Mtoto wa nje ya ndoa

Mtoto wa nje ya ndoa

Pole bibie,

Ninafurahi unajijua mkosaji ila ushauri mmoja ninao ni hivi:

"Only the TRUTH can set you FREE"
mara nyingi wanaume na wanawake husaliti ndoa zao na kujifanya jeuri huku wakitaka ndoa zao zidumu au hata kulazimisha kuwa ndoa zao zidumu kwa vitisho na vipigo. Na mara nyingi njia hizi hazisaidii hata siku moja. Na wengi husahau kuwa katika kuwa mkweli na muwazi, msamaha wa kweli hutokea na pendo kuchipukia upya.

"Every person is humbled by the Truth"

Siwezi semea mumeo maana simfahamu kitabia wala mwenendo na wala siwezi kukusemea wewe maana kitabia sikujui. Ila jifunze kuwa mkweli. Ukweli hulipa siku zote hata kama atachukia sana ataheshimu kuwa ulimwambia ukweli na wala hukumdanganya. Umweleze kuanzia mwanzo ilivyokuwa na wala usifiche jambo lolote.

ukianza kuwa slective katika yale utakayomweleza basi ujue hata msamaha wa kweli hautapatikana.

Pole ila na hili liwe fundisho kwa wanawake wengine na wanaume wengine.
KWANZA MAINDAINDA FAHAMU WEWE SI WA KWANZA.
WAPO WENGI NA WENGINE WAMEZAA WATOTO WAWILI AU ZAIDI NA WOTE SI WA HAO WAUME ZAO.

Usijione mkosaji kwa kiasi hicho.Kila mtu anamaskeleton yake kwenye kabati.

Kwa suala la kukiri makosa kwa mumeo, mimi sikubaliani nalo.

Kwanza ZINGATIA MASLAHI ya huyo mtoto au watoto kama mnao wengine hayakavyo athirika kwa damage ya huo ukweli unaotaka kumweleza.

IFIKE MAHALA KWENYE MAISHA YETU tuweze kuishi na makosa tuliofanya kwenye maisha yetu BILA KUATHIRI WENGINE kwa kigezo cha kukiri makosa.
Unafikiri hata huyo Mumeo utamuumiza kwa kiasi gani kwa taarifa hiyo?

WAPO WENGI SANA KAMA WEWE MAMA, ACHANA NA HIYO HABARI, SAHAU KAMA LILIWAHI TOKEA.Akija huyo bwana kudai mtoto jibu NI RAHISI MTOTO SIYE WAKE ni wa huyo Mumeo.

SWALI:Je, umewahi taka kujua kama huyo baba yako ndiye biological father wako.

Achana na hiyo habari,BABA NI BABA, hakuna cha Biological wala Baba Mlezi.
 
Mi mwanamke nitakaye muoa akubali kuishi kwa raha na amani na upendo wa hali ya juu kuishi na watoto wangu wa 3 wa nje ya ndoa.
 
Mama some secrets are better to be left where they are.

Hivi wahenga walikuwa na maana gani walipoanzisha ule msemo wa kitanda hakizai haramu? hii ya maindainda haiwi covered hapa?
 
Hivi wahenga walikuwa na maana gani walipoanzisha ule msemo wa kitanda hakizai haramu? hii ya maindainda haiwi covered hapa?

Kitanda kimezaaa haramu hapo Sinza jmosi mwanaume kashtukia analea mtoto wa Mpemba na anamiaka 4 sasa mtoto huyo.Jamaa kajua mimba yake kumbe kuna mwanaume mwenzie amemzidi kite kwa hiyo kitanda cha huyu jamaa kimezaa haramu.
 
Kitanda kimezaaa haramu hapo Sinza jmosi mwanaume kashtukia analea mtoto wa Mpemba na anamiaka 4 sasa mtoto huyo.Jamaa kajua mimba yake kumbe kuna mwanaume mwenzie amemzidi kite kwa hiyo kitanda cha huyu jamaa kimezaa haramu.

mh! Fidel naomba unisaidie kaka yangu
Nini maana halisi ya msemo huo wa kitanda hakizai haramu?
 
mh! Fidel naomba unisaidie kaka yangu
Nini maana halisi ya msemo huo wa kitanda hakizai haramu?

Mbona nimekupa maelezo hapo Mwana!
Wewe si upo na mzee na mnaburudika kama kawaida....sasa ukipata mimba au ujauzito hatutegemei mtoto azaliwe Mwarabu wakati wewe na mmeo ni wandengeleko original. Lakini kitanda si ndipo mnapo fanyia shughuli hakiwezi kutoa kitu haramu Mwana
 
Lakini Fidel huu msemo huwa wanambiwaga wale ambao wamesingiziwa watoto kwa maana ya kuwafanya wakubali tu kuwa ni wao kwa vile wako ndoani au huwa siuelewagi vizuri mimi?
 
Lakini Fidel huu msemo huwa wanambiwaga wale ambao wamesingiziwa watoto kwa maana ya kuwafanya wakubali tu kuwa ni wao kwa vile wako ndoani au huwa siuelewagi vizuri mimi?

Yeah kweli iwa wanaambiwa wanaume wanao bambikiwa watoto au mtoto anamlea mtoto kumbe wa dume lenzie yaaaani inauma mi naua mtu haki ya nani.
 
Nakushauri uendelee kukaa kimya huku ukitubu kivyako, ili kudhibiti athari za dhambi uliyotenda ibaki kukuchoma wewe mwenyewe huku mumeo na mwanao wakiendelea kubaki katika amani.... Hebu fikiria adha ya kisaikolojia utakaompa mwanao ambaye kwa miaka mingi alidhani mumeo aliyemjali na kumthamini kwa raha na karaha na kujua kuwa ni ni babake mzazi, ghafla ukubwana unamwambia after all si babake... na babake ni fulani.... Mwanao atakudharau na kukulaani maishani. Pia heshima, na kuaminiana baina yako na mumeo ndio utavizika mara utakapotoboa siri hiyo... Na kwanza hicho kiranga cha kumwambia huyo bwana unayedai kukupa ujauzito kuwa wewe una mimba yake ni cha kujitakia mwenyewe..au uliona ufahali kufanya hivyo. Na kumbuka wataalamu wanatuambia kuwa tangu kipimo cha DNA kilipoingia nchini taarifa zinasema kuwa kati ya asilimia 40 hadi 60 ya sampuli zinazopelekwa kupimwa ili kubaini kama mtoto ni wa baba husika wa ndoa (biological father) zinaonyesha to the contrally!!!!!. ACHA DHAMBI ZIKUGUGUNE MWENYEWE NA MWACHE MUMEO NA MWANAO WAENDELEE KAMA VILIVYO VINGINEVYO UTAHAMISHA MACHUNGU NA DHAMBI ZAKO KWA WASIOHUSIKA.
 
Pole dada, Mimi binafsi nina jambo linalofanana na lako,miaka sita iliyopita nilikuwa na uhusiano na dada mmoja ambaye kwa wakati ule alikuwa na mchumba wake, ambaye walikuwa wakiishi sehemu tofauti tofauti,kazi ya huyu dada ilikuwa inamfanya awe asafiri mara kwa mara na hivyo kuwa anakutana na mwenza wake .Lakini katika mahusiano yetu huyu dada alipata uja uzito,kilichotokea ni kwamba alikuwa ajasafiri katika kipindi cha miezi mitatu hivi, hiyo ilifanya ajue wazi muhusika ni nani, na wakati huo maandalizi ya Ndoa yao yalikuwa yamekamilika.Baada ya miezi minne wakafunga ndoa wakati yule dada akiwa mja mzito,tulipojadiliano juu ya huo huja uzito alikubali kutotoa ,lolote na liwe.Kweli akajifungua mtoto wa kiume copyright na baba mimi,na akawa anataka niendelee kuwa baba wa mtoto wakati yeye ni mke wa mtu?Nilikataa katakata.
Na jambo baya zaidi nilipoamia kwenye makazi yangu mapya nikagundua kuwa tunaishi wote mtaa mmoja kwa tofauti ya nyumba kama 10 hivi.
Nime-avoid sana mawasiliano naye.Japo yeye analazimisha.Sipendi mke wangu ajue wala mume wake.
Hivyo kumueleza au kutomueleza mume wako kunategemeana na jinsi yeye alivyo kitabia, kama high tempered utalimwa talaka ya haraka.Kumueleza kunategemeana na tabia ya mtu.kumueleza kutamfanya akose imani kwako.
Kwa uliyoeleza hapo juu sheikh nashawishika zaidi kusema kuwa Wanawake ndiyo WANAFANYA DUNIA IZUNGUKE.

MUNGU wangu!!!!?????!!!!!
 
bado tu ile ishu ya mtoto wa kupaka inaendelea humu?
anyway nashauri huyo mtoto amfehem baba yake maana ndivyo ilivyo kwani kuna sheria mpya ya DNA itapita hivi karibuni ambapo mama uliyetotoa nje utalia na kusaga meno
 
Pole dada, Mimi binafsi nina jambo linalofanana na lako,miaka sita iliyopita nilikuwa na uhusiano na dada mmoja ambaye kwa wakati ule alikuwa na mchumba wake, ambaye walikuwa wakiishi sehemu tofauti tofauti,kazi ya huyu dada ilikuwa inamfanya awe asafiri mara kwa mara na hivyo kuwa anakutana na mwenza wake .Lakini katika mahusiano yetu huyu dada alipata uja uzito,kilichotokea ni kwamba alikuwa ajasafiri katika kipindi cha miezi mitatu hivi, hiyo ilifanya ajue wazi muhusika ni nani, na wakati huo maandalizi ya Ndoa yao yalikuwa yamekamilika.Baada ya miezi minne wakafunga ndoa wakati yule dada akiwa mja mzito,tulipojadiliano juu ya huo huja uzito alikubali kutotoa ,lolote na liwe.Kweli akajifungua mtoto wa kiume copyright na baba mimi,na akawa anataka niendelee kuwa baba wa mtoto wakati yeye ni mke wa mtu?Nilikataa katakata.
Na jambo baya zaidi nilipoamia kwenye makazi yangu mapya nikagundua kuwa tunaishi wote mtaa mmoja kwa tofauti ya nyumba kama 10 hivi.
Nime-avoid sana mawasiliano naye.Japo yeye analazimisha.Sipendi mke wangu ajue wala mume wake.
Hivyo kumueleza au kutomueleza mume wako kunategemeana na jinsi yeye alivyo kitabia, kama high tempered utalimwa talaka ya haraka.Kumueleza kunategemeana na tabia ya mtu.kumueleza kutamfanya akose imani kwako.
Najaribu kufikiria kuwa huyo Mama kaolewa, na mtoto si wa Mume wake, na bado kakuganda na anataka uendelee kuwa baba wa mtoto.

Na siku anakujia na gia kuwa amekuletea MTOTO KWANI AMEKUKUMBUKA baba yake.

Hii nadhani ni kali kidogo kama utaanzisha thread yake mkuu na kutupa changamoto unazokutana nazo, ili tupate kujifunza.
 
cha kufanya mueleze ukweli hata kama ataamua kukuacha lakini roho yako itakua na amani, utaanza maisha mapya, bora maisha mapya yenye amani kuliko ya siku nyingi yasio na amani,unadhani siku akija fahamu mwenyewe bila kumfahamisha si ndo atakua kama kifaru,mfahimshe kwani,ukitumbukia kwenye shimo wakati unatembea sio uzembe ila kesho yake kutumbukia tena kwenye shimo hilohilo ni uzembe
 
Ukweli ..... Ukweli ..... Ukweli;

Kwa nini unajisikia hauko huru? Kwa sababu kuna ukweli umefichwa haujasema. Hata kama hutasema ukweli huo siku moja utatoka na utatoka na madhara zaidi. Kuna stori mwaka juzi ya Dreva aliyenyang'anywa gari la serikali akauawa. Mwili wake ulikutwa umeharibika vibaya. Kuthibitisha ilitafutwa DNA. Ya mtoto wake ikakataa. Ya ndugu yake ikakubali. Fikiria aibu aliyoipata huyo mke wake!!!

Mkificha ukweli siku moja utatoka!! Kuna siku huyo baba atajua kupitia mlango wa nyuma. Akithibitisha anaweza kukufanyia kitu mbaya kuliko unavyofikiria. Ninawachukia makuadi wa uongo wanaokushauri useme uongo. Tafuta muda na mazingira muafaka, mbwagie hilo shuzi, kwa ustaarabu sana. Lazima atakusamehe tu. Ni kweli ataumia, lakini maumivu yake yatakuwa manageable akiambiwa na wewe mwenyewe. Maumivu yake yatasambaa kamba bomu ikiwa atajua kupitia njia zingine na usijipe moyo eti haiwezekani. Inawezekana na itatokea!! Ndo maana unajihisi kukosa amani.

Pole kwa yote. Ni kweli huwa tunaweza kuanguka! Lakini kuanguka kwetu kunapotoa kitu cha kudumu kama mtoto, hapo ujanja wetu unakuwa mmoja tu. Kusema ukweli. Ukweli tu NDO UTAKAO KUWEKA HURU.

Ukikaaa kimya, manake unakubali kuteseka. Lakini hatari yake ni hii, akijua kupitia njia nyingine halafu wewe ndo useme niliogopa hatakubali. Ataona kuwa usaliti wako unaendelea. Ukisema ukweli wote, hata kwa mimi, Ni guarantee kuwa hilo kosa huwezi rudia (OK at least na mtu yule yule au mazingira yale yale). Kusema ukweli kunaonesha kukubali 'responsibility'.

Kusema uongo, ni sawa na mbuni kuzika kichwa kwenye mchanga akiamini kuwa hataonekana!! Huyo mtoto baba yake yupo na ulivyosema, huyo mwanaume anajua kuwa huyo ni mwanae. Huoni kuwa unakalia bomu kwa kutomwambia mumeo?? Siku akisikia kwa huyo mwanaume? Utabisha? utalia? Utajinyonga.

Toka nje ya gamba la uongo! Halitakulinda.
 
Wana JF,
Naendelea kushukuru kwa ushauri wenu. Bado naendelea kusema kuwa nitasema. Nimetafuta muda muafaka na huu ni mapema mwezi ujao. Sitafuti shahidi wala wazazi, akiamua awaambie mwenyewe watu au akiamua kumlea kimyakimya sawa, au akimkataa sawa, nitamuelewa ingawa nitasikitika mno. Nampenda sana mume wangu na ni mwanaume mzuri, hastahili haya.

Haya mambo hayafichiki kamwe, na hakuna kibaya kama kujua umedanganywa kwa muda mrefu. Siku moja nilielezewa kwa kina hii hadithi, kumbe inafuatiliwa, yuko humu humu JF.

Sitasahau siku moja kidogo nivunje mguu hospitali nikiwahi vipimo vya maabara, na afadhali nilivifuata maana kuna data hazikuwa zina tally kabisa na za mume wangu na hili lingeleta balaa kubwa. Jamani DNA wala sipimi, hakuna siri katika hili, mwana si wake kwa kumzaa ingawa anampenda sana. Sitaki tabu na msongo wa mawazo, liwalo na liwe. kila jambo baya lina repercussions zake and I am ready to face them.
Nimekataa kila aina ya msaada kutoka kwa baba mzazi, atamlea mtoto wake endapo tu baba mlezi atamkataa, kwa bahati mbaya mazingira yanatufanya tuonane mara kwa mara.
 
pole maindainda!

hapo shutuma zote zinakuja kaw mwanamke lakini wanaume hawajui ni jinsi gani mioyo ya akina mama imebeba mizigo, na niw ao ndio wabebehsayo hiyo mizigo, ni ngumu mno, kutunza siri kama hiyo!! binafsi siwezi na najua unavyoumia hasa kama unaipenda familia yako, na huku kunyamaza kunasababisha matatizo mengi akina mama hawana furaha depression kwa sana, ukali usio na sababu, na hii huweza kupeleka kukosekana kwa amani katika ndoa, hata kama hujasema maana hilo jambo litakuwa linakera na kukufanya kukosa amani ya nafsi!! jipe moyo, mungu ni mwema atakupa nguvu, ujasiri na busara utalitenda hili na utakuwa huru, kama usemavyo jipe muda, angalia mambo yanavyoenda utapata uamuzi!! usikate tamaa na majibu ya kuumiza, hakuna ajuae maumivu uyapatayo!! kila la kheri !!
 
Kama ni mimi ungeweza kuniambia .... Isingekuwa ni big deal.

I am different charater on this palnet.

Ungekuwa na maswali machache tu ya kunijibu ili kutegeneza hii issue.

Ni uwuzi, tena uwazi kabisa kabisa..ungekuokoa...But dont do this to ua husband...maana mimi naye inawezekana tunatofautiana sana.

Lakini kwanza ..tell me all this very HONESTLY...hata kama ukisikia kufa...Just tell it as it was....Jibu kama mimi ni mume wako!

Was you forced into the act?

What really drove you to that ..Chap?

Ulikuwa fully aware when you went with him?

Unafikiri mimi ningetakiwa nifanye nini ... ili usiende naye ..hapa nina maana there was ..weakness in my part ndio maana..ukapata hiyo nafasi.

Na

Kabala sijaendelea..?

Ilikuwaje Baba wa mtoto akajua kuwa una mtoto naye?

Did you tell him?

Why?

Ulivyomuabia ..didi you fill Highhh..yaani ulikuwa unajisikai vizuri..yaani kama umemkomesha mumeo .....kitu kama hicho..just be very frankly...

Let me get all this answers before you get my advice...!

I am sure all will be very fine..if this is true..story..!


Damn, You are Good! Thanks! You will Do GREAT as a Marriage Counseller or as a Lawyer....!
 
Back
Top Bottom