1. Hana uhalali wa mtoto mwanamme yeyote nje ya ndoa yake ya halali
2. Na anapobambikwa au kujibambika mtoto mwanamme pasipo na ndoa ya halai hata kama atakubaliana
na mzinifu mwenzake( mfano kama katika maisha ya unyumba bila ya kuwepo ndoa halali) basi ndio pale
jina la "mtoto wa haramu (bastard)" ndipo humuangukia yule mtoto. Maana yake ni mtoto wa baba wa
kubandikiwa.
3.Katu mtoto hawi haramu kwa mama yake. Atakuwa wa zinaa pale yule mwanamke hayupo kwenye ndoa,
lakini akiwa katika ndoa halali, basi baba wa mtoto ni mume tu, si vinginevyo kama suala lile limebakia
absolutely ndani ya moyo wa yule mwanamke.
4. Litabakiaje tu ndani wa moyo wako???. Hii itawezekana tu ikiwa zinaa ilipita kiajali/accident kwa mfano
rape ambapo akijitokeza mwanamme(rapist) au akitambuliwa na victim baada ya vyombo kufanya kazi zao
ipasavyo na rapist ku-confess, basi adhadu inayostahili hupewa yule rapist tu sio victim, kifo!!!
5. Katu hawezekani mwanamme kujua uingiaje wa mimba, potelea mbali kujua mimba ile ni kutokana na
yeye kama ilikuwa ni ajali tu, hapa kuna namna!!! Haya ni mawasiliano na maridhiano ambalo ni kosa jipya
mbali na kitendo cha zinaa chenyewe, na ndio mtego mkubwa uliyojinasisha wewe.
6. Upumbavu wa mawasiliano na makubaliano ya namna hii pengine sijui kama hukuwahi hata kumsimulia
shoga yako mama nanihii. Kama umefanya hivyo basi ni mtego mwengine huo na kosa jipya la tatu.
7. Ni haramu kujifaharisha kwa maovu yake mtu, kwa maana safari ya kujikwamua huwa complicated. Kama
hapa wewe ulikuwa na kosa mbele ya Mwenyezi Mungu tu kwa kitendo cha zinaa, na kingekuwa kitendo
cha nobility (heshima kubwa) kwako kama ungekuwa humo ndani ya ndoa, yaani hujaolewa kukataa na
katu kutomtaja yoyote kuwa ndio uliyezini nae, hata huyo jamaa. Na hata kama adhabu ingekufika kwa
maana usingekuwa na njia isipokuwa kukubali kitendo cha zinaa tu peke yake kwa maana mimba ingekuwa
wazi. Lakini hapa Mwenyezi Mungu alishakuhifadhi kwa kukujaalia kuwemo ndani ya ndoa, nini
kilichokupelekea wewe kuutawanya na kuudhihirisha uchafu wako??? Ametakasika Mwenyezi Mungu, ni
wewe mwenyewe.
8. Hata hivyo, bado una nafasi ya (1) kuzuia kusababisha fitina hapa ulimwenguni na (2) kutubia kwa
Mwenyezi Mungu, sambamba na (3) kumuomba msamaha mumeo ili upone na adhabu ya huko akhera.
Haya yote yako mikononi mwako. Lakini lazima uwe very sincere, very sincere kama unavyoanza kuonyesha
hapa. Na wala usijidanganye hata siku moja kwamba haya yataishia hapa duniani tu, kwa maana huo ni
mtego mwengine wa kishetani ambao ukiuingia ndio basi tena, moto huooooo, unakusubiri. Hili ni lazima
kesho akhera lifike. Ila ninaloelekea kukushauri mwisho wake utakuwa ni kwamba kama utafanya vizuri
katika kipengele na. 3 basi mumeo atasafisha moyo wake hapa hapa duniani na atatengeneza huruma
juu ya mkewe hapa hapa duniani ili ziwe ndio nguvu zake za kusimama na kumtetea mkewe juu ya jambo
hilo dhidi yake huko kesho mbele ya haki. Ama kipengele no. 1 na 2 ni rahisi kuvitekeleza. No. 1 kinahitaji
majuto, ujasiri, utulivu na No. 2 kinahitaji sincererity
1. Kuzuia kusababisha fitina hapa duniani:
- Never ever speak, hata salamu, hata kumtizama njiani huyo jamaa, ikitokea jicho halina pazia na
kumuona basi geuza macho chini na upite na zako, maisha na milele mpaka uzoee hivvo. Never
kujibu salamu yake sembuse kuzungumza nae.
- Kumbuka ni makosa haramu kumuambia mtoto jambo hili, na wala SIO HAKI YAKE kama
wanavyodai baadhi ya wengi eti mtoto kulijua. Nani ana haki ya kudhalilishwa???
2. Kutubia kwa Mwenyezi Mungu:
- Hili ni rahisi kidogo. Linajumuisha (a) kusitisha mara moja kosa, (b) kujutia kosa lako lile
(c) kutia nia katu kutofanya tena (d) kuomba msamaha (hapa ni M.Mungu na mumeo) na
(e) kulipa fidia kwa waathirika na kosa kama ipo (hapa haipo zaidi ya kumtaka radhi mumeo,
kumbuka yule jamaa hatambuliki kisheria na familia na ndoa yake viko safe). Ni familia yako
wewe, integrity yako na ndoa yako ndio viko maweni hapa. Hivi vipengele a, b, c, d, e ni lazima
vipambwe na SINCERERITY, SINCERERITY, SINCERERITY.
Kumbuka, japokuwa usisafirie hili, kwamba weeeengi watakaokwenda kesho akhera na mazigo
mazito zaidi ya hayo ya kwako.
3. Kumuomba msamaha mumeo:
- Ni lazima umtayarishe kwa muda mrefu, hata ikiwezekana matayarisho ya muda sawa na
maisha mliyoishi kama mke na mume au kiasi cha kuwa mzoefu mahiri wa vipengele No. 1 & 2 hapo
juu ili apokee vizuri maombi yako. Kwa kifupi badilika kitabia to his appreciation.
- Msamaha wako uwe sambamaba na SINCERERITY yako hapo juu ya kwamba unamuomba huruma
yake kama mumeo kwanza kwa kumdhalilisha yeye na pili kujidhalilisha wewe mwenyewe na
kwamba katika yote hayo wewe ndio msababishaji. Hivyo akuhurumie kwa mateso yanayokusibu
moyoni mwako kwa maisha yote haya, na vile vile akusaidie katika kukamilisha kuutafuta msamaha
wa Mwenyezi Mungu ili uokoke na adhabu ya moto.
- Ni vizuri ukawa unahadithia baadhi ya sifa za matukio matukio yaliyojiri katika muda wote wa
maisha yenu ambayo mmeishi pamoja yanaashiria heshima, mapenzi na matukuzo juu yake kama
mumeo ukiondosha kosa hilo, na kama kuna practical tranformation umepitia kuelekea hapo.
- Ikiwezekana iwe usiku mwingi kidogo watu wote wamelala
Kila la kheri, anza sasa