Mkuu mleta mada nadhani hapa unachanganya hoja! Viongozi wa vyama vya siasa pamoja na wabunge wanagombea na kuchaguliwa kwa njia ya ushindani na sifa zao; ili mtu achaguliwe kwanza lazima awe mwanachama, aombe nafasi hiyo na awe na sifa. Sasa katika hoja yako Muislam au mkristo hawezi kuwa kiongozi au mbunge kama hajaomba nafasi hiyo na kukidhi mahitaji. Kwa CHADEMA hatuwezi kuwalaumu kwa safu ya uongozi au idadi ya wabunge wakristo pasipo sisi kujiuliza je wasio wakristo waliomba nafasi hizo, na kama waliomba walikuwa na sifa, n.k. Tofauti yake na swala la tume ya katiba ni kwamba hawa wameteuliwa; hivyo mteuzi alikuwa na nafasi ya kuzingatia vigezo kama vya uwiano wa kidini endapo angeona inafaa!
kwanini Chadema haikumpeleka Abdalla safari?