Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

Mtei amefilisika kimawazo - Zitto

Mbunge wa Kigoma Kaskazini-CDM amesema Mzee Edwin Mtei amefilisika kimawazo kwa kauli yake kwamba tume ya Katiba ina Waislam wengi kuliko wakristo.

Source:JAMBO LEO.

zito ndo ovyo kabisa kijana mmbichi ndumilakuwili na mlamba nyayo za wapumbavu.mnafiki mzindaki,ovyooo
 
Mchukia Uonevu said:
Naona kuna hoja ya kujadili hapa. Kama concern ya mzee Mtei ni kuwa na uwakilishi sawa kati ya waislam na wakristo kwenye tume aliyounda rais Kikwete, na kama muundo wa tume ilihitajika wajumbe kutoka Zanzibar na Bara, unadhani wale walioteuliwa kutoka Zanzibar wawe dini gani? (Kama asilimia zaidi ya 98 wa waznzibar ni waislam?)
Mchukia Uonevu said:
Hivi mkuu,hapo kwenye red,hayo tu mahitaji yaliyotupelekea kuwa na haja ya kuandika katiba mpya?

Wajumbe wa bara,wajumbe 3 au 4 kati ya 15 ndio waislam,wengine wote wakristo! Kwa waislam wa Tanganyika kutolalamika ina maana hawajui athari za uwiano huu,au ni vipi?

Mchukia-Uonevu,

..Hii ni Tume ya Katiba ya TANZANIA, kwa msingi ili kuondoa mabishano yasiyokuwa na tija, Raisi alipaswa kuweka uwiano wa 50--50 baina ya Waislamu na Wakristo.

..mimi naamini Znz wapo Wakristo 4,5,6, wenye qualifications za kuwa kwenye tume ya Katiba ya TANZANIA. tatizo ninaloliona mimi ni kwamba Raisi hakuona ulazima wa kuwateua, na hilo ni kosa.

..pia haiyumkiniki kwamba huku Tanganyika hakuna Waislamu zaidi ya hao wanne walioteuliwa ambao wanafaa kuwemo kwenye tume ya Katiba.

..sidhani kama JK na SHEIN ni Wadini. I think they r aloof.

[/B]

Joka Kuu,

Unanisikitisha ndugu yangu unaangalia tume kwa minajili ya dini zao badala ya competence. Kama tunaangalia kwa mujibu wa dini zetu basi nadhani JK ni mdini sana kwani serikali yake zaidi ya 70% ni WAKRISTO JE MBONA UNALIKWEPA HILI!!!!!!

VILEVILE CHADEMA NI WADINI WAKUBWA MAANA 83% OR MORE YA WABUNGE WAO NI WAKRISTO JE WAISLAMU WASEMEJE????
 
Wakuu,
Mzee Mtei hajatoa kauli hii kwa bahati mbaya. Chadema imeonekana kama chama kilichostawi zaidi katika ukristo. Na ndio maana mbunge makini kama Zitto anaandamwa sana na "kashfa za kutengeneza" bila kuweka bayana anachokosea ni kipi, pengine kwa sababu hayuko dini rasmi ya chama.
Labda tujikumbushe uwakilishi wa waislam VS wakristo ndani ya CHADEMA kwenye vyombo vya maamuzi,na hata wagombea wa ubunge,rais, n.k. kwenye uchaguzi wa mwaka 2010. Hawa ni wagombea ubunge tu, bado hatujatazama madiwani, BAVICHA,baraza kuu,n.k

[TD="class: xl65"]
Jina la mgombea na jimbo atokalo
[/TD]
[TD="class: xl65, width: 64"] Dini
[/TD]

[TD="class: xl66"]KILIMANJARO.[/TD]
[TD="class: xl67"][/TD]

[TD="class: xl67"]1 Moshi Mjini. Philemon Ndesamburo[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl67"]2 Hai Freeman Mbowe[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl67"] 3Moshi Vijijini. Anthony Komu[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl67"]4 Rombo Joseph Selasini.[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl67"]5 Vunjo John Mrema.[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl67"]6 Mwanga Shafi Yaperi Msuya.[/TD]
[TD="class: xl69"]Muislam[/TD]

[TD="class: xl67"]7 Siha Eng. Humprey Tuni.[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl67"]8 Same Magharibi Eneza Elikunda Mshana.[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl67"]9 Same Mashariki Naghenjwa Livingstone Kaboyoka[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl67"][/TD]
[TD="class: xl68"][/TD]

[TD="class: xl70"]MANYARA.[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]1 Kiteto Victor Kimesera.[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]2 Mbulu Mustapha Akunaay[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]4 Hanang Rose Kamili[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]5 Babati Mjini Pauline Philipo Gekul[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]6 Babati Vijijini Francis Peter Qamara[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl66"]MARA[/TD]
[TD="class: xl67"][/TD]

[TD="class: xl71"]1 Tarime Mwita Mwikwabe[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]2 Rorya Martine Ochola Ndira.[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]3 Musoma Mjini. Vincent Nyerere.[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]4 Mwibara David Chiriko[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]5 Bunda Elias Kajeri Maarungu[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]6 Serengeti Marwa Ryoba Chacha[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]7 Musoma Vijijini Michael M. Makenji[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl66"]DAR ES SALAAM[/TD]
[TD="class: xl67"][/TD]

[TD="class: xl71"]1 Ubungo John Mnyika.[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]2 Kawe Halima Mdee.[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]3 Ukonga James Binagi[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]4 Kinondoni Philip Nyanchini Mogendi[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]5 Kigamboni Maulidah Komu.[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]6 Ilala Naomi Kaihula.[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]7 Temeke Dikson Nghilly[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl71"]8 Segerea Fred Mpendazoe.[/TD]
[TD="class: xl68"]Mkristo[/TD]

[TD="class: xl66.we ni mpuzi,nani hajui swala la udini la cdm walitengeneza mabwana ccm na wake zao cuf?cdm kama m2 ana sifa anapewa uongozi ndo mana zito yumo.cuf kimekufa bada ya kuendekeza ugaidi.ccm wao wanatamba sasa sababu ya mdini jk.waislam walivistukia ccm na cuf baada ya kuona vyote vinaendekeza ugaidi
 
Nimesema sana kuhusu UNAFIKI wa Wadanganyika. Vijana wa CDM wanamwona Zitto kama msaliti kwa sababu anapingana na mzee Mtei lakini hawaoni kwamba Mtei ana makosa kwa kupigania Udini kinyume cha itikadi ya chama chake..Vijana narudia kusema kwamba hakuna hata siku moja Udini ama ukabila umeweza kuondolewa kwa kushirikishwa kwa viongozi wa dini ama makabila isipokuwa pale walipotugawa sisi kwa makundi hayo kama alivyofanya mkoloni..

Njia pekee ya kupiga vita Ukabila na Udini ni kutowahusisha viongozi wa dini ama maswala ya dini ktk serikali na ndio maana katiba ya mwanzo ilisema wazi kwamba NCHI YETU HAINA DINI isipokuwa watu wake..Na Nyerere alipiga vita Ukabila na Udini kisha akatukumbusha mwaka 1995 baada ya sisi kupoteza malengo hayo.. Leo tunarushiana madongo hapa ni kutokana na kushindwa kuhakikisha Udini unapigwa vita.

Hivyo kisheria hata nisipokuwa Muislaam au mkristu sintokuwa nimevunja sheria ila sheria ndio italinda maamuzi yangu binafsi hatulazimishani kuwa waislaam au wakristu. Ni uamuzi wa kila mmoja wetu na hauingiliani na mtu mwingine wala serikali, tena basi kama kuna mzazi atamlazimisha mwanaye kuingia dini yake anaweza shitakiwa kwa makosa hayo. Katiba itakayo undwa italinda maamuzi ya kila mmoja wetu kuhusiana na imani yake ya dini.

Kila mahala mnazungumzia waislaam hivi ama vile kwa kutukisia waislaam wana njama yao.. Je what if! Mtei anachoogopa ni kuvunjwa kwa muafaka wa MuO ikiwa hakuna wakristu wengi ndani ya kamati hii kuulinda muafaka!..Hili ni jambo ambalo linatutatiza sisi waislaam kuona serikali ikishirikiana na kanisa ktk kutoa huduma za ELIMU na AFYA! Je kuna mkristu hata mmoja ambaye anaona serikali haitakiwi kushirikiana na kanisa ktk maswala haya? sidhani, kila mmoja wenu anaiona haki ya kanisa kwanza kwa sababu ni chombo chenu kinachofanya kazi kama Non governmental Organisation (NGO) ambayo kwa maajabu ni mbia na serikali.. hata maana ya neno hili linafutwa ghafla kwa muafaka.

Sasa kama munaamua kumshambulia Zitto kwa sababu ni muislaam na anapingana na mzee Mtei basi mjiandae kwa mengi maana hatutakubali kuona katiba yetu inatawaliwa na mfumo ule ule ulotufikisha hapa tulipo vijana wanapass mtihani wa darasa kumbe hawajui kusoma na kuandika..Ni ufisadi mtupu, hao jamaa wa kanisa mnaowatetea they careless about religion kwanza ni matumbo yao..
 
Mkuu Fundimchundo,

Naona kuna hoja ya kujadili hapa. Kama concern ya mzee Mtei ni kuwa na uwakilishi sawa kati ya waislam na wakristo kwenye tume aliyounda rais Kikwete, na kama muundo wa tume ilihitajika wajumbe kutoka Zanzibar na Bara, unadhani wale walioteuliwa kutoka Zanzibar wawe dini gani? (Kama asilimia zaidi ya 98 wa waznzibar ni waislam?)
Hivi mkuu,hapo kwenye red,hayo tu mahitaji yaliyotupelekea kuwa na haja ya kuandika katiba mpya?

Wajumbe wa bara,wajumbe 3 au 4 kati ya 15 ndio waislam,wengine wote wakristo! Kwa waislam wa Tanganyika kutolalamika ina maana hawajui athari za uwiano huu,au ni vipi?

Kwenye suala la uteuzi wa nafasi mbalimbali katika uongozi sio kwa chama tawala tu,hata vyama vya upinzani hufanya uteuzi,kwa CDM ikoje? na hapa tuitazame CDM, CCM na CUF. Kama tukiamini katika demokrasia,assume CDM ingeshinda na kupata dhamana ya kuunda serikali,unadhani kwa list hiyo ya swait ,(ambayo kwa hesabu za haraka 86% ni wakristo) hapo juu,baraza la mawaziri la CDM lingeundwa na watu waliotoka dini gani? Kwa sababu naona hata maeneo CDM iliposimamisha wagombea waislam ni yale maeneo ambayo hata chance ya kupata kura ni kama hakuna.(Sikumbuki kama CDM walipiga kampeni mkioa ya Lindi na Mtwara). Kwa kifupi uwiano wa kidini aliohoji Mtei,uwiani huo CHADEMA ukoje? Hivi chadema waislam huwa hawajitokezi kwenye nafasi za uongozi? Nilisoma tamko la Katibu Mkuu,Itikadi na uenezi (CDM)_John Mnyika,aliandika, chama kinapitia wasifu wa kila mjumbe aliyeteuliwa,na kisha chama kitatoa tamko kuhusu uteuzi huo. Hili la Mtei(waislam wengi) ndio tamko la chama baada ya kupitia wasifu huo au kuna tamko lingine? Naamini katika mageuzi,siamini katika udini. Connecting the dots,naanza kupata sura halisi ya viongozi wa CDM! Napata msingi mkuu wa Chadema.

Tutakuwa kama wale ndege wenye shingo ndefu kama tutaendelea kudai kuwa katika nchi hii yetu udini haupo. Malalamiko kuhusu Katiba si tu kwa wazanzibari kuona kuwa wanaonewa bali hata wenzetu waislamu kuona kuwa wananyimwa haki yao ya msingi ya kuwa na mahakama inayoendana na imani yao na kukataliwa kwa nchi yao kujiunga na OIC. Wengine wamefikia hatua ya kudai kuwa hata mchango wa wazee wetu katika kudai uhuru wetu ni lazima uangaliwe kidini na wenzetu wapewe heshima ya kuwa wao ndio walioleta uhuru katika nchi yetu. Wakristu wenzangu kila kukicha hawaishi kuonyesha jinsi nchi inavyoelekea kwenye utawala wa Sharia kwa kutoa upendeleo kwa waislamu!

Kwa hali hii basi itakuwa ni kamati ya ajabu ambayo haitaangalia muingiliano wa dini katika taifa letu. Ili pawe pana dhana ya haki kutendeka, basi kuna haja ya kuhakikisha kuwa pande hizo zenye usongo basi ziwakilishwe ipasavyo. Lakini hili haliwezekani ilhali Zanzibar wanapewa parity katika uwakilishi wa kamati hii ambayo inazungumzia katiba ya nchi ambayo wengi wa wawakilishi wao hawachelei kuonyesha kuwa haitaki (kama si kwa maneno basi vitendo). Ndio maana wengine tunasema kuwa badala ya kukazania mjadala wa Katiba basi tuanze kwa kuungalia Muungano wetu na uwakilishi katika vyombo vyetu. Tutakachokubaliana ndicho kitakachoongoza upatikanaji wa nchi itakayokuwepo au zitakazokuwepo.

Kukimbilia kudai alichokisema Mtei ni mfano wa udini wa Chadema ni sawa na wale wanaohusisha kutamkwa kwa Takbir kwenye mikutano ya CUF kama ushahidi wa uislamu wa chama hicho.

Mtei ameongea kama raia na ajibiwe kama raia mwengine na si vinginevyo.

Amandla........
 
Nimesema sana kuhusu UNAFIKI wa Wadanganyika. Vijana wa CDM wanamwona Zitto kama msaliti kwa sababu anapingana na mzee Mtei lakini hawaoni kwamba Mtei ana makosa kwa kupigania Udini..Vijana narudia kusema kwamba hakuna hata siuku moja Udini ama ukabila umeweza kuondolewa kwa kushirikishwa kwa viongozi wa dini ama makabila isipokuwa pale walitakiwa kuwafgawa watu kwa makundi hayo kama alivyofanya mkoloni.. Njia pekee ya kupiga vita Ukabila na Udini ni kutowahusisha viongozi wa dini ama maswala ya dini ktk serikali na ndio maana katiba ya mwanzo ilisema wazi kwamba NCHI YETU HAINA DINI isipokuwa watu wake..

Hivyo kisheria hata nisipokuwa Muislaam au mkristu sintokuwa nimevunja sheria. Ni uamuzi wangu ambao hauingiliani na mtu mwingine wala serikali, tena basi kama kuna mzazi atamlazimisha mwanaye kuingia dini yake anaweza shitakiwa kwa makosa hayo. Katiba itakayo undwa italinda maamuzi ya kila mmoja wetu kuhusiana na imani yake ya dini.

Kila mahala mnazungumzia waislaam hivi ama vile kwa kutukisia waislaam wana njama yao.. Je what if! Mtei anachoogopa ni kuvunjwa kwa muafaka wa MuO ikiwa hakuna wakristu wengi ndani ya kamati hii kuulinda muafaka!..Hili ni jambo ambalo linatutatiza sisi waislaam kuona serikali ikishirikiana na kanisa ktk kutoa huduma za ELIMU na AFYA! Je kuna mkristu hata mmoja ambaye anaona serikali haitakiwi kushirikiana na kanisa ktk maswala haya? sidhani, kila mmoja wenu anaiona haki ya kanisa kwanza kwa sababu ni chombo chenu kinachofanya kazi kama Non governmental Organisation (NGO) ambayo kwa maajabu ni mbia na serikali.. hata maana ya neno hili linafutwa ghafla kwa muafaka.

sasa kama munaamua kumshambulia Zitto kwa sababu ni muislaam na anapingana na mzee Mtei basi mjiandae kwa mengi maana hatutakubali kuona katiba yetu inatawaliwa na mfumo ule ule ulotufikisha hapa tulipo vijana wanapass mtihani wa darasa kumbe hawajui kusoma na kuandika..Ni ufisadi mtupu, hao jamaa wa kanisa mnaowatetea they careless about religion kwanza ni matumbo yao..

Sasa, Mkuu, tukisema na wewe unamtetea Zitto kwa sababu ni muislamu mwenzako tutakosea? Ikiwa unasumbuliwa na zahanati za kikristu kutoa huduma kwa wananchi wote bila kujali dini yao, tukuweke kwenye kundi gani? Si watu kama nyie ndio mtaona kuwa Katiba ni lazima isawazishe uwanja.

Udini upo, kukataa kuujadili ni kujidanganya.

Amandla.....
 
Nimesema sana kuhusu UNAFIKI wa Wadanganyika. Vijana wa CDM wanamwona Zitto kama msaliti kwa sababu anapingana na mzee Mtei lakini hawaoni kwamba Mtei ana makosa kwa kupigania Udini..Vijana narudia kusema kwamba hakuna hata siuku moja Udini ama ukabila umeweza kuondolewa kwa kushirikishwa kwa viongozi wa dini ama makabila isipokuwa pale walitakiwa kuwafgawa watu kwa makundi hayo kama alivyofanya mkoloni.. Njia pekee ya kupiga vita Ukabila na Udini ni kutowahusisha viongozi wa dini ama maswala ya dini ktk serikali na ndio maana katiba ya mwanzo ilisema wazi kwamba NCHI YETU HAINA DINI isipokuwa watu wake..

Hivyo kisheria hata nisipokuwa Muislaam au mkristu sintokuwa nimevunja sheria. Ni uamuzi wangu ambao hauingiliani na mtu mwingine wala serikali, tena basi kama kuna mzazi atamlazimisha mwanaye kuingia dini yake anaweza shitakiwa kwa makosa hayo. Katiba itakayo undwa italinda maamuzi ya kila mmoja wetu kuhusiana na imani yake ya dini.

Kila mahala mnazungumzia waislaam hivi ama vile kwa kutukisia waislaam wana njama yao.. Je what if! Mtei anachoogopa ni kuvunjwa kwa muafaka wa MuO ikiwa hakuna wakristu wengi, jambo ambalo linatutatiza sisi waislaam kuona serikali ikishirikiana na kanisa ktk kutoa huduma za ELIMU na AFYA? Je kuna mkristu hata mmoja ambaye anaona serikali haitakiwi kushirikiana na kanisa ktk maswala haya? sidhani kila mmoja wenu mnaiona haki ya kanisa kwa sababu ni chombo chenu kinachofanya kazi kama Non government Organisation (NGO) ambayo mbia na serikali.. hata maana ya neno hili linafutwa ghafla kwa muafaka.

sasa kama munaamua kumshambulia Zitto kwa sababu ni muislaam na amnapingana na mzee Mtei basi mjiandae kwa mengi maana hatutakubali kuona katiba yetu inatawaliwa na mfumo ule ule ulotufikisha hapa tulipo vijana wanapass mtihani wa darasa la sabab hata kusoma na kuandika hawajui. Hao jamaa wa kanisa mnaowatetea they careless about religion kwanza ni matumbo yao..

Mkandara,

Mie hawa ndugu zangu nawauliza kila mara mbona serikalini more than 70% ya viongozi ni wakristo je hakuna competent muslim kushika nafasi hizo ? Na mbona waislamu wakilalamika mnakuja jamvini na nguvu zote kutetea mfumo uliopo. Hakuna mtu anajibu. Nimewauliza katika thread ya mahakama ya kadhi na OIC hadi tumefika thread 100 na kitu au zaidi sipati majibu zaidi ya kebehi na kuitwa kauli mbali mbali chafu.

Mzee mtei amechemka vibaya na wasipoangalia Chadema inazama katika ile bahari ya udini kama ilivyozama CUF. Nimeshaanza kuona dalili mbaya inawaandama Chadema na uhusiano wao wa siasa za kibaguzi. Ni vema wakamtema hicho kizee na kumtoa katika mahusiano na Chadema ili wafike mbali mbali otherwise hawatafika mahali guaranteed. TANZANIA HAINA DINI NA WALA SIO NCHI YA KIKRISTO!!!! Watu wake ndio wana dini.

Kumshambulia Zitto ni upuuzi kwani amesema ukweli na kukwepa hoja ya msingi ya ubaguzi wa dini. Mtei hana tofauti yeyote na racist wa rangi ya mtu au gender ya mtu kwani ukishaanza kuangalia watu kwa dirisha la colour, race or religion wewe ni racist huna tofauti na wabaguzi wengine!!!!
 
Sasa, Mkuu, tukisema na wewe unamtetea Zitto kwa sababu ni muislamu mwenzako tutakosea? Ikiwa unasumbuliwa na zahanati za kikristu kutoa huduma kwa wananchi wote bila kujali dini yao, tukuweke kwenye kundi gani? Si watu kama nyie ndio mtaona kuwa Katiba ni lazima isawazishe uwanja.

Udini upo, kukataa kuujadili ni kujidanganya.

Amandla.....
Namtetea Zitto kwa sababu he is right, na ndivyo chama chake kinavyoamini, sio nyie mlojipanga nyuma na Mtei dhidi hata ya maamuzi ya chama chenu..
Swala la MoU sio kutoa huduma kwa wananchi wote bali ni ule Ubia wa kanisa na serikali ni kinyume cha katiba iliyopo. Mbona Lowassa mlimnyima Richmond na kupiga makelele au yeye alitaka kuupelekea Umeme kwa wamasai wa Monduli?..mnatuletea uchumi wa kina Robin hood kuibia serikali kwa sababu tu wanapelekea huduma wananchi.
 
Mkandara,

Mie hawa ndugu zangu nawauliza kila mara mbona serikalini more than 70% ya viongozi ni wakristo je hakuna competent muslim kushika nafasi hizo ? Na mbona waislamu wakilalamika mnakuja jamvini na nguvu zote kutetea mfumo uliopo. Hakuna mtu anajibu. Nimewauliza katika thread ya mahakama ya kadhi na OIC hadi tumefika thread 100 na kitu au zaidi sipati majibu zaidi ya kebehi na kuitwa kauli mbali mbali chafu.

Mzee mtei amechemka vibaya na wasipoangalia Chadema inazama katika ile bahari ya udini kama ilivyozama CUF. Nimeshaanza kuona dalili mbaya inawaandama Chadema na uhusiano wao wa siasa za kibaguzi. Ni vema wakamtema hicho kizee na kumtoa katika mahusiano na Chadema ili wafike mbali mbali otherwise hawatafika mahali guaranteed. TANZANIA HAINA DINI NA WALA SIO NCHI YA KIKRISTO!!!! Watu wake ndio wana dini.

Kumshambulia Zitto ni upuuzi kwani amesema ukweli na kukwepa hoja ya msingi ya ubaguzi wa dini. Mtei hana tofauti yeyote na racist wa rangi ya mtu au gender ya mtu kwani ukishaanza kuangalia watu kwa dirisha la colour, race or religion wewe ni racist huna tofauti na wabaguzi wengine!!!!
Mkuu hawa watu ni wanafiki tena wabaya sana kiasi kwamba leo wanapingana hata na maamuzi ya chama chao wenyewe dhidi ya imani zao za dini na ndio utajua kwamba wameingia Chadema kwa sababu ya imani yao ya dini, hapo ndio utajua kwamba CDM imeingiliwa lakini nitakwenda nao sambamba hadi kieleweke!

Kama Tume hii ingekuwa na wakristu zaidi ya waislaam usingesikia hata huyo Mtei akisema kitu wakisubiri tu waislaam waseme halafu waambiwe hawana elimu sawa kama wakristu, maana majibu wanayo mdomoni kila siku hata kutetea ufedhuli. Utaweza vipi tetea Muafaka wa MoU wakati unapinga muafaka wa CUF na CCM kuhusiana utawala wa Zanzibar ambao ni kinyume cha katiba!.

Mimi nachoomba kila siku ni tume hii na kamati ya bunge ya katiba watuletee Katiba ambayo inapiga vita - RUSHWA, UDINI na UKABILA maana Nyerere mwaka 1995 aliomba rais awe mtu anayeweza kupambana na vitu hivyo kumbe katiba ikiwa legelege basi huwezi kumpata rais mzuri vile vile. Katiba iwe kali inayokata kotekote kuhakikisha hakuna ubia wa aina yoyote na vyombo vya dini na serikali, vyombo hivi vijitegemee kama NGO nyinginezo. Shule na Hospital zao ziwe Private wakikusanya fedha wanakojua wenyewe na serikali itawazesha tu wananchi wake kutibiwa ktk Hospital hizo wakati ikiimarisha shule na Hospitali zake.
 
.......an interlude............

binafsi nampongeza mzee mtei (not necessarily kumuunga mkono) kwa uchokonozi aliouanzisha. umetuwezesha watu kuanza kufikiria nje ya visanduku!

pia nimefurahishwa sana na kijana zitto kwa kuwa bold na kusema "hapana mzee..hapa umekosea!".

controversies kama hizi zikijitokeza katika mijadala muhimu ya kitaifa kama hii ni mtaji mzuri sana for a healthy debate. ili mwishoni tupate katiba nzuri na imara inabidi ipitie kwenye hatua ya majadiliano makali kama haya....majadiliano ambayo yatapondaponda na kujeruhi mioyo, roho, nafsi na hisia zetu. ni tanuru kali lakini litalokuja kuleta sustainable outcome.

tuendelee na mjadala, lakini bila kutoana macho!

.......end of interlude..............
 
iyo katiba mpya kuliko kushuudia mahakama ya kadhi na nchi inaingizwa oic..bora tumwagane damu kupigania iman zetu ili tuone Jesus na mwamedi nani kamanda.
 
Namtetea Zitto kwa sababu he is right, na ndivyo chama chake kinavyoamini, sio nyie mlojipanga nyuma na Mtei dhidi hata ya maamuzi ya chama chenu..
Swala la MoU sio kutoa huduma kwa wananchi wote bali ni ule Ubia wa kanisa na serikali ni kinyume cha katiba iliyopo. Mbona Lowassa mlimnyima Richmond na kupiga makelele au yeye alitaka kuupelekea Umeme kwa wamasai wa Monduli?..mnatuletea uchumi wa kina Robin hood kuibia serikali kwa sababu tu wanapelekea huduma wananchi.

Aliyekuambia nani kuwa chama ni kama msaafu? Ni watu wenye imani kama yako ndio mliotufikisha hapa. Mtei kama raia ana haki ya kutofautiana na chama chake. Kama vile ambavyo Fundi Mchundo anayo.

Wakati mkidai Mahakama ya Kadhi mlikataa kabisa kusikia hoja ya kuwa nchi yetu haina dini. Leo kwa sababu mnaona mnaweza kutimiziwa azma yenu kinyemela ndiyo mnatambua umuhimu wake?

Unaelewa kweli maana ya memorandum of understanding? Utaingiaje ubia kwa kupitia MoU bila mkataba? Si nyinyi wenye mtazamo wa kidini ambao mnachukua uelewana uliopo kati ya mashirika ya kikristu na serikali katika kutoa huduma muhimu kwa wananchi wote wa nchi kwa miwani ya kidini? hata pale mnapofahamishwa kuwa hakuna mahali ambapo mashirika ya kiislamu yamezuiwa kuingia MoU kama hiyo na serikali! Nyinyi, ambao mmesoma kwenye shule za misheni na ndugu zenu wakiugua mnawakimbiza Bugando au KCMC leo bila aibu mnadai kuwa hiyo MoU haiwafaidii nyie bali ni kwa faida ya wamisheni peke yao!

Kama adha, katika tatizo lote la Richmond mnamuona Edward peke yake na mnasahau yule waziri aliyesaini mkataba hotelini London! Mnamsahau Rostam na kiongozi mkuu wa Tanesco. Au hamjawasahau bali mnatetea Umma wenu kama mlivyoelekezwa kwenye vitabu vyenu? Hapo hapo unakiri kuwa tulimkataa Edward ingawa alikuwa mmisheni mwenzetu! Au unajua kuwa alikuwa ameslimu wakati wa Richmond?

Udini upo. Na hayo maneno yako hapo juu yanakusuta maana yanaonyesha ulivyouoga!

Amandla......
 
Tutakuwa kama wale ndege wenye shingo ndefu kama tutaendelea kudai kuwa katika nchi hii yetu udini haupo. Malalamiko kuhusu Katiba si tu kwa wazanzibari kuona kuwa wanaonewa bali hata wenzetu waislamu kuona kuwa wananyimwa haki yao ya msingi ya kuwa na mahakama inayoendana na imani yao na kukataliwa kwa nchi yao kujiunga na OIC. Wengine wamefikia hatua ya kudai kuwa hata mchango wa wazee wetu katika kudai uhuru wetu ni lazima uangaliwe kidini na wenzetu wapewe heshima ya kuwa wao ndio walioleta uhuru katika nchi yetu. Wakristu wenzangu kila kukicha hawaishi kuonyesha jinsi nchi inavyoelekea kwenye utawala wa Sharia kwa kutoa upendeleo kwa waislamu!

Kwa hali hii basi itakuwa ni kamati ya ajabu ambayo haitaangalia muingiliano wa dini katika taifa letu. Ili pawe pana dhana ya haki kutendeka, basi kuna haja ya kuhakikisha kuwa pande hizo zenye usongo basi ziwakilishwe ipasavyo. Lakini hili haliwezekani ilhali Zanzibar wanapewa parity katika uwakilishi wa kamati hii ambayo inazungumzia katiba ya nchi ambayo wengi wa wawakilishi wao hawachelei kuonyesha kuwa haitaki (kama si kwa maneno basi vitendo). Ndio maana wengine tunasema kuwa badala ya kukazania mjadala wa Katiba basi tuanze kwa kuungalia Muungano wetu na uwakilishi katika vyombo vyetu. Tutakachokubaliana ndicho kitakachoongoza upatikanaji wa nchi itakayokuwepo au zitakazokuwepo.

Kukimbilia kudai alichokisema Mtei ni mfano wa udini wa Chadema ni sawa na wale wanaohusisha kutamkwa kwa Takbir kwenye mikutano ya CUF kama ushahidi wa uislamu wa chama hicho.

Mtei ameongea kama raia na ajibiwe kama raia mwengine na si vinginevyo.

Amandla........

FundiMchundo,
Sidhani kama ni sahihi kwa mtu mmoja kama wewe kuwasemea waislam. By the way,nani kakuambia kuwa madai ya waislam ni mahakama ya kadhi na OIC pekee? Hata hivyo kazi ya tume ni kukusanya maoni kutoka kwenye makundi yote ya jamii,yakiwemo ya kidini, na kuyawakilisha kwenye katiba,bila kujali mkusanya maoni anatoka dini gani. Au tuamini kuwa maoni yakitolewa na mtu wa itikadi A,mjumbe wa tume mwenye itikadi B ataya-ignore?

Hebu tuambie,Edwin Mtei ana wadhifa gani katika CDM? Na hili alilotoa ndio tamko la Chadema? Kama sio tamko rasmi la chama,na tukiamini viongozi wengine wa CDM wamemsikia,wametoa tamko gani dhidi ya kauli yake hiyo?(kukubali au kukanusha).Ingelikuwa tamko hili kalitoa Zitto Kabwe,unadhani ingechukua dakika ngapi kabla ya viongozi wa CDM hawajajibu?
 
.......an interlude............

binafsi nampongeza mzee mtei (not necessarily kumuunga mkono) kwa uchokonozi aliouanzisha. umetuwezesha watu kuanza kufikiria nje ya visanduku!

pia nimefurahishwa sana na kijana zitto kwa kuwa bold na kusema "hapana mzee..hapa umekosea!".

controversies kama hizi zikijitokeza katika mijadala muhimu ya kitaifa kama hii ni mtaji mzuri sana for a healthy debate. ili mwishoni tupate katiba nzuri na imara inabidi ipitie kwenye hatua ya majadiliano makali kama haya....majadiliano ambayo yatapondaponda na kujeruhi mioyo, roho, nafsi na hisia zetu. ni tanuru kali lakini litalokuja kuleta sustainable outcome.

tuendelee na mjadala, lakini bila kutoana macho!

.......end of interlude..............
Mkuu wangu nitakukumbusha kitu kimoja muhimu sana ufahamu. Viongozi wa Palestine waliwahi kusema kwamba wataizamisha Israel ndani ya bahari wakiwa na maana kuuondoa utawala wa kukoloniwa madarakani.. Huu ni msemo ulotumiwa na kina Che, Castro, Mao Tse Tung na hata Mandela South Afrika enzi za makaburu lakini nini kimewakuta Wapalestina?
Dunia nzima wanaamini kwamba lengo la nchi za kiarabu ni kuipiga mabomu Israel hadi izamishwe baharini.. Maneno haya yamewaponza Wapalestina badala ya kuwanufaisha kama waliotangulia..Sasa jiulize kama Wapestine wana nia hiyo, wakiisha izamisha Israel baharini wao wataishi wapi?..haiingi akilini lakini ndio walishasema maana siku hizi mpigania Uhuru huitwa gaidi..

Kwa hiyo kauli yoyote ile inaweza kuwa na ukweli wala sii uongo, lakini inategemea na itakavyo tafsirika na muhimu sana kutumia busara ktk maswala mazito kama haya maana inaweza kabisa kula kwako. Mzee Mtei alikosea na tumkosoe kama alivyokosolewa Malecela ktk swala la Muungano japokuwa alisema kweli. Ifahamike tu kwamba kuwepo kwa serikali tatu kama tunavyodai baadhi yetu kuna athari zake.

Kuwa na serikali tatu kwa jinsi sisi tulivyo na ktk mazingira yetu ni hatua moja karibu kuvunja muungano kuliko kuuimarisha muungano amini maneno yangu. Na maadam binafsi yangu sintojali mojawapo nayapokea kama yalivyo lakini najua fika serikali tatu itakuwa mwanzo wa kuvunja muungano. Kama leo tupo radhi kumkosoa rais wetu JK, tupo radhi kumkosoa mwenyekiti Mbowe, katibu mkuu Dr.Slaa na naibu katibu mkuu wa chama Zitto tunashindwa vipi kumkosoa Mzee Mtei..
 
Aliyekuambia nani kuwa chama ni kama msaafu? Ni watu wenye imani kama yako ndio mliotufikisha hapa. Mtei kama raia ana haki ya kutofautiana na chama chake. Kama vile ambavyo Fundi Mchundo anayo.

Wakati mkidai Mahakama ya Kadhi mlikataa kabisa kusikia hoja ya kuwa nchi yetu haina dini. Leo kwa sababu mnaona mnaweza kutimiziwa azma yenu kinyemela ndiyo mnatambua umuhimu wake?

Unaelewa kweli maana ya memorandum of understanding? Utaingiaje ubia kwa kupitia MoU bila mkataba? Si nyinyi wenye mtazamo wa kidini ambao mnachukua uelewana uliopo kati ya mashirika ya kikristu na serikali katika kutoa huduma muhimu kwa wananchi wote wa nchi kwa miwani ya kidini? hata pale mnapofahamishwa kuwa hakuna mahali ambapo mashirika ya kiislamu yamezuiwa kuingia MoU kama hiyo na serikali! Nyinyi, ambao mmesoma kwenye shule za misheni na ndugu zenu wakiugua mnawakimbiza Bugando au KCMC leo bila aibu mnadai kuwa hiyo MoU haiwafaidii nyie bali ni kwa faida ya wamisheni peke yao!

Kama adha, katika tatizo lote la Richmond mnamuona Edward peke yake na mnasahau yule waziri aliyesaini mkataba hotelini London! Mnamsahau Rostam na kiongozi mkuu wa Tanesco. Au hamjawasahau bali mnatetea Umma wenu kama mlivyoelekezwa kwenye vitabu vyenu? Hapo hapo unakiri kuwa tulimkataa Edward ingawa alikuwa mmisheni mwenzetu! Au unajua kuwa alikuwa ameslimu wakati wa Richmond?

Udini upo. Na hayo maneno yako hapo juu yanakusuta maana yanaonyesha ulivyouoga!

Amandla......
Well sasa unataka mjadala uwe wa dini maana naona tunapelekana (NYINYI na SISI) ambako sintopenda zaidi kuingia. Kwanza kabisa nimeshasema kwamba swala la mahakama ya kadhi lipo kikatiba na kisheria maana tunafuata mfumo wa kisheria wa cultural law na ndio unaotambulika hata ktk ndoa za waislaam, mirathi na kadhalika kisheria. Sio kwamba hakuna kitu hiki kipo isipokuwa walicholalamika waislaam ni kwamba sheria hazifuatwi inavyopaswa kwa sababu baadhi ya hukumu zimefuata secular wakati ndoa ilikuwa ya kiislaam.

Zipo kesi za madai hata za wakristu ktk ndoa ama talaka ambazo zimeamuliwa ki secular wakati waliofunga ndoa ni wakatoliki ambao dini inawakataza kuachana isipokuwa kwa zinaa (kama sijakosea)..waumini wanaweza kulalamikia sheria na maamuzi ya korti zetu na ikaswihi, Hivyo hata Kanisa linaweza kabisa kuiomba serikali inapofikia maswala la kuvunja ndoa za waumini wake, mirathi au yaliyopo ktk cultural law wapelekwe mahakimu wanaoijua sheria ya dini yao. wakristu hawakatazwi kufanya hivyo ila maadam siku hizi tunapuyanga tu mambo mengi ya dini yamepuuzwa. Hakuna kosa kisheria na hakuna mahala waislaam wanakiuka katiba ila ndivyo ilivyotakiwa kuwa. Binafsi napingana na mahakama ya kadhi kwa sababu waislaam wenyewe wanafanya mengi kinyume cha imani ya dini leo utaka kuwahukumu baada yaa.

Mkuu wangu memorundum of Association ni kinyume cha sheria, na ndio maana ikaitwa makubaliano ya muafaka ambayo kisheria yanakosa nafasi. Hakuna mkataba baina ya serikali na serikali na ndio maana ikaitwa Muafaka kama ulivyofanywa wa CUF na CCM. Nionyehse mahala poppote ktk katiba kunaporuhusu vyama viwili kuandaa mbele ya uchaguzi jinsi ya kuongoza Zanzibar. Nionyeshe hata kipengele kimoja cha katiba yetu kinachoruhusu hivyo?. BTW nenda katazame tafsiri ya Muafaka (Memorundum of understanding) halafu rudi tujadili hapa. Na sasa nakuelewa zaidi kwa nini unamshabikia Mtei maana unajionesha wazi kuwa na siasa za NYINYI na SISI, binafsi yangu nazungumzia serikali kutokuwa na mahusiano na kanisa, na nachojua mimi wewe sio kanisa wala CSST.
 
FundiMchundo,
Sidhani kama ni sahihi kwa mtu mmoja kama wewe kuwasemea waislam. By the way,nani kakuambia kuwa madai ya waislam ni mahakama ya kadhi na OIC pekee? Hata hivyo kazi ya tume ni kukusanya maoni kutoka kwenye makundi yote ya jamii,yakiwemo ya kidini, na kuyawakilisha kwenye katiba,bila kujali mkusanya maoni anatoka dini gani. Au tuamini kuwa maoni yakitolewa na mtu wa itikadi A,mjumbe wa tume mwenye itikadi B ataya-ignore?

Hebu tuambie,Edwin Mtei ana wadhifa gani katika CDM? Na hili alilotoa ndio tamko la Chadema? Kama sio tamko rasmi la chama,na tukiamini viongozi wengine wa CDM wamemsikia,wametoa tamko gani dhidi ya kauli yake hiyo?(kukubali au kukanusha).Ingelikuwa tamko hili kalitoa Zitto Kabwe,unadhani ingechukua dakika ngapi kabla ya viongozi wa CDM hawajajibu?

Mbona unaji-contradict, ndugu yangu? Mara siwezi kuwasemea waislamu halafu unadai kuwa hicho nilichokizungumzia ni kiduchu tu kati ya madai ya waislamu?

Utaka kutuambia kuwa hawa jamaa watakusanya hayo unayoyaita maoni ya wananchi bila ya kuyafanyia tathmini kabla ya kuyaingiza kwenye katiba? Au unaamini kuwa wananchi wote watakubaliana kwa hiyo hawa jamaa kazi yao itakuwa ni kuyachukua maoni yao na kuyaingiza vile yalivyo kwenye Katiba? Haujui kuwa watu wenye umuhimu katika suala kama hili ni wale wanaouliza masuali, sikia majibu na kuyatasfiri kabla ya kuyaingiza kwenye katiba? Wote tunajua jinsi wenzetu wa visiwani wanavyo-march lockstep katika masuala yeyote. Wote tunajua jinsi walivyo na donge kuhusu kukataliwa kujiunga na OIC. Hawa si watahitaji mtu mmoja tu kutoka bara kulazimisha hoja yao kama demokrasi itatumika katika uchambuzi wao? Wote tunajua kuwa huko visiwani kuna Mahakama ya Kadhi na hawana tatizo nayo. Hawa si watahitaji mmoja tu kutoka Bara kulazimisha hoja hii? Na hivyo hivyo kwa masuala mengine mengi yenye kuwagusa waislamu.

Hawa watu ni binadamu. Sitastaajabu kama watavutia kwao, wakristu, waislamu, wazanzibari, wabara n.k. Kama si hivyo, unadhani kuna hata mmoja atakayeenda kuwauliza mashoga kuhusu matatizo yao na Katiba yetu?

Mtei ni muasisi wa Chama na hana cheo katika chama, kwa hali hiyo hawezi kuwa msemaji wa Chama. Zitto ana nafasi katika Chama kwa hiyo analosema lina uzito kichama kuliko alilosema Mtei. Sasa mbona yeye kusema hauoni kama kunatosha hadi viongozi wengine waseme?

Zitto angedai parity katika ujumbe wa kamati hii, nae kuna ambao wangemuunga mkono na wengine kutofautiana nae. Nae kama angeonekana kwenda kinyume na msimamo wa chama, bila shaka mmoja wa viongozi wenzake wangemsema. Kama alivyofanya yeye kwa Mtei. Ndio demokrasi.

Amandla......
 
Wakuu lakini mheshimiwa Zitto amefafanua kwamba mzee Mtei amefilisika vipi kimawazo?

Au yeye muono wake wa hiyo tume umesimamia wapi?

Mzee Mtei aliombwa na rais Mwinyi wakti huo atoe maoni yake kuhusu mfumo wa kodi Tanzania kwamba unatakiwa ubadilishwe na kaja na wazo safi sana la kuondokana na kodi za mfumo wa kijamaa na kuleta kodi za mfumo wa kibepari na pia kutuletea VAT ambayo ndio tunaitumia mpaka leo.

Kwahio ni mtu ambae tunatakiwa kuchambua kwa makini kauli zake ni sio kuzibeza na kuzipuuza tukitumia ushabiki wa vyama.

Kama ilivyo kwa CCM kuwa na Mkapa CDM nayo ina Mtei.
 
Joka Kuu,

Unanisikitisha ndugu yangu unaangalia tume kwa minajili ya dini zao badala ya competence. Kama tunaangalia kwa mujibu wa dini zetu basi nadhani JK ni mdini sana kwani serikali yake zaidi ya 70% ni WAKRISTO JE MBONA UNALIKWEPA HILI!!!!!!

VILEVILE CHADEMA NI WADINI WAKUBWA MAANA 83% OR MORE YA WABUNGE WAO NI WAKRISTO JE WAISLAMU WASEMEJE????

Mdondoaji,

..lakini CDM walisimamisha wagombea Waislamu maeneo ya Lindi,Mtwara,Tabora, etc etc na wagombea hao wakashindwa. Sasa ktk mazingira hayo kwanini uwaite CDM wadini???

..mimi napendekeza usawa baina ya DINI hizi mbili. Uteuzi wa wajumbe wa tume ya Katiba ulikuwa ni a good opportunity kuelekea kwenye USAWA.

..Zingatia kwamba hizi ni nafasi za KUTEULIWA na Raisi. Kwa mtizamo wangu JK ahakikishe kwamba hizi nafasi za KUTEULIWA kuna USAWA kati ya DINI hizi mbili ili kutuepusha na malalamiko yasiyokuwa na tija.
 
Jokaku, unapopambana na Udini huwezi kuwahakikisha kuwepo uuwiano wa makundi hayo ndio utawagawa zaidi kwa sababu watakuwa wakipimana kwa malengo hayo na kuwaambia kila mmoja wenu atajihusisha kwa maslahi ya kundi lake. Mkoloni walifanya hivyo na tukagawanyika.. Kufikiria kugawa nafasi sawa pasipo vigezo vya maana ni sawa na kumwagia mafuta cheche za udini uliopo, kesho watu watatazama kila nafasi ya ajira kwa jicho la dini ya mtu alochaguliwa.

jamani tupige vita Udini kwa kutazama ni wapi watu wamechaguliwa kwa sababu ya dini au makabila yao kiupendeleo, lakini sio kuanzisha zogo la kutaka ajira zitazame kwanza dini ya mhusika tutajimaliza wala sii muda. Unapotaka kuzima moto unamwagia maji au mchanga na sio kuukokea zaidi kwa kuuwekea kuni kavu..Na kwa nini leo tunabishana sana hapa JF? ni kwa sababu Mtei kaukoka moto na matokeo yake ndio haya, tunaanza kutazamwa kwa imani ya dini zetu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom