Khatima ya Zanzibar na Mustakbali wa Muungano

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,112
Utangulizi


Mtafiti mmoja kutoka Argentina, Boaventura Santos de Sousa, aliwahi kuandika kwamba &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];mwandishi ingawa huandika kuhusu yaliyopita huwa anajaribu kueleza yaliyopo, siyo yaliyopita. Lakini, kwa kufanya hivyo, huwa pia anajiweka mbali na hali ya sasa na kwa hakika anaandika kwa ajili ya siku zijazo'.


Muungano wa Zanzibar na Tanganyika umepita katika masaiba kadhaa tokea kuasisiwa kwake takriban miaka 45 iliyopita lakini mtikisiko ulioukumba katika siku za karibuni ni mkubwa sana. Ni mkubwa kwa sababu umegusa kiini cha Muungano huu ambapo suala linaloulizwa ni iwapo kwa kule kukubali kushirikiana katika baadhi ya mambo, je, Zanzibar na Tanganyika zimejifuta na hivyo kupoteza hadhi zake kama nchi? Hilo limekuwa ndiyo suala kubwa linaloulizwa na Wazanzibari hasa baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutamka Bungeni kwamba Zanzibar si nchi.


Hakuna awezaye kubisha kwamba tokea kuasisiwa kwake, Muungano huu umejengeka kutokana na misingi ya khofu, kutiliana shaka na kutokuaminiana baina ya pande mbili zinazouunda, ambako wakati mwengine kumepelekea hata kutishia uhai wa Muungano wenyewe.


Muungano umekuwa gumzo kuu katika takriban kila mjadala wa katiba na siasa katika nchi yetu. Umejitokeza na kujionyesha hivyo katika mwaka wa mwanzo wa Muungano kuhusiana na sakata la kuwa na Ubalozi wa iliyokuwa

Ujerumani Magharibi kwa upande wa Tanganyika na Ubalozi wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki kwa upande wa Zanzibar, kuhusiana na uwakilishi wa Zanzibar katika Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki na uanzishwaji wa Benki

Kuu ya Tanzania (BOT) mwaka 1964 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; 1966, wakati wa kuunganisha vyama vya ASP na TANU kuunda Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977, katika mjadala wa marekebisho ya Katiba wa 1983/84 na hatimaye kujiuzulu kwa

Rais wa pili wa Zanzibar Sheikh Aboud Jumbe, wakati wa kuondolewa katika Uwaziri Kiongozi kwa mwandishi wa makala haya na hatimaye kufukuzwa katika CCM na wenzake 6 mwaka 1988, katika harakati za madai ya kutaka

kura ya maoni kuhusiana na Muungano huo mwaka 1989/90, wakati wa mjadala wa kuanzishwa vyama vingi mwaka 1991, katika sakata la Zanzibar kujiunga na Umoja wa Nchi za Kiislamu (OIC) mwaka 1993, wakati wa mjadala wa

G-55 kudai kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano mwaka 1994, katika mjadala wa marekebisho ya 11 na 14 ya Katiba ya Muungano mwaka 1994/95, wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 1995 na ule wa 2000 na karibuni kabisa kuhusiana na suala la matarajio ya ugunduzi wa mafuta visiwani Zanzibar na harakati za kuanzisha Shirikisho la Afrika Mashariki.


Ukiondoa kuibuka kwake katika mijadala mikubwa ya kikatiba na kisiasa nchini, kwa upande mwengine katika uendeshaji wa shughuli za Serikali za kila siku, &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];matatizo na vikwazo kadhaa ya kiutawala na kiutendaji' vimekuwa vikiripotiwa kila mara kwamba vinakwamisha uimarishaji wa Muungano.


Tume na Kamati kadhaa zimeundwa kuainisha matatizo ya Muungano na kupendekeza njia za kuyatatua. Serikali ya Jamhuri ya Muungano imeunda Tume na Kamati zifuatazo, miongoni mwa nyingi, kuhusiana na masuala haya:



  1. Kamati ya Mtei
  2. Tume ya Jaji Francis Nyalali (1991)
  3. Kamati ya Shellukindo (1994)
  4. Kamati ya Shellukindo 2 ya kuandaa Muafaka juu ya Mambo ya Muungano baina ya SMZ na SMT.
  5. Kamati ya Jaji Mark Bomani (1995)
  6. Kamati ya Jaji Robert Kisanga (1998)
  7. Kamati ya 'Harmonization'
  8. Kamati ya Masuala ya Simu (Kamati ya Kusila)


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) nayo kwa upande wake iliunda Kamati zifuatazo kwa madhumuni hayo hayo:



  1. Kamati ya Baraza la Mapinduzi (Kamati ya Amina) ya 1992
  2. Kamati ya Rais ya Kupambana na Kasoro za Muungano (Kamati ya Shamuhuna) ya 1997
  3. Kamati ya Rais Kuchambua Ripoti ya Jaji Kisanga (Kamati ya Salim Juma Othman)
  4. Kamati ya Kuandaa Mapendekezo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya Kero za Muungano (Kamati ya Ramia) ya 2000
  5. Kamati ya Baraza la Mapinduzi juu ya Sera ya Mambo ya Nje
  6. Kamati ya Rais ya Wataalamu juu ya Kero za Muungano ya 2001
  7. Kamati ya Baraza la Mapinduzi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki
  8. Kamati ya Mafuta
  9. Kamati ya Madeni baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano wa Tanzania
  10. Kamati ya Suala la Exclusive Economic Zone (EEZ)
  11. Kamati ya Masuala ya Fedha na Benki Kuu
  12. Kamati ya Rais ya Masuala ya Simu (1996 &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG];1999)
  13. Kamati ya Baraza la Mapinduzi juu ya matatizo na kero za Muungano na taratibu za kuyaondoa (2004)


Ukiacha Tume, Kamati na Ripoti hizo, kuanzia mwaka 1985 kulianzishwa utaratibu wa Kamati ya Pamoja ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano na Waziri Kiongozi wa Zanzibar pamoja na Mawaziri wa Serikali zetu mbili ambao ulitarajiwa uwe ndiyo jukwaa la kuzungumzia matatizo kutoka kwa washiriki wakuu wa Muungano huu na kuyapatia ufumbuzi unaofaa. Utaratibu huu uliachwa kwa muda mrefu lakini sasa umerejeshwa upya kufuatia agizo la Rais Jakaya Kikwete alilolitoa katika mkutano na mawaziri na watendaji wakuu wa Serikali yake huko Ngurdoto, Arusha mwezi Februari, 2006.


Mikutano, Makongamano, Semina na Warsha vimefanywa kujadili masuala haya na kupendekeza hatua za kuchukuliwa. Wasomi na wanafunzi wamefanya tafiti kadhaa na kujipatia shahada na stashahada hadi ngazi ya Ph.D juu ya Muungano lakini bado matatizo yako pale pale na yanaongezeka kila kukicha.


Yanayoonekana na kuelezwa kama matatizo, mapungufu, dosari, kasoro na, kwa msamiati wa sasa, kero yamekuwa ndiyo yale kwa yale. Nini basi kiini cha haya? Na vipi tutayatatua?


Mimi nimeamua kutoa changamoto kupitia waraka huu kwa kuitazama historia ya Muungano, jinsi ulivyoundwa, matatizo yanayoukabili, nafasi na hadhi ya Zanzibar katika Muungano na nini khatima ya Zanzibar na mustakbali wa Muungano huko tuendako. Nitakayoyaeleza yanaweza yakaonekana ni machungu kwa wakati huu wa sasa lakini kama asemavyo Santos de Sousa yanaweza yakawa ndiyo ufumbuzi kwa siku zijazo.




Asili na Sababu za Muungano


Maoni yanayotolewa kuhusu asili na sababu za Muungano yamekuwa yakitofautiana mno. Wapo wanaouleza Muungano huu kuwa ni wa pekee katika bara la Afrika, kwani ndiyo pekee ulioweza kudumu katika kutimiza azma na malengo ya kuleta umoja wa Afrika (Pan-Africanism),[2] na pia wapo wanauona kuwa ni &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];jaribio la kusisimia la ukoloni mdogo wa nchi moja ya Kiafrika kuiteka na kuitawala nchi nyengine ya Kiafrika.'[3]


Kutokana na maelezo na hoja nyingi na zinazokinzana kuhusu asili na sababu za Muungano, si rahisi kusema moja kwa moja kuwa maelezo yepi au hoja ipi ni sahihi. Utangulizi (Preamble) wa Mkataba wa Muungano wenyewe unataja sababu kuu ya kuunganisha nchi za Zanzibar na Tanganyika kuwa ni &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];maingiliano ya muda mrefu ya watu wa nchi mbili hizi na mahusiano yao ya kidugu na kirafiki &[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; na &[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; kuendeleza umoja wa watu wa Afrika.' Lakini miaka 45 sasa baada ya uzoefu wa Muungano huu, Wazanzibari wanajiuliza kweli haya ndiyo madhumuni ya Muungano huu?


Wazo la kuungana linaweza kurudishwa nyuma tokea zama za harakati za ukombozi wa nchi za Afrika. Waasisi na wakuu wa harakati za kupigania Uhuru waliiona mipaka ya nchi zao iliyowekwa na wakoloni kuwa ni &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];mbinu za kibeberu' zilizotekelezwa kwa ajili ya manufaa na maslahi yao. Kutokana na hisia hizo, mazungumzo ya kuanzisha aina fulani ya umoja miongoni mwa nchi huru za Afrika yalitawala duru za siasa katika miaka ya 5o na 60.


Nadharia mbili zilijichomoza. Ya kwanza, ikishadidiwa na Kwame Nkrumah wa Ghana, ilikuwa ikitaka kuasisiwa kwa nchi moja tu ya Afrika nzima iliyoungana ikiwa na Serikali moja kwa bara zima. Nadharia hii ilipingwa na baadhi ya viongozi, wakiongozwa na Julius Nyerere waTanganyika, ambao walisisitiza haja ya kuanza na miungano ya maeneo (regional unions) chini ya mfumo wa Shirikisho badala ya kuwa na mpango wa Serikali moja.[4]


Katika kulifikia lengo hilo, viongozi wa kisiasa wa nchi tatu za Afrika Mashariki &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Kenya, Ugandana Tanganyika walikuwa wakifanya mikutano ya mara kwa mara kipindi chote cha kati ya mwaka 1961 na 1963 kuona jinsi gani wanaweza kutimiza ndoto hiyo. Mfumo wa Muungano uliokuwa ukiandaliwa ulikuwa ni ule wa Shirikisho. Tamko la Pamoja la viongozi hao lilisema:


"Sisi, viongozi wa wananchi na Serikali za nchi za Afrika Mashariki tunayakinisha nia zetu kuhusu kuwepo kwa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki. Mkutano wetu wa leo unasukumwa na hisia za umoja wa Afrika (Pan-Africanism), na siyo tamaa za maslahi binafsi ya eneo hili. Ijapokuwa Zanzibar haikuwakilishwa katika mkutano huu, tunapaaswa kuweka bayana kwamba nchi hiyo inakaribishwa kushiriki kikamilifu katika mikutano yetu kwa ajili ya uundwaji wa Shirikisho ."[5]


Lakini Umoja wa Afrika (Pan-Africanism) hauonekani kuwa ndiyo dhamira pekee au kama ndiyo dhamira halisi ya Muungano. Wengi wanaamini, na mimi nikiwa mmoja wao, kwamba dhana hiyo ilitumiwa tu kuficha njama za muda mrefu za Nyerere kutaka kuimeza na kuitawalaZanzibar. Katika mwaka 1961, wakati Tanganyika inakaribia kupata Uhuru wake, Nyerere alinukuliwa akisema:


"If I could tow that island [Zanzibar] out in the middle of the Indian Ocean, I would do it &[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; I fear it will be a very big headache for me."[6]


Yaani, "Kama ningekuwa na uwezo wa kuvikokota visiwa vile [Zanzibar] na kuvitupa nje kabisa, katikati ya Bahari ya Hindi, basi ningefanya hivyo Nakhofia vitakuja kuniumiza kichwa sana".


Imani hii inatiliwa nguvu na mahusiano ya karibu na ya muda mrefu yaliyokuwepo kati ya chama kilichokuwa kikitawala Tanganyika, TANU, na ASP ambacho kilishika hatamu za utawala baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964, mwezi mmoja tu baada ya Zanzibar kupata uhuru wake kutoka Uingereza hapo Desemba 10, 1963. Zilikuwepo taarifa tokea mwaka 1959 kwamba TANU na ASP zitakaposhika madaraka zitaziunganisha nchi mbili hizi kuwa Jamhuri moja.


Wakati juhudi za kuanzisha Shirikisho la Afrika Mashariki zikiwa zinafifia, Nyerere aliona fursa Zanzibar ambayo hakutaka kuipoteza. Katika mazungumzo ya siri kati yake na Rais Abeid Amani Karume wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, wakakubaliana kuziunganisha nchi mbili hizi. Hakukuwa na ushirikishwaji wa aina yoyote ule wa wananchi wa nchi hizi mbili katika maamuzi haya makubwa. Usiri uliogubika hatua hii kubwa unafichuliwa na si mwengine bali Nyerere mwenyewe pale aliposema:


"[Tanganyika] tulipeleka polisi wetu Zanzibar. Baada ya kuyashinda matatizo kadhaa tukaungana. Sisi wenyewe kwa khiyari zetu tulikubaliana kuungana. Karume na mimi tulikutana. Peke yetu wawili tu tulikutana. Nilipomtajia wazo la Muungano, Karume hakufikiri hata mara mbili. Pale pale alinitaka kuita mkutano wa waandishi wa habari kutangaza azma yetu. Nilimshauri asubiri kidogo kwani ilikuwa bado ni mapema mno kuweza kuviarifu vyombo vya habari."[7]


Taarifa hizi ziliendelea kubaki kuwa siri hadi tarehe 26 Aprili, 1964 pale Redio ya Tanganyika ilipotangaza kwamba siku hiyo Marais wawili hao watakutana katika Bunge la Tanganyika kubadilishana Hati za Muungano ambazo zimeunganisha Zanzibar na Tanganyika kuwa Jamhuri moja. Hivyo inaonekana wazi kwamba tokea awali Muungano huu ulikosa ridhaa ya watu. Haukuwa Muungano wa watu, ulioundwa na watu, kwa maslahi ya watu. Bali ulikuwa na umeendelea kuwa ni Muungano uliosimamishwa kwa ridhaa ya watawala pekee.




Kiini cha matatizo ya Muungano


Ukitazama kwa jicho la sheria, kiini cha matatizo ya Muungano kinatokana na tafsiri ya Mkataba wa Muungano (Articles of Union) wa 1964. Hizi ndizo hati zinazounda, kupitia mkataba wa kimataifa, Jamhuri ya Muungano. Suala kubwa lililoumiza na linaloendelea kuumiza vichwa vya wengi na hivyo kuendelea kuulizwa ni mfumo gani wa Muungano ulikusudiwa kuwekwa na Mkataba huu? Ni muungano wa moja kwa moja (unitary) au wa shirikisho (federal)?


Mfumo uliopo sasa ambao ulianza kutekelezwa 1964 ni ule wa serikali mbili ile ya Jamhuri ya Muungano na ile ya Zanzibar. Tanganyika haikuwekewa serikali yake tofauti; madaraka yake kwa yale mambo yasiyo ya Muungano yalielezwa kwamba yatasimamiwa na kuendeshwa na Serikali hiyo hiyo ya Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo, uhalali wa kisheria wa muundo huu umeendelea kuhojiwa na hata kupingwa kwamba hauwakilishi ipasavyo makusudio yaliyomo katika Mkataba ulioanzisha Muungano wenyewe.


Mkataba wa Muungano wenyewe hauelezi bayana aina au mfumo wa muungano inaouanzisha lakini uko wazi kuhusiana na mgawanyo wa madaraka (distribution of power) inaouweka na idadi ya mamlaka (number of jurisdictions) zitakazokuwepo. Ibara ya (iii) (a) ya Mkataba huo inaanzisha &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Bunge na Mamlaka ya Utendaji' (Parliament and Executive) ndani ya na kwa ajili yaZanzibar ikiwa na mamlaka kamili kuhusiana na mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kwaZanzibar. Kwa upande mwengine, Ibara ya (iv) ya Mkataba huo inaanzisha &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Bunge na Mamlaka ya Utendaji' (Parliament and Executive) ya Jamhuri ya Muungano ikiwa na mamlaka kamili katika eneo lote la Jamhuri ya Muungano kuhusiana na mambo ya Muungano na, pia, ikiwa na mamlaka kamili ndani ya, na kwa ajili ya Tanganyika kuhusiana na mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kwa Tanganyika. Kwa hivyo, katika sehemu ya pili, mamlaka mbili tofauti zimechanganywa pamoja.


Mjadala mkubwa na mkali umekuja kuhusiana na tafsiri ya Ibara hiyo ya (iv) na kule kuchanganya kwake mamlaka mbili hizo.


Haya si masuala ya kisheria tu kama ambavyo baadhi yetu wanataka tuamini (ingawa nayo ni muhimu mno kama ilivyodhihirika hivi karibuni), bali pia ni masuala ya kisiasa kwa vile yanahusisha uwezo wa maamuzi, madaraka na mamlaka, na zaidi mchango wa gharama za uendeshaji na mgawanyo wa rasilimali na mapato kati ya wahusika wakuu. Mambo haya, katika uzoefu wa nchi za wenzetu, ndiyo yaliyopelekea kuvunjika kwa miungano yao kwani huzaa kutiliana shaka na kutokuaminiana. Kwa vile yanachukua sura ya kisiasa (kutokana na sababu nilizozitaja), haya hayana chama wala itikadi kama nitakavyoonyesha huko mbele. Kamaalivyowahi kusema Prof. Issa Shivji:


"Ultimately, the question of the Union is primarily a political question and no amount of rhetoric about blood and cultural ties will matter when it comes to realpolitik."[8]


Yaani, "Mwisho wa yote, suala la Muungano linabakia kimsingi kuwa ni suala la kisiasa, na inapofikia kwenye siasa hasa, hotuba na kauli kali za jazba kuhusiana na mahusiano ya damu na ya kidugu, zote hazitafaa kitu."


Kwa hakika, kinyume na inavyojaribiwa kuonyeshwa na wengi kwamba Tanganyika imepoteza kila kitu katika muundo huu wakati Zanzibar imekabidhi sehemu tu ya madaraka yake, muundo wa Serikali mbili umepelekea wengi

kuamini kwamba kilichofanyika ni kiini macho tu kwani ni Zanzibar iliyokabidhi sehemu muhimu ya mamlaka yake (mahusiano ya nchi za nje, ulinzi na usalama, uraia, kodi na ushuru, sarafu, nguvu kuu za kuendeshea uchumi na

mengineyo) kwa Tanganyika na kisha Tanganyika ikajigeuza jina na kujiita Jamhuri ya Muungano. Na haya si maoni ya ngumbaru (kwa lugha ya Mwalimu Julius Nyerere) bali ni maoni ya watu wazito wakiwemo aliyekuwa Spika wa

Bunge na ambaye sasa ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa ambaye alisema kwa jinsi mambo yalivyofanyika, Zanzibar inaonekana kama vile ni invited guest' (mgeni aliyealikwa) katika Muungano.[9] Naye

msomi mashuhuri ulimwenguni, Prof. Ali Mazrui alisema baada ya Muungano Zanzibar imepoteza kila kitu muhimu wakati Tanganyika imebadilika jina tu na kuwa Tanzania huku ikiwa na mamlaka zaidi lakini ikibaki na Rais wake, nembo yake ya Taifa, wimbo wake wa Taifa na hata kiti chake katika Umoja wa Mataifa.[10]




Mkataba wa Muungano haujafuta Serikali ya Tanganyika


Katika makubaliano ya kimataifa yaliyounda Muungano, ambayo hata hivyo katika muda wote wa uhai wa Muungano yamekuwa hayafuatwi, hakuna kifungu hata kimoja kilichotoa au kuagiza kwamba Serikali ya Tanganyika ifutwe kwa

mujibu wa makubaliano hayo. Serikali ya Tanganyika, kama ilivyo ile ya Zanzibar, imelindwa na kifungu cha (v) kinachosomeka kwamba: "The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their respective territories".Kinachosemwa hapa ni kwamba "Sheria zilizopo za Tanganyika na za Zanzibar zitaendelea kufanya kazi na kuwa na nguvu katika maeneo yao."


Wataalamu wa katiba na sheria wanafahamu kwamba katiba ndio sheria mama ya sheria zote za nchi. Hivyo Katiba ya Tanganyika imelindwa na inapaswa kuwepo na Serikali yake iwepo, pamoja na viongozi wake kuwepo na

kusimamia mambo yasiyo ya Muungano. Katiba na sheria zaTanganyika ndizo zilizotakiwa zitumike katika eneo la Tanganyika kwa yale mambo yaliyokuwa hayamo kwenye Muungano kama ambavyo Katiba (au kabla ya hapo Matangazo ya Kikatiba Constitutional Decrees) na sheria za Zanzibar zinavyotumika katika eneo la Zanzibar kwa yale mambo ambayo si ya Muungano. Hiyo ndio tafsiri ya maeneo yao'.


Wazanzibari wanafahamu kwamba Serikali ya Tanganyika imefutwa kwa makusudi na Bunge laTanganyika kinyume na Makubaliano ya Muungano ili kujipa nafasi kuitumia Serikali ya Muungano, kama kwamba ndio Serikali ya Tanganyika. Lengo ni hatimaye kuiuwa Serikali yaZanzibar na kufanya Tanganyika mpya ikiwa na jina jipya la Tanzania lenye mipaka mipya, yaani kuwa nchi moja yenye Serikali Moja.


Hiyo ndio ghilba iliyofanywa na viongozi wa Tanganyika mara baada ya kuwekwa saini makubaliano. Kwa kusaidia kufichuwa ukweli wa hadaa hii, msomaji anashauriwa asome Sheria Na. 22 ya mwaka 1964 inayoitwa "Union of Tanganyika and Zanzibar Act, 1964."


Sheria hii ilipitishwa na Bunge la Tanganyika Aprili 25, 1964, siku moja kabla Muungano kuanza kufanya kazi. Ilikusudiwa kuthibisha kukubalika Muungano huo wa Tanganyika na Zanzibarupande wa Tanganyika (ratification). Kifungu cha (viii) cha Makubaliano ya Muunganokinaagiza ifanyike hivyo kwa pande zote mbili za Muungano.


Inasikitisha kusoma katika kifungu Na. 2 cha sheria hiyo kwamba:


"Existing law means the written and unwritten law as it exists immediately before Union Day but does not include the Constitution of Tanganyika in so far as it provides for the Government of the Republic of Tanganyika or any declaration or law or any provision which expires with effect from commencement of the Interim Constitution".


("Sheria iliyopo maana yake ni sheria iliyoandikwa na isiyoandikwa kama ilivyo kabla tu ya siku ya Muungano lakini haijumuishi Katiba ya Tanganyika kwa mintaraf ya kuiweka kwake Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika au tamko, sheria au kifungu chochote ambacho kinafutika kwa kuanza kufanya kazi Katiba ya Muda (ya Muungano))."


Kwa hivyo, wakati Bunge la Tanganyika linapitisha sheria ya kuridhia, ratify, kuwepo kwa Muungano kwa upande wa Tanganyika, sheria hiyo ilianza kupinga vifungu vya makubaliano hayo. Mfano mwengine ni kifungu Na. 7 cha sheria hiyo kinachosema:


"On the commencement of the Interim Constitution of the United Republic of Tanganyikaand Zanzibar, the Constitution of Tanganyika will cease to have effect for the Government of Tanganyika as a separate part of the United Republic".


("Itapoanza kufanya kazi Katiba ya Muda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika naZanzibar, Katiba ya Tanganyika itasita kuwa na maana kwa Serikali ya Tanganyika kamasehemu moja ya Jamhuri ya Muungano.")


Kwa maneno mengine, sheria ambazo zilitakiwa zitumike kwa Tanganyika kwa mambo ambayo si ya Muungano zilipewa maana mpya kwamba eti zisijumuishe Katiba ya Tanganyika.


Jambo moja lililo wazi, pamoja na hatua hii ya kuifuta Katiba ya Tanganyika, ni kwamba kule kuendelea kutambua kuwepo kwa sheria nyengine za Tanganyika bado kunamaanisha kuwepo kwa mamlaka ya Tanganyika ambako sheria hizo kwa mambo yote yasiyo mambo ya Muungano ziliendelea na zinaendelea kutumika hadi leo.


Zaidi, inapaswa ifahamike kwamba kufuta Katiba ya Tanganyika kulikofanywa na vifungu vya sheria hii hakukubadilisha makubaliano yaliyokwishatiwa saini kati ya Serikali mbili zilizounda Muungano, yaliyosema kwamba sheria za nchi mbili hizi zitaendelea kutumika katika maeneoyao. Bunge la Tanganyika, na hata hili la Muungano, halikuwa na mamlaka kutafsiri vifungu vya Mkataba wa Muungano.


Utaratibu wa kisheria ni kwamba kama Mkataba ulitakiwa kutafsiriwa basi ni walioandika rasimu ya mkataba huo ndio walipaswa kutoa tafsiri ya vifungu vyake, tafsiri ambayo ingepaswa iwe sehemu ya Mkataba huo. Na wala makubaliano yale hayakufuta wadhifa wa Rais wa Tanganyika. Si hivyo tu, bali pia Katiba ya Muungano ambayo ilitakiwa iwe ya muda tu kwa mwaka mmoja(interim) ilikuwa ni ile ya Tanganyika iliyofanyiwa marekebisho kwa ajili ya kutumika kwa Serikali ya Muungano.


Haikuruhusiwa kutumika kuiongoza Tanganyika kwa sababu Tanganyika ilikuwa na Katiba yake na Rais wake. Mwalimu Nyerere alikuwa na vyeo viwili, Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Makubaliano na Katiba ya Muungano na Rais wa Tanganyika kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika, kama alivyokuwa Mzee Karume ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Makubaliano na Katiba ya Muungano na akaendelea kubaki kuwa Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa Tangazo la Katiba ya Zanzibar (Constitutional Decrees).


Hivyo ndivyo makubaliano yalivyo hadi hii leo. Waliobadilika ni watu tu. Kufanya vyenginevyo ni kinyume na makubaliano yale na ndio sababu ya migogoro ya Muungano. Yaliyofanyika ni ujanja uliokuwa hauna nia njema kwa Zanzibar kama alivyosema Prof. Issa Shivji, mtaalamu wa Katiba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


"Lakini yote ya kuepusha Serikali ya Tanganyika kuwepo yalifanywa kwa makusudi kabisa, ili itumike Serikali ya Muungano kama ndio Tanganyika. Katika Sheria ile Na. 22 ya 1964, Rais wa Tanganyika amejipa madaraka ya kutunga na kutoa maagizo yanayohusu Muungano kwa kutumia amri (decrees) za sheria ya Tanganyika.
Siku ile inapopitishwa sheria ile zilipitishwa pia Decrees mbili zilizotokana na vifungu Na. 6 (3), cha 8 na cha 5 cha sheria hiyo Na. 22 ya 1964, yaani The Provisional Transitional Decree 1964, na ile ya Interim Constitution Decree 1964 ambazo zote hazikuwa halali maana ni Decrees zilizopitishwa na Bunge la Tanganyika zilizotokana na Sheria Na. 22 ya 1964 ya Tanganyika."


Miongoni mwa mambo yaliyodhihirisha kuwa hakukuwa na nia njema katika Muungano huu tokea awali ni pale wafanyakazi wa Serikali ya Tanganyika wote walipopandishwa vyeo kwa pamoja na kuwa wafanyakazi wa Muungano kama kifungu cha 3 (1) cha Provisional Transitional Decree kinavyosema:


"Every person who holds office in the service of the Republic of Tanganyika immediately before the Union Day, shall on Union Day be deemed to have been elected, appointed or otherwise selected to the corresponding office in the service of the United Republic."


Yaani kila mfanyakazi aliyekuwa wa Serikali ya Tanganyika mara kabla ya siku ya Muungano kufumba na kufumbuwa, pengine kwa uchawi wa kifimbo cha Mwalimu Nyerere, anakuwa mara moja mfanyakazi wa Serikali ya Muungano kuanzia siku ya Muungano. Huu tuuiteje kama si ujambazi wa kikatiba (constitutional banditry)?


Vivyo hivyo, kifungu cha 6 (i) cha Decree kinasema mara tu baada kuanza Muungano, Mahkama ya Tanganyika na Majaji wake wote nao watakuwa ndio Mahkama na Majaji wa Jamhuri ya Muungano kinyume na Makubaliano ya Muungano. Mpaka leo Katiba zote mbili hazitambuwi Mahkama (ukiondoa Mahkama ya Rufaa) kama ni suala la Muungano. Nembo ya Tanganyikainatumika kama nembo ya Serikali ya Muungano na Idara ya Mwanasheria Mkuu wa Tanganyikainachukuliwa kama Idara ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Muungano.


Haya yote hayamo na ni kinyume na Makubaliano ya 1964. Yote haya na kile kifungu cha 7 cha Sheria Na. 22 ya 1964 kinachofuta kuwepo kwa Serikali ya Tanganyika hayakubadilisha na wala hayana mahusiano na Makubaliano ya Muungano ya 1964. Yote haya yalifanywa na Bunge la Tanganyika kwa maslahi ya Tanganyika nje ya Makubaliano.


Aliyekuwa Spika wa Bunge na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Pius Msekwa, analifahamu vyema suala hili. Katika waraka wake alioutoa kwenye Semina kuhusu Muungano hapo Hoteli ya Mkonge, Tanga tarehe 25-27 Februari 1994 anasema:


"The Transitional Decree, 1964 published on 01/05/64, transferred persons who were holding office in the public service of the Republic of Tanganyika to the corresponding office in the public service of the United Republic of Tanzania. By the same decree the High Court of Tanganyika also became the High Court of UnitedRepublic of Tanzania and the public seal of Tanganyika became public seal of theUnited Republic."


Athari za hatua hizi kwa Zanzibar ziko wazi. Tanganyika imejigeuza Tanzania na imechukua mamlaka ya mambo muhimu ya Zanzibar huku ikijipa hadhi ya kuwa juu ya Serikali ya Zanzibarkinyume na Mkataba wa Muungano. Hii ndiyo siri ya viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kung'ang'ania mfumo wa Serikali mbili na kukataa kata kata mabadiliko yoyote ya mfumo huo kwani Tanganyika inanufaika nao kwa kuwa yenyewe ndiyo imekuwa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Muungano'. Kukubali muundo wa Serikali tatu ni kuzifanya Tanganyika na Zanzibar ziwe na hadhi na fursa sawa katika Muungano, jambo ambalo Tanganyika hailitaki maana kulikubali ni kukubali kupoteza fursa zote inazozipata hivi sasa kwa kujikweza kwake na kujifanya kuwa ndiyo Muungano'.


Ushahidi wa wazi wa hoja yangu hii ni kwamba mtu anapoangalia taasisi zote za Muungano zilizoundwa chini ya Katiba au sheria za Muungano ambazo zinazikutanisha Serikali mbili zilizopo sasa, ataona kuwa wajumbe wanaowakilisha upande wa Serikali ya Muungano wote ni kutoka Tanganyika. Hoja inayojitokeza ni kwamba Serikali ya Muungano ni ya shirika ambapoZanzibar ni sehemu ya ushirika huo, kwa nini basi wajumbe wanaowakilisha Serikali hiyo ya Muungano watoke upande wa Tanganyika peke yake? Jawabu ni rahisi. Serikali ya Muungano kwa hakika ni Serikali ya Tanganyika iliyojivika joho la Muungano.


Rais Jakaya Kikwete amekaririwa hadharani akisema matatizo ya Muungano hayatokani na muundo bali yanasababishwa na viongozi. Hoja, maelezo na mifano niliyoitoa hapo juu inatosha kumuonyesha Rais kwamba kauli yake si sahihi. Vyote viwili muundo na pia kukosekana kwa nia njema upande wa viongozi ni sababu za kuwepo kwa matatizo yasiyokwisha ya Muungano.


Sisi katika CUF tumesema wazi kwamba kuna haja ya kuuimarisha Muungano wetu kwa kurekebisha kasoro hii ya msingi. Njia ya kufanya hivyo ni kuzionyesha wazi wazi mamlaka zote tatu zilizomo katika Mkataba wa Muungano ili kuondosha khofu za kudhani mmoja anafaidika katika muundo huu na mwengine anakandamizwa. Serikali ya Zanzibar ionekane wazi wazi, Serikali ya Tanganyika ionekane wazi wazi, na Serikali ya Muungano ionekani wazi wazi. Hapo hapatakuwa na hofu ya mkubwa kummeza mdogo, wala mdogo kupendelewa na kupewa uwakilishi unaozidi kiwango chake.




Uvunjwaji wa Mkataba wa Muungano


Mbali na suala la muundo wa Muungano, maeneo mengine mengi yanayogusa msingi wa Mkataba wa Muungano yaliendelea kuvunjwa na Serikali ya Tanganyika ikivaa joho la Muungano.


Kifungu cha (viii) cha Mkataba wa Muungano kinaweka sharti kwamba Mkataba huo hautokuwa halali hadi pale Bunge la Tangayika na Baraza la Mapinduzi likishirikiana na Baraza la Mawaziri la Zanzibar yatakapopitisha sheria za kuridhia Mkataba huo. Upo ushahidi wa kutosha kwamba Bunge la Tanganyika lilikutana na kuuridhia Mkataba huo tarehe 25 Aprili, 1964. Hakuna ushahidi wowote kwamba Baraza la Mapinduzi likishirikiana na Baraza la Mawaziri la Zanzibaryalikaa kuuridhia Mkataba huo. Kwa hakika ushahidi ulioibuliwa na Prof. Issa Shivji katika kitabu chake cha karibuni kabisa, Pan-Africanism or Pragmatism? Lesssons of Tanganyika-Zanzibar Union umeweka wazi pasina chembe ya wasiwasi kwamba Mkataba huo haujaridhiwa na upande wa Zanzibar hadi hii leo. Ndiyo kusema, Mkataba wa Muungano haujapata uhalali wa kisheria hadi leo.


Kifungu cha (iii) cha Mkataba wa Muungano kiliorodhesha mambo 11 tu ambayo ndiyo yaliyokubaliwa na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika kuwa mambo ya Muungano. Hata hivyo, kipindi cha miaka 45 ya Muungano kimeshuhudia mambo hayo yakiongezwa isivyo halali kwa kutumia chombo kisicho na mamlaka ya kufanya hivyo yaani Bunge la Muungano na sasa kufikia 23 lakini ukiyanyumbua yanafikia 35. Ikumbukwe kwamba kila hatua ya kuongeza mambo ya Muungano maana yake ni kuchukua mamlaka ya Zanzibar na kuyahaulisha kwa Serikali ya Muungano ambayo kama tulivyokwisha onyesha kwa hakika hasa ni Serikali ya Tanganyika.


Kifungu cha (vii) cha Mkataba huo kinataka Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mashauriano na makubaliano na Makamu wa Rais ambaye pia ni Rais wa Zanzibar kuunda Tume ya Katiba kwa lengo la kutayarisha rasimu ya Katiba ya Kudumu ya Muungano na baadaye kuifikisha rasimu hiyo mbele ya Bunge la Katiba (Constituent Assembly) litakalokuwa na wajumbe idadi sawa kati ya Zanzibar na Tanganyika kama watavyokubaliana viongozi hao wawili. Hatua hii muhimu sanakikatiba ilitakiwa itekelezwe ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tokea tarehe ya Muungano. Hadi hii leo hakuna Tume ya Katiba iliyoundwa wala Bunge la Katiba lililoundwa na kuitishwa kwa madhumuni ya kupitisha Katiba ya Kudumu ya Muungano. Kilichofanyika ni kuwa siku moja kabla ya kumalizika mwaka mmoja uliotakiwa, Bunge la Muungano lilitakiwa kupitisha sheria ya kuahirisha kwa muda usiojulikana tarehe ya kutekelezwa kwa hatua hii na hadi leo imesahaulika kabisa.


Lakini mbali na dhoruba hizo dhidi ya Mkataba wa Muungano, rungu kubwa zaidi ambalo ndilo lililotumika kuimaliza Zanzibar lilikuwa ni kule kuunganishwa kwa vyama vya ASP na TANU na kuzaliwa CCM huku ikijipa madaraka juu ya vyombo vyengine vyote vya maamuzi katika nchi ikiwemo Serikali na Bunge na Baraza la Wawakilishi. Chini ya dhana ya Chama kushika hatamu(Party Supremacy) iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere kwa lengo la kujilimbikizia madaraka yeye na Chama alichokuwa akikiongoza kama milki yake binafsi, CCM iliweza kutoa maagizo na maamuru mazito bila ya kujali madaraka ya Serikali ya Zanzibar yaliyotolewa kupitia Mkataba wa Muungano na hivyo kujinyakulia uwezo wote wa kuitawala Zanzibar ipendavyo huku viongozi wa Zanzibar wanaohoji wakituhumiwa kwamba wanapinga nidhamu ya Chama.




Matatizo yatokanayo na kiini cha tatizo


Kiini cha tatizo la msingi la Muungano ambalo kwa mtazamo wa CUF ni muundo wake unaotokana na tafsiri potofu ya Mkataba wa Muungano (Articles of Union) ndicho kimepelekea kujitokeza kwa matatizo mengine katika miaka 45 hii na ambayo yanaongezeka kila uchao.


Mtu anapoangalia matatizo au hizi zinazoitwa kero atagundua kuwa karibu yote yanatokana ama na mshirika mmoja (mara nyingi Zanzibar) kutokuuamini au kuutilia shaka upande mwengine, au mshirika wa pili (mara nyingi Tanganyika ikivaa joho la Muungano) kuamini kwamba ina haki ya moja kwa moja kuamua na kutekeleza mambo fulani bila ya kulazimika kupata ridhaa ya upande wa pili ambao inahisi kama imeubeba tu. Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa tatizo linarudi kwenye muundo. Zanzibar haifahamu mamlaka ya Muungano katika Serikali ya Muungano yanaishia wapi ambapo mamlaka kwa mambo yasiyo ya Muungano kwa ajili yaTanganyika yanaanza. Tanganyika nayo kwa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];kuwemo' kwake katika Serikali ya Muungano kunaifanya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];ishindwe kufahamu' ni vipi na wapi Zanzibar inapata mamlaka ya kuhoji mambo ambayo &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];yameshatamkwa' kwamba ni ya Muungano hata kama hayakuwemo katika Mkataba wa asili wa Muungano. Hali hii inaonekana katika kila kile kinachoitwa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];kero' za Muungano.


Mifano inaweza kutolewa kwa takriban mambo yote, lakini kwa madhumuni ya waraka huu tuchukue mifano ya mambo matatu yafuatayo yanayozusha malalamiko:



  1. Umilikaji wa Mafuta na Gesi asilia.



  1. Uchangiaji katika gharama za Muungano na mgawanyo wa mapato yanayotokana na Muungano.



  1. Uwakilishi wa Zanzibar katika Bunge la Muungano.


Umilikaji wa Mafuta na Gesi asilia


Kwanza, kuingizwa kwake katika orodha ya mambo ya Muungano (kama ilivyo kwa mambo mengi yaliyoongezwa baadaye) hakukufuata taratibu za Serikali ya Muungano (ambayo pia ni Serikali ya Tanganyika kwa mambo yasiyo ya Muungano) kuishauri na kupata ridhaa ya Zanzibar. Pili, Zanzibar inataka kujua ikiwa mafuta yanapaswa kuwa suala la Muungano na hivyo mapato yatakayopatikana yanufaishe pande zote mbili, kwa nini madini mengine yanayopatikana Bara kama vile dhahabu, almasi au tanzanite hayakufanywa pia kuwa ya Muungano na hivyo kunufaisha pande mbili pia? Kwa hivi sasa, ambapo si mambo ya Muungano, mapato yake yanaponufaisha Tanganyika peke yake, yanaingia katika mfuko (account) upi wa matumizi? Tatu, ikiwa mapato yatakayopatikana kutokana na mafuta yataingia katika mfuko wa Muungano, kuna uhakika gani wa kutumika kwa shughuli za Muungano tu wakati hakuna mifuko tofauti ya fedha kwa shughuli za Muungano na zile za Tanganyika zisizo za Muungano?


Uchangiaji katika gharama za Muungano na mgawanyo wa mapato yanayotokana na Muungano


Je, mtu anaposema Zanzibar haichangii gharama za uendeshaji wa vyombo na taasisi za Muungano kwa sababu tu Serikali ya Zanzibar haitoi fungu la fedha na kuliingiza katika Serikali ya Muungano, Tanganyika ambayo hata

Serikali haina inachangia vipi na kiasi gani? Ikiwa mchango wake unatolewa na Serikali ya Muungano, kwani hii siyo serikali ya shirika ambapoZanzibar ni mbia? Vipi basi Zanzibar itakiwe ichangie mara mbili kwa kutumia hadhi mbili

tofauti? Na ikichangia (iwapo itachangia), ina uhakika upi kwamba itakachotoa hakitatumiwa na Serikali ya Muungano kwa shughuli za Tanganyika zisizo za Muungano ikitumia mamlaka yake kwa madhumuni hayo? Vivyo

hivyo kwa mapato yatokanayo na vyombo na taasisi za Muungano, tunajua Zanzibar inapata mgao wake na kiasi chake kimewekwa wazi (ingawa hakikubaliki kwa Wazanzibari). Masuala yanakuja: Yale mapato yanayobaki katika

Serikali ya Muungano, kuna kipi cha kuonyesha mpaka wa matumizi yake kwa Muungano na kwa shughuli za Tanganyikazisizo za Muungano? Uadilifu na uwajibikaji wa matumizi yatokanayo na mgao huu wa mapato utaonekana vipi?


Uwakilishi wa Zanzibar katika Bunge la Muungano

Wananchi wengi wa Tanganyika wanahoji vipi Zanzibar iliyo ndogo na ambayo ina watu wasiozidi milioni moja inawakilishwa na wabunge wa kuchaguliwa 50 wakati Dar es Salaam yenye wananchi wengi zaidi ina wabunge wa kuchaguliwa 7 tu? Wabunge hawa

wanashiriki mijadala yote ya Bunge ikiwemo ya mambo yasiyo ya Muungano (ambayo kwa usahihi yatakuwa ni mamlaka ya Tanganyika kwa mambo yasiyo ya Muungano yanayosimamiwa na Serikali ya Muungano). Wanapata wapi uhalali wa kufanya hivyo

wakati Wazanzibari hawapangiwi shughuli hizo (kwa mfano elimu, afya, kilimo, maji, umeme, habari, michezo, biashara, viwanda,

serikali za mitaa n.k.) na Serikali ya Muungano wala hawasimamiwi katika mambo hayo na Bunge la Muungano? Uko wapi mpaka wa mamlaka ya Wazanzibari katika ushiriki wa Bunge hilowakati wao wana Serikali yao inayopanga na Baraza la Wawakilishi lao linalosimamia mamboyao kama hayo yasiyo ya Muungano?


Mifano hii inatosha kuonyesha kwamba karibu matatizo yote, kama si yote, yanatokana na mkanganyiko na mgongano wa maslahi kati ya pande mbili ambao nao unasababishwa na mfumo usio wazi kuhusiana na mgawanyo wa madaraka kati ya mamlaka tatu za Muungano zinazotambuliwa katika Mkataba wa Muungano.


http://mfumokristo.blogspot.com/2012/05/khatima-ya-zanzibar-na-mustakbali-wa.html
 
Nafasi ya Zanzibar katika Muungano



Baada ya kuangalia kiini cha matatizo ya Muungano kinachotokana na muundo wa Muungano, sasa tuangalie nafasi ya Zanzibar katika Muungano huu, hasa kufuatia kauli za kuidhalilishaZanzibar zilizotolewa na wanasiasa wa Tanganyika hivi karibuni wakiongozwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.


Kutokana na kule kule kujaribu kujisahaulisha kuwepo kwa Mkataba wa Muungano ambao ndio sheria kuu (grundnorm) ya Muungano na kuifanya Katiba inayoitwa ya Jamhuri ya Muungano kuwa ndiyo Katiba mama na hivyo kuikweza kwamba eti iko juu ya Katiba ya Zanzibar, zimetolewa kauli kwamba kufuatia hatua ya kuungana na Tanganyika, Zanzibar imepoteza hadhi na sifa ya kuwa nchi.


Waliosema hivi wanasahau kwamba Zanzibar ina Katiba yake ambayo ina hadhi sawa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, na kwamba zote mbili zinapaswa kutafsiri kisawa sawa Makubaliano ya Muungano.


Katiba ya Zanzibar inatamka wazi wazi kwamba Zanzibar ni nchi. Utangulizi (Preamble) wa Katiba hiyo ambao unaeleza dhamira ya Wazanzibari wakiwa ndiyo wenye Katiba hiyo (sponsors of the Constitution) unabainisha wazi wazi dhamira ya Wazanzibari kulinda na kudumisha nchiyao na yale yote yanayoitambulisha Zanzibar kama nchi. Sehemu ya Utangulizi huo inasomeka:


"NA KWA KUWA tunazingatia na kuthamini kazi nzuri ya Kimapinduzi iliyofanywa na Viongozi wa Mapinduzi, wakiongozwa na Mwasisi wa Chama cha ASP na Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, ambaye fikra zake zitaendelezwa na kudumishwa daima, kizazi baada ya kizazi katika kupambana na Ukoloni, Ubepari Unyonge, Uonevu na Dharau, na badala yake kudumisha Uhuru na Umoja, Haki na Usawa, Heshima na Utu;"


Ni bahati mbaya kwamba baadhi ya watu wamekuwa wakinukuu vibaya kifungu cha (1) cha Katiba ya Zanzibar kinachosema “Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” kumaanisha kwamba kwa kuwa kwake sehemu ya Jamhuri ya Muungano kunaiondolea na kuipotezea Zanzibar hadhi yake ya kubakia kuwa nchi. Tafsiri hiyo si sahihi kama ilivyofafanuliwa na Jaji Abdullahi D. Zuru kutoka Nigeria, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kupitia Sheria(Law Review Commission) Zanzibar.


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilimuagiza Jaji Zuru kuipitia Katiba ya Zanzibar na kupendekeza marekebisho ikibidi. Jaji Zuru amesema katika ripoti yake kuhusu kifungu cha (1) cha Sura ya Kwanza, Sehemu ya Kwanza ya Katiba ya Zanzibar kuwa:


"Mtu akisoma kwa makini Utangulizi (Preamble) na Katiba yote kwa jumla, ataelewa kwamba Zanzibar ni dola yenye mamlaka yake kamili (sovereign state) na kwamba wale waliotunga Katiba hii hawakuwa na nia ya kusalimisha na kuachia mamlaka (sovereignty)ya Zanzibar wakati wa kuundwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, ambao ulizaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo, mtu akisoma maelezo ya kifungu cha (1) cha Katiba anapigwa na butwaa na kushangaa kwa nini kifungu hicho cha kwanza kwa kinyemela (surreptiously) kimesalimisha au kimepuuza mamlaka hayo."


Jaji Zuru anaendelea kusema kuwa anaamini kwamba waanzilishi wa hatua ya kuzileta pamojaZanzibar na Tanganyika kuwa Jamhuri moja, hawajakusudia kuwa hatua hiyo ipoteze (erode)uhuru wa nchi yoyote kati ya nchi mbili kamili zilizohusika.


Kinyume na hayo, maoni yake ni kwamba nia ilikuwa kuimarisha uhuru wa kila moja ya nchi hizo mbili sambamba na ule wa Muungano utakaozaliwa. Mtaalamu huyo anafahamisha kwamba kisheria, "Haki mbili zikikutana ndani ya mtu mmoja, ni sawa na kusema kwamba ziko ndani ya watu wawili."


Labda tuiweke kwa Kiingereza, kama alivyoandika mwenyewe, kwa kufahamika zaidi: "It is a trite law that when two rights meet in one person, it is the same as if that were in two persons."


Anaendelea kusema kwamba ni imani ya Tume yake kabisa kuwa ulipoundwa Muungano,Zanzibar ilikusudia na ilisisitiza juu ya kuendeleza mamlaka yake ndani ya utaratibu wa Muungano. Anafafanua:


"Kutokana na haya, tunaamini kwamba hadhi ya Zanzibar kama inavyoelezwa katika kifungu cha (1) imepotoshwa kwa sababu (kifungu) hakielezi nia ya wenye katiba (sponsors of this constitution) na madaraka yaliyotolewa na watu wa Zanzibar..."


Labda turudi nyuma kidogo tufahamishe kuwa Tume ya Jaji Zuru imeeleza mwanzoni kuwa madaraka waliyo nayo Baraza la Wawakilishi, ambalo ndilo lililotunga Katiba hiyo mwaka 1984, yanatokana na wananchi na kwamba Baraza linayashikilia madaraka hayo kama amana (trust)kwa niaba ya wananchi hao. "Kwa hiyo, kushindwa kwa Serikali kusimamia misingi ya katiba ni sawa na kwenda kinyume na amana waliyokabidhiwa na watu wa Zanzibar ."


Haya yanaelezwa wazi katika kifungu cha 9 cha Katiba ya Zanzibar kinachosema,


"9.-(1) Zanzibar itakuwa ni nchi ya kidemokrasia na haki za kijamii.
(2) Kwa hiyo hapa inaelezwa rasmi kwamba:-
(a) Mamlaka ya kuendesha nchi ni ya wananchi wenyewe ambapo nguvu na uwezo wote wa Serikali kufuatana na Katiba utatoka kwa wananchi wenyewe."


Tukiendelea na hoja, Jaji Zuru anasema maelezo ya kifungu cha (1) cha Katiba, ambacho ndicho kama mlango wa kuingilia kwenye Katiba yenyewe, yanampa msomaji wa nje sura ya kwambaZanzibar si nchi yenye mamlaka yake wenyewe. "Kwa hiyo, tunachukulia maelezo haya kama ni kwenda kinyume na nia ya watu wa Zanzibar ambayo iko wazi na bayana katika Utangulizi(Preamble) na sehemu nyengine zinazohusika katika Katiba."


Kutokana na haya Tume imependekeza kifungu hiki kiandikwe upya ili kuwakilisha nia ya watu wa Zanzibar. Kisomeke kama ifuatavyo:


"Zanzibar ni, na itabaki dola yenye mamlaka, na itakuwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa matakwa na masharti yaliyotajwa katika Mkataba wa Muungano baina ya Dola ya Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika.”


Kwa madhumuni ya uelewa zaidi tutanukuu tena kwa Kiingereza kama alivyoandika mwenyewe Jaji Zuru:


"Zanzibar is and shall remain a sovereign state, and shall exist as an integral part of the United Republic of Tanzania, in accordance with the terms and conditions stipulated in the Articles of Union between the State of Zanzibar and the Republic of Tanganyika.”


Kifungu cha 2 (2) cha Katiba ya Zanzibar kinasema, "Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali, Rais wa Jamhuri ya Muungano akishauriana na Rais anaweza kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa."


Tume inasema kwa vile Rais wa Zanzibar ndiye mlinzi wa dhamana (custodian) wa mamlaka ya watu wa Zanzibar, anapaswa kuchukuwa jukumu la mbele (vital role) katika uamuzi na ukataji wa mipaka ya kiutawala ya Zanzibar. Hivyo, haitoshi 'kushauriana' tu, bali lazima ridhaa na kauli(consent and approval) ya Rais wa Zanzibar ipatikane.


Mapendekezo ya Tume ya Jaji Zuru yalipelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Disemba 19, 2001, lakini hadi hii leo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haijachukua hatua zozote kuyafikisha mbele ya Baraza la Wawakilishi ili kurekebisha mapungufu ya kiuandishi ya Katiba ya Zanzibar na kutafsiri kisawasawa dhamira ya wananchi wa Zanzibar.


Tukiachana na mapendekezo hayo, tuangalie Sura ya Kumi na Tatu ya Katiba ya Zanzibar. Kifungu cha 132 (1) kinachosema:


"132.- (1) Hakuna sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumikaZanzibar mpaka sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya Muungano tu na ipitishwe kulingana na maelezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Sheria kama hiyo lazima ipelekwe mbele ya Baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika.
(3) Pale sheria ndogo inapoundwa kwa mujibu wa uwezo uliowekwa chini ya vifungu vya (1) na (2) sheria hii itatumika tu pale itapotimiza shuruti zote zilizowekwa kwa matumizi ya Sheria mama kama ilivyoamrishwa katika kifungu hiki."


Hapa mambo mawili yanajitokeza. Kwanza kati ya mambo yote ya Muuungano, zaidi ya yale kumi na moja ya asili, yaliyoongezwa katika orodha ya mambo ya muuungano (xii –xxiii) ni moja tu, kuhusu uandikishwaji wa vyama vya siasa, ambapo mswada ulipelekwa Baraza la Wawakilishi, ukajadiliwa na kupitishwa.


Ndiyo maana imo katika vitabu vya sheria (Statute Books) vya Sheria za Zanzibar. Mambo mengine yote hayamo katika vitabu ya sheria vya Zanzibar na anayevitekeleza anaweza kushtakiwa kwa kwenda kinyume na matakwa ya Katiba ya Zanzibar.


Mambo hayo yaliyoongezwa juu ya Makubaliano ya Muungano ya asili, yaani, yale kumi na moja (11) ni haya, kama yanavyoelezwa katika Nyongeza ya Kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano:-

(xii) Mambo yote yanayohusika na Sarafu na Fedha kwa ajili ya malipo yote halali (pamoja na noti); mabenki; fedha za kigeni na usimamizi juu ya mambo yanayohusika na fedha za kigeni.​
(xiii) Leseni za Viwanda na Takwimu.​
(xiv) Elimu ya Juu.​
(xv) Maliasili ya Mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya motokaa na mafuta aina ya petroli na aina nyinginezo za mafuta au bidhaa za mafuta, na gesi asilia.​
(xvi) Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania na mambo yanayohusika na kazi za Baraza hilo.​
(xvii) Usafiri na Usafirishaji wa Anga.​
(xviii) Utafiti.​
(xix) Utabiri wa Hali ya Hewa.​
(xx) Takwimu.​
(xxi) Mahkama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano.​
(xxii) Uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana nayo.​
(xxiii) Uvuvi wa Bahari Kuu.​


Yote haya yameingizwa katika orodha ya mambo ya Muungano kinyume na sheria na taratibu, na bila ya ridhaa ya Zanzibar kwa mujibu wa Katiba. Hivyo ni batili na hayana nguvu za kisheria.


Pili, Matamko na Matangazo ya Kisheria ya Rais wa Muungano (Presidential Decrees and Orders) ambayo hutolewa kutokana na nguvu anazopewa ama na katiba au sheria mama pale yanapokuwa yanahusu mambo ya Muungano yaliyoongezwa isivyo halali ambayo yenyewe yanatokana na sheria batili zilizotungwa kinyume na matakwa ya kifungu cha 132 (3) cha Katiba ya Zanzibar nayo yatakuwa ni batili na hayatakuwa na nguvu za kuweza kusimama kisheria.


Mfano ni Amri ya Rais (Presidential Order) iliyotangazwa mwaka 1969 wakati wa Mwalimu Julius Nyerere kuanzishwa kwa Shirika la Uendelezaji Petroli Tanzania (TPDC), na kulipa mamlaka shirika hilo kuwa na nguvu kisheria hadi katika Visiwa vya Zanzibar itakuwa ni batili chini ya masharti ya kifungu cha 132 (3) cha Katiba ya Zanzibar.


Kifungu kinachofuata yaani 133 (1) kinasema:


"133.-(1) Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi au kwa utaratibu uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu ya kisheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
(2) Masharti yaliyomo katika kijifungu hiki hayatalizuwia Bunge kutumia mamlaka ya kutoza kodi ya aina yoyote inayohusiana na mambo ya Muungano kwa mujibu wa madaraka ya Bunge hilo, kwa kujuwa kwamba mashauriano baina ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano yamefanywa na kukubalika sehemu zote mbili kabla kupitishwa sheria."


Si jambo la siri kwamba kulikuwa na mvutano mkubwa kati ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Dk. Salmin Amour na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hadi leo wananchi wa Zanzibar wanaiona TRA kama ndiye adui mkubwa wa uchumi wao, iliyoua biashara visiwani na kuwatia Wazanzibari katika ufukara usiosemeka.


Ni wazi basi kwamba uundwaji wa TRA haujatimiza masharti ya kifungu cha 133 (2) cha Katiba ya Zanzibar.


Inawezekana kukazuka hoja kwamba pale Katiba ya Zanzibar inapopingana na Katiba ya Muungano ni ile ya Muungano ndio yenye nguvu. Ndio. Hii ni kuhusu vifungu vinavyowiana na Makubaliano ya Muungano kama yalivyokuwa yamekubaliwa na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika hapo mwaka 1964. Vyengine vyote ni batili na hapo moja kwa kwa moja Katiba ya Zanzibar ndiyo itakayosimama.


Kwa msingi wa hoja hizi, ni ukweli usio na ubishi kwamba Zanzibar imeendelea kubaki na hadhi yake kama nchi hata baada ya kuingia katika Muungano na Tanganyika na ndiyo maana Katiba yake, pamoja na mapungufu madogo madogo, bado imelinda kwa nguvu zote hadhi hiyo.


Naelewa kwamba kuna watu wanatumia uamuzi wa Mahkama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano katika kesi maarufu ya Machano Khamis Ali na wenzake 18 dhidi ya SMZ uliotamka kwamba Zanzibar si nchi na kwamba kosa la uhaini haliwezi kutendeka Zanzibar kuwa ni msingi wa hoja kwamba vifungu nilivyovitaja vya Katiba ya Zanzibar vinakuwa havina maana yoyote pale vinaposititiza hadhi ya Zanzibar kama nchi.


Ni muhimu kueleweka kwamba uamuzi huu wa Mahkama ya Rufaa umejaa utatanishi. Kwanza, ulitolewa wakati Serikali ikiwa tayari imeondosha mashtaka dhidi ya watuhumiwa na kuwaachia huru. Kwa msingi huo, mtu anajiuliza uamuzi huo wa Mahkama ya Rufaa wakati unatolewa ulikuwa na uhalali upi kisheria. Lakini pili, mtaalamu wa masuala ya katiba anayeongoza hapa Tanzania, Prof. Issa Shivji amefanya mapitio ya uamuzi huo na kubainisha makosa mengi sana ya kisheria yaliyomo. Kubwa katika makosa hayo ni kule Majaji wanaohusika kudharau na kutoitumia kabisa Katiba ya Zanzibar katika kufikia uamuzi wao. Katika hitimisho lake, Prof. Shivji anasema:


“The conclusion from this quick examination of the Zanzibar Constitution is that Zanzibar is a sovereign and a state, albeit its sovereignty is limited and the jurisdiction of the Executive and the Legislature is limited to non-Union matters in Zanzibar while its Judiciary, as epitomised by the High Court, has unlimited jurisdiction. A Mzanzibari owes allegiance to the State of Zanzibar and therefore an offence of treason can be committed against the state of Zanzibar. This is irrespective of the fact that treason may be stipulated as an offence in the union law; nevertheless it can be tried in the courts of Zanzibar.” [11]


“Hitimisho la upembuzi huu wa haraka wa Katiba ya Zanzibar ni kwamba Zanzibar ni dola na ni nchi, ijapokuwa nguvu yake ya kidola ina mipaka na uwezo wa Mamlaka ya Utawala na Mamlaka ya Kutunga Sheria umewekewa

mipaka kwa mambo yasiyo ya Muungano ndani ya Zanzibar wakati Mamlaka ya Utoaji Haki, ikiwa inaongozwa na Mahkama Kuu, ina uwezo kamili usio na mipaka. Mzanzibari ana utii kwa Dola ya Zanzibar na hivyo kosa la uhaini

linaweza kutendeka dhidi ya Dola ya Zanzibar. Hii ni bila ya kujali kwamba uhaini unaweza kuainishwa kuwa ni kosa kupitia sheria ya Muungano; lakini bado kosa hilo linaweza kuhukumiwa katika Mahkama za Zanzibar.”

Mfumo Kristo: KHATIMA YA ZANZIBAR NA MUSTAKBALI WA MUUNGANO
 
Muungano wa Serikali tatu utaongeza gharama?


Baada ya kuangalia nafasi ya Tanganyika na ya Zanzibar katika Muungano na madaraka yao, na kuonyesha kwamba njia pekee ya kushughulikia matatizo ya msingi ya Muungano ni kwa kurejea katika Mkataba wa Muungano na hivyo kuanzisha mfumo wa Serikali tatu, ni vyema tutafakari kidogo suala la gharama za uendeshaji wa mfumo huo.


Wapinzani wa Muungano imara chini ya msingi madhubuti wa Shirikisho la Serikali tatu wamekuwa wakiibua mara kwa mara hoja ya kuongezeka kwa gharama za utawala na uendeshaji kama kikwazo cha kukwamisha juhudi za kuuimarisha Muungano.


Hoja hii imeonekana ni dhaifu na isiyo na msingi kabisa kufuatia kuundwa kwa Tume ya Pamoja ya Fedha (Joint Finance Commission) ambayo ripoti zake za awali zimekaliwa na Serikali ya Muungano hadi leo baada ya kutoa picha halisi ya jinsi mchango wa Muungano unavyopaswa uwe. Tume hiyo imeipa kazi kampuni ya PriceWaterhouseCoopers kufanya uchambuzi halisi wa mambo yepi ni ya Muungano halisi na yepi ni ya Tanganyika na yepi ni ya Zanzibar. Baada ya orodha kupatikana, watafiti wakatafuta matumizi halisi ya bajeti ya vifungu hivyo kwa muda wa kiasi cha miaka 10 iliyopita. Watafiti hao walikwenda mbali zaidi ya hapo na kukusanya mapato yote kwa kila kifungu cha mambo ya Muungano halisi. Mwishowe, wakalinganisha iwapo mapato yanakidhi matumizi au yana nakisi (upungufu)?


Kilichojitokeza ni kwamba kwa mwaka wa fedha 2003/2004 pekee, matumizi halisi kwa vifungu vya Muungano yalikuwa Shs. 537,258.4 bilioni na mapato halisi kwa mwaka huo yalikuwa ni Shs. 1,030,826.1 bilioni. Tofauti ya vifungu hivyo vimetoa ziada ya ya Shs. 493,567.7 bilioni kwa mwaka huo. Ziada hii haiingizi mapato yanayotokana na misaada kutoka nje au mikopo. Ziada hii hutumika kwa shughuli za Tanganyika zisizo za Muungano.


Ukweli huu unaonyesha hata kama kungekuwa na Serikali tatu kusingekuwa na haja yoyote kwa Serikali ya Zanzibar na ile ya Tanganyika kulipia fedha za ziada kama wahusika watatunza na kuweka kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi ya mambo ya Muungano halisi badala ya yale ya Tanganyika kuchanganywa na ya Muungano. Mambo yasiyokuwa ya Muungano yaTanganyika yalipotengwa nje ya yale ya Muungano, gharama za mambo ya Muungano zimejidhihirisha wazi bila ya kujificha na kuonesha kwamba zinaweza kulipiwa kupitia mapato ya mambo ya Muungano pekee na ziada kubaki. Lakini hili limekuwa rahisi kwa kukubali ukweli kwamba kuna mafungu matatu ya mapato na matumizi katika Serikali zetu mbili. Mafungu hayo ni la SMZ kwa mambo yake yasiyo mambo ya Muungano, la Serikali ya Muungano kwa mambo ya Muungano, na la Serikali ya Muungano inayofanya kazi za Tanganyika kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano. Kinachohitajika sasa ni hili kuliweka wazi kwa viongozi kuweka nia njema na kuuweka sawa muundo wa Muungano wetu ili uzionyeshe waziwazi mamlaka zote tatu.










Vipi tutoke hapa tulipo?


Inakaribia miaka 45 sasa tangu uundwe Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kulikuwa na wakati wa kutosha kurekebisha kasoro zilizopo. Hilo halikuwezekana kutokana na ubabe wa Mwalimu Nyerere ambaye aliamua kuwatia shemere Wazanzibari na kuhakikisha Muungano unakwenda kama alivyotaka yeye hata baada ya ‘kuondoka madarakani'.


Si jambo la kuficha kwamba wananchi wa pande zote mbili za Muungano wamechoshwa na unafiki uliopo na wanadai Katiba ya kweli kweli itakayoweka misingi mipya ya ushirikiano.


Kama nilivyoeleza mwanzoni, kiini cha matatizo ya Muungano ni kutokuheshimiwa kwa Mkataba wa Muungano (Articles of Union) ambao kisheria ni Mkataba wa Kimataifa unaopaswa kuheshimiwa kwa kuzingatia masharti yote yanayohusu mikataba ya kimataifa.


Haidhuru sasa ni takriban miaka 45 tokea kuanza kwa hatua za kuukanyaga kanyaga Mkataba wa Muungano mara tu baada ya kutiwa saini na Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, na Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, lakini ukweli utabaki kuwa huo ulikuwa ndiyo msingi pekee, nasisitiza tena, pekee, uliokubaliwa na viongozi hao wawili kuongoza mahusiano ya nchi zetu mbili kupitia Muungano.


Wakati sasa umefika tukubali kwamba suluhisho la matatizo haya siyo kuendelea kuunda Tume au Kamati au kuandaa warsha, semina, makongamano na mikutano. Suluhisho ni kutekeleza kwa dhati Mkataba wa Muungano (Articles of Union) ambao ni mkataba wa kimataifa wa nchi mbili huru.


Kujaribu kulazimisha kutumia Katiba inayoitwa ya Jamhuri ya Muungano kama ilivyo sasa ambayo inakosa uhalali wa kisheria kuzima madai ya wananchi wa Zanzibar hakuwezi kukubalika tena katika zama hizi.


Kwa msingi huo, hakuna njia ya mkato ya kuyashughulikia matatizo ya Muungano bila ya kwenda kwenye kiini cha matatizo hayo ambacho ni kutokuheshimiwa kwa Mkataba wa Muungano. Wahenga wamesema, Mwiba uchomeapo ndipo utokeapo. Ili kuyaheshimu Makubaliano ya Muungano, yafuatayo ni lazima yafanyike:



  1. Kwa kuwa Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar la mwaka 1964 ambalo lilikuwa ni Baraza la Mapinduzi halikupewa nafasi ya kuuridhia (ratify) Mkataba wa Muungano, hivyo basi kwanza kabisa, na kabla ya kuchukua hatua nyengine yoyote, ni lazima Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar kwa sasa ambalo ni Baraza la Wawakilishi lipewe nafasi ya kuuridhia Mkataba huo ili kuupa uhalali wa kisheria kwa upande wa Zanzibar na hivyo kuupa uhalali wa kisheria Muungano wenyewe kama yalivyo masharti ya kifungu cha (viii) cha Mkataba huo wa Muungano.



  1. Kwa ujumla tuupitie tena Mkataba wa Muungano na kurekebisha vifungu vyenye utatanishi. Kama Muungano huu haukuwa na mtego, ulikuja kwa ridhaa za Serikali zetu mbili, vipi tunashindwa kukaa tena tukaupitia baada ya miaka 45 na kuuweka kwenye hali ya kuvutia hata majirani zetu wakajiunga?



  1. Katiba ya Zanzibar itumike Zanzibar kwa mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kama yalivyo masharti ya kifungu cha (v) cha Mkataba wa Muungano.



  1. Katiba ya Tanganyika (ile iliyokuwepo kabla ya kurekebishwa kuingiza mambo ya Muungano) nayo irejee kutumika Tanganyika kwa mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kama yalivyo masharti ya kifungu cha (v) cha Mkataba wa Muungano.



  1. Kwa kutumia Katiba ya Tanganyika, iundwe Serikali ya Tanganyika inayoshughulika na mambo yasiyo ya Muungano, kama Serikali ya Zanzibar inavyoshughulika na mambo yake ambayo si ya Muungano.



  1. Serikali ya Muungano ishughulike na yale mambo 11 tu ya asili yaliyokubaliwa kuwa ndiyo mambo ya Muungano kwa mujibu wa kifungu cha (iv) cha Mkataba wa Muungano.



  1. Mambo mengine yote 12 yaliyoongezwa katika orodha ya mambo ya Muungano kinyume na Mkataba wa Muungano yaondolewe katika orodha hiyo na yarudi katika mamlaka za Zanzibar na Tanganyika.



  1. Wafanyakazi wa Tanganyika wasihusike na mambo ya Muungano, wawe katika "civil service" (mfumo wa wafanyakazi Serikalini) wa Tanganyika, kama walivyo wa Zanzibar kwa Zanzibar (wasio wa taasisi za Muungano).



  1. Urejee utaratibu wa kuwepo kwa Makamu wawili wa Rais wa Muungano kama yalivyo masharti ya kifungu cha (iii) (b) cha Mkataba wa Muungano ambapo Rais wa Zanzibar na Rais wa Tanganyika wawe Makamu wa Rais wa Muungano kwa mujibu wa nyadhifa zao.



  1. Iundwe Tume ya kutayarisha rasimu ya Katiba ya Kudumu ya Muungano ambayo itakuwa na idadi sawa ya wajumbe kutoka Zanzibar na Tanganyika kama yalivyo matakwa ya kifungu cha (vii) (a) cha Mkataba wa Muungano.



  1. Liundwe Bunge la Katiba (Constituent Assembly) litakalokuwa na idadi sawa ya wajumbe kutoka Zanzibar na Tanganyika ambalo litakuwa na majukumu ya kupokea rasimu iliyotayarishwa na Tume ya Katiba na baada ya hapo kupitisha rasmi Katiba ya Kudumu ya Muungano kama yalivyo matakwa ya kifungu cha (vii) (b) cha Mkataba wa Muungano.


Itaonekana kwamba msingi wa hatua zote zilizoorodheshwa hapa ni kuheshimu mapatano ya nchi zetu mbili yaliyomo katika Mkataba wa Muungano. Haya yalibidi yafanyike ndani ya mwaka mmoja tokea kusainiwa kwa Makubaliano ya Muungano. Hata hivyo, Waingereza wanasema,"Better late than never" (Bora kuchelewa kuliko kutofanya kabisa). Wakati ndio huu ikiwa tunataka Muungano wa kweli, Muungano wa haki kwa pande zote mbili.


Wasioitakia mema CUF wanaweza kudai kwamba hatua hizi zinazopendekezwa haziashirii nia njema ya kuendeleza na kuimarisha Muungano. Sisi katika CUF hatuamini hivyo. Tunaamini katika kuwa wakweli na wawazi, kwamba hivyo ndivyo yalivyo makubaliano katika Mkataba unaoanzisha Muungano.


Ulimwengu unabadilika kwa kasi. Zama za kuendesha mambo kwa ubabe na ukichwa ngumu zimepitwa na wakati. Tuache ile tabia ya kuyaona mapendekezo ya kubadili mfumo wa Muungano kuwa yana nia ya kuuvunja Muungano huo. Muungano ili udumu unahitaji ridhaa ya walioungana. Muasisi wa Muungano huu, Mwalimu Nyerere mwenyewe, aliwahi kueleza umuhimu wa ridhaa katika masuala haya na kuonyesha kwamba ridhaa ya mshirika mmojawapo ikiondoka, Muungano hauwezi kusimama. Alisema mwaka 1968:


"If the mass of the people of Zanzibar should, without external manipulation, and for some reason of their own, decide that the Union was prejudicial to their existence, I could not bomb them into submission … The Union would have ceased to exist when the consent of its constituent members was withdrawn." [12]


"Iwapo wananchi walio wengi wa Zanzibar wataamua, bila ya msukumo wa kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, kwamba Muungano unaathiri kuendelea kuwepo kwao, siwezi kuwalazimisha kwa kuwapiga mabomu … Muungano utasita kuendelea pale ridhaa ya washirika wake itakapoondolewa."


Wazanzibari ni watu wenye historia ya maingiliano ya jamii za watu mbali mbali na hivyo hawawezi kukataa umoja, alimradi tu umoja huo uwe na maslahi na faida kwao. Mfumo uliopo sasa hauinufaishi Zanzibar na hivyo haukubaliki kwa Wazanzibari. Koti la Muungano kama lilivyo sasa linabana sana. Wakati umefika tushone koti jipya kwa mujibu wa mahitaji ya zama hizi.


Hitimisho: Mazungumzo ya dhati yenye nia njema ndiyo njia


CUF, kama ulivyo Muungano tunaoujadili, imekumbana na dhoruba nyingi katika kipindi kifupi cha kuwepo kwake. Miongoni mwa dhoruba hizo ni kupakaziwa kila ubaya ili kuwazuia wananchi wasikiunge mkono ikiwemo hoja kwamba hakiutaki Muungano na kwamba pindi kikishika madaraka kitauvunja Muungano huo. Hoja hii ni dhaifu mno inayolenga kutimiza malengo ya kisiasa badala ya kushughulikia hasa kiini cha matatizo ya msingi ya Muungano.


Si siri kwamba kwa kushindwa kushughulikia kiini cha matatizo haya kumewapelekea wananchi kuona kwamba Muungano huu haupo kwa maslahi yao. Na kwa Wazanzibari, kutokana na Serikali ya Muungano kila uchaguzi unaopokaribia kuamua kumimina maelfu kwa maelfu ya askari wa vikosi vyake ambao, kwa kushirikiana na askari wa vikosi vya SMZ, wamekuwa wakitumika kuwaadhibu Wazanzibari kwa kujaribu kutumia haki yao ya kidemokrasia na kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka, wanafikia hatua hata ya kuuona ni Muungano wa kikandamizaji. Hisia za namna hii zinapata nguvu zaidi pale wanapomuona Rais wa Jamhuri ya Muungano anafikia kujua na kukiri kwamba chama chake hakina nafasi ya kushinda uchaguzi huru na wa haki lakini viongozi wake watatumia mabavu kubaki madarakani na yeye akashirikiana nao kufanikisha hilo. Mwandishi mashuhuri wa kimataifa, Jonathan Power, anaripoti:


"The governing party [in Zanzibar] is part of the mainland's goverining CCM, but, as [President] Mkapa says, there are some militant people in my party. They don't want to lose power even if it means fiddling the vote." [13]


"Chama kinachotawala [Zanzibar] ni sehemu ya chama cha CCM kinachotawala Bara, lakini kama anavyosema [Rais] Mkapa, kuna wahafidhina katika chama changu. Hawako tayari kuachia madaraka hata kama hiyo inamaanisha wizi wa kura."


Yaliyofuata katika utekelezaji wa mpango huo yataingia katika historia ya Tanzania kama mojawapo ya matukio ya unyama mkubwa kuwahi kufanywa na askari wazalendo dhidi ya wananchi wenzao kwa sababu tu ya itikadi tofauti za kisiasa na kuwazuia wasitekeleze haki yao ya kidemokrasia na kikatiba. Matukio hayo yenyewe ni matokeo ya kupuuzwa kwa njia ya mazungumzo na makubaliano ya Muafaka ambayo awali Rais mstaafu Mkapa aliahidi mbele ya Watanzania na ulimwengu kwamba atayasimamia kikamilifu.


Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2005, niliandika makala katika gazeti la Mwananchi Jumapili nikiwa na lengo la kuwaondolea mashaka wenzetu wa chama kinachotawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi kwa ujumla kuhusu mambo kadhaa tunayotuhumiwa nayo. Kuhusu Muungano niliandika:


"… Muungano ni nguzo moja nyengine ya nguvu na maslahi ya Zanzibar na ya Wazanzibari wenyewe. Wanaosema kwamba CUF haitaki Muungano na kwamba itauvunja ni waongo. CUF, kama ilivyo CCM, ni chama chenye nguvu Visiwani na Bara. Na kama CCM ina uwezo wa kutawala pande zote, CUF ina uwezo huo mara mbili zaidi. Msimamo wetu ni kwamba kuna hitilafu na kasoro mbali mbali katika Muungano lakini hizo tutazijadili kwa pamoja na Serikali ya Muungano na naamini tutaweza kuzipatia ufumbuzi."[14]


Na huo unabaki kuwa ndiyo msimamo wa CUF katika kutatua hizi zinazoitwa kero za Muungano. Mazungumzo makini, ya kina na yenye kuambatana na nia njema kwa wahusika wote ndiyo njia pekee ya matumaini katika kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayolikabili Taifa letu. Hakuna mbadala wa mazungumzo. Nje ya mazungumzo ni fujo.


Lakini wakati tunazungumzia namna ya kutatua matatizo haya kwa lengo la kuwa na Muungano imara, ni vyema tuelewe kwamba tunahitaji kwanza kuhakikisha kuwa tumetatua tatizo la mgogoro wa kisiasa Zanzibar ambao unaendelea kumong'onyoa misingi ya umoja wa visiwa hivi na kuathiri maendeleo yake. Tunahitaji kuwa na Zanzibar imara isiyoyumba ili kuwa na Muungano imara usiyoyumba. Naomba nifikie Hitimisho kwa kunukuu kutoka katika Utangulizi wa Manifesto ya Uchaguzi ya CUF, pale tuliposema:


"Mtazamo wetu ni kwamba Wazanzibari tutakuwa na nguvu na sauti licha ya udogo wetu ikiwa tutakuwa na mfumo shirikishi badala ya tenganishi na kwamba tunaweza kuyafikia, kwa umoja wetu, mengi ambayo hatukuweza kuyafikia kwa kugawanyika kwetu."[15]

Mfumo Kristo: KHATIMA YA ZANZIBAR NA MUSTAKBALI WA MUUNGANO
 
Muungano wa Serikali tatu utaongeza gharama?


Baada ya kuangalia nafasi ya Tanganyika na ya Zanzibar katika Muungano na madaraka yao, na kuonyesha kwamba njia pekee ya kushughulikia matatizo ya msingi ya Muungano ni kwa kurejea katika Mkataba wa Muungano na hivyo kuanzisha mfumo wa Serikali tatu, ni vyema tutafakari kidogo suala la gharama za uendeshaji wa mfumo huo.


Wapinzani wa Muungano imara chini ya msingi madhubuti wa Shirikisho la Serikali tatu wamekuwa wakiibua mara kwa mara hoja ya kuongezeka kwa gharama za utawala na uendeshaji kama kikwazo cha kukwamisha juhudi za kuuimarisha Muungano.


Hoja hii imeonekana ni dhaifu na isiyo na msingi kabisa kufuatia kuundwa kwa Tume ya Pamoja ya Fedha (Joint Finance Commission) ambayo ripoti zake za awali zimekaliwa na Serikali ya Muungano hadi leo baada ya kutoa picha halisi ya jinsi mchango wa Muungano unavyopaswa uwe. Tume hiyo imeipa kazi kampuni ya PriceWaterhouseCoopers kufanya uchambuzi halisi wa mambo yepi ni ya Muungano halisi na yepi ni ya Tanganyika na yepi ni ya Zanzibar. Baada ya orodha kupatikana, watafiti wakatafuta matumizi halisi ya bajeti ya vifungu hivyo kwa muda wa kiasi cha miaka 10 iliyopita. Watafiti hao walikwenda mbali zaidi ya hapo na kukusanya mapato yote kwa kila kifungu cha mambo ya Muungano halisi. Mwishowe, wakalinganisha iwapo mapato yanakidhi matumizi au yana nakisi (upungufu)?


Kilichojitokeza ni kwamba kwa mwaka wa fedha 2003/2004 pekee, matumizi halisi kwa vifungu vya Muungano yalikuwa Shs. 537,258.4 bilioni na mapato halisi kwa mwaka huo yalikuwa ni Shs. 1,030,826.1 bilioni. Tofauti ya vifungu hivyo vimetoa ziada ya ya Shs. 493,567.7 bilioni kwa mwaka huo. Ziada hii haiingizi mapato yanayotokana na misaada kutoka nje au mikopo. Ziada hii hutumika kwa shughuli za Tanganyika zisizo za Muungano.


Ukweli huu unaonyesha hata kama kungekuwa na Serikali tatu kusingekuwa na haja yoyote kwa Serikali ya Zanzibar na ile ya Tanganyika kulipia fedha za ziada kama wahusika watatunza na kuweka kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi ya mambo ya Muungano halisi badala ya yale ya Tanganyika kuchanganywa na ya Muungano. Mambo yasiyokuwa ya Muungano yaTanganyika yalipotengwa nje ya yale ya Muungano, gharama za mambo ya Muungano zimejidhihirisha wazi bila ya kujificha na kuonesha kwamba zinaweza kulipiwa kupitia mapato ya mambo ya Muungano pekee na ziada kubaki. Lakini hili limekuwa rahisi kwa kukubali ukweli kwamba kuna mafungu matatu ya mapato na matumizi katika Serikali zetu mbili. Mafungu hayo ni la SMZ kwa mambo yake yasiyo mambo ya Muungano, la Serikali ya Muungano kwa mambo ya Muungano, na la Serikali ya Muungano inayofanya kazi za Tanganyika kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano. Kinachohitajika sasa ni hili kuliweka wazi kwa viongozi kuweka nia njema na kuuweka sawa muundo wa Muungano wetu ili uzionyeshe waziwazi mamlaka zote tatu.










Vipi tutoke hapa tulipo?


Inakaribia miaka 45 sasa tangu uundwe Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kulikuwa na wakati wa kutosha kurekebisha kasoro zilizopo. Hilo halikuwezekana kutokana na ubabe wa Mwalimu Nyerere ambaye aliamua kuwatia shemere Wazanzibari na kuhakikisha Muungano unakwenda kama alivyotaka yeye hata baada ya ‘kuondoka madarakani’.


Si jambo la kuficha kwamba wananchi wa pande zote mbili za Muungano wamechoshwa na unafiki uliopo na wanadai Katiba ya kweli kweli itakayoweka misingi mipya ya ushirikiano.


Kama nilivyoeleza mwanzoni, kiini cha matatizo ya Muungano ni kutokuheshimiwa kwa Mkataba wa Muungano (Articles of Union) ambao kisheria ni Mkataba wa Kimataifa unaopaswa kuheshimiwa kwa kuzingatia masharti yote yanayohusu mikataba ya kimataifa.


Haidhuru sasa ni takriban miaka 45 tokea kuanza kwa hatua za kuukanyaga kanyaga Mkataba wa Muungano mara tu baada ya kutiwa saini na Rais wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, na Rais wa Jamhuri ya Tanganyika, Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, lakini ukweli utabaki kuwa huo ulikuwa ndiyo msingi pekee, nasisitiza tena, pekee, uliokubaliwa na viongozi hao wawili kuongoza mahusiano ya nchi zetu mbili kupitia Muungano.


Wakati sasa umefika tukubali kwamba suluhisho la matatizo haya siyo kuendelea kuunda Tume au Kamati au kuandaa warsha, semina, makongamano na mikutano. Suluhisho ni kutekeleza kwa dhati Mkataba wa Muungano (Articles of Union) ambao ni mkataba wa kimataifa wa nchi mbili huru.


Kujaribu kulazimisha kutumia Katiba inayoitwa ya Jamhuri ya Muungano kama ilivyo sasa ambayo inakosa uhalali wa kisheria kuzima madai ya wananchi wa Zanzibar hakuwezi kukubalika tena katika zama hizi.


Kwa msingi huo, hakuna njia ya mkato ya kuyashughulikia matatizo ya Muungano bila ya kwenda kwenye kiini cha matatizo hayo ambacho ni kutokuheshimiwa kwa Mkataba wa Muungano. Wahenga wamesema, Mwiba uchomeapo ndipo utokeapo. Ili kuyaheshimu Makubaliano ya Muungano, yafuatayo ni lazima yafanyike:



  1. Kwa kuwa Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar la mwaka 1964 ambalo lilikuwa ni Baraza la Mapinduzi halikupewa nafasi ya kuuridhia (ratify) Mkataba wa Muungano, hivyo basi kwanza kabisa, na kabla ya kuchukua hatua nyengine yoyote, ni lazima Baraza la Kutunga Sheria la Zanzibar kwa sasa ambalo ni Baraza la Wawakilishi lipewe nafasi ya kuuridhia Mkataba huo ili kuupa uhalali wa kisheria kwa upande wa Zanzibar na hivyo kuupa uhalali wa kisheria Muungano wenyewe kama yalivyo masharti ya kifungu cha (viii) cha Mkataba huo wa Muungano.



  1. Kwa ujumla tuupitie tena Mkataba wa Muungano na kurekebisha vifungu vyenye utatanishi. Kama Muungano huu haukuwa na mtego, ulikuja kwa ridhaa za Serikali zetu mbili, vipi tunashindwa kukaa tena tukaupitia baada ya miaka 45 na kuuweka kwenye hali ya kuvutia hata majirani zetu wakajiunga?



  1. Katiba ya Zanzibar itumike Zanzibar kwa mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kama yalivyo masharti ya kifungu cha (v) cha Mkataba wa Muungano.



  1. Katiba ya Tanganyika (ile iliyokuwepo kabla ya kurekebishwa kuingiza mambo ya Muungano) nayo irejee kutumika Tanganyika kwa mambo yote yasiyo mambo ya Muungano kama yalivyo masharti ya kifungu cha (v) cha Mkataba wa Muungano.



  1. Kwa kutumia Katiba ya Tanganyika, iundwe Serikali ya Tanganyika inayoshughulika na mambo yasiyo ya Muungano, kama Serikali ya Zanzibar inavyoshughulika na mambo yake ambayo si ya Muungano.



  1. Serikali ya Muungano ishughulike na yale mambo 11 tu ya asili yaliyokubaliwa kuwa ndiyo mambo ya Muungano kwa mujibu wa kifungu cha (iv) cha Mkataba wa Muungano.



  1. Mambo mengine yote 12 yaliyoongezwa katika orodha ya mambo ya Muungano kinyume na Mkataba wa Muungano yaondolewe katika orodha hiyo na yarudi katika mamlaka za Zanzibar na Tanganyika.



  1. Wafanyakazi wa Tanganyika wasihusike na mambo ya Muungano, wawe katika “civil service” (mfumo wa wafanyakazi Serikalini) wa Tanganyika, kama walivyo wa Zanzibar kwa Zanzibar (wasio wa taasisi za Muungano).



  1. Urejee utaratibu wa kuwepo kwa Makamu wawili wa Rais wa Muungano kama yalivyo masharti ya kifungu cha (iii) (b) cha Mkataba wa Muungano ambapo Rais wa Zanzibar na Rais wa Tanganyika wawe Makamu wa Rais wa Muungano kwa mujibu wa nyadhifa zao.



  1. Iundwe Tume ya kutayarisha rasimu ya Katiba ya Kudumu ya Muungano ambayo itakuwa na idadi sawa ya wajumbe kutoka Zanzibar na Tanganyika kama yalivyo matakwa ya kifungu cha (vii) (a) cha Mkataba wa Muungano.



  1. Liundwe Bunge la Katiba (Constituent Assembly) litakalokuwa na idadi sawa ya wajumbe kutoka Zanzibar na Tanganyika ambalo litakuwa na majukumu ya kupokea rasimu iliyotayarishwa na Tume ya Katiba na baada ya hapo kupitisha rasmi Katiba ya Kudumu ya Muungano kama yalivyo matakwa ya kifungu cha (vii) (b) cha Mkataba wa Muungano.


Itaonekana kwamba msingi wa hatua zote zilizoorodheshwa hapa ni kuheshimu mapatano ya nchi zetu mbili yaliyomo katika Mkataba wa Muungano. Haya yalibidi yafanyike ndani ya mwaka mmoja tokea kusainiwa kwa Makubaliano ya Muungano. Hata hivyo, Waingereza wanasema,“Better late than never” (Bora kuchelewa kuliko kutofanya kabisa). Wakati ndio huu ikiwa tunataka Muungano wa kweli, Muungano wa haki kwa pande zote mbili.


Wasioitakia mema CUF wanaweza kudai kwamba hatua hizi zinazopendekezwa haziashirii nia njema ya kuendeleza na kuimarisha Muungano. Sisi katika CUF hatuamini hivyo. Tunaamini katika kuwa wakweli na wawazi, kwamba hivyo ndivyo yalivyo makubaliano katika Mkataba unaoanzisha Muungano.


Ulimwengu unabadilika kwa kasi. Zama za kuendesha mambo kwa ubabe na ukichwa ngumu zimepitwa na wakati. Tuache ile tabia ya kuyaona mapendekezo ya kubadili mfumo wa Muungano kuwa yana nia ya kuuvunja Muungano huo. Muungano ili udumu unahitaji ridhaa ya walioungana. Muasisi wa Muungano huu, Mwalimu Nyerere mwenyewe, aliwahi kueleza umuhimu wa ridhaa katika masuala haya na kuonyesha kwamba ridhaa ya mshirika mmojawapo ikiondoka, Muungano hauwezi kusimama. Alisema mwaka 1968:


“If the mass of the people of Zanzibar should, without external manipulation, and for some reason of their own, decide that the Union was prejudicial to their existence, I could not bomb them into submission … The Union would have ceased to exist when the consent of its constituent members was withdrawn.” [12]


“Iwapo wananchi walio wengi wa Zanzibar wataamua, bila ya msukumo wa kutoka nje, na kwa sababu zao wenyewe, kwamba Muungano unaathiri kuendelea kuwepo kwao, siwezi kuwalazimisha kwa kuwapiga mabomu … Muungano utasita kuendelea pale ridhaa ya washirika wake itakapoondolewa.”


Wazanzibari ni watu wenye historia ya maingiliano ya jamii za watu mbali mbali na hivyo hawawezi kukataa umoja, alimradi tu umoja huo uwe na maslahi na faida kwao. Mfumo uliopo sasa hauinufaishi Zanzibar na hivyo haukubaliki kwa Wazanzibari. Koti la Muungano kama lilivyo sasa linabana sana. Wakati umefika tushone koti jipya kwa mujibu wa mahitaji ya zama hizi.


Hitimisho: Mazungumzo ya dhati yenye nia njema ndiyo njia


CUF, kama ulivyo Muungano tunaoujadili, imekumbana na dhoruba nyingi katika kipindi kifupi cha kuwepo kwake. Miongoni mwa dhoruba hizo ni kupakaziwa kila ubaya ili kuwazuia wananchi wasikiunge mkono ikiwemo hoja kwamba hakiutaki Muungano na kwamba pindi kikishika madaraka kitauvunja Muungano huo. Hoja hii ni dhaifu mno inayolenga kutimiza malengo ya kisiasa badala ya kushughulikia hasa kiini cha matatizo ya msingi ya Muungano.


Si siri kwamba kwa kushindwa kushughulikia kiini cha matatizo haya kumewapelekea wananchi kuona kwamba Muungano huu haupo kwa maslahi yao. Na kwa Wazanzibari, kutokana na Serikali ya Muungano kila uchaguzi unaopokaribia kuamua kumimina maelfu kwa maelfu ya askari wa vikosi vyake ambao, kwa kushirikiana na askari wa vikosi vya SMZ, wamekuwa wakitumika kuwaadhibu Wazanzibari kwa kujaribu kutumia haki yao ya kidemokrasia na kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka, wanafikia hatua hata ya kuuona ni Muungano wa kikandamizaji. Hisia za namna hii zinapata nguvu zaidi pale wanapomuona Rais wa Jamhuri ya Muungano anafikia kujua na kukiri kwamba chama chake hakina nafasi ya kushinda uchaguzi huru na wa haki lakini viongozi wake watatumia mabavu kubaki madarakani na yeye akashirikiana nao kufanikisha hilo. Mwandishi mashuhuri wa kimataifa, Jonathan Power, anaripoti:


“The governing party [in Zanzibar] is part of the mainland’s goverining CCM, but, as [President] Mkapa says, there are some militant people in my party. They don’t want to lose power even if it means fiddling the vote.” [13]


“Chama kinachotawala [Zanzibar] ni sehemu ya chama cha CCM kinachotawala Bara, lakini kama anavyosema [Rais] Mkapa, kuna wahafidhina katika chama changu. Hawako tayari kuachia madaraka hata kama hiyo inamaanisha wizi wa kura.”


Yaliyofuata katika utekelezaji wa mpango huo yataingia katika historia ya Tanzania kama mojawapo ya matukio ya unyama mkubwa kuwahi kufanywa na askari wazalendo dhidi ya wananchi wenzao kwa sababu tu ya itikadi tofauti za kisiasa na kuwazuia wasitekeleze haki yao ya kidemokrasia na kikatiba. Matukio hayo yenyewe ni matokeo ya kupuuzwa kwa njia ya mazungumzo na makubaliano ya Muafaka ambayo awali Rais mstaafu Mkapa aliahidi mbele ya Watanzania na ulimwengu kwamba atayasimamia kikamilifu.


Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2005, niliandika makala katika gazeti la Mwananchi Jumapili nikiwa na lengo la kuwaondolea mashaka wenzetu wa chama kinachotawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi kwa ujumla kuhusu mambo kadhaa tunayotuhumiwa nayo. Kuhusu Muungano niliandika:


“… Muungano ni nguzo moja nyengine ya nguvu na maslahi ya Zanzibar na ya Wazanzibari wenyewe. Wanaosema kwamba CUF haitaki Muungano na kwamba itauvunja ni waongo. CUF, kama ilivyo CCM, ni chama chenye nguvu Visiwani na Bara. Na kama CCM ina uwezo wa kutawala pande zote, CUF ina uwezo huo mara mbili zaidi. Msimamo wetu ni kwamba kuna hitilafu na kasoro mbali mbali katika Muungano lakini hizo tutazijadili kwa pamoja na Serikali ya Muungano na naamini tutaweza kuzipatia ufumbuzi.”[14]


Na huo unabaki kuwa ndiyo msimamo wa CUF katika kutatua hizi zinazoitwa kero za Muungano. Mazungumzo makini, ya kina na yenye kuambatana na nia njema kwa wahusika wote ndiyo njia pekee ya matumaini katika kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayolikabili Taifa letu. Hakuna mbadala wa mazungumzo. Nje ya mazungumzo ni fujo.


Lakini wakati tunazungumzia namna ya kutatua matatizo haya kwa lengo la kuwa na Muungano imara, ni vyema tuelewe kwamba tunahitaji kwanza kuhakikisha kuwa tumetatua tatizo la mgogoro wa kisiasa Zanzibar ambao unaendelea kumong’onyoa misingi ya umoja wa visiwa hivi na kuathiri maendeleo yake. Tunahitaji kuwa na Zanzibar imara isiyoyumba ili kuwa na Muungano imara usiyoyumba. Naomba nifikie Hitimisho kwa kunukuu kutoka katika Utangulizi wa Manifesto ya Uchaguzi ya CUF, pale tuliposema:


“Mtazamo wetu ni kwamba Wazanzibari tutakuwa na nguvu na sauti licha ya udogo wetu ikiwa tutakuwa na mfumo shirikishi badala ya tenganishi na kwamba tunaweza kuyafikia, kwa umoja wetu, mengi ambayo hatukuweza kuyafikia kwa kugawanyika kwetu.”[15]

Mfumo Kristo: KHATIMA YA ZANZIBAR NA MUSTAKBALI WA MUUNGANO

Hakuna neutrality katika discussion yako. ok umejadiri lakini bahati mbaya umejikita kwenye chuki zaidi kwa watanganyika (hii ni tafasiri yangu). Hata hivyo kwa akili ya kawaida sijui kama nchi ilitakiwa isimame baada ya haya mambo 11 ya muungano.
Serikali mbili ni sera ya CCM, na ni wazi kwamba wananchi wengi hawajahusishwa katika kuamua mfumo huo, ni kama ambavyo CUF wanayo sera ya serikali tatu na ambayo hakuna uhakika kama wananchi wanaikubali. lakini CUF ikishinda automatically serikali tatu zimekubalik. Likewise kwa CCM yenye sera ya serikali mbili inaposhinda (hapa nina maana ya ushindi genuine si wa kuchakachua) sera yake inatumika.
Hopefully katiba inayotafutwa inaweza kuja na suruhisho la malalamiko ya wazanzibar kama kweli ni genuine kiasi hicho.
 
Hakuna neutrality katika discussion yako. ok umejadiri lakini bahati mbaya umejikita kwenye chuki zaidi kwa watanganyika (hii ni tafasiri yangu). Hata hivyo kwa akili ya kawaida sijui kama nchi ilitakiwa isimame baada ya haya mambo 11 ya muungano.
Serikali mbili ni sera ya CCM, na ni wazi kwamba wananchi wengi hawajahusishwa katika kuamua mfumo huo, ni kama ambavyo CUF wanayo sera ya serikali tatu na ambayo hakuna uhakika kama wananchi wanaikubali. lakini CUF ikishinda automatically serikali tatu zimekubalik. Likewise kwa CCM yenye sera ya serikali mbili inaposhinda (hapa nina maana ya ushindi genuine si wa kuchakachua) sera yake inatumika.
Hopefully katiba inayotafutwa inaweza kuja na suruhisho la malalamiko ya wazanzibar kama kweli ni genuine kiasi hicho.



Kwa sasa CUF wameibadilisha sera yao kwa haraka sana na imekuwa MUUNGANO WA MKATABA hiyo ndio sera ya CUF kwa sasa, naomba ufuatilie maoni ya katiba huko Zenji utaona kuwa hata hao CUF hawataki muungano.

Kwa7bu:

Wazanzibari wengi (79%) wamekuwa wakitoa maoni yao kwa kusema hv:

Tunataka mamlaka Ya Zanzibari kamili (sovereignt), tena hawaishi hapo tuu, huendelea kwa kusema;
Hayo Mamlaka yawe hivi;
Zanzibar iwe na kiti chake UN,
'' ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Mambo ya nje kila mmoja (Tanganyika & Zenji) wawe na zake;
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, iwe na Police wake;
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, iwe na sarafu, Gesi na mafuta yasiwe ya muungano, uchumi wake na Benki yake;
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, utaifa wake na passport yake;
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, Bandari, Biashara yake ya kimataifa zisiwe za muungano;
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, takwimu yake;
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, jeshi lake;
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, etc.

Sasa hapo utaona kuwa hiyo ndio sera ya CUF, Jee kuna muungano hapo??
Ktk mjumuisho wa maoni mikoa 2 ya Zenji 79% wamesema hivo, na Baraza la Wakilishi limewataka wananchi wao watulie mpaka hapo maoni yao yasiposikilizwa ndio wao wataamua.

Me naona hakuna haja ya kulazimishana ktk hili la muungano kwa7bu nina uhakika kwa vijana huko Zenji walivolivalia buti basi machafuko ya muungano lazima yatatokea ikiwa SMZ na SMT watalazimisha huu muungano.
 
MziziMkavu,
Lakini Umoja wa Afrika (Pan-Africanism) hauonekani kuwa ndiyo dhamira pekee au kama ndiyo dhamira halisi ya Muungano. Wengi wanaamini, na mimi nikiwa mmoja wao, kwamba dhana hiyo ilitumiwa tu kuficha njama za muda mrefu za Nyerere kutaka kuimeza na kuitawalaZanzibar. Katika mwaka 1961, wakati Tanganyika inakaribia kupata Uhuru wake, Nyerere alinukuliwa akisema:

"If I could tow that island [Zanzibar] out in the middle of the Indian Ocean, I would do it … I fear it will be a very big headache for me."[6]



Yaani, "Kama ningekuwa na uwezo wa kuvikokota visiwa vile [Zanzibar] na kuvitupa nje kabisa, katikati ya Bahari ya Hindi, basi ningefanya hivyo … Nakhofia vitakuja kuniumiza kichwa sana".
Ni kwa bahati mbaya sana Nyerere leo hayupo na watu wengi walishindwa kumuuliza Nyerere kwa nini alisema haya, lakini watu woote wanaomshutumu Nyerere kwa maneno haya hawasemi hata siku moja chanzo cha yeye kufikia kusema maneno haya. Jamani Nyerer hakuwa mwenzawazimu kuropoka maneno pasipokuwa na mwanzo ama swali. Hata kushuka kwa Quran kulitanguliwa na kisa, sababu na umuhimu wa Aya za Mwenyezi Mungu na sio kila kinachoandikwa hakikuwa na mwanzo..

Kufikia mwaka 1961, wakati wa Cold war, Zanzibar ilikuwa inaogopwa Afrika kama nchi pekee ktk ukanda wa mashariki yenye ushirikiano wa RUSSIA na wanaharakati wake wamejikita ktk kupambana na uongozi wa wageni wa Sultan.. Historia yake inajieleza zaidi ya maneno ya Nyerere.. Na alisema wazi wala sii mara moja, hofu yake juu ya ya Ukomunist ilivyoingia nchi Zanzibar alifikia kusema maneno haya lakini alipuuzwa na viongozi wa kimataifa, CIA na hata majirani hadi pale ilipobainika kabla ya Uhuru na Mapinduzi kuwa alokuwa akiyasema yana ukweli..

Wazungu wanasema - If you can't beat join them..Na hakika hofu yake ilijitokeza ktk Mapinduzi, toka kina Hanga, Omar Sharrif hadi Abraham Babu hawa wote walikuwa wamebobea ktk Ukomunist kiasi kwamba hata yeye mwenyewe akamezwa na Wakomunist, Mwisho wake leo kaadhirika yeye kushindwa kwa maamuzi yake kuhusu Ujamaa na Kujitegemea. Kila kona ya dunia hadithi ni yeye kashindwa na Ujamaa wake - Everything happened kama alivyohofia..

Tazama basi, kamati zote zilizowahi kukaa zilitokana na kero za Wazanzibar tu, hakuna hata kamati moja iloundwa kwa sababu ya madai kutoka bara. Marekebisho ndani ya Katiba yamefanywa kutokana na madai ya viongozi wa Zanzibar lkakini leo wanahoji kwa nini yaliongezwa!...Yaani hata siwaelewi watu hawa..

Wazanzibar mnanishangaza sana, ni watu ambao mnapenda sana kujisifia kuwa Ustaarabu, wacha Mungu na watu ambao hawakuwa na Ubaguzi walipendana kwa kuishi watu wa makabila tofauti japokuwa ubaguzi ulokuwepo hauzingumzwi asilani..Sasa maajabu hawa watu wasiokuwa na Ubaguzi ndio wao leo wanatuita Wabara Machogo,makafir na wanataka wabara waondoke Zanzibar na kwamba ati Zanzibar imetawaliwa na Bara kama kwamba Wazanzibar hawa amini ktk Pan Africanism hata kama haikusemwa na Nyerere au Nkurumah.

Je, Abdallah K. Hanga, Abrahaman Babu, Omar Sharrif, Karume waliamini nini kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar, Je, waliamini ktk umoja wa nchi za kiafrika?..Haisemwi kamwe na Mzanzibar yeyote isipokuwa haya ni mawazo ya Nyerere tu. Huu ni UNAFIKI mkubwa sana ndani ya UISLAAM na ndio nyie mnaupa jina baya Uislaam. I mean jamani Uislaam gani mnaotutangazia ama hizi mila chafu za waarabu ndio mnazitumia!

Na kubwa kuliko yote Wazanzibar wengi wepesi kujiita Waafrika ktk magazeti na Mitandao lakini kamwe hutawasikia wakijisifia kwa Uafrika wao. Utawasikia mimi Mu Oman, mimi M - Yemen na wengine huchukia hata wakiitwa Wapemba..Yaani hata siwaelewi kabisa..
 
Hizi discusion za haka kamkoa kweli mi zina nibore kweli, kila siku kelele tu, mbona mikoa mingine haipigi kelele? kamepewa rais, jaji wao, tena kama marais 3 halafu wote wakisha stafu tu mafao wanachukua huku bara, si kaende tu, kila siku maneno vitendo zero.Aaaaah
 
MziziMkavu,
Ni kwa bahati mbaya sana Nyerere leo hayupo na watu wengi walishindwa kumuuliza Nyerere kwa nini alisema haya, lakini watu woote wanaomshutumu Nyerere kwa maneno haya hawasemi hata siku moja chanzo cha yeye kufikia kusema maneno haya. Jamani Nyerer hakuwa mwenzawazimu kuropoka maneno pasipokuwa na mwanzo ama swali. Hata kushuka kwa Quran kulitanguliwa na kisa, sababu na umuhimu wa Aya za Mwenyezi Mungu na sio kila kinachoandikwa hakikuwa na mwanzo..

Kufikia mwaka 1961, wakati wa Cold war, Zanzibar ilikuwa inaogopwa Afrika kama nchi pekee ktk ukanda wa mashariki yenye ushirikiano wa RUSSIA na wanaharakati wake wamejikita ktk kupambana na uongozi wa wageni wa Sultan.. Historia yake inajieleza zaidi ya maneno ya Nyerere.. Na alisema wazi wala sii mara moja, hofu yake juu ya ya Ukomunist ilivyoingia nchi Zanzibar alifikia kusema maneno haya lakini alipuuzwa na viongozi wa kimataifa, CIA na hata majirani hadi pale ilipobainika kabla ya Uhuru na Mapinduzi kuwa alokuwa akiyasema yana ukweli..

Wazungu wanasema - If you can't beat join them..Na hakika hofu yake ilijitokeza ktk Mapinduzi, toka kina Hanga, Omar Sharrif hadi Abraham Babu hawa wote walikuwa wamebobea ktk Ukomunist kiasi kwamba hata yeye mwenyewe akamezwa na Wakomunist, Mwisho wake leo kaadhirika yeye kushindwa kwa maamuzi yake kuhusu Ujamaa na Kujitegemea. Kila kona ya dunia hadithi ni yeye kashindwa na Ujamaa wake - Everything happened kama alivyohofia..

Tazama basi, kamati zote zilizowahi kukaa zilitokana na kero za Wazanzibar tu, hakuna hata kamati moja iloundwa kwa sababu ya madai kutoka bara. Marekebisho ndani ya Katiba yamefanywa kutokana na madai ya viongozi wa Zanzibar lkakini leo wanahoji kwa nini yaliongezwa!...Yaani hata siwaelewi watu hawa..

Wazanzibar mnanishangaza sana, ni watu ambao mnapenda sana kujisifia kuwa Ustaarabu, wacha Mungu na watu ambao hawakuwa na Ubaguzi walipendana kwa kuishi watu wa makabila tofauti japokuwa ubaguzi ulokuwepo hauzingumzwi asilani..Sasa maajabu hawa watu wasiokuwa na Ubaguzi ndio wao leo wanatuita Wabara Machogo,makafir na wanataka wabara waondoke Zanzibar na kwamba ati Zanzibar imetawaliwa na Bara kama kwamba Wazanzibar hawa amini ktk Pan Africanism hata kama haikusemwa na Nyerere au Nkurumah.

Je, Abdallah K. Hanga, Abrahaman Babu, Omar Sharrif, Karume waliamini nini kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar, Je, waliamini ktk umoja wa nchi za kiafrika?..Haisemwi kamwe na Mzanzibar yeyote isipokuwa haya ni mawazo ya Nyerere tu. Huu ni UNAFIKI mkubwa sana ndani ya UISLAAM na ndio nyie mnaupa jina baya Uislaam. I mean jamani Uislaam gani mnaotutangazia ama hizi mila chafu za waarabu ndio mnazitumia!

Na kubwa kuliko yote Wazanzibar wengi wepesi kujiita Waafrika ktk magazeti na Mitandao lakini kamwe hutawasikia wakijisifia kwa Uafrika wao. Utawasikia mimi Mu Oman, mimi M - Yemen na wengine huchukia hata wakiitwa Wapemba..Yaani hata siwaelewi kabisa..
Je Wa Zanzibar Hawataki Muungano wenu je mtawaachia wajitawale Wenyewe pasipo na kumwagika Damu?Mkuu Mkandara
 
Je Wa Zanzibar Hawataki Muungano wenu je mtawaachia wajitawale Wenyewe pasipo na kumwagika Damu?Mkuu Mkandara
Nini maana ya KUTAWALIWA? na ukisha nijibu hilo naomba unipe vigezo ambavyo vinaashiria Zanzibar inatawaliwa na bara kama sio wao kuitawala Bara kwa tafisri zenu. Hivi mimi naweza vipi kukataa kuwa Mtanzania maanake najiuliza, nisipokuwa Mtanzania naitwa nani?.
 
Nini maana ya KUTAWALIWA? na ukisha nijibu hilo naomba unipe vigezo ambavyo vinaashiria Zanzibar inatawaliwa na bara kama sio wao kuitawala Bara kwa tafisri zenu. Hivi mimi naweza vipi kukataa kuwa Mtanzania maanake najiuliza, nisipokuwa Mtanzania naitwa nani?.
Unataka nikujibu nini na kila kitu kipo hapo juu kwenye hiyo thread yangu. Jiulize wewe Mwenyewe kwanini Serikali ya Muungano ya Tanzania inaitawala na kuingilia masuala ya ndani ya

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar? kisha utapata jibu lako wewe mwenyewe. kuna Serikali 2 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Yaani (Tanganyika na Zanzibar) na kuna Serikali ya Mapinduzi Zanzibar sasa nauliza kwanini na iweje masuala ya Serikali

ya Mapinduzi Zanzibar yaingiliwe na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Hebu jijibu wewe mwenyewe?Mkuu Mkandara
 
Last edited by a moderator:
Unataka nikujibu nini na kila kitu kipo hapo juu kwenye hiyo thread yangu. Jiulize wewe Mwenyewe kwanini Serikali ya Muungano ya Tanzania inaitawala na kuingilia masuala ya ndani ya

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar? kisha utapata jibu lako wewe mwenyewe. kuna Serikali 2 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Yaani (Tanganyika na Zanzibar) na kuna Serikali ya Mapinduzi Zanzibar sasa nauliza kwanini na iweje masuala ya Serikali

ya Mapinduzi Zanzibar yaingiliwe na Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania? Hebu jijibu wewe mwenyewe?Mkuu Mkandara
Hiyo serikali ya Muungano ni serikali ya kina nani?.. Si Wanzanzibar na Wabara ndio wameunda muungano huo ama? Mkuu wangu unajua hasa maana ya muungano au unazungumza tu vitu visivyojulikana mkidhani muungano ni sawa na JUMUIYA. Uliona wapi Federal Government haihusiki na maswala yanayohusu Muungano?. Hivi unataka kunambia Obama ni rais wa Illinois hawezi kuingilia maswala ya state nyingine ktk muungano wao. Ni yapi hayo ya serikali ya mapinduzi ambayo mliyakubali kikatiba leo yawe ya Zanzibar? na yapi ni ya bara. Haya nambie wakati Mwinyi alipokuwa rais alikuwa akiingilia maswala ya bara au... Mbona nyie mnaingilia kila siku ya bara kwa kutumia kiti cha muungano na hatusemi..
 
Hiyo serikali ya Muungano ni serikali ya kina nani?.. Si Wanzanaibar na Wabara ndio wameunda muungano huo ama? Mkuu wangu unajua hasa maana ya muungano au unazungumza tu vitu visivyojulikana mkidhani muungano ni sawa na JUMUIYA. Uliona wapi Federal Government haihusiki na maswala yanayohusu Muungano?. Hivi unataka kunambia Obama ni rais wa Illinois hawezi kuingilia maswala ya state nyingine ktk muungano wao. Ni yapi hayo ya serikali ya mapinduzi ambayo mliyakubali kikatiba leo yawe ya Zanzibar? na yapi ni ya bara. Haya nambie wakati Mwinyi alipokuwa rais alikuwa akiingilia maswala ya bara au?
Kuna Masuala

yanayohusiana na Muungano na kuna Masuala yanayohusu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo iweje Masuala ya Serikali ya Mapinduzi

Zanzibar Serikali ya Muungano iyaingilie kati? huo sio Uzushi wa hali ya juu? Kuna Serikali mbili hapo mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Acha kuleta Maneno ya Pumba zako kama hujuwi mambo ya Siasa bora ukae kimya usiinglie mambo kama huyajuwi

mkuu Mkandara Usifananishe United State of America na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni vitu 2 Tofauti kabisa.
 
Kuna Masuala

yanayohusiana na Muungano na kuna Masuala yanayohusu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo iweje Masuala ya Serikali ya Mapinduzi

Zanzibar Serikali ya Muungano iyaingilie kati? huo sio Uzushi wa hali ya juu? Kuna Serikali mbili hapo mkuu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Acha kuleta Maneno ya Pumba zako kama hujuwi mambo ya Siasa bora ukae kimya usiinglie mambo kama huyajuwi

mkuu Mkandara Usifananishe United State of America na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni vitu 2 Tofauti kabisa.
Nime kuuliza maswala yapi ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar? kwa sababu sio kweli maswala ya dhahabu na madini yanayopatika bara sio ya Muungano ati ni ya bara.. inawezekana vipi
 
Nime kuuliza maswala yapi ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar? kwa sababu sio kweli maswala ya dhahabu na madini yanayopatika bara sio ya Muungano ati ni ya bara.. inawezekana vipi
Maswala yanayohusu serikali ya Mapinduzi Zanzibar Serikali ya muungano inayaingilia kati yapo mengi tu mojawapo ni hii hapa : [h=2]Membe akalia 200bn za Zanzibar Bonyerza hapa https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/303380-membe-akalia-200bn-za-zanzibar.html Mkuu Mkandara[/h]
 
Last edited by a moderator:
Utiaji Saini wa Mkataba wa Muungano na Matokeo Yake {UHARAMU WA MUUNGANO}





Dr Harith Ghassany

“Hapana shaka yoyote kuwa Mkataba [wa Muungano] uliandaliwa kwa siri sana. Maofisa wawili [wa Kiingereza] Brown na Fifoot walihusika kwa karibu sana. Hakukuwa na mshauri wa kisheria kwa upande wa Zanzibar. Karume hakuliarifu Baraza la Mapinduzi. Jumbe alikuwa hajui.

Inawezekana Babu alikuwa anafahamu kuwa kulikuwa kuna kitu kinaendela, na inawezekana alishiriki katika mazungumzo ya kijumla, lakini hakutarajia kuwa Muungano utafanyika kwa haraka namna ile. Salim Rashid [Katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi] aliuona Mkataba [wa Muungano] kwa

mara ya kwanza pale ‘bahasha yenye Mkataba ulipowasili Ikulu kwa ajili ya kutiwa saini na Karume’.
Karume alimuelekeza Salim asimuonyeshe Dourado ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wa wakati huo. Salim alimuambia Karume kuwa

Mkataba wa Muungano ulihitajia ushauri wa kisheria. Salim akapanga kumleta Nabudere, wakati huo alikuwa ni mwanasheria kijana kutoka Uganda ambaye Salim alionana naye London lakini Nabudere alipofika Zanzibar Mkataba wa Muungano ulikuwa tayari umo katika mchakato wa kusainiwa.
Katika mahojiano na muandishi [Issa Shivji], Nabudere alithibitisha kuwa wafuasi wa chama cha Umma, Salim Rashid na Ali Mahfoudh walimuita ende Zanzibar. Alipofika Zanzibar, aliwekwa peke yake afanye kazi ndani ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Wakati huo, Mwanasheria Mkuu Dourado, alikuwa hayupo.

Rais wa kwanza wa Zanzibar, marehemu Mzee Abeid Amani Karume

Nabudere alipewa kopi ya Mkataba wa Muungano ambayo ilikuwa bado haijatiwa saini. Alitumia baadhi ya siku kuzipitia nyaraka husika za sheria za Zanzibar na makabrasha mengineyo. Baadae akenda Ikulu kuonana na Karume. Alimuarifu Karume kuwa kimsingi [Muungano] ulikuwa ni uamuzi wa

kisiasa. Utaifa wa Zanzibar utakabwa sana lakini uamuzi wa mwisho wa kisiasa anao yeye Karume.
Karume akasema yeye hana matatizo na Muungano kwa hiyo Nabudere akasema basi atakuwa hana mchango [wa kisheria]. Baadae Karume akashuka chini na Nabudere na kumuambia kuwa Nyerere amekuja kuonana nae. Nyerere alikuwa na Roland Brown. Jumla walikuwepo watu wane. Nabudere akajuulishwa na Nyerere.

Hakukuwa na mazungumzo khasa juu ya Mkataba wa Muungano. Baada ya kidogo, Nabudere akaondoka. Alipotoka nje ya Ikulu aliwaona baadhi ya wafuasi wa Umma waliokuwa wakiupinga Muungano. Nabudere alionana na Babu jioni ya siku ile. Inavyoonsha Babu aliwasili Zanzibar siku hiyo hiyo.

Nabudere alimueleza Babu kuhusu mkutano wake na Karume. Babu akasema kuwa yeye hana matatizo na Muungano. Nabudere akasafiri asubuhi ya siku ya pili au baada ya siku moja.

Nabudere hakuweza kuzikumbuka tarehe za kuwasili na kuondoka kwake Zanzibar. Na hakushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Muungano, na wala hakushiriki katika mazungumzo yoyote yale ya Mkataba wa Muungano.
Inawezekana Nabudere alifika Zanzibar siku chache kabla ya Mkataba kutiwa saini. Inawezekana alikutana na Karume tarehe 22 au 23 [Januari], lakini

kwa vyovyote hakushiriki katika mazungumzo juu ya Mkataba wa Muungano na wala hakutoa ushauri wowote ule wa kisheria.
Kwa hiyo kauli alioyoitowa Dourado miaka 20 baadae kuwa Zanzibar haikupata ‘ushauri wa kisheria au wa kikatiba kutoka kwa Mwanasheria wake Mkuu’ ni ya kweli.

Pia ni kweli kuwa Karume hakupewa ushauri wowote ule wa kisheria, na inawezekana sana kama ilivoonekana mara nyingi, kuwa alikuwa hajali kuhusu sheria au mambo ya kisheria katika uendeshaji nchi au mambo mengineyo.

Jumbe aliuona Mkataba wa Muungano kwa mara ya kwanza baada ya mawaziri wa Zanzibar kurudi kutoka Dar es Salaam ambako walikwenda kushuhudia kuidhinishwa kwa Mkataba wa Muungano ndani ya bunge la Tanganyika.
Jumbe anasema alimuambia Karume kuwa kulikuwa kuna kitu hakipo barabara. ‘Vipi sisi tunayo serikali lakini Tanganyika haina!’ Jumbe alifanya kama kusema tu. Kama ilivyo kawaida yake, Karume akapuuza: Tutarekebisha baadae.

Prof. Issa Shivji
Kama hawana serikali [ya Tanganyika] si shauri yao wenyewe!
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini Zanzibar tarehe 22 Aprili 1964…Tamko rasmi la safari ya Nyerere kwenda Zanzibar ambayo ilikuwa ni ya mara ya kwanza kutokea kufanyika mapinduzi, ilielezewa kuwa ilikuwa ni ”safari ya heshima.” Safari hiyo ilidumu kwa masaa mawili tu.

Nyerere alikwenda na Ronald Brown na Fiffot. Picha ya utiaji saini [Mkataba wa Muungano] ipo mpaka leo, na inamuonyesha Abdulaziz Twala, Kasim Hanga na Ali Mwinyigogo kutoka upande wa Zanzibar na Oscar Kambona, Job Lusinde na Bhoke Munanka kutoka upande wa Tanganyika.”
Kuuidhinisha Mkataba wa Muungano

Kutoka Issa G. Shivji, Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union.
Mkataba wa Muungano ni mkataba wa kimataifa ambao ulitiwa saini na viongozi wawili wa nchi mbili. Katika mfumo wa kisheria wa kawaida ambao unafuatwa na Zanzibar na Tanganyika, mikataba ya kitaifa inahitajia kuidhinishwa na mabaraza ya kisheria ili kuipa nguvu za kisheria.

Kifungu viii cha Mkataba [wa Muungano] kinasema wazi kuwa Mkataba wa Muungano ‘lazima uidhinishwe kisheria na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi la Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na pamoja na Baraza la Mawaziri liidhinishe na liipe nguvu za kisheria Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ya Zanzibar’.

Ni muhimu kuwa kifungu hichi hakizungumzi tu juu ya uidhinishaji wa Mkataba wa Muungano bali kinalazimisha sharti juu ya mabaraza mawili kutoka Tanganyika na Zanzibar kuudhinisha na kuupa nguvu kwa ajili ya serikali za nchi zote mbili.
Hilo ndilo khasa lililofanywa na Bunge la Tanganyika. Tarehe 25 Aprili 1964 (ambayo ilikuwa ni siku ya Jumamosi), Rais wa Tanganyika, Julius Nyerere,

aliliita bunge kwa ajili ya kuuidhinisha Mkataba wa Muungano. Wajumbe wengi wa Baraza la Mapinduzi walikuwepo wakati Bunge la Tanganyika lilipokuwa likijadili muswada wa sheria mpya wa kuuidhinisha kisheria Mkataba wa Muungano.
Aliusisitiza uhusiano mrefu wa kihistoria baina ya watu wa Tanganyika na watu wa Zanzibar, ambao umeufanya muungano baina yao uwe kama ni kitu cha kawaida.

Pia alitilia nguvu hamu ya watu wa Afrika kuujenga Umoja wa Afrika. Alilitilia mkazo suala la kuundwa kwa shirikisho la Afrika Mashariki na kuwa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar hautoziathiri [kwa vibaya] juhudi zao katika kuelekea kwenye Umoja wa Waafrika. Kurasa 82-83.

Wakati mchakato wa kuuidhinisha [Mkataba wa Muungano] kwa upande wa Tanganyika ulifuatwa hatua kwa hatua na ulifuata taratibu kama zinavatakiwa na sheria ya Mkataba wa Muungano, hayo hayawezi kusemwa kuwa yalifuatwa kwa upande wa Zanzibar. Ukurasa 85.

Jumbe na Salim Rashid [Katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi] wote wawili hawakubali kuwa kuliwahi kufanywa mkutano wa Baraza la Mapinduzi kuuidhinisha Mkataba wa Muungano. Kwa mujibu wa kiapo aliochoapa Salim Rashid Mahakama Kuu ya Zanzibar, katika kesi ya Rashid Salum Adiy na

watu 9 wengine dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na watu 4 wengine (Nambari 20 ya 2005), ameshuhudia [Salim] kuwa hajawahi kuulizwa na wala hakuwahi kuitisha kikao cha Baraza la Mapinduzi kuudhinisha Mkataba wa Muungano. Hajawahi kuulizwa na hakuwahi

kumpa taarifa mwandishi yoyote kuiandika sheria ya kuuidhinisha Mkataba wa Muungano. Ukurasa 89.
“Katika kipindi chote cha utawala wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere, uhakika wa kisheria wa Muungano ulinyimwa jukwaa. Ikionekana ni usaliti kujadili au hata kuutaja Mkataba wa Muungano wa 1964.

Hayati Mwalim julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa vile Mwalimu Nyerere alivimiliki vyombo rasmi vya habari na kwa sababu kulikuwa hakuna vyombo huru, maovu yake makubwa ya uvunjaji wa Katiba hayakuweza kuripotiwa.” Profesa Hamza M. Njozi kwenye dibaji ya kitabu cha Rais Mstaafu Mzee Aboud Jumbe, The Partner-ship: Tanganyika

Zanzibar Union 30 Turbulent years ambacho kilichapishwa mwaka 1994 na Al Khayria Press Ltd na kuenezwa na Amana Publishers.
Mkataba wa Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Jumuiya ya Mataifa (United Nations)
Kutoka Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru, Ukurasa 334.

“Ukweli unabakiya kuwa Mkataba wa Muungano baina ya Jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya watu wa Zanzibar haukuwahi kusajiliwa katika Seketeriet ya Umoja wa Mataifa [UN].

Kwa mujibu wa Andrei Kolomoets wa Ofisii ya Mambo ya Kisheria ya Umoja wa Mataifa “Kama ulisajiliwa basi kungelikuwepo rekodi katika Data Base na shahada ya usajili ingelikuwepo. Nimecheki, haipo.”
Kamisheni ya Katiba na Bunge la Katiba

Kutoka Issa G. Shivji, Pan-Africanism or Pragmatism: Lessons of Tanganyika-Zanzibar Union.
Itakumbukwa kuwa Mkataba wa Muungano uliagiza kuchaguliwa kwa kamisheni ya katiba na kufuatiliwa na bunge la katika ndani ya mwaka mmoja

kutokea siku ya kutiwa saini Mkataba wa Muungano ili katiba ya Muungano ipatikane.
Haikufanyika na wakati wa kuyatekeleza hayo ukaakhirishwa moja kwa moja. Kisheria ilifanywa hivyo pale bunge la Muungano lilipopitisha Sheria ya Bunge inayoitwa Sheria ya

Bunge la Muungano, 1965 (Nambari 18)…Kwa hiyo kimyakimya, kisirisiri, bunge la Muungano limeubadilisha Mkataba wa Muungano na Sheria za Muungano.

Inaweza kuhojiwa kama (a) upande mmoja wa bunge la Muungano una mamlaka ya kuubalilisha Mkataba wa Muungano ambao ni mkataba wa kimataifa na (b) kuibadilisha sheria ya Zanzibar ambayo inasemekana kuwa ilipitishwa na Baraza la Mapinduzi kuudhinisha Mkataba wa Muungano.

Inaweza ikahojiwa, na kwa njia safi na ilio wazi zaidi, kuwa njia nzuri ingelikuwa kwa viongozi watendaji wawili, Karume na Nyerere, na Nyerere kwa uwezo wake kama ni mkuu wa ‘Tanganyika’, angelipatana upya kuhusu Mkataba wa Muungano.

Lakini kisiasa njia hiyo ingelikuwa ni msiba kwa sababu ingeliuunja muungano hapo hapo. Ukurasa 163-164.

Kama unamjuwa adui yako na unajijuwa wewe mwenyewe, utakuwa huna wasiwasi wa matokeo ya vita hata viwe mia. Lakini kama unajijuwa wewe mwenyewe lakini humjui adui yako, basi kwa kila vita utakavyoshinda basi pia utashindwa. Na kama humjui adui yako na hujijui wewe mwenyewe basi utashindwa katika kila vita – Sun Tzu. Mfumo Kristo: Utiaji Saini wa Mkataba wa Muungano na Matokeo Yake {UHARAMU WA MUUNGANO}

 
Kero za Muungano zinapotikisa Umoja wa Kitaifa

KIASI cha mwaka au hata miwili, kabla ya Uhuru wa Tanganyika, Mwalimu Julius Nyerere, alinukuliwa kwenye karamu moja ya chakula cha jioni mjini Dar es salaam akisema maneno yafuatayo kuhusu Zanzibar:


“Kama ningeweza kukivuta kisiwa kile mpaka katikati ya Bahari ya Hindi ningefanya hivyo”.

Huku akionyesha wasi wasi dhahiri na kukerwa kwake na Zanzibar Mwalimu alisema: “kwa kweli sitanii kuna wasiwasi mkubwa kitatuletea matatizo makubwa huko mbele”.

Miaka mitano baadaye Tanganyika na Zanzibar ziliungana kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, April 26, 1964.

Kwa Watanzania, Aprili unabeba matukio matatu makubwa ya kihistoria. Tukio moja ni hili la nchi mbili, (Tanganyika na Zanzibar) kuungana; la pili ni kuuawa kwa mmoja wa waasisi wa Mungano huo, aliyekuwa Rais wa Zanzibar, mzee Abeid Amani Karume, miaka minane baadaye, Aprili 7, 1972.

Na tukio la tatu ni kufariki katika ajali ya gari kwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine ambaye rekodi yake haijavunjwa, Aprili 12, 1984. Yote haya yaligusa kwa namna moja au nyingine mustakabali wa Muungano.

Miaka 48 ni muda mrefu kwa uhai wa Muungano kama wetu, ikizingatiwa kwamba Muungano kama huu ulijaribiwa na nchi nyingine barani

Afrika, kama vile kati ya Senegal na Gambia uliojulikana kama Sene-gambia, na ukafa katika kipindi kifupi sana pengine kutokana na kukosekana kwa utashi madhubuti wa viongozi wa nchi hizo, au kutokana na mifumo ya miungano hiyo kutokidhi matakwa na matarajio ya wananchi walio wengi wa nchi husika.


Vivyo hivyo, licha ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutimiza miaka 48 mwezi huu, hatuwezi kusema kwamba umesafiri kwenye barabara iliyonyooka siku zote kufika hapa ulipo, wala hatuwezi kujitapa kwamba Muungano huu umekidhi utashi (wa viongozi) na matarajio ya wananchi walio wengi kuweza kuitwa “Muungano maridhawa” asilimia mia kwa mia.


Tumeshuhudia mawimbi na tufani na meli yetu bado inaendelea kusukwasukwa. Tunapoadhimisha miaka hiyo 48 ya Muungano, siku kumi na moja tu zijazo kuanzia leo, yatupasa kutazama nyuma kuona wapi tumejikwaa, wapi tumelegea, wapi tujisahihishe ili tuweze kwenda mbele. Yote haya yataka utashi na uzalendo wa kweli.


Hatutaweza kufanya hivyo bila kutazama nyuma kuona na kubaini ukweli juu ya utashi uliozaa Muungano, misingi na mihimili ya Muungano; utekelezaji wake na mitafaruku iliyojitokeza na kuzua tufani.

Je, kifo cha Karume au kung’atuka kwa Mwalimu Nyerere kumebakiza au kumepunguza utashi na usimamizi wa Muungano? Nini hatima ya Muungano?

Aprili 21, 1964 Rais Karume alipokea simu kutoka kwa Rais Nyerere akimwomba wakutane mjini Dar es Salaam kesho yake. Kweli, siku iliyofuata, Karume aliruka kwa ndege kwenda Dar Es Salaam, akakutana na Mwalimu na kuzungumza mengi ambayo hatujapata kuambiwa. Karume alirejea Zanzibar siku hiyo hiyo adhuhuri.


Siku moja au mbili nyuma kabla ya ziara ya Karume, Mwalimu alikuwa amemwagiza Mwanasheria Mkuu wa Tanganyika, Roland Brown, kuandaa rasimu ya Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar “bila mtu mwingine kujua”.

Naye Karume, aliporejea Zanzibar kutoka Dar Es Salaam, aliwaagiza wasaidizi wake kuandaa mapokezi ya Mwalimu Nyerere aliyetarajiwa

kufika Zanzibar (Unguja) kesho yake asubuhi, Aprili 22, 1964. Mwalimu (na ujumbe wake) waliwasili Unguja siku hiyo kama ilivyopangwa akiwa na rasimu ya Mkataba wa Muungano mkononi, na kumkabidhi Karume aupitie na kuutia sahihi Mkataba huo ulioandikwa kwa Kiingereza.


Mkataba huo ulitiwa sahihi siku hiyo hiyo na Nyerere na Karume na kushuhudiwa na wasaidizi wao.

Nyerere alirejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo baada ya kutiwa sahihi kwa Mkataba wa Muungano, maarufu kwa jina la “Hati ya Muungano” au kwa lugha ya kigeni “Articles of Union”. Mkataba uliofikiwa na viongozi hao wawili ulikuwa na hadhi ya kimataifa. Na ili Mkataba wa

kimataifa upate nguvu, utambuliwe na kutumika katika nchi husika ni sharti uridhiwe (to ratify) na mabunge ya nchi husika.

Kwa hiyo, Bunge la Tanganyika na lile la Zanzibar (Baraza la Wawakilishi) yaliitishwa haraka haraka na kuridhia Mkataba huo, Aprili 25, 1964, na Aprili 26, 1964 Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulitangazwa rasmi.
Tutazame kwa ufupi tu maswali yaliyoibuka juu ya uhalali wa Muungano na jinsi ulivyofikiwa, kero na mitafaruku inayousibu Muungano tangu mwanzo hadi sasa.

Imeelezwa mara nyingi na duru za Muungano kwamba, Nyerere alitoa wazo la Muungano kwa Karume, naye (Karume) akakubali sawia. Kuna ukweli gani kwa taarifa hiyo?


Ni mambo yapi yalikuwamo katika Mkataba wa Muungno? Kuna hoja pia kwamba Mkataba wa Muungano haukuwa na ridhaa ya wananchi; na hivyo si halali. Watetezi wa hoja hii wanakwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa, ili mkataba huo uwe halali, ilitakiwa kura ya maoni (referendum) kama ambavyo mapendekezo ya muafaka wa Zanzibar kati ya CCM na CUF umerejeshwa kwa Wazanzibar kupata kura ya maoni. Hoja hii ni sahihi kiasi gani?


Kumbukumbu zilizopo (na imeandika mara nyingi juu ya hili) zinaonyesha kwamba kabla na baada ya Uhuru wa Tanganyika, kisiwa cha Zanzibar kilimnyima usingizi Mwalimu Nyerere kiasi cha kutamani “kukivuta hadi katikati ya Bahari ya Hindi”, kama angekuwa na uwezo wa kufanya hivyo; lakini hakuwa na uwezo huo kwa sababu yeye hakuwa Mungu.


Kwa hiyo, pengine njia pekee aliyoona Nyerere inafaa, ni “kukidhibiti” kisiwa hicho na kukisogeza karibu kwa njia ya Muungano. Hakuna ushahidi kuonyesha kwamba Karume alikubali sawia pendekezo la Mwalimu la Muungano, lakini kuna ushahidi kuonyesha kuwa, mwanzoni Karume alikuwa mzito kupokea au kujadili pendekezo la Mwalimu.


Kwanza, Mwalimu aliwatuma Oscar Kambona na Bibi Titi Mohamed kwenda kumshawishi Karume juu ya nchi zao Kuungana, lakini yaelekea Karume hakuweza kutoa jibu lililonyooka.

Alipowatuma tena Kambona na Bibi Titi Mohamed na kuwatumia pia baadhi ya viongozi wa Zanzibar – Kassim Hanga na Salehe Sadallah

kumshawishi Karume akubali hapo ndipo Karume alipoanza kuuona “mwanga”. Hilo ni jibu la kwanza.

Itakumbukwa pia kwamba, wakati Nyerere akijaribu kuzima hofu yake juu ya kisiwa hiki kama alivyosema mwanzo, Marekani nayo ilijawa na hofu kwa kisiwa hicho kuendelea kuserereka kwenda (kutekwa) kambi ya Ukomunisti (Urusi) kifikra na kimahusiano kiasi cha kuitwa “Cuba ya Afrika).

Kwa hiyo, wazo la Nyerere la Muungano lilishabikiwa vile vile na Marekani kwa kuamini kwamba kama Zanzibar ingemezwa ndani ya “tumbo pana la Tanganyika”, harakati za Kikomunisti zikiongozwa na kina Abdulrahman Babu na vijana wengine kama Kassim Hanga, wenye fikra za mrengo wa kushoto, zisingefurukuta. Hilo ni jibu la pili.


Wakati huo huo Karume na Serikali yake alikuwa anakabiliwa na changamoto ndani na nje ya Serikali yake mwenyewe, kwamba alikuwa ameshindwa kutetea na kuendeleza dhana ya “Mapinduzi” iliyofanikisha Mapinduzi ya Januari 12, 1964, na hivyo alikabiliwa na tishio la kupinduliwa wakati wowote.


Kwa wana harakati wengi, Karume alionekana kuyaasi au kuyauza Mapinduzi. Kwa hiyo, Karume aliingia katika Muungano ili kujiponya mwenyewe na mahasimu wake ndani ya serikali waliomsakama na kutaka kumpindua. Hii ni sababu ya tatu.

Kwa sababu hizo tatu, na ile hofu ya Nyerere juu ya Zanzibar kuwa karibu na Tanganyika, tunaweza kusema kwamba Muungano huu

ulifikiwa kwa msukumo wa “hofu” na kwa pande zote mbili mmoja kutaka “kujiponya” na tishio lake la kufikirika. Hii haikuwa ndoa ya hiari, bali ilikuwa ndoa ya kulindana (marriage of convenience) na kujiponya.


Chini ya Mkataba wa Muungano, Tanganyika na Zanzibar zilikubali kushirikiana katika mambo kumi na moja tu, ambayo ni Katiba, mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Polisi, Mahakama, hali ya hatari na Uraia.

Mengine ni Uhamiaji, Mikopo na biashara ya nje, utumishi, kodi ya mapato na Bandari. Orodha ya mambo ya Muungano imekuwa

ikiongezwa kila mara kwa utaratibu ambao Wanasheria wa mambo ya Katiba wanadai ni kinyume cha Mkataba wa Muungano. Mambo hayo sasa yamefika 22.


Profesa Issa Shivji, katika kitabu chake “The Legal Foundation of the Union in Tanzania’s Union and Zanzibar’s Constitution” anabainisha kuwa Bunge la Tanzania halina mamlaka ya kuongeza au kupunguza mambo yaliyokubaliwa kwenye Mkataba wa Muungano. Kufanya hivyo ni kukiuka ibara ya 5(i) ya Mkataba.


Msomi huyo anaeleza kuwa marekebisho kama hayo yanaweza kufanywa tu kwa njia ya kura ya maoni (referendum), ambao ndio utaratibu pekee unaojulikana duniani kwa nchi zenye Muungano kama wetu.

Anayosema Profesa Shivji yamefafanuliwa vizuri na Mahakama ya Rufaa ya Canada, katika shauri la A.G of Canada for Nova Scotia Vrs A.G. Canada (1951) S.C.R 31.

Ni maoni pia ya mtaalamu wa Katiba za nchi mbali mbali, K. C Wheare, katika kitabu chake, “Modern Constitutions (Edition 1966), London, Oxford University Press – Uk. 84, kama alivyoelezea Profesa Shivji.

Kwa hiyo, Bunge, hata kama litakaa kama Bunge la Katiba (Constituent Assembly), haliwezi kubadili Mkataba wa Muungano wa 1964. Huu

ndio msimamo na mwongozo wa kisheria (wa mahakama) kama inavyobainishwa na Mahakama ya Mamwinyi ya Uingereza, katika shauri la A.G for Canada Vrs A.G for Ontario: (1973) A.G. 326 (PC); na katika hukumu za Mahakama ya Rufaa ya India, katika shauri la Kesavananda Vrs State of Kerala (1973) S C. 1461; Smt Indira Gandhi Vrs Raj Narain (1976) 2 S.C.R 3475 na katika kesi ya Minerva Mills Vrs Union of India: AIR (1980) SC 1789.


Kitendo cha Bunge la Muungano cha kubadili mambo ya msingi yale 11 yaliyomo katika mkataba kinyume cha utaratibu, kimekuwa ni moja ya sababu za Wazanzibari kurejea hoja ya “kutaka kumezwa”: na pale wanapojiamlia kutenda watakavyo, kinyume na baadhi ya marekebisho kiasi cha kuitwa “wakorofi”, serikali ya Muungano imekosa nguvu wala kauli inapobaini hayo; kero za Muungano huibuka,

mitafaruku kuzuka, Muungano huyumba na utatuzi huwa mbali kwa imani kwamba suala la Muungano ni nyeti na lisilozungumzika.

Muungano uliofikiwa na waasisi wake, Mwalimu Nyerere na Karume mwaka 1964 ni halali na hauwezi kubatilika kwa sababu tu haukufikiwa kwa njia ya kura ya maoni (referendum) ya wananchi. Utaratibu wa kura ya maoni ni mpya kwa mfumo wa sheria za nchi za Jumuiya ya

madola. Ulianza kutumika miaka ya 1970 (1976). Kwa hiyo wakati Nyerere na Karume wanafikia Muungano wa nchi zao walikuwa sahihi walivyofanya kwani Katiba iliruhusu.

Hapa nchini, utaratibu, uhalali na umuhimu wa kura ya maoni ni matokeo ya marekebisho ya Katiba ya 1984 pale Katiba hiyo ilipoingiza ibara ya 8(i)(a) inayosomeka: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo,

wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi”. Tangu sehemu hiyo ya Katiba itungwe 1984, ni lazima wananchi watoe maoni yao kwa kura ya maoni, ni muundo gani wa Muungano wanataka.

Mengine yaliyokubaliwa katika mkataba huo ni pamoja na Rais wa Serikali ya Muungano, kwa kushauriana na Rais wa Zanzibar, kuteua

Tume ya kupendekeza Katiba ya Muungano na kuitisha Bunge la Katiba ndani ya mwaka mmoja tangu tarehe ya Muungano, kupitisha Katiba ya Muungano.


Itakumbukwa kuwa pia Muungano wetu ulifikiwa haraka haraka bila maandalizi ya kutosha kiasi kwamba serikali ya Muungano ilianzishwa bila kuwa na Katiba ya nchi. Kwa sababu ya uharaka huo aina ya “zima moto”, ilibidi Katiba ya Tanganyika ya 1962 itumike pia kama

Katiba ya Muungano kwa kuifanyia marekebisho madogo, hadi hapo Muungano utakapopata Katiba yake.

Hadi muda wa mwaka mmoja unamalizika, si Tume ya Katiba iliyoteuliwa, wala si Bunge la (kutunga) Katiba lililoitishwa. Ukimya huo ulifuatiwa na kutungwa kwa sheria Na. 18 ya 1965 ya kuongeza muda huo “hadi hapo hali itakaporuhusu”, huku kero za Muungano zikiibuka kwa kasi.

Mbali na kuongezwa kwa mambo ya Muungano kinyume cha Mkataba wa Muungano, mengine ni pamoja na kufutwa kwa nafasi za Makamu na Makamu wawili wa Rais, kuingizwa kwa mfumo wa chama kimoja ndani ya Muungano, na uteuzi wa Tume ya kupendekeza Katiba mwaka 1976, tofauti na aina ya Tume iliyotajwa ndani ya Mkataba na mengine. Yote haya na mengine yamezidisha badala ya kupunguza kero za Muungano.


Katika sehemu ya pili ya makala haya, tutajibu maswali yafuatayo: kwa nini Rais Nyerere hakuteua Tume ya Katiba wala kuitisha Bunge la Katiba na kusababisha Muungano kuendeshwa kwa Katiba ya mpito kwa miaka 13? Je, Katiba ya 1977 ni halali chini ya mkataba wa Muungano?


Je, kifo cha Karume na kung’atuka kwa Mwalimu madarakani mwaka 1985 kuliathiri vipi utashi wa Muungano na kwa kiasi gani? Je, kitendo cha Zanzibar kuwa na bendera yake, wimbo wa taifa na ngao ya taifa ndani ya Muungano ni sehemu ya mkataba? Kwa nini haya yafanyike leo na si wakati wa enzi za waasisi wa Muungano huo?


KATIKA sehemu ya kwanza ya makala haya ya gazeti hili, toleo lililopita, tuliona jinsi mkataba (Hati) wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ulivyoandaliwa na kutiwa sahihi haraka haraka bila kumhusisha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, na kutangazwa Aprili 26, 1964.
Tuliona pia jinsi idadi ya mambo ya Muungano yaliyokubaliwa chini ya Mkataba huo ilivyoongeza kutoka 11 kufikia 22 na kuleta utata wa kikatiba na kero za utekelezaji.

Ingawa Mkataba ulitaka iundwe Tume ya kupendekeza Katiba na hatimaye kuitishwa kwa Bunge la Katiba (Constituent Assembly), ili kuupatia Muungano Katiba yake ndani ya mwaka mmoja, si Tume iliyoundwa, wala Bunge kuitishwa hadi baada ya miaka 13 (1977), na hivyo Muungano uliendeshwa kwa Katiba ya kuazima kutoka Tanganyika, kwa maana kwamba Katiba ya Tanganyika ndiyo iliyotumika pia

kama Katiba ya Muungano, kwa kufanyiwa marekebisho ya hapa na pele.
Katika sehemu hii ya makala, tutaona kwa nini Rais Nyerere alishindwa kuteua Tume ya kupendekeza Katiba hadi 1977, na athari zake

kwa Muungano. Tutaona pia jinsi kifo cha Abeid Karume mwaka 1972 na kung’atuka kwa Mwalimu madarakani mwaka 1985 kulivyoathiri au kupunguza utashi wa Muungano miongoni mwa raia wa nchi hizi mbili, migogoro na kero zilizofuatia, kiasi cha kutishia mustakabali wa Muungano kwa ujumla.

Mkataba wa Muungano uliridhiwa na Mabunge ya nchi zote mbili, Aprili 25, 1964 na kuwa Sheria zinazojulikana kama Sheria za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Na. 22 ya 1964, kwa upande wa Tanganyika, na Sheria ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika kwa upande wa Zanzibar. Sheria zote mbili zinajulikana katika ujumla wake kama (Acts of the Union) Sheria za Muungano. Mkataba wa Muungano ni sehemu ya Katiba ya nchi.

Inapokuwa hivyo, Bunge la nchi moja halina uwezo wa kubadili / kurekebisha Katiba wala mfumo wa Muungano bila ya ridhaa ya Mabunge yote mawili; kufanya hivyo ni kukiuka Mkataba wa Muungano.
Vivyo hivyo, uwezo wa Bunge la Katiba wa kurekebisha Katiba haujumuishi uwezo wa Bunge wa kubadili muundo asilia wa Muungano.

Mapema Julai, 1964, serikali ilitangaza Shindano la kutafuta jina wakilishi la Muungano na maombi 1,534 yalipokewa kutoka nchini na kutoka nchi za nje kama Urusi, Uingereza, Pakistani, Sweden, China, France, Australia, Poland, Italia na hapa nchini.
Jina la “Tan-zan-ia” ndilo lililoshinda, likifuatiwa na mengine ambayo ni Tanzan, Tangbar na Zantan. Mwalimu alitangaza jina hilo Oktoba 29, 1964 ambalo mshindi wake hajafahamika mpaka sasa .

Uteuzi wa Tume ya kupendekeza Katiba na kuitishwa kwa Bunge la Katiba lilikuwa ni sharti la kikatiba. Kwa mantiki hii, Bunge la Kawaida halikuwa na uwezo wa kutunga Sheria Na. 18 ya 1965 kuahirisha uteuzi huo. Kwa nini Nyerere alifikia hatua hiyo?
Kama tulivyoeleza mwanzo, ni kwamba Nyerere na Karume kila mmoja aliingia kwenye Muungano shingo upande (bila kupenda); kila

mmoja akitaka kuganga tatizo lake, bila hivyo, pengine pasingekuwa na Muungano, kwa maana kwamba utashi wa Muungano haukuwapo.
Punde, Nyerere na Karume walianza kutambuana vizuri, kwamba kulikuwa na tofauti kubwa kati yao kimaumbile, kielimu na kimalengo kiasi

kwamba haikuwa rahisi tena kwao kutenda kwa pamoja, kwa amani na utulivu.
Hapa kulikuwa na Mwalimu Nyerere msomi, makini wa kutenda, “mjanja” na mwenye “maono”. Hapa pia kulikuwa na Karume, mtu mzima, baharia mzoefu wa mambo ya kimataifa na mwenye kutumia hoja ya nguvu badala ya nguvu ya hoja.

Ilifika mahali watu hawa wakawa wamechokana kiasi kwamba Karume alisikika akimjibu Mwalimu, akisema, “…kama ni hivyo tuvunje Muungano”. Karume alikuwa na ujasiri wa kumkatalia Nyerere baadhi ya mambo baada ya hofu iliyomwingiza kwenye Muungano kupita, na akaweza kusimama kwa miguu yake, na kushika hatamu za uongozi wa nchi bila kupingwa.

Ugomvi wa kwanza ulikuwa juu ya muundo wa Muungano. Inaelezwa kwamba, Karume alitia saini Mkataba wa Muungano akiamini kwamba alikuwa akiingia Mkataba wa kuunda serikali ya Shirikisho ambapo kungekuwa na Serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Shirikisho, yaani Muungano.

Dhana hii inathibitishwa na Balozi wa Zanzibar, jasusi wa CIA, Frank Carluci, katika taarifa aliyotuma Washington, Aprili 23, 1964 akisema: “Karume bado anaamini kwamba ametia saini Mkataba wa kuunda Shirikisho, na kwamba kila nchi itaendelea kubakia huru, ila zitashirikiana kwa mambo kadhaa yaliyotajwa katika Mkataba”.
Hii ilithibitishwa pia na MwanaSheria Mkuu wa Zanzibar Wolfango Dourado baadaye akisema kwa kulalamika. “…. Karume alitarajia kuona
Shirikisho …. rasimu ya Mkataba ilifanywa kwa siri na Rowland Brown (Mwanasheria Mkuu wa Tanganmyika).…..na mimi sikuhusishwa kabisa. Itakuwaje Mwanasheria Mkuu wa upande mmoja apuuzwe kabisa, asihusishwe, wala kushauriwa? Ndiyo maana tuna matatizo (ya Muungano) hadi leo ….”

Mwanzoni Karume alijipa moyo juu ya hili, na alisikika wakati fulani akimwambia Thabit Kombo: “Usijali, sisi tutakuwa na Baraza letu la Wawakilishi wakati wao (Watanganyika) hawana; na hilo walilo nalo na sisi tumo….. kwa nini tuwe na hofu?”.
Alichoamini Karume, ndicho kinachoelekea kuwa ukweli wenyewe, kwa sababu Hati ya Mkataba inatambua kuwapo kwa nafasi ya Rais wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania), akisaidiwa na Makamu wawili wa Rais – mmoja upande wa Zanzibar ambaye pia ndiye Rais wa Zanzibar, na mwingine upande wa Tanganyika, na kwamba, kwa mujibu wa ibara ya 4 ya Mkataba na kifungu cha 8(i) cha Sheria Na. 22 ya 1964, pamoja na “Presidential Decree” kifungu cha 4, iliyochapishwa kama Taarifa ya Serikali Na. 245 ya 1/5/1964, inatamkwa kuwapo kwa Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar.

Inatamkwa pia kwamba, kufuatia Muungano huo, Sheria za Tanganyika na Sheria za Zanzibar zitaendelea kuwa na nguvu na kuheshimika katika nchi husika.

Pengine kilichomtibua zaidi Rais Karume ni ile Sheria ya Rais (Decree) ya 1964 (The Interim Constitution Decree, 1964 – Govt Notice No. 246 of 1/5/1964) kuhusu marekebisho ya Katiba ya Tanganyika (The Republican Constitution) ili kuifanya ihudumie pia Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Muungano kwa pamoja na kwa wakati mmoja, na kuitwa “Katiba ya Muda ya 1964”, na kumfanya ajiulize mara mbili: ni aina gani ya Muungano alimo, wala asipate tafsiri sahihi kule anakoelekea.

Kwa mfano, Karume alitarajia kuona Bunge la Tanganyika, Bunge la Zanzibar na Bunge la Muungano yakifanya kazi; lakini alichoona ni Bunge la Zanzibar na Bunge la Muungano pekee na kupata tafsiri kwamba Tanganyika ndiyo imekuwa Tanzania, na kuanza kujenga hofu ya Zanzibar kutaka kumezwa na Tanganyika.

Hofu ya Karume ilizidi kuongezeka pale masuala ya Muungano yalipoanza kuongezwa kinyemela kwa maagizo / Sheria (Decree) ya Rais, kabla hata Muungano haujapata Katiba yake.
Wolfango Dourado amenukuliwa akisema, “Karume alikuja kutambua akiwa amechelewa kwamba Nyerere alikuwa amemburuza. Ndipo na yeye akaanza kwenda kivyake …”.

Shinikizo lilitolewa na Nyerere kwa Karume kumtaka kumwondoa Dourado, lakini Karume alikataa kata kata. Dourado alikuja kuondolewa tu 1977 wakati wa Rais Aboud Jumbe, kufuatia kifo cha Karume.
Katika mazingira tete kama haya, ambapo waasisi hawa wa Muungano walikuwa wameanza kuwa mbali mbali juu ya suala zima la

Muungano, haikuwa rahisi kwa Rais Nyerere kushauriana na mwenzake na kufikia muafaka wa kuteua Tume ya kupendekeza Katiba.
Miaka mitano baadaye (1977), Tume ya pamoja kati ya TANU na ASP iliyopewa jukumu la kupendekeza kuunganishwa kwa vyama hivyo viwili, ndiyo pia iliyopewa jukumu la kupendekeza Katiba ya Muungano, tofauti na Tume iliyotarajiwa kuundwa chini ya Mkataba wa Muungano.

Utata wa kisheria unaozuka juu ya Katiba ya 1977 ni kwamba, wakati Tume iliyopendekeza Katiba hiyo ilikuwa ya vyama vya siasa, na kwa kuwa vyama vya siasa halikuwa suala la Mungano, Tume hiyo ilivuka mipaka kwa kufanya kazi kama Tume iliyoteuliwa kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano. Na vivyo hivyo kwa Bunge lililoitishwa kupitishwa Katiba hiyo.
Kama tulivyoonyesha hapo juu, ni kwamba, kero za Muungano ni za Kikatiba na kiutekelezaji zaidi kuliko kisiasa. Na tutambue pia kwamba,

Mkataba wa Muungano uliandaliwa kidharura kukidhi hali ya matishio yaliyokuwa yakizikabili nchi hizi mbili wakati huo. Alichofanya tu Mwanasheria Mkuu Roland Brown, kwa kusaidiana na Mwandishi Mkuu wa Miswada nchini Tanganyika, ni kuweka mifupa (skeleton) ya

Mkataba, na ilikuwa juu ya Wanasheria kuweka minofu baadaye ili Mkataba huo uweze kutekelezeka vizuri.
Hilo halikufanyika; Muungano umeendelea hadi sasa kwa Mkataba usio na minofu na kuzaa misuguano mikavu yenye maumivu. Hata kwa yale yaliyo wazi ndani ya Mkataba huu utekelezaji wake umekuwa kinyume cha inavyotakiwa; nguvu badala ya busara, usiri badala ya

uwazi, jazba badala ya uvumilivu na kuheshimu hoja za wengine, vimetumika kuzima maoni na tafsiri sahihi ya Muungano kwa madai kwamba muundo na suala zima la Muungano huo ni nyeti, lisilozungumzika wala kuhojika.
Kwa jinsi hii kero za Muungano zimezidi kuongezeka, nasi tumezika kichwa mchangani kwa tabia ya mbuni na kutikisa umoja wa kitaifa. Tunaambiwa, hata ule Mkataba wa Muungano haupo, umefichwa au umepotea.

Baadhi ya misukosuko iliyowahi kutishia umoja huo ni pamoja na Rais wa Zanzibar, Alhaji Aboud Jumbe, kuondolewa madarakani 1984, kwa sababu tu ya kutumia haki yake ya kikatiba, chini ya ibara ya 125, inayoruhusu mtu kudai/kutaka tafsiri ya kikatiba iwapo tafsiri hiyo au utekelezaji wake unabishaniwa kati ya Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.

Mitikisiko mingine ni Zanzibar kutaka kujiunga na Jumuiya ya nchi za Kiislamu kama dola, kundi la Wabunge 55 (G.55) kudai kurejeshwa kwa Serikali ya Tanganyika, Zanzibar kuwa na bendera na wimbo wake wa Taifa; Zanzibar kuwabagua Watanzania kwa misingi ya Wazanzibari na “Wazanzibara”, Zanzibar kutoitambua Tanzania Bara linapokuja suala la (utafiti) maliasili ya mafuta Visiwani japo hilo ni jambo la Muungano, na mingine.

Baadhi ya vituko hivi vinaweza kuwa ni ukorofi tu, lakini ukipitia kwa makini Mkataba wa Muungano (Articles of the Union) na Sheria za Muungano (Acts of Union), utabaini kwamba baadhi kati ya hivyo si vituko wala ukorofi, bali ndivyo unavyosomeka Mkataba, ila watu wameaminishwa vinginevyo.
Ndiyo maana Serikali ya Muungano imenyoosha mikono kwa baadhi ya “vituko” vya Serikali ya Mapinduzi vinavyoweza kuonekana kama ni uvunjaji wa Katiba, wakati “vituko” hivyo ndivyo vilivyowekwa kwenye Mkataba wa Muungano.

Moja kati ya hivyo ni hili la Zanzibar kuwa na bendera na wimbo wake wa Taifa. Kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano, hakuna kitu kinachoitwa Tanzania Bara wala Tanzania Visiwani.

Kifo cha Karume na kung’atuka kwa Mwalimu mwaka 1985 kumeathiri au kuimarisha vipi utashi na uthabiti wa Muungano?
Ni kwamba, kifo cha Karume kiliondoa misuguano kati ya waasisi wawili wa Muungano, vinginevyo tusingekuwa na Muungano leo. Udikteta ulipungua Visiwani na kuzua hali tete ambayo haikuwa ya manufaa kwa Muungano.

Kwa mfano, kufuatia kifo cha Karume, Chama cha ASP kilifanya Mkutano Mkuu wake wa kwanza Desemba, 1972 tangu 1962. Karume alikuwa amesema kuwa hapatakuwa na uchaguzi Zanzibar hadi baada ya miaka 50 tangu Mapinduzi. Hivyo, kama angeendelea kutawala, uchaguzi wa kwanza Zanzibar ungekuwa mwaka 2014.

Udhaifu huu unaonekana kurithiwa na kutetewa na Rais wa sasa wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, ambaye anaonekana hataki mabadiliko (hata enzi hizi za mfumo wa vyama vingi), eti kwa kufanya hivyo kutafuta “historia”.

Uimla huu si uzushi. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa ASP, Mzee Thabit Kombo, anakiri hilo katika kitabu cha Minael – Hosanna Mdundo, “Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha” uk. 182, kwa kusema, “…… sasa (watu) wanaweza kutoa dukuduku zao na hata kuikosoa Serikali kama mambo yao hayakwenda vizuri. Nani alithubutu kuuliza kitu kuhusu mwenendo wa mtu au wa Serikali wakati wa Baraza la Mapinduzi (enzi za Karume) la kwanza?”

Kung’atuka kwa Nyerere mwaka 1985 kwa upande wa pili, kuliondoa ile dhana kwamba Muungano hauhojiki. Watu wamepata nafasi ya kuhoji mfumo, muundo na utekelezaji wa Muungano kwa lengo la kuboresha hayo, kabla ya hapo lilikuwa ni jambo linalokaribia uhaini.
Kitendo cha Mwalimu, ambaye Dourado anamwelezea kuwa alikuwa “mkaidi na mwenye kiburi” (vain and arrogant) cha kuatamia tafsiri na

utekelezaji wa Muungano, ndicho moja ya sababu ya gari la Muungano kupata pancha, kuacha njia na kuingia porini.
Tatizo la kero za Muungano ni la Kikatiba zaidi kuliko kisiasa. Kwa hiyo ni lazima litatuliwe Kikatiba. Juhudi zozote nje au mbali na mtazamo huu ni sawa na kuficha ugonjwa, au kujaribu kutibu dalili za ugonjwa badala ya kutibu ugonjwa wenyewe.

Ni Mwalimu mwenyewe, aliyetuasa kuwa “afichaye ugonjwa, kilio kitamuumbua”. Nasi tunaposherekea miaka 44 ya Muungano, Aprili 26, 2008, yatupasa kuliweka hilo akilini mwetu
Imeandikwa na Joseph Mihangwa- Gazeti la RaiaMwema
 
kipanya_26_-_05_-_2012_20120531_1948461845.jpg
 
Back
Top Bottom