Mtoto wa nje ya ndoa

Mtoto wa nje ya ndoa

Wakuu,
Nawashukuru.
Hii mada nzito na muendelee kujifunza, haiyumkini msipite njia yangu.
Wadau wote wapo humu jamvini, kuelezea kilichotokea ngumu. Sitaki kesi.
Kuelezea kilichojiri ni kama kumuamsha simba aliyelala,si vyema japokuwa ningependa mjue. Humu JF nimegundua kuna wengi walio na matatizo kama ya kwangu.
Nawashukuruni sana kwa ushauri wenu.
 
Wakuu,
Nawashukuru.
Hii mada nzito na muendelee kujifunza, haiyumkini msipite njia yangu.
Wadau wote wapo humu jamvini, kuelezea kilichotokea ngumu. Sitaki kesi.
Kuelezea kilichojiri ni kama kumuamsha simba aliyelala,si vyema japokuwa ningependa mjue. Humu JF nimegundua kuna wengi walio na matatizo kama ya kwangu.
Nawashukuruni sana kwa ushauri wenu.

eh dada maindainda hata hujatwambia kama ushasolve mambo yako unadai wengi tunamatatizo kama yako ,,mamy umejuaje wakati hutujui kabisaa
lakini all the best katika ndoa yako
 
alipokosea ni kumwambia jamaa kuwa ana mimba yake..hata kama akinyamaza ipo siku jamaa ataijia mtoto wake tu..na hapo ndipo itakuwa mbaya zaidi.
 
eh dada maindainda hata hujatwambia kama ushasolve mambo yako unadai wengi tunamatatizo kama yako ,,mamy umejuaje wakati hutujui kabisaa
lakini all the best katika ndoa yako


Fl,
Wameniambia kadhaa kuwa wana ishu kama hii.
Yote katika kusaidiana na kupeana mawazo.
 
thanx maimanda all the best na umwambia huyo baba wa mtoto asikufate iwe mwanzo na mwisho
good lucky
 
Ndugu zangu,
Katika posts za mwisho zinazohusiana na hii thread nilithubutu kusema kuwa - hawezi kamwe kumfuata mtoto. Kwa maneno anayosema ninamuona ana kila dalili ya kumfuata mtoto huyu. Jamani wanaume mkoje? Kwani kama mtoto lazima ukae naye? Hapo ndipo ndoa itakaposambaratika. Kichwa kinauma, nimechoka kabisa, adhabu hii nimejipa mwenyewe
 
Ndugu zangu,
Katika posts za mwisho zinazohusiana na hii thread nilithubutu kusema kuwa - hawezi kamwe kumfuata mtoto. Kwa maneno anayosema ninamuona ana kila dalili ya kumfuata mtoto huyu. Jamani wanaume mkoje? Kwani kama mtoto lazima ukae naye? Hapo ndipo ndoa itakaposambaratika. Kichwa kinauma, nimechoka kabisa, adhabu hii nimejipa mwenyewe

Mpige mkwara mzito!

Huyo Jamaa anayo nyumba ya kwake ; I mean ana familia?
Basi muhakikishie kuwa utamwaga ugali akimwaga mboga!
 
Lakini njia nyepesi zaidi ni kumfahamisha mwenzio; nendeni kwa mchungaji na mkatubu kuiponya ndoa yenu!

Poleni kwa kujeruhiana!
 
Sidhani kama atajali, nadhani ndoa yake imeshamshinda

Basi huyo ni Sadist; anaona au ameamua kukufanya weye ni sababu; yaelekea ulimpa ile kitu tamu kuzidi ya home kwake! Do pole sana!
Basi option B applies; hakuna dawa kama toba; ukitubu unasamehewa!

Tububi nyote kwani wote ni wakosaji na muongozwe sala ya toba na kasisi mnayemuamini mkisindikizwa na wazee wenye hekima wa kike na wa kiume!

Mkitubu mtapona na ndoa yenu itapata amani!
Na mkishasameheana hakuna kukumbushiana wala kujudge using makosa yenu ya zamani!
 
Kweli hapa kama mwanaume niliyeoa, mke wangu akija na taarifa kama hizi sijui, sijui nitafanya nini?? nitatamani dunia ipasuke inimeze nisionekane na wala kuishi na upuuzi wako. Sitakupenda tena sababu tunda langu ambalo linanifanya niwe unique, tunda ambalo linanifanya nitembee kifua mbele, yaani uwanja wangu wa nyumbani wewe umegawa kwa wengine. Hamu ya tendo la ndoa na wewe litakwisha, maana uwanja tayari utakuwa umevamiwa na magugu maji, nitahisi hamkufanya mara moja tuuu, mliendelea tena na tena kwani mlamba ASALI halambi mara moja. Bado ntahisi una wanaume dizaini hiyo wengi tuu, ntahisi hunijali wala kutambua mchango na uwepo wangu kwako. Nitajiuliza kwa nini uliamua kufunga ndoa na mimi ilhali bado una matamanio ya nje! HASIRA zitazidi kunipanda sitataka kukuona tena mbele ya upeo wa macho yangu wala karibu yangu, nitajiuliza siku zote hizi ulikaa kimya iweje leo unakuja KUNIUA na taarifa hii. Sitaweza kukupiga wala kukutukana ila nitahitaji unujibu maswali yangu kwa ufasaha. 1/ kwa nini ulilala na huyo mwanaume ilhali ukijua wewe ni mwana NDOA? 2/Ulikosa nini kwangu mpaka utoke nje ya NDOA 3/Kama ulishikwa na hamu ya GHAFLA kwa nini hukunipigia simu mie hata km umesafiri ningeweza ongea na wewe nikakupa ushauri wa kufanya na ukaepuka matamanio. baada ya hayo sasa itabaki kichwani mwangu maswali yasiyo na majibu kibao tu. kama aliweza vua nguo akapanda kitandani jamaa akammega kwa ridhaa yake, hatashindwa tena kunisaliti huyu. alilifurahia hilo tendo ndo maana miaka yote hii alikaa kimyaa!! Huyu hana tofauti na muuaji, fikiria (if) jamaa angekuwa na NGOMA, leo hii si ningekuwa na GRIDI ya taifa. Nikiendelea kuishi naye ikitokea kutoelewana tu na mimi ntahisi ataenda kwa yule jamaa yake akampe pumziko, au ntajua jamaa anampa kiburi. Kwa kweli MAISHA yangu yote utakuwa umeyaharibu!! hakutakuwa na raha tena ya MAISHA, NDOA itakuwa NDOANO, na mwisho wetu utakuwa hapo. NI KHERI LAWAMA KULIKO FEDHEHA

MY TAKE
SIKUSHAURI CHOCHOTE- ila kwa mwanaume MKE ni KIDONDA, kwa hiyo jitayarishe kwa lolote hata kulimwa RISASI(SIKUTISHI)
 
Dada, ulishawahi kujiuliza mumeo ana siri ngapi moyoni ambazo hajawahi kukuambia?? Wala usitake kuzijua! Utamuumiza mtoto wako, manake labda yeye anao watoto 5 nje already so this may not be news!. Endelea kuumia na hiyo siri yako mpenzi, ndo adhabu yako ya kuzini. Tubu ki-ukweli Mungu akusamehe! u don't need to go and confess kwake!
Guys, have you ever imagined kama wanaume wangekuwa ndo wanabeba mimba hiyo familia ingevyokuwa na watoto wachina, wadhungu, wahindi heheheheeh!Mungu!!, namshangaa siku zote!
 
Chimunguru umemfuatilia Dada toka mwanzo?; jamaa ndiye alianza kumtenda na mbaya zaidi hakutubu kiuhakika na dada yetu roho ikamwuma na ibilisi akammeza; hata sisi yanatutokea haya usikimbilie kuchukua mihasira tuu wakati pengine weye ndo sababu!

@ King'asti unamtakia kifo cha shinikizo la damu mwenzio; she has to come clean I'm telling you; huyu hakumsamehe mumewe toka moyoni ndio maana akatoka na kulipa kisasi! sasa pamoja na kutubu anahitaji kusamehewa hata kama hii ndoa itakwisha kitu amabcho sikitegemei kwani both parties are guilty!
 
DADA PLZ DO NOT TELL HIM U WILL REGRET ALL UA LIFE........LET NATURE TAKE IT'S CAUSE.....ATAKAPO JUA EITHER HUYO MUMEO AU MTOTO NDO HAPO UTAJUA JINSI YA KUJIELEZEA.......PLLZ USIMWAMBIE PLZ.....UTAJUTA DADANGU....PLZ PLZ MUME SAWA ANAKUPENDA LAKINI HATOKUSAMEHE NAKWAMBIA SIMSEMEI....LAKINI NDO HIVYO....nyamaza endelea tu kuishi till further NOTICE.:fencing::mad2::rant:
 
Back
Top Bottom