ukawapa million 2 kila mmoja after 5 months ukiwakagua utakuta hawana hata mia wachache sana wataweza kuiongeza hiyo hela.

Juzi natoka shambani kwenye gari nikakaa na kijana analalamika amemaliza chuo na mzazi ataki kumpa mtaji na mzazi anao uwezo wa kumpatia mtoto mtaji, nikamuuliza mzazi anataka nini? Akajibu mzazi anataka arudi nyumbani asubirie ajira, mzazi anamwambia nimeshakusomesha nimemalizana na wewe, hii haijakaa poa wazazi inabidi tupambane tu hold future ya watoto sasahivi elimu sio tena ufunguo wa maisha.

Kingine umaskini sio kitu kizuri umaskini ni mbaya na unadharililisha SIO SIFA kwakua mzazi "ulifight"kupata maisha na umeyapata basi hata watoto nao watafute njia zao za kufanikiwa😁😁, hapana maisha yanabadilika miaka inabadilika kufanikiwa tena kwa "kuhustlle" sio rahisi saana bali ni mfumo na kuna njia za kufanikiwa tutengeneze watoto wetu njia za mafanikio na sio kua mbinafsi kwa kisingizio cha kwamba na wewe ulihangaika kuyapata maisha.

Tunajua wazazi ni Mungu wa pili hapa duniani lakini msifanye mambo ambayo watoto watamchukia Mungu wa pili, mtoto akiwa Mkubwa fanya kutoa ushauri tu auchukue au asichukue ni juu yake, "usiwatreat" Kama vile walipokua watoto wapo kwako, shida yawazazi wengi wana "wajudge" watoto wao kwa past experience labda alipokua mtoto alikua mkorofi, mwizi, anapenda wanawake n.k
 
Hapo kwenye ubinafsi umepiga kwenye mshono. Nakumbuka ubinafsi wa Mzee wetu umetufanya tuishi maisha ya unknown to known kila siku. Tunatumia nguvu nyingi sana kupambana na maisha sema tu elimu nayo imetupa balance kidogo.
 
Hapo kwenye ubinafsi umepiga kwenye mshono. Nakumbuka ubinafsi wa Mzee wetu umetufanya tuishi maisha ya unknown to known kila siku. Tunatumia nguvu nyingi sana kupambana na maisha sema tu elimu nayo imetupa balance kidogo.
Na wazazi wengi wapo hivyo tu, unakuta uwezo kidogo anao lakini anakimbilia kwenye chaka la yeye kupambana kufika alipo so anajitenga kabisa na wewe, lakini hilo swala linatafuna familia pia maana hata kwenye familia hamuwezi kushirikians zaidi ya kua wabnafsi tu
 
Na wazazi wengi wapo hivyo tu, unakuta uwezo kidogo anao lakini anakimbilia kwenye chaka la yeye kupambana kufika alipo so anajitenga kabisa na wewe, lakini hilo swala linatafuna familia pia maana hata kwenye familia hamuwezi kushirikians zaidi ya kua wabnafsi tu
Sana. Elimu ya malezi hawakuwanayo mkuu. Mimi now days nafundisha watoto wangu kila kitu wakione kawaida tu kuliko kuwafichaficha.
 
Back
Top Bottom