Dah pole sana dada....mm naona hapo kwa jinsi wanaume walivyo ni bora ubaki na siri moyoni usimwambie itakuathiri wewe pamoja na mwanao....sio wewe tu walio wabambikia watoto wanaume zao.
Kwa hiyo wewe vumilia tu weka siri moyoni mpaka mtoto atakapo kuwa na kuanza kujitegemea ndipo utamwonyesha baba yake na sio sasa hivi.Ukisema ukweli utakuja kuumia tena sana...utatengwa na ndugu pamoja na jamii inayo kuzunguka.
Naongea hivi kuna binamu yangu imemtokea kama wewe akamwambia mwanaume ikawa balaa akaambulia kuachika na sasa hivi anatanga tanga tu na ndugu wamemtenga kabisa vile vile jamii inayo mzunguka inamwona mtu wa ajabu wanaona kama ni kosa kubwa sana.
Lakini angeweka siri moyoni yote haya yasingetokea na angeishi na jamaa kwa raha mstarehe....si mnajua ukweli unauma kwa hiyo pindi usemapo ukweli uwe tayari kubeba lawama,kudharaulika na mengine mengi.Ni bora uacha tu na uweke siri moyoni watu wasijue kabisa.
Hakuna kitu kinacho uma kama kujua.....sasa usitake hii ikutokeee wewe weka siri jamaa aendelee kuhudumia na mtoto aendelee kumwita baba ingawa ni wa kambo.Ukimwambia tu jamaa itamuuma sana na itaweza kukuathiri wewe na mwanao hapo nyumbani wewe chuna tu imradi maisha yanasonga mbele.
Pole sana endelea kuweka siri moyoni.