Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

sidhani kuambiwa ukweli ni sawa na kutukana

huwezi kusema Dr slaa kajinyea au lema kapata bwana ni sawa na zitto alichofanya

kwa hili Zitto kasema ukweli ingawa yeye ndiye bingwa wa kubwabwaja matapishi; kuna tatizo na kauli ya Mtei, there are certain things we dont say in public

Mkuu suala la dini ni nyeti sana na kwa bahati mbaya sana ni vigumu kulitenganisha na fikra za watu. Suala la mahakama za kadhi ni mfano dhahiri hapa, utaona litakavyosumbua akili za watu. Tutapona tu endapo tutasimama kwenye kauli moja kuwa Tanzania sio nchi ya kidini na haifungamani na dini yoyote na wajumbe wafanye kazi kama vile ni wapagani na hawajui kama kuna mungu kuondoa influence ya dini zao kwenye maamuzi
 
angalizo................

katiba mpya ikitengenezwa bila ya kuwa na mitizamo inayokinzana na kusigana hata ndani ya familia zetu (achilia mbali vyama vya siasa), hiyo haitastahili kuitwa "katiba mpya" na itakufa upesi sana na kwa style ile ile iliyoundiwa!

katiba siyo siasa...it's rather an instrument for checking down extremes za wanasiasa, watu binafsi, etc. kwa hiyo katika stage hii acha insanity, madness, etc vyote vi-prevail.

kachumbari ni tamu kuliko ingredients zake ukizila individually! pia, nondo za kujengea nyumba na madaraja mazuri hutokana na chuma chakavu!

it's within these lines that mimi binafsi sioni tatizo kwenye kauli ya mtei kwa upande mmoja na kwa upande mwingine sina tatizo kabisa na alichokisema zitto (kama kweli amenukuliwa vizuri).
hivi kweli tuache kuyapa uhuru mawazo na feelings za watu eti tu kwa kuchelea wengine watasemaje?
tukificha uchi, tutazaa kweli??
 
Kama kweli Mtei katoa pumba hizo ni lazima aombe radhi. Mimi ni Mkristo, lakini ujinga wa wazee kama Mtei hautufai. Afute kauli yake haraka!
 
Hivi udini ni upi kati ya kuteua watu wengi wa dini moja na kusema kuwa walioteuliwa wengi ni watu wa dini moja?

Nasubiri jibu hapa, otherwise nitauliza hili swali over and over again hadi nipate jibu.
 
attachment.php



Mwenyekiti wa CHADEMA akiwa na mkewe ambaye ni binti wa mwanzilishi wa Chadema bwana Edwin Mtei



Edwin Mtei ambaye ni mwanzilishi wa CHADEMA na pia baba mkwe wake Mwenyekiti wa Chadema bwana Freeman Mbowe (Mbowe kaoa binti yake Mtei) aliyoa kauli ya malalamiko kuwa wajumbe wa katiba mpya wengi ni waislam.

Hivi kama huu ndio mwelekeo wa kimawazo wa baba mkwe je Freeman Mbowe kama mwenyekiti wa Chama atakuwa na mtazamo gani?

Inamaana mtu kama Zitto Kabwe na waislam wengine ndani ya CHADEMA watajiskiaje kama hii ndio kauli not only ya muasisi wa huki chama bali pia ni baba mkwe wake mwenyekiti wa chama chao?

Kwa kweli hii imenitisha sana na kusema ukweli naona hii sumu ya udini itatupeleka pabaya na hasa kama inayinyizwa na mtu kama Edwin Mtei
 
Haya kaka ZZK tunasubiri hekima zako ambazo bado ni Tajiri.

Hiyo Tume sio tu imejaa uislam bali hata idadi ya uzanzibari haulingani na matakwa ya katiba husika maana kwa asilimia kubwa katiba husika haitawahusu hao wa Zanzibari kwa sababu masuala ya Muungano hayatajadiliwa.
 
Sasa wewe ulitaka rais aanze kutafuta mkristo wa kutoka Zanzibar amuweke kwenye tume huoni huo kama ndio udini wenyewe?

Swala lilikuwa sio kupata watu wa dini fulani , malengo ni kupata watu watakaosaidia kusimamia mchakato wa katiba mpya na rais aliweka wazi watu watume majina, kwanini nyie hamkutafuta majina ya wakristo wa Zanzibar mkampelekea rais? Mbona jina la Mwesiga Baregu mlipeleka?

Sasa hapa kama unavyoona swala la dini halipo na halisaidii.

Kwa hiyo unataka kutuambia Zanziba walioenda shule ni waislamu tu na hamna mkristo?
 
Huyu ndumila kuwili "zitto" katokea huku tena. Nae anatafuta ucelebrity sio
zitto robo yuko cdm na robo3 yuko ccm yaani ni kirusi fulani hivi cha hatari.
 
Kama hali ya udini ndiyo iko hivi kama tunavyoshuhudia hapa JF tutegemee nini huko mtaani? Ningependa tujadili wajumbe wa hii tume based on intellectual capacity and not otherwise.

Mimi ni Mkristu/Roman Catholic na sioni tatizo kwa tume kuwa na waislam wengi.Cha msingi huwa ninaangalia competency kwanza ndipo busara nyingine za uwiano zifuate.Ni jambo la hatari kujadili udini na ukabila katika mazingira yanayoweza kutugawa na kutuondolea utaifa wetu.Uzalendo wetu uko mashakani.Kwa picha hii ninayoiona CIA,MOSSAD,M15 na wengineo wakituchomekea hii dhana ya Udini tutamalizana wenyewe kwa wenyewe.Hatua ambayo Nigeria imefikia ndipo tunakoelekea sasa.Wanasiasa,viongozi wa dini,na watu wenye ushawishi katika jamii tuache kutoa matamshi bila kufikiria athari.tuna maadui ambao tunahitaji umoja wa kitaifa kupambamana nayo kama matabaka na mapengo ya kiuchumi,ombwe la fikra na uongozi,social vices kama ufisadi na ukosefu wa maadili.tunahitaji utaifa kuliko mgawanyiko wa kiimani au kikabila kukabiliana na haya.Mahakama ya kadhi au kujiunga na OIC sio issue,ili mradi Refferundum imependekeza hivyo.Tuache uoga na hoja nyepesi bila kuzingatia athari

We are a people bedevilled by so many challenges which of course, we've barely scratched the surface of. The leadership deficit has aggravated our economic decline and retardation, and threatens not only our social cohesion but our very identity as a people. In times like these, a strong and transformational leadership is what is required to mobilize our abundant human and natural resources for us to realize our full potentials, but this deficit forms the bane of our problems. Paradoxically, while we acknowledge the failure of leadership, and the incapacity or inability of the present crop of leaders to do much to salvage our pathetic situation, we are still waiting on them

Whatever the case, it is our generation which will suffer most because the present crop of leaders have little to lose; we will live with the consequences of their actions while our children’s future becomes increasingly uncertain

We are in a terminal decline, the question is are we doing enough to address this? What can we or should we do to reverse this certain reality?

wew ni mkristo wa jina, kama ungekuwa mkristo anaye fahamu imani yake vyema usingesema hakuna tatizo kwa tume kuwa na waislamu wengi.
 
Kati ya hao waliochaguliwa na Rais haujui kuna Wajumbe ambao Mmoja ya Wazazi wao ni Mristo au Muislamu?

Kenya walimetoa Katiba Shwari na Murua kabisa ilikuwa na Viongozi wawili yaani Majaji wawili Wahindi wa Kikenya

Kenya wahindi ni asilimia 2 tu; lakini Katiba yao imewafurahisha Wakristo na Waislamu wote kwahiyo Tume sio

Udini; Tume ni Fikra na Uwajibikaji na Usawa wa wawakilishi na Sio Udini...

READ BELOW HOW PEOPLE OF THE WORLD SAID ABOUT TANZANIA

"It may be dirt poor, but it's more or less equally dirt poor, without the class or tribal strife that has ripped apart so

much of Africa. Whatever the leaders of Tanzania have done wrong since it was formed in 1964, they've


done a few things right... It means there is no war, and when your borders touch Rwanda, Burundi, Mozambique and

Congo."
 
wew ni mkristo wa jina, kama ungekuwa mkristo anaye fahamu imani yake vyema usingesema hakuna tatizo kwa tume kuwa na waislamu wengi.

mna chuki ya asili,watu wabaya sana nyie,mungu atawachapa viboko kwa chuki zenu na hamtakaa mfanikiwe milele.mkiambiwa chama cha kanisa mnabisha ona sasa.
 
Haya kaka ZZK tunasubiri hekima zako ambazo bado ni Tajiri.

Hiyo Tume sio tu imejaa uislam bali hata idadi ya uzanzibari haulingani na matakwa ya katiba husika maana kwa asilimia kubwa katiba husika haitawahusu hao wa Zanzibari kwa sababu masuala ya Muungano hayatajadiliwa.

Nampongeza Mzee Mtei kwa kusema Ukweli ambao wengi wanaogopa kusema. Mzee Mtei ni mwanafalsafa, kaona mbali

Watu wengine wangi imewauma ila wanaogopa Kusema.... Vasco da Gama ni Mdini namba moja.

Kidonda hutibiwa kwa kuoshwa na kuwekwa Hydrogen peroxide, inauma sana.

Hii statement ya Mzee Mtei itasaidia sana.Watanzania tafakari na fikiria. Acheni uvivu wa kufikiri. Mzee Mtei katupa mwanga wa kuona mbali.

Ni kweli kabisa kati ya wajumbe wote, waislamu ni wengi zaidi....Huo ndo ukweli.

Kutoka Zanzibar wapo 15 - halafu kati ya wale wa Tanzania bara (marehemu tanganyika) wapo waislamu tena karibu nusu.

So Waislamu kama 22 na wakristo kama 8. - Tanzania fanyeni analysisi


Wakristo hawajatendewa haki. Kikwete ana mpango fulani hapo.
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.

Sikupenda Mh Zito haya maneno yamtoke. Kwanza Mzee Mtei ni kama babu yake, ni kweli tuna watania mababu na mabibi zetu, lakini hatuwatukani na tena si kwa kashfa mbele ya halaiki ya watu. Pili ni huyu huyu mzee anayemtukana kwa kufilisika mawazo ndiye muanzilishi wa chama ambacho yeye anajivunia nacho na anachokitumikia kama watanzania walio wengi.

Kama Zito ni gamba nigeona ni sawa au ndiyo katika mbio za kujiunga nao?

Zito tafadhali umwombe mzee wa watu msamaha na wananchi wote kwa kauli hii mbaya, jitetee kimagamba kuwa mwandishi alikusikia isivyo.

Vinginevyo ujitoe CDM na kama unabaki utakuwa na laana itakayokufuata maisha yako yote. Nisawa na mtu anayemwona baba yake amepungukiwa kwa uzee na yeye kwa vile amejaa tele anamdharau anamtukana na kumsononesha moyo wake.


Kumbuka Zito leo umemtukana Baba mwanzilishi wa chama chako ambaye ni sawa na baba yako mzazi, je kesho kuimatendo utawafanyia nini? Kimbia laana mwanangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom