Mtu kauza kiwanja. baada ya kupokea hela kagoma kutransfer umiliki wa kiwanja chake kwenda kwa mnunuzi

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
habari wadau.

wataalamu wa sheria naomba majibu yenu.

JUMA anamiliki kiwanja chenye sqm 1200.

amepatwa na shida ameamua kumuuzia AMINA sehemu ya kiwanja chake. kamuuzia sqm 400 na yeye JUMA amebaki na Sqm 800.

wameandikishana kwenye mkataba wao wa makubaliano. kuwa baada ya kupokea hela JUMA ata surrender hati yake ya mwanzo yenye sqm 1200 na atagawanya kiwanja chake ili AMINA apate hati yenye Sqm 400 alizouziwa na yeye JUMA apate hati mpya yenye sqm 800.

mauziano yakafanyika na JUMA akaenda kulipwa pesa zake na AMINA via BANK.

baada ya JUMA kupokea hela zake akamuahidi AMINA wataanza mchakato wa kugawanya hati wiki ijayo.

ghafla JUMA akasafiri kwenda kijijini kwao kwamba ana dharura ya kuuguza mgonjwa.

akakaa huko kijijini mwezi mzima na baada ya kurudi nyumbani kwake amegoma kutoa ushirikiano kwenye kugawanya hati hiyo.

AMINA akaamua kwenda kumfungulia shauri Baraza la Ardhi kata kwamba JUMA amegoma kukabidhi kiwanja alichokiuza na haeleweki sababu ni nini.

JUMA alivyoulizwa kwa nini hafanyi hivyo. anadai aliuza kwa bei ndogo na alikuwa na mapepo ndiyo yalimfanya auze. hivyo anatafuta hela kwa sasa akizipata atamrudishia AMINA hela zake.

baraza la ardhi kata limemuambia AMINA aende akadai haki yake mahakama za juu. Baraza limempa AMINA cheti cha kushindwa kusuluhisha mgogoro huo.

AMINA amechanganyikiwa akamfungulie kesi ya aina gani ? maana kila mtu anashauri kivyake

1. Je AMINA aende baraza la ardhi la wilaya ajkamfungulie kesi ya kudai ardhi aliyouziwa

2. Aende mahakama ya wilaya aende akamfungulie kesi ya madai kwa uvunjanji wa mkataba wa mauziano

3. Aende akamfungulie kesi ya jinai ?

ama aende mahakama gani na akamfungulie kesi ya aina gani ?

wanasheria ni vizuri mkatoa maoni yenu. mtu kama huyu kesi gani ni sahihi kumfungulia ?
 
Kabla ya yote lazima ujue Ana taka nini uyo amina kiwanja au pesa zirudi?
 
Huyo Juma itakuwa ni tapeli mashuhuri na huenda ndiyo michezo yake hiyo. Sijajua utaratibu ukoje kumuuzia mtu kwa kummegea kipande cha kiwanja kutoka kwenye kiwanja kimoja (sqm 1200). Kama viko separate (sqm 800 na sqm400) means kila kimoja kina hati yake so ni rahisi kufanya transfer ya sqm 400. Wataalamu waje kutuelimisha na hili pia.
 
habari wadau.

wataalamu wa sheria naomba majibu yenu.

JUMA anamiliki kiwanja chenye sqm 1200.

amepatwa na shida ameamua kumuuzia AMINA sehemu ya kiwanja chake. kamuuzia sqm 400 na yeye JUMA amebaki na Sqm 800.

wameandikishana kwenye mkataba wao wa makubaliano. kuwa baada ya kupokea hela JUMA ata surrender hati yake ya mwanzo yenye sqm 1200 na atagawanya kiwanja chake ili AMINA apate hati yenye Sqm 400 alizouziwa na yeye JUMA apate hati mpya yenye sqm 800.

mauziano yakafanyika na JUMA akaenda kulipwa pesa zake na AMINA via BANK.

baada ya JUMA kupokea hela zake akamuahidi AMINA wataanza mchakato wa kugawanya hati wiki ijayo.

ghafla JUMA akasafiri kwenda kijijini kwao kwamba ana dharura ya kuuguza mgonjwa.

akakaa huko kijijini mwezi mzima na baada ya kurudi nyumbani kwake amegoma kutoa ushirikiano kwenye kugawanya hati hiyo.

AMINA akaamua kwenda kumfungulia shauri Baraza la Ardhi kata kwamba JUMA amegoma kukabidhi kiwanja alichokiuza na haeleweki sababu ni nini.

JUMA alivyoulizwa kwa nini hafanyi hivyo. anadai aliuza kwa bei ndogo na alikuwa na mapepo ndiyo yalimfanya auze. hivyo anatafuta hela kwa sasa akizipata atamrudishia AMINA hela zake.

baraza la ardhi kata limemuambia AMINA aende akadai haki yake mahakama za juu. Baraza limempa AMINA cheti cha kushindwa kusuluhisha mgogoro huo.

AMINA amechanganyikiwa akamfungulie kesi ya aina gani ? maana kila mtu anashauri kivyake

1. Je AMINA aende baraza la ardhi la wilaya ajkamfungulie kesi ya kudai ardhi aliyouziwa

2. Aende mahakama ya wilaya aende akamfungulie kesi ya madai kwa uvunjanji wa mkataba wa mauziano

3. Aende akamfungulie kesi ya jinai ?

ama aende mahakama gani na akamfungulie kesi ya aina gani ?

wanasheria ni vizuri mkatoa maoni yenu. mtu kama huyu kesi gani ni sahihi kumfungulia ?
Mkuuu mjomba wangu mmoja alidhulumiwa na mtu kama huyu akaenda mahakamani sometimes akaenda takukuru....wakasimamia shoot akapeqa hatiyake....
 
Ulikosea kutoa fedha kabla ya kukabidhiwa hati.
Yaani baada ya muamala Juma akawa anamiliki vyote, fedha na kiwanja, wewe unamiliki ahadi tu!

Ongelea uhalisia. Acha story za vijiweni

hati gani hiyo inatoka kabla ya fedha?

Utaratibu wa hati sio mwepesi kabisa.

Hata kiwanja ukinunua manispaa ama kwa serikali.. hati hupewi kabla ya hela
 
Kwa izo facts Naona Cause of action ni breach of contract so obviously ni Kesi ya madai
 
Kesi ya ardhi ni kesi ya madai. Kwa hiyo baraza la ardhi la Wilaya au Mahakama kuu, depending on the value.
Lakini, Kuna Mambo lazima yawe wazi.

1. Mkataba ulisimamiwa na Nani? Wanasheria, hakimu, afisa mamlaka mapato ... etc ni Nani aliandika affidavit?

2. Ruhusa ya kamishna wa ardhi kama ilihitajika, kwa sababu contract inaweza kuwa null.

3. Kukata kiwanja Kuna taratibu zake na lazima upate approval from planning authority. JE hiyo request ikiwa denied? Hiyo issue ingepata approval kwanza KABLA ya kusaini
 
Kesi ya ardhi ni kesi ya madai. Kwa hiyo baraza la ardhi la Wilaya au Mahakama kuu, depending on the value.
Lakini, Kuna Mambo lazima yawe wazi.

1. Mkataba ulisimamiwa na Nani? Wanasheria, hakimu, afisa mamlaka mapato ... etc ni Nani aliandika affidavit?

2. Ruhusa ya kamishna wa ardhi kama ilihitajika, kwa sababu contract unaweza kuwa null.

3. Kukata kiwanja Kuna taratibu zake na lazima upate approval from planning authority. JE hiyo request ikiwa denied? Hiyo issue ingepata approval kwanza KABLA ya kusaini

1.Mkataba wake ulisimamiwa na diwani wa kata ya eneo ambao kiwanja lilipo

2. Kiwanja chake waliuziana bila hizo requeast kufanyika. Maana huyo juma hizo sqm 1200 alizipata baada ya kurithi kiwanja kilichopimwa na serikali. Kipo kwenye ramani ya mipango miji ya mwaka 1988. Na kina hati ya serikali
 
Back
Top Bottom