Maindainda
Member
- Jun 1, 2008
- 40
- 6
Ndugu na rafiki zangu wa Jamii Forums,
Naomba msaada katika jambo hili.
Nina ndoa ya kama miaka kumi. Nina mume wangu ambae najua ananipenda, nami pia ninampenda. Miaka kadhaa iliyopita nilikutana na jambo ambalo limenitia simanzi sana na sijui hata nifanyeje, kuna wakati siamini kama ni jambo lililonitokea mimi maishani.
Kwa kifupi ni kwamba nina mtoto ambae najua si wa mume wangu! Amelelewa na huyu baba bila kujua kwa upendo mkubwa, kulipa ada za shule na mahitaji yote. Kusema kweli haijakuwa jambo rahisi maana kila anapomuita baba mimi moyo wangu hujaa simanzi. It happenned that I was at a wrong place with a wrong guy and it happenned. Si tabia yangu na wala sikujidhania kwamba siku moja naweza kuisaliti ndoa yangu.
Huyo baba mwenye mtoto ana mke, simpendi kimapenzi na wala hatuhusiani tena, ikiwa ni pamoja na kuwa hajawahi kumtunza mtoto huyu ingawa anaweza. Sikutaka afanye hivyo. Tatizo ni kuna wakati fulani aliwahi kusema kuwa atakuja kumchukua mtoto wake siku moja, kivipi sijui. Naona ana fujo maana sioni uwezekano wa jambo hili labda avunje ndoa yangu kwanza.
Sio kutokana na sababu hii ila kwa muda mrefu tangu nikiwa na mimba ile nimetaka kumwambia mume wangu ukweli lakini nimeshindwa. Maisha ya masikitiko na kuwaza jamani naona nashindwa na nataka nimwambie ukweli na atoe hukumu yake.
Naomba mnishauri hasa wanaume- ingekuwa wewe ungefanyaje? Nimwambie au niache?
Hili ni tukio la kweli, naomba ushauri usiwe katika yafuatayo:
1. Kusema kwamba mimi msaliti na mke mbaya-hilo nalijua na wengi wenu mnayajua haya na haitanisaidia sana.
2. Kusema nimefanya ngono zembe nikapime ukimwi - nimepima na sina
Naomba msaada.