Sagungu 1914
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 930
- 579
Ndugu wanajamii naomba msaada wenu wa kisheria, kuna jamaa tumepelekana kwenye baraza la ardhi la kata baada ya kung'ang'ania kwenye kiwanja Cha familia hii ni baada ya yeye kuja kuomba kukaa pale Kwa muda, tulipo taka kwenda kujenga akakataa kuwa kile kiwanja ameisha pewa na serikali ya Kijiji.
Tukachukua maamuzi ya kwenda kufungua shauri la ardhi kwenye baraza la ardhi la kata ambapo katika shauri lile la usuluhishi baraza lilimuamuru apishe katika kiwanja na tukarudishiwa.
Sasa Cha ajabu anakataa kutoka na anasema humo ndio hatoki tuende kokote. Naomba ushauri wenu wa kisheria Nini Cha kufanya baada ya hapo.
Asante.