Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

Kama sio Lulu basi kuna mwingine mwenye kesi ya kujibu. Concussion haitokei bila kugongwa ama kujigonga. Ila ile story ya Kanumba alilegea akaanguka inaweza kumtoa (after walau 3 years). Akitoka huko atakuwa mkubwa, anaweza kugombea ubunge wa vijana ccm

aje hata leo sisi ccm(magamba)tuna ubunge viti maalum
 
Hivi udini ni upi kati ya kuteua watu wengi wa dini moja na kusema kuwa walioteuliwa wengi ni watu wa dini moja?

Nasubiri jibu hapa, otherwise nitauliza hili swali over and over again hadi nipate jibu.
Jmushi!,

Udini ni pamoja na kupendelea upande mmoja. Hii ndicho kiini cha shuku na malalamiko ya Mzee Mtei sasa ikiwa JK kachagua wajumbe hawa kwa kupendelea upande wa waislaam ndicho alichokiona yeye na sijui kwa jicho lipi, tunataka yeye atuonyeshe na sii hesabu ya watu kwa majina yao maana ktk list ya wajumbe hao hakuna mtu hata mmoja ni kiongozi wa dini. Je kutokuwepo kwao (viongozi wa dini) ndio anachosema kuwa ni kosa au kuwepo kwa waislaam wengi?.

Hivyo jibu lake linajieleza na kwamba mzee wetu kachemsha kuzungumzia kuwepo kwa waislaam wengi akiwa na maana wamependelewa against WAO. Ndani ya chama chake mwenyewe hakuna uuwiano anao udai. Je, tukishuku chama kwa hilo ikiwa muasisi mwenyewe ndio mind set yake. Huyu mzee akae pembeni atuacvhie chama ambacho tumekichukua kikiwa na wabunge watano tu.. vijana wameifanya kazi kubwa sana kukiondoa pale kilipokuwa kufikia hapa kilipo na imetuvutia hadi kina sisi tunaopiga vita Ukabila na Udini baina ya watanzania na hatuwezi kupambana na Udini kwa kuwaridhisha makundi haya kama mkoloni alivyofanya.

Kasahau ama ameshindwa kutazama picha nzima ya Utaifa wetu isipokuwa pale palipomgusa yeye ama WAO..Tanzania kama Tiafa lina wanawake wengi kuliko wanaume almost 70% wamewakilishwa vipi ktk wajumbe hao?, Vijana chini ya umri wa miaka 35 ni asilimia 70 ya population mbona hakuna kijana hata mmoja? Haya Wanaoamini dini za kiasili ni asilimia 33 zaidi ya wakristu na waislaam mbona hawana mwakilishi na mengine mengi tu.

Mtu anaweza kuitwa Hassan lakini hata siku moja hajaenda kusali wala sijui hiyo kuran na wakristu vivyo hivyo. tena naweza sema sisi Wagandanyika ni WANAFIKI wakubwa inapokuja swala la dini. Tunapiga makelele sana kuhusu Udini lakini sisi wenyewe ndio mafirauni wakubwa, na huu umaskini haikuwa bahati mbaya ama Mungu hatupendi sisi bali umaskini huu umetufanya kuwa wanafiki kupita maelezo, tumeingia hata umaskini wa hali (fikra) afadhali hata hao wazungu wasioamini wala kuzifuata dini wanayafanya mema zaidi yetu. Civilization ni pamoja na kuondokana na fikra za kizamani za ukabila na Udini..
 
zito ni mwislam na ameshaingia kujadili zile hoja za kipumbavu za udini, HANGAIKENI NA DINI ZENU HII NCHI HAITAKUWA SAUDIA WALA VATICAN HII NI TANZANIA NA HAINA DINI..........
 
Zitto anaivuruga CDM, au chadema inamvuruga zitto?? Zitto anapanbana na maadui zake ndani ya chadema wasiotaka kuona chama kinatoka minoni mwa wenye malengo maalum!! Mtoeni zitto ili chama chenu kife ili tanzania iendelee kuwa na amani

Hii ndo taswira ndani ya CDM, viongozi wanabusara kuliko wanaowaongoza. Ila humu JF ukitoa maoni yako dhidi ya CDM au kiongozi wao basi wewe hautakuwa salama kwa matusi na kashfa. Ndo maana mjadala huu utamalizwa kwa droo si zitto wala Mtei atakaesakamwa.
 
I am christian.....

Ukijadili swala hili in political angle utaona makosa mengi ya Mtei kwa CDM

1. Anaweka gap kati ya CDM na waislam, lile gap ambalo lilikuweko, akina mbowe wamepigana kuli-fill mzee anarudisha tena juu mno
2. huwezi ukamkwepesha CDM na mtei...he is the final sayer!

hakuwa na sababu ya kusema yeye hata kama tuhuma zake ni za kweli
hakuwa na sababu ya kusema kivyake, kwani cdm ilisishasema italitolea tamko

angesema baada ya tamko la chama pia ingemweka pazuri kuwa yuko tofauti na chama

Juzi alimpinga zito na kusema chadema haitamsimaisha mtu anayejitangaza mapema!!

Mtei amechemka!! tena kaharibu kwani anaharibu taifa
 
kusema ukweli sio matusi--- mwaache zito afunguke hiyo ndio demokrasia usimtishe ana haki ya kuongea
 
Katika kauli zilizonishangaza ni hii ya Mzee Mtei kuhusu dini.
Mzee Mtei ameishi zama za Nyerere na nyakati hizo udini na ukabila ulipigwa vita sana.
Nilitarajia mzee awe daraja kati ya generation ya sasa na ile ya baada ya uhuru.
Kwamba mzee aturithishe thamani za nchi hii kama watu wamoja bila kubaguana.
Nilitaraji mzee angekuwa na mifano mzuri wa Nigeria, Kenya, Rwanda, Yugoslavia, Srilanka, Ireland,Spain n.k

Kitendo cha kutenga Watanzania kwa misingi ya dini ni cha kusikitisha sana.
Mkandara ameorodhesha makundi yasiyowakilishwa katika tume, mimi nauliza zaidi, hivi kama ni Waislam Vs Waristo, je wale wasio na dini au wasioamini au wenye dini zao za asili wamewakilishwa na nani?
Je hawa hawana haki katika nchi hii ila tu makundi aliyoyataja mzee Mtei!

Pili, Mzee mtei atuambie hivi tunaenda kuandika katiba ya nchi au tunakwenda kuandika Biblia na Misahafu.
Endapo kungekuwa na masangoma 4 au 5 wenye wanabusara sana katika mambo ya katiba na ambao tungependa watusadie, je hiyo katiba ingekosa uhalali kwasababu tu Hassan na William wameshirikiana na masangoma!

Mzee Mtei endapo tuna watu wanaoweza kutusaidia kufanya jambo la nchi hii, je tunaangalia uwezo wao au majina yao.
Wewe umekuwa waziri mwandamizi, hivi mzee wetu hukumbuki kuwa Bagamaoyo ni maarufu sana kwa viongozi na vigogo kuliko sisi makapuku! Hizo dini za Uislam na Ukristo wanashiriki vipi kwasababu zote zinakataza ushirikina. Kwani mzee dini ni nini hasa, kwasababu mtazamo wako dini ni majina.

Mzee Mtei hoja ya kuwa na wajumbe sawa kwa uwiano wa milioni moja na milioni 40 inamashiko.
Unaposema Zbar imeongeza idadi ya waislam ni kupotosha umma kwasababu unaelewa wazi kuwa asilimia 98 ya wzbar ni waislam na kwa kutumia hesabu za probability una majibu mazuri sana.
Ningeshangaa sana kama wajumbe wa zbar wangekuwa na idadi kubwa kuliko unayoidhani kidini.

Jambo la hatari zaidi ni pale unapojisahau kuwa wewe ni mtu maarufu na mshauri wa mambo ya kitaifa.
Ni nadra sana watu kuweza kutenganisha wewe na fungamano lako la kisiasa.
Kauli yako inatoa nafasi kwa wafitini, wachochezi kupata cha kusema dhidi ya chama chako.

Ingawa sote na wewe ukiwemo tuna uhuru wa kutoa maoni kama haki yetu ya msingi, kauli zako kama mtu mwenye hadhi,heshima na siri nyingi za taifa hili haziwezi kuchuliwa kwa urahisi tu kama Nguruvi3 msaga lami.
Hivyo kauli yako imeleta usumbufu katika jamii, chama chako na wazee wenzako mliolijenga taifa la umoja kwa pamoja.

Wenzako wanaona kuwa una lako jambo katika kuvunja daraja la kizazi kimoja na kingine, ya kwamba wewe unajua nguzo za daraja zipo wapi na ipi inashikilia daraja. Kwa bahati mbaya umeamua kwa makusudi kuishambulia nguzo hiyo.

Ningeshauri kuwa huenda baadhi yetu hatukukuelewa au tumekuelewa vibaya, basi vema urejee na kutoa ufafanuzi.
La sivyo ni vema basi ukachukua hatua za kuomba radhi ili kizazi hiki kifahamu kuwa busara ni pamoja na kusema Samahani.
 
NInyi wakuu mnao tilia shaka mawazo ya Mzee Mtei subirini muone 'zao' la hiyo tume ya katiba halafu mrudi hapa mseme!!

Lets wait and see!! Kila siku narudia kuwa ' this is maths na sio religious politics'

Nguruvi3, Waberoya, Mkandara & Co, mimi kama kijana mdogo najifunza mengi toka mabandiko yenu siwezi kuzua mjadala na ninyi, hii haimaanishi I am a coward 'nope'! Ila mtazamo wenu katika hili ni wa kupotoka na kupotosha!

Hakuna haja ya kuificha kweli chini ya mwamvuli wa 'UDINI'. Again sioni tofauti kati ya muislamu wa Zanzibar na wa Bara, these fellas are fighting the same course, ni wazi kabisa hata katika mitazamo ya masuala mbalimbali ya nchi hii watu hawa huungana, na katika hili tutegemee vivyo hivyo, na tukiendelea kujificha sasa katika mwamvuli huu wa UDINI sina shaka tutaendelea kuwa na katiba hii ya sasa. Masuala ya Imani za watu ni mambo yanayogusa watu moja kwa moja, leo hii mtu anaweza pendelea upande wa dini fulani kwa makusudi ili yeyote atayekuwa whistle blower anyooshewe kidole kuwa ndiye mdini.

Narudia kusema Mzee Mtei has a point!!
 
Kuna picha mbaya naivuta kutoka CHADEMA. Inawezekana Mtei 'ameropoka' Siri ambayo vigogo ndani ya CHADEMA wasingependa iropokwe.
 
Kama hali ya udini ndiyo iko hivi kama tunavyoshuhudia hapa JF tutegemee nini huko mtaani? Ningependa tujadili wajumbe wa hii tume based on intellectual capacity and not otherwise.

Mimi ni Mkristu/Roman Catholic na sioni tatizo kwa tume kuwa na waislam wengi.Cha msingi huwa ninaangalia competency kwanza ndipo busara nyingine za uwiano zifuate.Ni jambo la hatari kujadili udini na ukabila katika mazingira yanayoweza kutugawa na kutuondolea utaifa wetu.Uzalendo wetu uko mashakani.Kwa picha hii ninayoiona CIA,MOSSAD,M15 na wengineo wakituchomekea hii dhana ya Udini tutamalizana wenyewe kwa wenyewe.Hatua ambayo Nigeria imefikia ndipo tunakoelekea sasa.Wanasiasa,viongozi wa dini,na watu wenye ushawishi katika jamii tuache kutoa matamshi bila kufikiria athari.tuna maadui ambao tunahitaji umoja wa kitaifa kupambamana nayo kama matabaka na mapengo ya kiuchumi,ombwe la fikra na uongozi,social vices kama ufisadi na ukosefu wa maadili.tunahitaji utaifa kuliko mgawanyiko wa kiimani au kikabila kukabiliana na haya.Mahakama ya kadhi au kujiunga na OIC sio issue,ili mradi Refferundum imependekeza hivyo.Tuache uoga na hoja nyepesi bila kuzingatia athari

We are a people bedevilled by so many challenges which of course, we've barely scratched the surface of. The leadership deficit has aggravated our economic decline and retardation, and threatens not only our social cohesion but our very identity as a people. In times like these, a strong and transformational leadership is what is required to mobilize our abundant human and natural resources for us to realize our full potentials, but this deficit forms the bane of our problems. Paradoxically, while we acknowledge the failure of leadership, and the incapacity or inability of the present crop of leaders to do much to salvage our pathetic situation, we are still waiting on them

Whatever the case, it is our generation which will suffer most because the present crop of leaders have little to lose; we will live with the consequences of their actions while our children’s future becomes increasingly uncertain

We are in a terminal decline, the question is are we doing enough to address this? What can we or should we do to reverse this certain reality?

uku mtaani watu hawajui ata kama kuna iyo tume ya katiba,achilia mbali hayo majina...ila kuna siku tutafika kuanza kujadili iyo katiba,na upande wa dini moja haswa ukirsto ukiona maoni ya wenzao yamepewa nguvu,hapo ndio watu watarudi kwenye idadi ya wakirsto na waislamu wanaounda iyo tume..hapatatosha nakwambia,pamoja na upole wote wa hawa wakrsto...

Kauli ya Mzee Mtei inaweza kuwa tata..ila ni boooonge la precaution.
 
Alichosema mtei ni mawazo yake na zitto nae mawazo yake,hapa kikubwa kamati ya katiba ifanye kazi ya watanzania wote isijali huyu ana itikadi gani.kwa mtanzamo wa mtei ni kweli waislamu wengi kwenye kamati lakini ujue kuwa pale kuna wajumbe kumi na tano kutoka zanzibar na kumi na tano kutoka bara na ujue zanzibar asilimia 99 ni waislamu na ndio waliochaguliwa kuingia kwenye kamati. cha kulalamika hapo angesema kwasababu tanzania bara tupo wengi aslimia sabin na tano ya wajumbe watoke bara na ishirini na tano watoke zanzibar.Sisi tunataka katiba hata wanakamati wawe wapagani ilimradi wasivunje sheria na walete katiba ya watanzania wote. Mungu ibariki Tanzania.
 
Wazee wetu hawa ambao tayari wametumika sana na wameshavuka umri wa miaka 70 wangepumzika tu. Tumeweka umri wa miaka 18 kama umri wa mtu kuanza kushiriki SIASA. Tungeweka na ukomo wa umri wa kushiriki SIASA uwe miaka 70. Baada ya umri huu ni watu wachache sana wanabaki na akili zao timamu.
Ningemwelewa sana Mzee wetu Mtei kama angelalamikia walioteuliwa kuongoza tume hii ni wazee sana. Wametumika sana. Wamechoka. Ni Wastaafu wenye pensheni nzuri tu. Wangekaa wakala hii pensheni na vitukuu vyao basi. Hata kama walikuwa watumishi wazuri, waadilifu zamani. Inatosha. JK sasa hivi kila akipata nafasi ya kuteua anateua wazee hawa wastaafu ambao wamevuka 70! Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Lubuva. Mzee sana. Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Warioba. Mzee mwingine ambaye ametumika sana na atasaidiwa na wazee wengine ambao wametumika sana akina SAS, Butiko, Augustino,...Alipopata nafasi ya kuibadili CCM kaweka Mzee Msekwa. Mchovu mwingine. Ukatibu Mkuu wa CCM kaondoa Makamba kaweka Mukama, mstaafu mwingine! Orodha ni ndefu.
Nadhani Mzee Mtei alikuwa na agenda nyingine. Aseme tu kwamba hakumwona Mchagga kwenye Tume hii.
 
Mkuu wangu kwa kweli hata mie uwa nashangaa sana mitaani kwetu tunaishi kwa amani hakuna udini wowote humu JF sijui kwa nini hatupendani...mie binafsi marafiki zangu wengi ni Wakiristo kuliko Waislam, na juzi wamenialika pasaka..

mbona mnapenda sana minuso nyie watu..msisikie pilau kosa!!
 
Zitto ajatoa maoni yake,amemtukana na kumdhalilisha sana Mzee Mtei.
Mzee Mtei kwa sasa ni "liability" ndani ya CHADEMA sio "asset" kama alivyo Zitto. Tume haikuteuliwa kwa kuangalia DINI ya mtu. Wenye mawazo kama ya Mzee Mohamed Said na Faiza Foxy wako wengi nchi hii!
 
mbona mnapenda sana minuso nyie watu..msisikie pilau kosa!!

Mkuu wangu siku hizi watu wote wanapenda minuso tu halafu swala la pilau halina kabila siku hizi hata Wachaga, Wasukuma, Wakinga, wote wanakula tena sana tu...hata wewe nyumbani kwenu mnapenda sana mpunga unazuga tu humu JF.
 
Katika kauli zilizonishangaza ni hii ya Mzee Mtei kuhusu dini.
Mzee Mtei ameishi zama za Nyerere na nyakati hizo udini na ukabila ulipigwa vita sana.
Nilitarajia mzee awe daraja kati ya generation ya sasa na ile ya baada ya uhuru.
Kwamba mzee aturithishe thamani za nchi hii kama watu wamoja bila kubaguana.
Nilitaraji mzee angekuwa na mifano mzuri wa Nigeria, Kenya, Rwanda, Yugoslavia, Srilanka, Ireland,Spain n.k

Kitendo cha kutenga Watanzania kwa misingi ya dini ni cha kusikitisha sana.
Mkandara ameorodhesha makundi yasiyowakilishwa katika tume, mimi nauliza zaidi, hivi kama ni Waislam Vs Waristo, je wale wasio na dini au wasioamini au wenye dini zao za asili wamewakilishwa na nani?
Je hawa hawana haki katika nchi hii ila tu makundi aliyoyataja mzee Mtei!

Pili, Mzee mtei atuambie hivi tunaenda kuandika katiba ya nchi au tunakwenda kuandika Biblia na Misahafu.
Endapo kungekuwa na masangoma 4 au 5 wenye wanabusara sana katika mambo ya katiba na ambao tungependa watusadie, je hiyo katiba ingekosa uhalali kwasababu tu Hassan na William wameshirikiana na masangoma!

Mzee Mtei endapo tuna watu wanaoweza kutusaidia kufanya jambo la nchi hii, je tunaangalia uwezo wao au majina yao.
Wewe umekuwa waziri mwandamizi, hivi mzee wetu hukumbuki kuwa Bagamaoyo ni maarufu sana kwa viongozi na vigogo kuliko sisi makapuku! Hizo dini za Uislam na Ukristo wanashiriki vipi kwasababu zote zinakataza ushirikina. Kwani mzee dini ni nini hasa, kwasababu mtazamo wako dini ni majina.

Mzee Mtei hoja ya kuwa na wajumbe sawa kwa uwiano wa milioni moja na milioni 40 inamashiko.
Unaposema Zbar imeongeza idadi ya waislam ni kupotosha umma kwasababu unaelewa wazi kuwa asilimia 98 ya wzbar ni waislam na kwa kutumia hesabu za probability una majibu mazuri sana.
Ningeshangaa sana kama wajumbe wa zbar wangekuwa na idadi kubwa kuliko unayoidhani kidini.

Jambo la hatari zaidi ni pale unapojisahau kuwa wewe ni mtu maarufu na mshauri wa mambo ya kitaifa.
Ni nadra sana watu kuweza kutenganisha wewe na fungamano lako la kisiasa.
Kauli yako inatoa nafasi kwa wafitini, wachochezi kupata cha kusema dhidi ya chama chako.

Ingawa sote na wewe ukiwemo tuna uhuru wa kutoa maoni kama haki yetu ya msingi, kauli zako kama mtu mwenye hadhi,heshima na siri nyingi za taifa hili haziwezi kuchuliwa kwa urahisi tu kama Nguruvi3 msaga lami.
Hivyo kauli yako imeleta usumbufu katika jamii, chama chako na wazee wenzako mliolijenga taifa la umoja kwa pamoja.

Wenzako wanaona kuwa una lako jambo katika kuvunja daraja la kizazi kimoja na kingine, ya kwamba wewe unajua nguzo za daraja zipo wapi na ipi inashikilia daraja. Kwa bahati mbaya umeamua kwa makusudi kuishambulia nguzo hiyo.

Ningeshauri kuwa huenda baadhi yetu hatukukuelewa au tumekuelewa vibaya, basi vema urejee na kutoa ufafanuzi.
La sivyo ni vema basi ukachukua hatua za kuomba radhi ili kizazi hiki kifahamu kuwa busara ni pamoja na kusema Samahani.

Mkuu Nguruvi3,
Nimependa analysis yako ni ushauri mzuri kwa Mtei inabidi ausome na aufanyie kazi.
 
ZITTO, tafadhali acha jazba za kidini, uwe na adabu!Wewe wamwonaje Mtei? Ukweli unakuuma sio? Zanzibar hakuna wakristo? Inakuwaje wajumbe wote 15 wawe waislamu? Wewe inakupendeza hiyo? Tunamheshimu sana mzee Mtei sisi, tumechoka pamoja na unafiki wako sepa, tunakuvumilia kwa mengi, kwa dharau hizi huvumiliki tena! Rais akikosea tushangilie?
Taratibu kijana,
- Kwanza umesoma hiyo habari katika Jambo leo na kuhakikisha kuwa Zitto katamka hilo?
- Pili, unateremsha matusi hapa au wewe ni mbia wa Lusinde?
- Tatu, hili suala la udini tumeshalijadili hapa kuhusu uteuzi wa Waislamu kutoka ZNZ ambako zaidi ya 90% ya watu wake ni waislamu, tayari Makamo Mwenyekekiti wa Tume anatoka ZNZ na ni Mkristo.
- Nne, kama ungepewa wewe kazi ya uteuzi ungefanyaje? Ungeweka Waislamu wangapi na Wakristo wangapi? Waislamu na Wakristo wa madhehebu gani na kwa asilimia ngapi? Makundi mwengine kama vile wanawake/wanaume, vijana/wazee, Walemavu, Asasi za kijamii, Kanda/Mikoa/Wilaya/Kata/Mashina...ungeweka asilimia ngapi ngapi mpka uondokane na dhana ya ubaguzi?
 
Kwanini Zitto anasema yale yasiopendeza watu mnapenda kumhusiha na uasi? hatuna mawazo tofauti ni afya ya mijadala?
 
Zitto ajatoa maoni yake,amemtukana na kumdhalilisha sana Mzee Mtei.
Naweka majibu ya Zitto aliyo comment kwenye hii thread, halafu mkuu naomba na wewe utuonyeshe Zitto alipomtukana na kumdhalilisha Mzee Mtei

Nioneshe popote niliponukuliwa kusema unavyosema hapa.

Sijawahi kumjibu Mtei moja kwa moja hata siku moja. Kwenye suala hili msimamo wangu niliuweka wazi hat kabla Mtei Hajasema.
Walioandika wameunganisha tu tweets zangu na kauli ya Mtei ambayo siiungi mkono hata kidogo. Mzee was mistaken.
Tume ya Katiba imeteuliwa kwa mujibu wa sheria. Haina Udini. Ina wajumbe ninaowaheshimu sana. Twende tukatoe maoni. Tuache maneno yasiyo na maana yeyote.

Hebu tuache kujadili watu, tujiandae kutoa maoni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom