Dondoo Muhimu Kuhusu Upimaji Wa Shamba/Kiwanja Chako Hapa Tanzania

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Utangulizi.

Idadi ya mipango miji na vijiji kina kitengo cha upimaji na ramani. Kitengo hiki kimepewa jukumu la;-

✓ Kupima ardhi na

✓ Kutayarisha ramani (survey plan) za miji na vijiji.

Ramani zinazo tayarishwa ni hatua za kubuni, kutekeleza na kuratibu mipango ya maendeleo juu ya ardhi kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Maana Ya Upimaji (Cadastral Surveys)

Upimaji ni mchakato wa kuweka kumbukumbu za ardhi (kiwanja/shamba). Kumbukumbu hizi hunoti mahali shamba/kiwanja kilipo na bila kusahau ukubwa wa ardhi husika.

Kumbukumbu hizo zinahifadhiwa kwa;-

✓ Mchoro kwenye ramani (survey plan),

✓ Mahesabu/namba za ardhi husika (co-ordinates) na

✓ Kuweka alama za mipaka (beacons) katika ardhi husika.

Baada ya hapo ardhi ambayo ina sifa hizi tatu huidhinishwa na kusajiliwa na Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ya Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania.

Majukumu Ya Mpimaji Wa Ardhi (Surveyor).

Moja.

Kuweka mipaka ya viwanja vipya katika halmshauri husika (iwe ni mjini au vijijini).

Mbili.

Kurudisha mipaka ya ardhi ambayo imeshapimwa na mipaka yake (beacions zake zimepotea) imepotea.

Tatu.

Kuchora ramani za ardhi (kiwanja/shamba).

Taratibu Za Upimaji Wa Ardhi.

Afisa ardhi wa wilaya atafanya yafuatayo;- (Baada ya kupokea maombi kwa mmiliki wa ardhi inayotakiwa kupimwa).

✓ Atakagua eneo kuwa ni huru, halina mgogogro wa mipaka na halijaombewa mkopo (yaani halijawekwa rehani).

✓ Atahakikisha ardhi inayotakiwa kupimwa ina mchoro wa mipango miji ulioidhinishwa na Wizara ya Ardhi nyumba na makazi (approved town Plan drawing).

✓ Atahakikisha kuwa ardhi inayotakiwa kupimwa haina upimaji uliokwisha fanyika hapo nyuma kwa lengo la umilikishwaji ardhi (kiwanja/shamba) hiyo.

Hatimaye, Afisa Ardhi kukamilisha ukaguzi wake, mpima wa Jiji atatoa maelekezo ya upimaji (Survey instructions) kwa mpimaji yeyote atakayehusika na zoezi la upimaji.

Baada ya upimaji kukumilika, nyaraka zote huwakilishwa kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani kukaguliwa, kuthibitishwa na kusajiliwa kama kumbukumbu rasmi ya mipaka husika

Ili mmiliki wa ardhi aweze kupewa hati miliki ya ardhi katika wilaya husika anatakiwa kuwa na;-

✓ Kumbukumbu ya mipaka ya ardhi husika,

✓ Mahali ardhi yake ilipo na

✓ Ukubwa wa ardhi yake.

✓ Muhtasari wa kamati ya maendeleo ya kata (uwe umesainiwa na viongozi wanaohusika).

Ardhi ni eneo la juu la uso wa dunia. Ardhi hii ni mali ya Serikali na msimamizi wake mkuu ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ili mtu yeyote aweze kupewa hati miliki ya ardhi yake (kiwanja/shamba), anatakiwa awe na muhtasari wa Kamati ya Maendeleo ya Kata unaodhibitisha uhalali wa ardhi hiyo.

Faida Za Upimaji Wa Ardhi Kwa Taifa Na Mmliki Husika.

Moja.

Hupunguza tatizo la migogoro ya mipaka ya ardhi kwa kusuluhishwa kwa mujibu wa sheria ya Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania.

Mbili.

Huongeza sifa ya kuombea mikopo mbalimbali kwa sababu ardhi imeshapimwa.

Tatu.

Husaidia kurasmisha umiliki wa kipande cha ardhi (kiwanja/shamba).

Nne.

Ni utambulisho wa mahali ardhi (shamba/kiwanja) ilipo.

Tano.

Ni njia mojawapo ya kuongeza thamani ya ardhi husika.

Sita.

Husaidia kupangilia matumizi ya ardhi ili kuchangia maendeleo katika jamii ya wilaya/mkoa/nchi husika.

Kwa ufupi, hizi ndio dondoo za upimaji wa kiwanja au shamba lako katika wilaya unapowekeza. Karibu tena.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Kumekua na tabia ya wapima ardhi kutaka Hela kufika tu kwenye eneo hii Ni changamoto Kwa wananchi

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom