Mtoto wa nje ya ndoa

Mtoto wa nje ya ndoa

Maindainda dada yangu ata siku moja usijaribu kusema icho kitu iyo ni siri yako na ufe nayo na kuzikwa nayo
couse watt wa aina iyo wapo wengi sana'sawa uliteleza iyo sikulaumu pamoja na kwamba ulifanya makosa
je una watoto wengine na uyo mume wako wa ndoa?na kama unao elewa kwamba na hao pia atasema
sio wa kwake na mtafaruku huo utakua ni mkubwa ni mno usije ukafikiria ni kiraisi namna iyo unavyofikiria wewe
WANAUME tuangalie vizuri,gafla tunageukaga mbogo aswa katika mauala kama ayo so u have to take care Maindainda
kama umeelewa reply 4 me
 
Kwa wale wajuao sheria - Kisheria, huyu mtoto ni wa nani?

Kama ni wa Biological father, naweza kufanyaje awe wa kwangu?

Kama alivyoshauri Pundit, hata kama hayupo katika birth certificate, anaweza kushinda kwa kuangalia Vinasaba-DNA, kama ni mtu anaependa fujo au kuna watu hawajali ndoa zao au zimewashinda na wanaweza kutumia chochote ili mke/mume apate EXIT way. Najaribu kuwa mwangalifu hapa.

Kisheria kutembea na mke wa mtu au mume wa mtu ni kosa la madai hivyo kama an guts za kudai mtoto ajue pia kuwa anakabiliwa na civil suit na atatakiwa kulipa fidia kubwa kwa mume mtu.
 
Wahenga walisema kitanda hakizai haramu, hii ni kudhiilisha kuwa tangia zamani walikuwa wanateleza kama ulivyofanya wewe lakini inakuwa siri ya ndani na mara zote uhalali wa mtoto kwa babaye ni mama anayejua.
Kwa misingi hiyo usijaribu kutoa siri hii unless huna tena shida na ndoa yako hii, huyo aliyekupa mimba ni mkware tu na wala hawezi kuwa na sifa za kulea mtoto ambaye mmesha m raise katika maadili na miiko ya upande wababa anaye mlea maintain hivyo hivyo for the sake of your child vinginevyo mtoto ataathirika kisaikolojia na hata akichukuliwa na huyo unaye mpa haki ya u biological father hatakuwa na maisha mema atajihisi kutengwa hata akipewa mapenzi ya namna gani.

Pia usisahau kule nako kuna mke atakayekasirishwa kwa kitendo cha mumewe kuzaa nje hivyo hasira atamalizia kwa mtoto wako!
 
Ndugu na rafiki zangu wa Jamii Forums,

Naomba msaada katika jambo hili.

Nina ndoa ya kama miaka kumi. Nina mume wangu ambae najua ananipenda, nami pia ninampenda. Miaka kadhaa iliyopita nilikutana na jambo ambalo limenitia simanzi sana na sijui hata nifanyeje, kuna wakati siamini kama ni jambo lililonitokea mimi maishani.

Kwa kifupi ni kwamba nina mtoto ambae najua si wa mume wangu! Amelelewa na huyu baba bila kujua kwa upendo mkubwa, kulipa ada za shule na mahitaji yote. Kusema kweli haijakuwa jambo rahisi maana kila anapomuita baba mimi moyo wangu hujaa simanzi. It happenned that I was at a wrong place with a wrong guy and it happenned. Si tabia yangu na wala sikujidhania kwamba siku moja naweza kuisaliti ndoa yangu.

Huyo baba mwenye mtoto ana mke, simpendi kimapenzi na wala hatuhusiani tena, ikiwa ni pamoja na kuwa hajawahi kumtunza mtoto huyu ingawa anaweza. Sikutaka afanye hivyo. Tatizo ni kuna wakati fulani aliwahi kusema kuwa atakuja kumchukua mtoto wake siku moja, kivipi sijui. Naona ana fujo maana sioni uwezekano wa jambo hili labda avunje ndoa yangu kwanza. Sio kutokana na sababu hii ila kwa muda mrefu tangu nikiwa na mimba ile nimetaka kumwambia mume wangu ukweli lakini nimeshindwa. Maisha ya masikitiko na kuwaza jamani naona nashindwa na nataka nimwambie ukweli na atoe hukumu yake.

Naomba mnishauri hasa wanaume- ingekuwa wewe ungefanyaje? Nimwambie au niache?
Hili ni tukio la kweli, naomba ushauri usiwe katika yafuatayo:
1. Kusema kwamba mimi msaliti na mke mbaya-hilo nalijua na wengi wenu mnayajua haya na haitanisaidia sana.
2. Kusema nimefanya ngono zembe nikapime ukimwi - nimepima na sina

Naomba msaada.

Mshahara wa dhambi ni mauti.
Hakuna marefu yasiyo na ncha hata ukunyamaza sasa itakuja julikana tu hata ukiwa mzee kibibi!
Haraka mpigie magoti mumeo umweleze hata akikuacha sasa utapata mwingine, kuliko kusubiri uzeeni utalia kilio cha mbwa mwizi!
Juta dhambi yako ya usaliti na mwangukie mumeo,akikuelewa takusamehe, asipokuelewa utachezea kichapo na talaka.
Be prepared for anything-Hapo nimelipasua jipu usijali.:majani7:
 
Jamani mie naona ishu ni kwa huyu dada ni kweli kama wasemavyo ni UKWELI PEKEE NDIO UTAKAOKUWEKA HURU, but ili upate ushauri halali ambao unaweza kufikia asilimia 56 hivi lazima ueleze mazingira ya nini kilichotokea naona umeweka therusi ya picha weka full picha ili usaidike kuna maswali mengi sana ya kukuuliza lakini unaweza kuyamaliza kwa kutueleza mwanzo mwisho wanaume tunatofautiana sana, but for the time being..in any case kama mumeo ni MKURYA or MAASAI never ever tell him anything ....utajuta
 
Tarajia mambo kuwa mabaya na magumu sana! He will be mad and he will feel betrayed. He will probably loose your trust! The question is how you will get him back! Kwa sababu utakuwa unajua unachokifanya unatakiwa uwe mnyenyekevu na ujitoe kwa ajili ya kuirudisha imani kwake, show him how much you care about him. Vumilia hata kama itakuchukua mwaka au zaidi kumrudisha.
Put aside your proud, your altitude show him it was a mistake and you always wanted to tell him!
Kazi itakuwa ni ngumu lakini hakuna kinachoshindikana when a sincere and humble heart is expressed, hasira zitayeyuka taratibu and after all that EXPECT AN EVEN STRONGER BOND BTN YOU AND YOUR HUSBAND
 
Du am speechless.dada yangu kuwa mwangalifu na uamuzi utakaouchukua.wengi wetu tutasema ingekuwa ni mimi bora uniambie mtoto sio wangu ntakusamehe ila kumbuka sidhani kama kuna mtu humu ndani ameshawahi kutokewa na hili jambo kwahiyo hamna anayejua atakavyolichukulia swala hili.upande mwengine huwa tunachukia mtu anapodanganya na kutuficha jambo kama hili.we unadhani atakusamehe?na akikusamehe ataendelea kukupenda?i think you need proffesional help,hii ishu ni kubwa sana.cha muhimu unahitaji kutubu kwa mungu wako na pia unahitaji ujisamehe kwa kosa ulilofanya.natamani ulivyokuwa na mimba usingemwambia yule jamaa mwengine hii siri ungekufa nayo mwenyewe ila maji yakimwagika hayazoleki.
 
Haiingi kichwani this was more than a one night stand.kawaida kama kweli humpendi huyo jamaa sidhani kama baada ya siku hiyo mngeongea ila mpaka ilifika stage ukamwambia kuwa mimba ni ya kwake lazima mlikuwa na kauhusiano fulani.kwanini ulimwambia?
 
Hivi ni kwa nini mwanaume wa kiafrika akizaa nje ya ndoa inakuwa poa na wala si shida kwake kumpitisha mwanae kwa nduguze kujigamba kuwa amezaa, lakini kwa mwanamke inakuwa kama muuaji?

Mimi nadhani na wanaume muanze kufikiria jinsi wake zenu wanavyoumia mnapowaambia mmezaa nje! They (we) are also human being. Kutembea nje ya ndoa ni one thing lakini ukifikia kuwa na mtoto kwa kweli the pain does not end since the baby keeps reminding of the act (though the poor kids are innocent).

Nadhani hata wazazi wako na ndugu wanaweza kukutenga wakijua umezaa nje ya ndoa kama ni mwanamke ila mwanaume utasikia wanakwambia kamchukue mwanao.

Na hii inanifanya nione huyu mwanaume alozaa na mtoa maada kuwa yuko serious kwa kuwa kwake yeye kumchukua mtoto wala si kazi ni kiasi cha kumwambia mkewe nina mtoto bila hata kuwaza mara mbili kama ufanyavyo wewe mdau. And the woman will stay. But for you m friend; jua wazi ukimwambia mumeo umezini tu hata kama hukuzaa nje kuna uwezekano mkubwa sana wa kupigwa talaka na hakuna wa kukuombea msamaha kwani jamii yote haitakuelewa!

Hence you need to choose either to end your marriage by telling the truth or keep the secrecy for the sake of your family's happiness. Nakwambia hiyo itawa affect hata wanao ambao ni wa kwenye ndoa. They also may be required to take DNA test.

Na hii scandle itamfuata mwanao maisha yake yote. Kuna Prof namjua kila mtu anajua kuwa mama yake alimzaa nje na baba akampa talaka. Kilichomfanya mama ajulikane mtoto alikuwa mwarabu wakati wazazi ni black. SO there was no need of DNA and by then there was no such a thing in TZ.
 
Ujawajua wanaume ndugu yangu. Mkewe atamwambia na hakuna cha ugali wala mboga itakayomwagika. Ni wanaume wangapi wamezaa nje ya ndoa wengine mpaka watoto wanne na bado wako na wake zao?

Wanume wazinzi wala hawaogopi kuwambia wake zao kuwa wana watoto nje ya ndoa! Hasara ni kwa mwanamke tu kwani wanaume wao si watu wa kusamehe kwa suala kama hilo. Hapo ndio mtu unatamani kuua mtu. Maana jamaa limeiba mke wa mtu alafu linataka kuvunja ndoa. Very selfish of him!

Mpige mkwara mzito!

Huyo Jamaa anayo nyumba ya kwake ; I mean ana familia?
Basi muhakikishie kuwa utamwaga ugali akimwaga mboga!
 
Mh. I guess mnafanya kazi ofisi moja. Pole mwaya. Wala sikulaumu, bali nasali sana yasije kunikuta. Ni kweli kukaa na siri kunatesa sana. Eeh Muumba tulindie hizi ndoa. Namuhurumia mumeo sipati picha atakavyojisikia maana mioyo ya hawa wanaume ni kama glass. Nakushauri usimwambie ukiwa peke yako huwezi kujua reaction, anaweza kukuua.

Wana JF,
Naendelea kushukuru kwa ushauri wenu. Bado naendelea kusema kuwa nitasema. Nimetafuta muda muafaka na huu ni mapema mwezi ujao. Sitafuti shahidi wala wazazi, akiamua awaambie mwenyewe watu au akiamua kumlea kimyakimya sawa, au akimkataa sawa, nitamuelewa ingawa nitasikitika mno. Nampenda sana mume wangu na ni mwanaume mzuri, hastahili haya.

Haya mambo hayafichiki kamwe, na hakuna kibaya kama kujua umedanganywa kwa muda mrefu. Siku moja nilielezewa kwa kina hii hadithi, kumbe inafuatiliwa, yuko humu humu JF.

Sitasahau siku moja kidogo nivunje mguu hospitali nikiwahi vipimo vya maabara, na afadhali nilivifuata maana kuna data hazikuwa zina tally kabisa na za mume wangu na hili lingeleta balaa kubwa. Jamani DNA wala sipimi, hakuna siri katika hili, mwana si wake kwa kumzaa ingawa anampenda sana. Sitaki tabu na msongo wa mawazo, liwalo na liwe. kila jambo baya lina repercussions zake and I am ready to face them.
Nimekataa kila aina ya msaada kutoka kwa baba mzazi, atamlea mtoto wake endapo tu baba mlezi atamkataa, kwa bahati mbaya mazingira yanatufanya tuonane mara kwa mara.
 
Nadhani sasa hivi wanaume wengi watakuwa wanapima watoto wao DNA kwa siri kama hizi DNA tests ni accessible maana uaminifu umeshuka sana. Ila kuna watoto wanafanana na wazazi sana so hamna haja ya kupima. Pole tena mdau.

Ila nawashauri wamama wenzangu mnapokuwa kwenye safari za kikazi au masomoni msipende kuwa close na opposite sex ni rahisi kuingia mtegoni. Kwa sisi wanawake you can stay even two years without sex. Ila wanaume hawawezi kwa hiyo ukijifanya kuwa close nao ndio mambo kama haya hutokea wanakuingiza mtegoni. I am far from my family and I spend my time alone working or in social networks like these and sometimes having long walk. Kinga ni bora kuliko tiba. Yes women are strong, but men are smart they know how to get what they want.
 
Swali: Huyo ni mtoto wa kwanza katika familia yenu?
 
Huyu dada ana ufinyu wa fikra, hana hofu na Mungu. Umenichefua na thread lako asubuhi ya leo. Umalaya wako ndiyo umekufikisha hapo ulipo. Sasa linywe. Utamu wa kusema UONGO au kukaa kimya na UONGO utakufundisha kitu kwenye maisha yako, next time utakuwa mwaminfiu kwa wanaokuzunguka na MUNGU wako.

Thread kama hizi asubuhi ni mikosi. GOD have MERCY!
 
ndugu na rafiki zangu wa jamii forums,

naomba msaada katika jambo hili.

Nina ndoa ya kama miaka kumi. Nina mume wangu ambae najua ananipenda, nami pia ninampenda. Miaka kadhaa iliyopita nilikutana na jambo ambalo limenitia simanzi sana na sijui hata nifanyeje, kuna wakati siamini kama ni jambo lililonitokea mimi maishani.

Kwa kifupi ni kwamba nina mtoto ambae najua si wa mume wangu! Amelelewa na huyu baba bila kujua kwa upendo mkubwa, kulipa ada za shule na mahitaji yote. Kusema kweli haijakuwa jambo rahisi maana kila anapomuita baba mimi moyo wangu hujaa simanzi. It happenned that i was at a wrong place with a wrong guy and it happenned. Si tabia yangu na wala sikujidhania kwamba siku moja naweza kuisaliti ndoa yangu.

Huyo baba mwenye mtoto ana mke, simpendi kimapenzi na wala hatuhusiani tena, ikiwa ni pamoja na kuwa hajawahi kumtunza mtoto huyu ingawa anaweza. Sikutaka afanye hivyo. Tatizo ni kuna wakati fulani aliwahi kusema kuwa atakuja kumchukua mtoto wake siku moja, kivipi sijui. Naona ana fujo maana sioni uwezekano wa jambo hili labda avunje ndoa yangu kwanza. Sio kutokana na sababu hii ila kwa muda mrefu tangu nikiwa na mimba ile nimetaka kumwambia mume wangu ukweli lakini nimeshindwa. Maisha ya masikitiko na kuwaza jamani naona nashindwa na nataka nimwambie ukweli na atoe hukumu yake.

Naomba mnishauri hasa wanaume- ingekuwa wewe ungefanyaje? Nimwambie au niache?
Hili ni tukio la kweli, naomba ushauri usiwe katika yafuatayo:
1. Kusema kwamba mimi msaliti na mke mbaya-hilo nalijua na wengi wenu mnayajua haya na haitanisaidia sana.
2. Kusema nimefanya ngono zembe nikapime ukimwi - nimepima na sina

naomba msaada.

mdogo wangu mzuri, naandika kwa herufi kubwa ili kusaidia kuuweka msisitizo ktk jambo hili. Nashauri nashauri tena usije jaribu kusema kwa mumeo maisha ya mtoto akiwa mdogo mpaka akiwa anajitegemea au never on your whole life say this ni hatari kuliko unavyodhani, mtoto atauawa na baba yake anae kaa naye kwani kumbuka gharama anazo pata, pia mwambie huyo baba mwingine kuwa kumbe ulikosea kumwambia kuwa ni mwanae, mchanjie kabisa akitaka kuleta mwambie kuwa hujawahi kuwa nae kabisaaaa, na pia mwambie akitaka akuuwe wewe kuliko kuitenganisha ndoa yako au kusababisha maisha ya mtoto kuwa mashakani, nasikia uchungu sn nikifikiria nini kitatokea kwa mtoto na wewe, siyo rahisi wanavyofikiria wengine, inauma kuliko kidonda chakuchomwa na kisu, usikubali mdogo wangu heri ufe kuliko kusema, na huyo baba mwingine akitaka kukulazimisha useme mwambie aende polisi akaseme au akileta utamshikisha ugoni akafie lupango, mwambie akuache ili mtoto wenu akuwe atajua akiwa mkubwa.
Ni mimi kaka yako.
 
Mmmh makubwa haya!!! Kwanini ulifanya hivyo lakini? Anyway, nakushauri usitoboe siri hiyo kwa mumeo hata siku moja!!! Atakuua wewe pamoja na mtoto...dare not to do so. Chondechonde sister!!!
Ndugu na rafiki zangu wa Jamii Forums,

Naomba msaada katika jambo hili.

Nina ndoa ya kama miaka kumi. Nina mume wangu ambae najua ananipenda, nami pia ninampenda. Miaka kadhaa iliyopita nilikutana na jambo ambalo limenitia simanzi sana na sijui hata nifanyeje, kuna wakati siamini kama ni jambo lililonitokea mimi maishani.

Kwa kifupi ni kwamba nina mtoto ambae najua si wa mume wangu! Amelelewa na huyu baba bila kujua kwa upendo mkubwa, kulipa ada za shule na mahitaji yote. Kusema kweli haijakuwa jambo rahisi maana kila anapomuita baba mimi moyo wangu hujaa simanzi. It happenned that I was at a wrong place with a wrong guy and it happenned. Si tabia yangu na wala sikujidhania kwamba siku moja naweza kuisaliti ndoa yangu.

Huyo baba mwenye mtoto ana mke, simpendi kimapenzi na wala hatuhusiani tena, ikiwa ni pamoja na kuwa hajawahi kumtunza mtoto huyu ingawa anaweza. Sikutaka afanye hivyo. Tatizo ni kuna wakati fulani aliwahi kusema kuwa atakuja kumchukua mtoto wake siku moja, kivipi sijui. Naona ana fujo maana sioni uwezekano wa jambo hili labda avunje ndoa yangu kwanza. Sio kutokana na sababu hii ila kwa muda mrefu tangu nikiwa na mimba ile nimetaka kumwambia mume wangu ukweli lakini nimeshindwa. Maisha ya masikitiko na kuwaza jamani naona nashindwa na nataka nimwambie ukweli na atoe hukumu yake.

Naomba mnishauri hasa wanaume- ingekuwa wewe ungefanyaje? Nimwambie au niache?
Hili ni tukio la kweli, naomba ushauri usiwe katika yafuatayo:
1. Kusema kwamba mimi msaliti na mke mbaya-hilo nalijua na wengi wenu mnayajua haya na haitanisaidia sana.
2. Kusema nimefanya ngono zembe nikapime ukimwi - nimepima na sina

Naomba msaada.
 
najibu kaka mimi mwanaume; mke wangu akinieleza tu NDOA INAFIKA KIKOMO, NO DISCUSSION NAOA KIGOLI MWINGINE. SIPENDI DHARAU. HAKUNAGA CHA KUMPENDA SANA (PLZ NDO NILIVYO).
MAINDA MAINDA!!!
Ninachoona hapo umefikia hiyo hatua si kwa sababu unaumia eti kwa kusikia mtoto akimwita babaye. nadhani huyo baba wa nje ndo anakupa presha. ila sikuona sababu toka mwanzo ya kumwambia yule mzee wa nje kwamba unamimba yake. dah hapa ni mistake....ukiwa ndani ya ndoa, ukipata mimba nje, unakomaa kwamba ni ya ndani.
swali; unamwambia mmeo coz unaumia kutunza siri au unapresha kutoka nje?????
 
haaah...kumbe hii thread ni ya mwaka 2008 duh sikutazama. jamani maindainda rudi jamvini utupe feedback je ulimweleza? bado umechil?
 
Back
Top Bottom