Mtoto wa nje ya ndoa

Mtoto wa nje ya ndoa

Huhuhumu ndani, maisha magumu wewe na kila mtu na siri yake. Sijui nifanyeje, kila kukicha ninawaza hii dilemna

Mainda asante kwa email. Mimi nilidhani hili limeshakwisha lakini naona limerudi tena na najua jinsi unavyoishi kwa kihoro cha kujua huyo jamaa haoni vizuri ukiishi kwa raha. Mimi nakushauri ni bora uondoke tu hapo ulipo pamoja na kuwa unapapenda sana lakini huna namna ila ni kuondoka tu kama bado hujafanya hivyo na huko uendako iwe ni siri kubwa ili asipafahamu na kutopata muda wa kukusumbua.
 
ehee maindainda, tell us, what happened then? au ndo umeshatoweka baada ya tukio?, lete majibu ilikuwaje ili watu wengine humu wajifunze....
 
Endele kutubu kimoyo moyo kama hilo limetokea.

Kama wampenda mumeo na wampenda pia mtoto ni mbaya kuliko jambo jingine lolote kama ikitokea leo Mumeo anajua kuwa mtoto sie wake na sidhani ni rahisi kihivyo kuamini pia hao wengine ni wake (kama wapo au watatoke).




Hakuna mtu anayefika duniani pasipo kuandikwa na Mungu. Maumivu unayopata rohoni ni yako tu lakini yatakuwa yako, ya Mumeo na Mwanao pindi utakapodiriki kubwatuka jambo hilo na sikio la Mumeo liipata. Labda kama huyo baba aliyekuzalisha kafa, lakini kama yupo tegemea lolote laweza kutokeakama ifuatavyo:
  1. mumeo kukosa imani na wewe milele.
  2. Mume kuanza kutembea nje nae kama alikuwa hafanyi hivyo.
  3. Mume kumchukia huyo mtoto na kuona anahudumia kiumbe ambacho amebambikiwa.
  4. Mume kukufukuza hapo na huyo mtoto.
  5. Mume kumletea vurugu huyo mwanaume ulie zaa nae na hilo kuatarisha ndoa ya huyo mume na yako pia.
  6. Mtoto kukuchukia daima kutokana na kuficha siri hiyo kuu.
  7. Huyo Mwanaume uliyezaa nae kama akikataa kwa kuogopa kuvunja ndoa yake, utajikuta kwenye msukosuko mkubwa wa kifamilia na huyo mume, mkewe,mumeo, mwanao, familia na majirani.
  8. Hata Mumeo akikusamehe, bado ikiwa mtoto akijua huyo si baba yake anaweza kufanya lolote hata kumtafuta huyo baba uliezaa nae na hapo ndo itakula kwako kama mke wa huyo mwanaume hajui hilo.
  9. Ndugu pia kama walikuheshimu watakudharau na pengine kuchochea uachike au mtoto apelekwe kwa baba yake kwani mumeo ataonekana "Bushoke" kwa kule damu ya mwenzie kwa muda wote huo.
  10. Kama Mume hana roho ngumu anaweza hata kujiua, kuua mtoto na wewe pia kwa aibu na hasira ya kubambikiwa na kufichwa ukweli kwa muda wote huo.
Fikiri tena na tena ni afadhali uwe mvumilivu hivyo hivyo mpaka mtoto akioa/kuolewa a utakuwa mbali nae na hiyo huzuni yako inaweza kupungua. Kama usingeweza kumweleza mumeo kuwa umemegwa na jamaa kama isingekuwa ni huyo mtoto, basi kwa kuwa umeweza kuficha hiyo siri muda wote huo, we endelea mpaka ufe nayo kwani mbona wenzako wengi tu wanatuficha na kutubambikia?? kama dhambi basi ushaitenda na haiwezi kufutika kwa kumweleza Mumeo ukweli kwani bado utakuwa hujamsaidia huyo mwanao, utamtika katika mitihani mizito sana katika maisha yake kwa kuto amini yupi ni baba yake. Kama (utamkosa huyo milele). Mwache aendelee hivyo hivyo bana kwani wote wanaoita baba ni lazima awe amemzaa??

Vinginevyo madhara yake ni makubwa kuliko hayo unayofikiri.Ukishindwwa kabisa mpeleke akaishi mbali nanyi ili usisikiea akiita Baba jambo ambalo linakuumiza roho.
 
au ndo kishatutoka/katangulia mbele ya haki baada ya tukio, mbona haji hapa kutupatia updates.....
 
au ndo kishatutoka/katangulia mbele ya haki baada ya tukio, mbona haji hapa kutupatia updates.....

quote_icon.png
Originally Posted by Maindainda
Jamani mtanisamehe jamaa yupo humuhumu JF, details za kutoa nitachagua


Kama si weye Mzee UBUNGOX2 ambaye kisa kina kuhusu, basi Maindax2 hayupo serious na kisa chake! toto fix! ahaaaa! kazi kweli.
 
Mimi niliwahi kusikia case kama ya kwako kutoka kwa dada wa Ki Nigeria
Angalia kama ushauri huu aliofanya yy kama utakufaa.
1.Kama una muda na uwezo wa kutafuta solution ya sehemu ya kuishi ya kwako-tayarisha makao mapya kabisa,ukijua kubwa analoweza kukufanyia mumeo ni kukufukuza kama sio to kill you-depending na level ya akili yake.
2.hakikisha uko tayari kwa kila kitu, muite mumeo somewhere umuulize kama ulivyotuuliza sisi kuwa je ingemtokea yeye ingekuwaje
3.Akiishakupa jibu lake ndio utaamua umuambie i.e kusudi ukae nae au uhame kabla ili atakapokuuliza kilichokutoa kwake umuambiekuwa ni jibu alilokupa.
Ukiniuliza mimi ningefanyaje, ningemuita huyo bwana mtia mimba nikamuuliza kama anamtaka mtoto basi amch
ukue na kama hamtaki basi ninam adopt na wewe nakuchukulia kama % kubwa ya wanawake walivyo, ni wangu nikiwa na wewe. Najua mvutano unaokuwepo mwanamke anapokuwa kwenye kipindi cha kupewa mimba -sio makosa yako kabisa hata asingekuwa huyo mkatili ala bla bla...... , ungeangukia kwa mwingine tu. Angalia kama inaweza kuwa njia ya msaada kwako.
Katabazi.
 
Mimi niliwahi kusikia case kama ya kwako kutoka kwa dada wa Ki Nigeria
Angalia kama ushauri huu aliofanya yy kama utakufaa.
1.Kama una muda na uwezo wa kutafuta solution ya sehemu ya kuishi ya kwako-tayarisha makao mapya kabisa,ukijua kubwa analoweza kukufanyia mumeo ni kukufukuza kama sio to kill you-depending na level ya akili yake.
2.hakikisha uko tayari kwa kila kitu, muite mumeo somewhere umuulize kama ulivyotuuliza sisi kuwa je ingemtokea yeye ingekuwaje
3.Akiishakupa jibu lake ndio utaamua umuambie i.e kusudi ukae nae au uhame kabla ili atakapokuuliza kilichokutoa kwake umuambiekuwa ni jibu alilokupa.
Ukiniuliza mimi ningefanyaje, ningemuita huyo bwana mtia mimba nikamuuliza kama anamtaka mtoto basi amch
ukue na kama hamtaki basi ninam adopt na wewe nakuchukulia kama % kubwa ya wanawake walivyo, ni wangu nikiwa na wewe. Najua mvutano unaokuwepo mwanamke anapokuwa kwenye kipindi cha kupewa mimba -sio makosa yako kabisa hata asingekuwa huyo mkatili ala bla bla...... , ungeangukia kwa mwingine tu. Angalia kama inaweza kuwa njia ya msaada kwako.
Katabazi.


Asante kwa ushauri. Ila sasa unawezaje kum adopt mtoto Tanzania wakati baba yake anaishi? Yani anakubali kukupa tu? Ila kwa wababa wengine wa kiafrika hiyo ni poa tu ndio maana watoto wengi wapo mtaani wanaokota makopo.
 
Kama si weye Mzee UBUNGOX2 ambaye kisa kina kuhusu, basi Maindax2 hayupo serious na kisa chake! toto fix! ahaaaa! kazi kweli.

Siyo fix bwana haya mambo yapo mengi kuliko unavyodhani, tangu enzi za baba na babu zetu.......dunia duara
 
Asante kwa ushauri. Ila sasa unawezaje kum adopt mtoto Tanzania wakati baba yake anaishi? Yani anakubali kukupa tu? Ila kwa wababa wengine wa kiafrika hiyo ni poa tu ndio maana watoto wengi wapo mtaani wanaokota makopo.

Kwa maelezo yako,huyo baba #.2 ana haki zaidi ya 75% kum adopt wala hilo kwamba baba yake anaishi sio tatizo na inakuwa rahisi zaidi kwa sababu anajulikana mpaka jina na kuwa yu hai.Hao wanaookota makopo wala si wote wako kama huyu wa kwako,wengine wazazi wao wako kwenye ndoa safi za kikristo/kiislamu ila wana yao ambayo ni madogo zaidi. All the best mamiiiiiii.
 
dawa ni kurudisha mtoto kwa baba yake na wee kuomba radhi

ullifanya makosa makubwa sana kumficha mumeo
na haya ndo malipo yake. hutaona furaha maishani.
 
unavyo ishi sasa ni adhabu ya tendo ulilolifanya na utakavyo ishi baadaye yaani baada ya kumwambia ukweli mume wako pia itakua adhabu vilevile.....so kama usha zoea maisha hayo... basi jisahaulishe.... na huyo jamaa ulozaa nae mwambie aache fujo
 
Da Sophy, soma vizuri mada kabla hujachangia. sijasema simtaki mume, bali huyo mwingine, na nina maana yangu ninaposema hivyo, najua ninachokiongea
Kumbe unamaana yako unaposema humpendi lakini moyoni yaelekea bado unampenda, ndiyo maana inakuwa vigumu kupokea ushauri. Basi nenda kawe small house
 
Sina cha kuchangia dada yangu zaidi ya kusema pole, na Mungu akutangulie katika kutatua tatizo lako. Wapo wanawake wengi wapatao mikasa kama yako. Ninaamini Mungu atakusaidia.

Endapo Mumeo ana moyo na akili kama zangu (well, huzifahamu) basi apatapo taarifa kama hii anaweza kufanya yafuatayo, maana watu kama sisi wenye uelewa mdogo, wenye kupenda na kuamini kuwa tupo pekeyetu hufanya:

1. Namuomba Mungu hapohapo aniue, maana I will never ever forget. Siwezi omba Mungu akuuwe wewe, au mimi nikuuwe maana kubaki kwangu duniani bado kutanifanya niwaze sana. Better nikikuuwa nami nijiuwe
2. kama Mungu hataniua, nitaomba ukichaa, hapo hapo...niwe kichaa maana aibu kubwa, machoni mwangu, moyoni mwangu....umenidhaharu, maana watu kama sisi wenye uelewa mdogo tunaamini dharau kubwa duniani ni mwenzako (mume au mke) kutoka nje ya ndoa.
3. Kama 1 na 2 itashindikana, Basi Nitajitaidi baada ya kunisimulia nitakuaga kuwa nipumzike maana usiku au asubuhi nitajiua.

Binafsi, sitoki nje. Sifahamu kuhusu mke wangu...na kama anatoka basi nisifahamu milele

Inawezekana wanaume wenye tabia (uelewa mdogo) kama zangu nipo peke yangu
 
Baba mkubwa; I feel your fear! Very touching argument you have here!

Lakini huoni ikiwa mmezaa tayari kuwa unawajibika kwa hao watoto pamoja na huyo; ni wako! God has mysteriuos way na our ways are not his way! Endelea kumuomba Mungu akusaidi kuliewa hilo!

Kujiuwa ni chukizo mbele ya Mungu hutakuwa umesolve chochote!
 
Baba mkubwa; I feel your fear! Very touching argument you have here!

Lakini huoni ikiwa mmezaa tayari kuwa unawajibika kwa hao watoto pamoja na huyo; ni wako! God has mysteriuos way na our ways are not his way! Endelea kumuomba Mungu akusaidi kuliewa hilo!

Kujiuwa ni chukizo mbele ya Mungu hutakuwa umesolve chochote!
Mkuu Maskini_Jeuri...Bahati mbaya jinsi nilivyo siwezi kuishi na taarifa niliyopewa na mke wangu kuwa mtoto huyu si wako, ni wa yule. Mkuu Maskini_Jeuri, ninakili huu udhaifu nilionao ndio ulionipelekea uamzi wa kutokuwepo kabisaa dunia maana I can not hold it. Ninaamini kuna wanaume wanaoweza kabisa kumuelewa mke na wakatatuwa na wakaendelea kuishi, but not me.....Ningependa niwe kama wao, lakini siwezi kuwa kama wao.......As soon as I hear from her, naamini I will either be mentally sick (Fully) au dead body...naongelea nilivyo mkuu maskini_jeuri...............To me, kama ni mke wangu wala asiniambie, tena wala nisijuwe.....
 
Kama aliyosema huyu mwanamke ni kweli I stand in the advice of you,asimtell maana hata ingekua ni mimi nisingeelewa na hata yule mtoto mapenzi nayompa sijui kama yasingkuwa tofauti baada ya kujua hili eithe positively au negatively.ila usirudie we mwanamke ni usaliti uliozidi humanity to the so called your beloved husband.

GET THIS VERY CLEAR AND TAKE IT VERY SERIOUSLY:


1. Mimi ningekuwa huyo mtoto unayemuogelea hapa... Nisingependa kumjua BABA zadi ya yule niliyemuona pale nyumbani. Yule aliyenipeleka shule. Yule aliyenipa feelings and emotional of care and all the attention. Singejali what my DNA constitutes etc. Leo hii Mama yangu akija na kuniambia kuwa The father I have been staying with, mpaka ni kawa mtu mzima sio Baba yangu kwa sababu tu ya DNA..nitamuona 'Mama is stupid'. Who cares about the DNA? Baba sio chemicals..which make the DNA ni UTU alionipa na kuutumia kunijali, kunipa mapenzi na kunilea..

2. Kutokana na Maelezo yako. Honestly speaking MOYO wako haukumsaliti Mumeo. Ila It was only feelings, emotions and your beautiful body... Sioni mahali ulipokuwa na kisasi cha NGUVU kwa Mumeo (ambayo hiyo ndio mbaya)... Kwa wanawake wengine They feel very very good wanapo_MSANIFU mume akiitwa Baba na Mtoto asiye wake..They Feel..”MSHENZI NIMEMUWEZA” etc..and you know that is evil...Wewe sikuoni hapo....DEEP IN YOU BADO MNA NDOA NA MUMEO...watch that...!!. Wanaume wa Kweli wanachohitaji kwa Mwanamke .."SIO MWILI KWANZA" ila “MOYO....” Kila mwanamke anaweza kunipa mwili wake but vigumu sana kuupata MOYO wake. Kama Mke wangu kabakwa...hakutoa moyo wake...kwa hao washenzi..Nasimama naye . Namtetea kabisa..... Lakini kama kwa akili timamu...kaamua kujitoa that is different story. Kama alipanga kabisa hiyo Game na kuwa fascinated nayo..hapo hatutelewana. Si unaona case yako? you was simply arroused on the ovulation day......So jua kuwa Bado una clear BOND na mumeo. Huhitaji kumvuruga. dont tell him. Haina maana yeyote...And don’t do it again….Yaani Kosa hilo...dont repeat. How?

3. You know why it happened? Maelezo yako yanatosha kabisa kujieleza. I tell you ni kitu kilikuwa kimjificha ndaniyako."Uncosciouse"

Go into your Past. Utaona kuwa kilichotokea na huyo bwana uliyezaa naye nje ya ndoa ni MARUDIO. Ni replay!!!

Yaani...tukio karibu kabisa na hilo limewahi kutokea huko nyuma. Kivipi?

Umeshawahi kurelate na mtu kama huyo..au karibu kumfanania huyo. Au hiyo enviroment uliyojikuta unakuwa helpless na ku_yield...Imejirudia..yaani inafanina au karibu kabisa ...na hiyo uliyojikuta.

AU:

Umekuwa na chuki kubwa sana na huyo bwana au mtu kama huyo..yaani una mchukia mtu mpaka ..unajikuta sexualy attracted..It happens many times..na dunia inashangaa hata wewe..tena huyo!!

Posibility zote hizo...KIUKWELI SIO KOSA LAKO HASA...ILA..NI VERY PSYCHOLOGICAL....Na zinaweza kukubeba....hakuna mtu atakuelewa...lakini be carefull na condition hizo nilizotitaja...maana ukijikuta hapo you can repeat the MISTAKE…the ACT..bila ridhaa yako.

4. Don’t bother to tell this to you husband. Chukulia kuwa it was just a bad dream. Ungemueleza kama ni Mimi...Narudia sio kuwa ni na oversimplyfiy..but because I understand the mechenics… I deely understand. Pole na endelea na masiha.[/QUOTE]
 
Maindainda Mama... Nimesoma kisa chako na mawazo ya wadau wengi waliokupa mawazo tofautitofauti. Ni jambo gumu sana ila ninakifanannisha na kisa cha kweli kilichomtokea mkubwa fulani hapa TZ. Hakusema ukweli kwa mumewe tangu mwanzo ila mume alikuja kufahamu wakati yule mtoto anatolewa mahali. Napenda kukwambia kuwa, mpaka leo hakuna mahusiano mazuri na kila mmoja anaishi kwake. Ninakuomba utujuze kinachoendelea kwani ni kisa cha siku nyingi tangu June 2008. Pole sana na hongera kwa kuwa mkweli kwa kila kitu.
 
Back
Top Bottom