Kesi ya ardhi kama hii sheria inasemaje? Mtu kununua kiwanja na kupata hati, ila akafungwa jela na Watu wakavamia kiwanja chake

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,531
Habari wadau

Nina imani humu kuna wataalamu wa sheria za ardhi. Na pia wapo watu wenye uzoefu na mgogoro wa ardhi kama huu wa baba yangu mdogo.

Mwaka 1988 baba yangu mdogo alinunua kiwanja maeneo ya yombo vituka kutoka manispaa ya temeke.

Alilipia malipo yote yaliyohitajika. Na kupewa hati ya kiwanja chake (certificate of occupancy)

Wakati anajipanga kuanza ujenzi mnamo mwaka 1990 akaamua kwenda kwenye kiwanja chake akawa amepanda miti ya miembe.

Akaendelea kulipia kodi za serikali za ardhi.

Mwaka 1994 baba mdogo alipata na kesi ya mauaji... alipigana na mtu kazini kwake bahati mbaya huyo mtu alifariki.

Kesi ikapelekwa mahakamani ikasikilizwa mwishoni kabisa baba mdogo akahukumiwa kufungwa miaka 30. Hivyo akapelekwa gerezani kutumikia hukumu yake.

Mwaka jana december baba mdogo akafanikiwa kutolewa jela. Na kurudi uraiani.

Baada ya kurudi uraiani. Akatuambia ndugu tumsaidie kujenga kwenye kiwanja chake hata chumba kimoja ili apate pa kuishi amalizie maisha yake. Wazo likapita.

Akaenda kwenye kiwanja chake ili aandae mazingira ya ujenzi. Shida kubwa alipofika kwenye kiwanja chake kakuta kuna familia inaishi.

Imejenga chumba na sebule. Na inadai hapo ni kwao wamerithi kutoka kwa baba yao. Ambaye ameshafariki toka mwaka 2013.

Wakamuitia Mjumbe na viongozi wa kata kudai baba mdogo anataka awazulumu kiwanja chao.

Baba mdogo akaeleza stori nzima ilivyokuwa na akatoa na documents za kiwanja chake alizopewa na manispaa ya temeke miaka ya 90. Akatoa hati ya kiwanja certificate of occupancy. Na document ingine aliyopewa wakati ana register imeandikwa certificate of title. Watu kuzicheki zile documents kweli ni halali.

Ile familia iliyokuwa inaishi yenyewe haina document yeyote ya kiwanja zaidi ya muhtasari wa kikao cha familia wakati wa mirathi.

Wanadai hapo ni kwao ila hawajui marehemu baba yao hati zake aliweka wapi. Hivyo hawana hati.

Mjumbe na watu wa kata wamemshauri baba mdogo aende mahakamani.

Maana wao hawamjui. Ila hiyo familia wanaijuia kwa miaka mingi inaishi hapo na hata majirani wote wanatambua kama ndio wamiliki wa hapo.

Na wakasema sheria inammilikisha kiwanja mtu mwingine. Kama ikitokea mmiliki hujakiendeleza kiwanja chako kwa miaka mingi.

Hivyo baba mdogo hana haki maana yeye ndie aliefanya ujinga wa kutoendeleza kiwanja chake mapema. Ama kuwaambia ndugu zake wakiendeleze kwa niaba yake wakati yupo jela

Naombeni msaada wa ushauri wataalamu wa ardhi. Je, mahakamani baba mdogo atatoboa kweli?
 
Mwambie apeleke malalamiko baraza la ardhi kata, baada ya hapo afungue kesi katika baraza la ardhi wilaya na maombi ni kuwa eneo limevamiwa na aiombe mahakama iwaondoe wale watu
 
Nionavyo anaweza shinda....ingekuwa enzi ya Magufuri mapema sana ila hivi sasa atachelewa kidogo na mizunguko itaongezeka kidogo pole ..🤔🤔🤔
 
Sheria ya ardhi inasema hivi mwenye hati ndiye mmiliki wa hiyo ardhi, ningekuwa mimi ningefika na kuboa hiyo nyumba ili wao ndio waangaike kwenda mahakamani.
 
Sheria ya ardhi inasema hivi mwenye hati ndiye mmiliki wa hiyo ardhi, ningekuwa mimi ningefika na kuboa hiyo nyumba ili wao ndio waangaike kwenda mahakamani
 
Anzieni kwenye baraza la ardhi, mkienda Mahakamani bila kuanzia katika baraza la usuluhishi ni msala
 
Asiende mahakamani ,kwanza tambua umiliki unataratibu zake ,baba Ako ndo mmiliki wa awali (tayari kashinda)

Kesi za ardhi hua haziazii mahakamani mojakwamoja ,nikweli division IPO ,ila hatua ya awali mwambie Mzee aende Baraza la usuluhishi ngazi ya Kata .......hao ndo wenye mamlaka ,asijichanganye kwenda huko mahakamani ,na ufunguaji kesi ni 15000 TU......
 
Kesi simple sana hiyo kikubwa ni kupata mwanasheria makini.
Mkuu hiyo kesi sio nyepesi hivyo kama unavyodhania!!kwani sheria ya ardhi ina kipengere kisemacho,endapo mtu atakaa kwenye ardhi kwa muda wa miaka 12 mfululizo hata kama sio mali yake,na majirani wakadhibitisha hilo,hiyo ardhi inakuwa ni mali yake!!
 
Awaambie waondoke kwenye nyumba yake. Hao ni wapangaji wake. Wao ndo waende mahakamani kudai nyumba siyo kiwanja. Mbona wataondoa haraka vibati vyao.

Ila kama mtoa mada hajapindisha.
sheria ya ardhi ina kipengere kisemacho,endapo mtu atakaa kwenye ardhi kwa muda wa miaka 12 mfululizo hata kama sio mali yake,na majirani wakadhibitisha hilo,hiyo ardhi inakuwa ni mali yake!!sio rahisi hivyo mkuu!!ukisikia ile kauli UKITAKA UBAYA DAI CHAKO,ndicho kitamkuta.endapo atachukua ushauri wako.
 
Naomba niwe tofauti kidogo na wengine! Ushauri wangu mumtafutie baba yenu huyo sehemu nyingine aishi. Epusheni huo mgogoro, inawezekana kweli ana haki na anaweza kushinda huko mahakamani lakini akaishia "kushinda" tu! Yangu ni hayo tu!
 
sheria ya ardhi ina kipengere kisemacho,endapo mtu atakaa kwenye ardhi kwa muda wa miaka 12 mfululizo hata kama sio mali yake,na majirani wakadhibitisha hilo,hiyo ardhi inakuwa ni mali yake!!sio rahisi hivyo mkuu!!ukisikia ile kauli UKITAKA UBAYA DAI CHAKO,ndicho kitamkuta.endapo atachukua ushauri wako.

Hakuna hii hebu weka kifungu cha sheria? Hii ni kwenye marejeo tuu. I.e precedent
 
Mkuu hiyo kesi sio nyepesi hivyo kama unavyodhania!!kwani sheria ya ardhi ina kipengere kisemacho,endapo mtu atakaa kwenye ardhi kwa muda wa miaka 12 mfululizo hata kama sio mali yake,na majirani wakadhibitisha hilo,hiyo ardhi inakuwa ni mali yake!!
duuh aisee so haijalishi ulipatwa na matatizo wao wanaangalia tu kipengele cha sheria?????
 
Back
Top Bottom