Kufoji barua ya uteuzi wa kusimamia mirathi ni kosa kisheria na chochote utakachofanya kupitia hizo barua za kufoji ni batili

Apr 26, 2022
64
100
Hii ni kwa mujibu wa uamuzi wa Mahakama Kuu kwenye kesi kati ya Juma Sylvester Mfumia dhidi ya Antony Adabu Mmasy, Rufaa ya Ardhi Namba 68 ya mwaka 2022, kesi ilisikikizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga (nitakwambia baadaye kwa nini nimeita uamuzi wa “Mahakama Kuu” wakati ilisikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi).

UTANGULIZI:

Kwenye hii kesi, kuna mtu anaitwa, Sadick Mfumi, alifoji barua za mirathi (fomu namba nne (IV) ya Mahakama ya Mwanzo), akidai kuwa ameteuliwa na Mahakama kusimamia mirathi ya marehemu Sylvester Mfumia. Kupitia fomu hiyo ikawa inatumika kufanya miamala mbali mbali mtaani ikiwemo kuuza ardhi, na kupata taarifa zingine benki.

Ndugu walipofuatilia Mahakamani wakaambiwa hakuna shauri la mirathi kama hilo lililomteua huyo mtu Sadick Mfumi kuwa msimamizi wa mirathi, isipokua alifoji tu barua ya kuteuliwa kusimamia mirathi ya marehemu.

Sasa kama nilivyosema, hii kesi ilisikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, lakini uamuzi wake una hadhi ya Mahakama Kuu. Na ukisoma jina la kesi, hii ni RUFAA (KESI) YA ARDHI (sio mirathi).

Labda unajiuliza ilikuaje, kesi ya ardhi ikasikilizwa kwenye Mahakama ya kawaida ya Hakimu Mkazi (Resident Magistrate Court)?

Maana kwa mujibu wa sheria za sasa, MAHAKAMA zilizoanzishwa chini ya ‘SHERIA ya Mahakama za Mahakimu’ (‘the Magistrates’ Courts Act’ au kwa kifupi tunaiita “MCA”), ambazo ni ‘Mahakama ya mwanzo (Primary Court)’, Mahakama ya Wilaya (‘District Court’) na Mahakama ya Hakimu mkazi (Resident Magistrate Court kwa kifupi tunaita “RM court)), hazina mamlaka ya kusikiliza na kuamua shauri au kesi ya ardhi.

Rejea sheria iliyoanzisha Mahakama za migogoro ya ardhi, kifungu cha nne, kifungu kidogo cha kwanza (Section 4(1) of the Land Disputes Courts Act [CAP. 216 R.E. 2019]), sheria inasema;

“Unless otherwise provided by the Land Act, NO MAGISTRATES’ COURT established by the Magistrates’ Courts Act shall have civil jurisdiction in any matter under the Land Act and the Village Land Act.”

Kwa ufupi, Migogoro au kesi za ardhi zina Mahakama zake ambazo ni Baraza la Ardhi la Kijiji (Village Land Council), Baraza la Kata (the Ward Tribunal), Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya (the District Land and Housing Tribunal kwa kifupi tunaita “DLHT”), Mahakama Kuu - Kitengo cha Ardhi, (the High Court - Land Division) na Mahakama ya Rufani ya Tanzania (the Court of Appeal of Tanzania). Soma kifungu cha tatu (3) cha sheria hiyo hiyo ya Land Disputes Courts Act [CAP. 216 R.E. 2019]).

Sasa kwa nini hii kesi ilisikilizwa Mahakama ya kawaida ya Hakimu Mkazi?
Tena hii ilikua ni rufaa kutoka Baraza la Ardhi na nyumba la wilaya (DLHT) hivyo ilitakiwa kwenda Mahakama Kuu moja kwa moja. Na inawezekana hata wewe umekuwa ukishangaa rufaa kutoka Baraza la Ardhi la Wilaya (DLHT) zinasikilizwa na Mahakimu kwenye Mahakama za Hakimu Mkazi (RM Court).

Ni kwa sababu Hakimu husika ana mamlaka ya nyongeza au ya ziada (kisheria tunaita Extended Jurisdiction).

Extended jurisdiction ni mamlaka ya ziada ambayo Hakimu aliyeko kwenye Mahakama ya chini (subordinate court) anapewa ili aweze kusikiliza kesi ambazo kisheria zilitakiwa kusikilizwa na Mahakama Kuu tu. Ndio sababu hata hii rufaa kati ya Juma Sylvester Mfumia Vs Antony Adabu Mmasy, ilisikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi.

(Kwa hiyo unaweza kufungua kesi yako Mahakama Kuu, lakini Mahakama Kuu wakatoa amri (transfer order) kesi irudi kule chini isikilizwe na Hakimu mwenye Extended Jurisdiction).

Sasa kwa kuwa hii kesi ilisikilizwa na kuamuliwa na Hakimu mwenye Extended jurisdiction, basi uamuzi wake ni uamuzi wa Mahakama Kuu maana Hakimu mwenye extended jurisdiction akikaa kusikiliza kesi iliyohamishiwa kwake kutoka Mahakama Kuu - anakaa kama Jaji wa Mahakama Kuu, na jengo alilokaa linachukuliwa kuwa ni Mahakama Kuu, hata ukitaka kukatia rufaa maamuzi yake, unaenda moja kwa moja Mahakama ya Rufani.

Na maamuzi ya Mahakama Kuu ni Sheria ndio maana nimeamua hata kuitafsiri hii kesi.

STORI YA KESI (FACTS):

Chanzo cha kesi ni mgogoro kuhusu umiliki wa ardhi au nyumba iliyopo Usagara mjini Tanga ambayo iliachwa na Marehemu Sylvester Mfumia.

Kesi ilianzia kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya (DLHT) Tanga, ambapo bwana Antony Adabu Mmasy alimshtaki bwana Juma Sylvester Mfumia akidai umiliki wa hiyo ardhi (kwamba yeye ndiye mmiliki halali).

UAMUZI WA BARAZA LA ARDHI:

Baada ya kuwasikiliza wote wawili, Baraza la Ardhi la Wilaya Tanga, likampa ushindi mlalamikaji, bwana Antony Adabu Mmasy akatangazwa kwamba ndiye mmiliki halali wa hilo eneo. Baraza likamwamuru Juma Sylvester Mfumia atoke kwenye hilo eneo na yeye au watu wake wasikanyage hapo tena na wasimsumbue mlalamikaji.

Bwana Juma Sylvester Mfumia hakuridhika na uamuzi wa Baraza la Ardhi la Wilaya (DLHT) la Tanga, akaamua kukata rufaa ambayo ndio hii iliyosikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Tanga. Kwenye rufaa yake, bwana Juma alikuwa na sababu sita za kupinga au kutoridhika na uamuzi wa Baraza. (Hata hivyo hazijatajwa zote kwenye uamuzi).

UAMUZI KWENYE RUFAA

Wakati wa kusikiliza rufaa, pande zote mbili zilikuwa na Mawakili. Bwana Juma Sylvester Mfumia ambaye ndiye alikata rufaa (Appellant), aliwakilishwa na Wakili Msomi Ngole Balele, na mjibu rufaa (Respondent) bwana Antony Adabu Mmasy, aliwakilishwa na Wakili Msomi Egbert Mujuni.

Pande zote mbili walikubaliana kwamba kesi isikilizwe kwa njia ya hoja za maandishi. Wote wawili wakawasilisha Mahakamani hoja zao kwa maandishi ndani ya muda waliopewa.

Baada ya Mheshimiwa Hakimu mwenye mamlaka ya nyongeza (Jaji) kusoma sababu zote za rufaa, na majibu ya mjibu rufaa na mwenendo wote wa kesi na hoja za maandishi za pande zote mbili, Mheshimiwa akaamua kuanza na sababu ya tatu ya rufaa.

Sababu namba tatu ya mkata rufaa alikua analalamika kuwa, Mh. Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya (DLHT), alijielekeza vibaya kisheria (erred in law and in fact) kwa kupuuza au kutoupatia uzito unaostahili ushahidi uliotolewa mbele ya Baraza na mashahidi wa msingi wawili wa mkata rufaa, shahidi namba moja na namba mbili ambao walithibitisha mbele ya Baraza kuwa hakukua na shauri lolote la mirathi namba 60 lililowahi kufunguliwa Mahakamani mwaka 2005 na kumteua Sadick Mfumia kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu Sylvester Mfumia.

Wakili wa upande wa Mrufani/mkata rufaa, Miss. Ngole Balele, akawasilisha hoja kwamba, shauri la mirathi namba 60 la mwaka 2005 linalodaiwa kumteua Sadick Mfumia kuwa msimamizi wa mirathi ya Marehemu Sylvester Michael Mfumia, halijawahi kuwepo isipokuwa limefojiwa tu.

Miss Ngole Balele, akathibitisha hoja yake kwa kutumia barua ya Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanga iliyokuwa inasema kuwa hilo shauri la mirathi linalosemwa halijawahi kuwepo Mahakamani.

Akijibu hoja ya kufoji, Wakili wa upande wa mjibu rufaa yeye aliwasilisha hoja kwamba, ni wajibu wa aliyekata rufaa kuthibitisha kuwa ardhi hiyo ilichukuliwa kwa udanganyifu. Akarejea kwenye Kesi ya Omary Yusufu Vs Rahma Ahmed Abdulkadr ya mwaka 1987, ambapo Mahakama ilitamka kuwa, ukileta madai ya udanganyifu kwenye kesi za madai, kiwango unachotakiwa kuthibitisha kinatakiwa kuwa juu zaidi ukilinganisha na kesi zingine za madai ambapo kiwango ni balance of probabilities (urari wa mizani).

“The standard of proof of fraud in civil cases is higher than a mere balance of probabilities”

Mahakama ikasema badala ya Mhe. Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Wilaya kumlaumu mkata rufaa kwa kushindwa kumuita Msajili aje kuthibitisha uwepo wa hilo shauri la mirathi namba 60 la mwaka 2005 kwenye Mahakama ya mwanzo ya Tanga mjini, angeweza hata yeye kutumia mamlaka yake kumuita afisa yeyote aliyepo ili ajiridhishe kuhusu uwepo wa hilo shauri la mirathi.

Mahakama baada ya kupitia mwenendo wote wa kesi, ikasema kwamba kuna barua iliyoandikwa kutoka kwa Msajili wa Mahakama tarehe 12/11/2019 (iliyokua inajibu malalamiko ya ndugu wa marehemu), hiyo barua inafaa kutumika kama kithibitisho au ushahidi (ni relevant).

Barua hiyo ilikua na kichwa chenye maneno yafuatayo “LALAMIKO LA NDUGU JUMA SYLVESTER MFUMIA JUU YA USIMAMIZI WA MIRATHI YA MAREHEMU SYLVESTER MICHAEL MFUMIA.”

Mahakama ikanukuu baadhi ya maneno ya hiyo barua kama ifuatavyo:

“Napenda kukiri kupokea barua yako isiyokua na kumbukumbu namba ya terehe 26 September, 2019, ikihusu mada tajwa hapo juu. Baada ya kupitia barua yako tulifanya ufuatiliaji wa suala lako na majibu yanaonyesha kwamba hakuna shauri la mirathi lilifunguliwa…”

“Ndugu Juma Sylvester Mfumia alifika katika Ofisi ya Hakimu Mkazi mfawidhi Mahakama ya Mwanzo Tanga mjini na kutoa lalamiko tajwa hapo juu kwamba Mahakama ya Mwanzo Tanga Mjini ilimteua bwana Sadick Mfumia katika jalada la mirathi No. 60/2005 na kwamba aliyekua msimamizi mteule wa familia ni yeye Juma Sylvester Mfumia.

Nilipitia rekodi za Mahakama ya Mwanzo mjini Tanga, lakini hakuna rekodi yeyote inayothibitisha kuwa ndugu Sadick Mfumia aliteuliwa kama msimamizi wa mirathi ya marehemu SYLVESTER MICHAEL MFUMIA, katika mirathi namba 60/2005 kama anavyodai mlalamikaji katika barua yake, kimsingi mirathi hiyo haipo.”

Mahakama ikasema kulingana na rekodi hizo, ni wazi kuwa, shauri la mirathi namba 60 la mwaka 2005 halikuwahi kusajiliwa katika Mahakama ya Mwanzo mjini Tanga.

Mahakama ikasema, hakuna shaka kwamba nyaraka - fomu namba IV (nne) inayosadikika kuwa ni Mahakama ndio ilimteua Sadick Mfumia kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu Sylvester Michael Mfumia, (nyaraka hiyo) ilifojiwa. Na kuwasilisha Mahakamani nyaraka iliyofojiwa haikubaliki.

Mahakama ikarejea maamuzi yake kwenye kesi ya Mohamed Athumani Bodo Vs Leila Kalebu Makundi Misc Civil Application No. 114 of 2022, HC at Temeke, ambapo iliamuliwa hivi kuhusu kuleta Mahakamani nyaraka zilizoghushiwa.

“...Kuwasilisha nyaraka ya kughushi Mahakamani haikubaliki. Kudanganya huku ukiwa chini ya kiapo ni machukizo kupita kiasi”

Mahakama ikasema hiyo fomu namba IV (nne) ndio chanzo cha maovu yote aliyofanya bwana Antony Adabu Mmasy (mjibu rufaa). Tukianza na Mahakamani hiyo fomu ilipotolewa, hiyo fomu haina hata muhuri wa Mahakama wala picha ya msimamizi wa mirathi kama inavyotakiwa.

Tuje kwenye benki ambapo kwa kutumia hiyo fomu namba IV (nne) waliyopelekewa, waliweza kutoa hati ambayo ilikua imewekwa kama dhamana NBC Bank.

Tuje kwenye ofisi za ardhi ambapo bwana Antony Adabu Mmasy (mjibu rufaa) alifanikiwa kujiuzia ardhi mwenyewe. Fomu za mauzo zilisainiwa baada ya kifo cha mmiliki. Mahakama haiwezi kutenda uovu wa namna hiyo, au kubariki hayo makosa ya kisheria (illegalities).

Mahakama ikaendelea kusema, huyo msimamizi feki wa mirathi (Sadick Mfumi) anatakiwa kukamatwa na kuziambia mamlaka aliipataje hiyo fomu namba IV (nne) ambayo ilimsaidia mjibu rufaa (Antony Adabu Mmasy) kufanya hayo maovu. Mahakama ikasema kwenye mabano hivi (May God punish them all) ikimaanisha “Mungu awaadhibu wote.”

UAMUZI WA BARAZA LA ARDHI UKATENGULIWA:

Kufikia hapo, Mahakama ikasema imeridhika kwamba hakuna hata haja ya kuendelea kujadili sababu zingine za rufaa zilizobaki.

Mahakama ikatumia mamlaka yake ya mapitio iliyo nayo chini ya kifungu cha 43(1)(b) cha Sheria ya Mahakama za Migogoro ya Ardhi (the Land Disputes Courts Act, kutengua mwenendo na hukumu ya Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya (DLHT) kwa kwa sababu ni batili.

Mahakama ikasema kila kitu kuhusu umiliki wa lile eneo lililokua linagombaniwa patabaki kana kwamba hakuna kesi iliyowahi kufunguliwa kabla. Nyumba au Kiwanja namba 409 Block Z Usagara Mashariki iliyopo mji wa Tanga itabaki kuwa mali ya marehemu Sylvester Michael Mfumia kwa sababu uuzwaji wake kwenda kwa Antony Adabu Mmasy (mjibu rufaa) umegubikwa na udanganyifu.

Mahakama ikamalizia kwamba Nyumba au kiwanja No. 409 Block Z Usagara Mashariki itakua ni sehemu ya mirathi ya marehemu Sylvester Michael Mfumia na inaweza kugawiwa kwa warithi wake. Mahakama ikasema yeyote anayetaka kupinga umiliki wake asubiri mpaka siku ya kupeleka orodha ya mali za marehemu kwenye Mahakama husika.

RUFAA IKAPITA NA GHARAMA JUU. (Mkata rufaa Juma Sylvester Mfumia akashinda rufaa, na Mahakama ikaamuru bwana Antony Adabu Mmasy amlipe bwana Juma gharama za rufaa).

Huu uamuzi ulitolewa na kusomwa tarehe 24/02/2023 na Mheshimiwa Hakimu mwenye extended jurisdiction M. Sabuni, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga.

IMETAFSIRIWA NA KULETWA KWAKO NAMI ZAKARIA MASEKE - Advocate /Wakili).
zakariamaseke@gmail.com
(0746575259 - WhatsApp).
Unaruhusiwa kushare tafsiri hii ya kesi ila usikopi na kuweka jina lako au kubadilisha chochote (heri uanze kuandika ya kwako mpya).
 
IMETAFSIRIWA NA KULETWA KWAKO NAMI ZAKARIA MASEKE - Advocate Pending Admission).
zakariamaseke@gmail.com
(0754575246 - WhatsApp).
Unaruhusiwa kushare tafsiri hii ya kesi ila usikopi na kuweka jina lako au kubadilisha chochote (heri uanze kuandika ya kwako mpya).
Duh! Hapa kuna Jinai au hakuna Jinai!!?? Naomba kuuliza!!??
 
asante kwa ufafanuzi mzuri. naomba kueleweshwa zaidi: Kwanini kesi hiyo haipo kwenye TANZLII? ......maana siku hizi kesi za high Court na Court of appeal zinawekwa Tanzania Lgal Information Institute (TANZLII).

natanguliza shukrani
 
Kesi ilisikilizwa RM (by RM with Extended Jurisdiction)hivyo nafikiri haiwezi kuwekwa kwa haraka katika mfumo wa kimahakama TANZLII kulinganisha na kesi zinazotoka HC moja kwa moja,kama unahitaji nakala ni vyema kumuomba mhusika.
 
Back
Top Bottom