Madaktari: Hiki ndicho kilichomuua Kanumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari: Hiki ndicho kilichomuua Kanumba

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Matola, Apr 10, 2012.

 1. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Daktari aeleza kilichomwua Kanumba

  NI BAADA YA JOPO LA MADAKTARI MUHIMBILI KUMFANYIA UCHUNGUZI, BABA YAKE AZUNGUMZA, WABUNGE WAANGUA KILIO

  Florence Majani na Suzzy Butondo | Mwananchi

  MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.

  Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe gazetini alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.

  "Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion," alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) "Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka" alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.

  "Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji."

  "Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki."

  Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.

  Alisema sehemu ya maini na majimaji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo.

  Baba mzazi azungumza
  Baba mzazi wa mwigizaji huyo, Charles Musekwa Kanumba alisema kwamba alipata taarifa za kifo cha mwanawe Jumamosi saa 10:00 alfajiri baada ya kupigiwa simu na dada wa marehemu, Sara Kanumba. "Sara aliniuliza: ‘Una taarifa yoyote kuhusu mwanao Kanumba?' Nikamjibu kuwa sina taarifa yoyote, ndipo aliponieleza habari za kifo hicho. Aliniambia Kanumba hatupo naye tena amefariki kwa kuanguka, amekorofishana na mpenzi wake." alisema taarifa hizo zilimsababisha aishiwe nguvu kwa kuwa kilikuwa kifo cha ghafla… "Basi kuanzia hapo, nilianza kupigiwa simu za kupewa pole, ndipo nilipoamini kumbe mwanangu amefariki."

  Akizungumzia kuchelewa kufika msibani, alisema kumetokana na tatizo la mawasiliano. Awali, alikuwa amepanga mtoto wake Kanumba akazikiwe Mwanza kwa babu yake ndiyo maana hakufika mapema msibani. "Nilikuwa nimepanga apitishwe hapa kwangu Shinyanga aagwe, halafu tumpeleke Mwanza kwa babu yake kumzika huko lakini alipokuja mama yake alinishauri kuwa huko kutakuwa na nafasi ndogo kwa sababu watu ni wengi pia alikuwa na marafiki wengi, wengine wa kutoka nje ya nchi kwa hiyo alinishawishi na tukakubaliana kumzika Dar es Salaam," alisema.

  Pia alikanusha uvumi kuwa hajafika msibani kwa kuwa walikuwa na ugomvi na marehemu akisema walishamaliza tofauti zao. Alisema anatarajia kufika leo usiku tayari kushiriki mazishi hayo.

  Wabunge kilio Jana, baadhi ya wabunge waliofika nyumbani kwa marehemu Kanumba waliangua vilio wakati walipotoa salamu zao za rambirambi.

  Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata hakuzungumza na badala yake aliimba kipande cha wimbo uliozungumzia kifo na maneno ya wimbo huo yalionekana kuwagusa wafiwa na kusababisha vilio kuanza upya huku baadhi wakipoteza fahamu.

  Mbunge mwingine, Neema Mwinyimgaya aliongeza majonzi masibani hapo alipounganisha msiba huo na wa mama yake… "Mama yangu amefariki miezi mitatu iliyopita, huko uliko mama, nakuomba umpokee kijana mwenzetu," alisema mbunge huyo na kushindwa kuendelea.

  Wabunge wengine waliohudhuria msiba huo ni Ismail Aden Rage (Tabora Mjini), Aboud Juma (Kibaha Vijijini), Mussa Azan Zungu (Ilala), Abbas Mtemvu (Temeke), Peter Serukamba (Kigoma Mjini) na Ritha Kabati (Viti Maalumu).

  Kova na mchango wa Kanumba
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema anakumbuka mchango wa Kanumba katika kuzuia uhalifu jijini.

  "Tulishirikiana naye pamoja na wasanii wengine kuandaa bonanza maalumu ambalo lilidhamiria kukabiliana na uhalifu hapa jijini na kwa kweli mchakato ule ulifanikiwa kwani uhalifu ulipungua kwa kiasi kikubwa" alisema Kova.

  "Kifo chake kimekuwa cha ghafla mno na nafikiri kujiweka tayari (kiimani) ni jambo ambalo kila mmoja anatakiwa kuwa makini nalo katika maisha yake," alisema Kova.

  Ratiba ya mazishi
  2:30 - Msafara kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili kupitia Barabara ya Umoja wa Mataifa na Ali Hassan Mwinyi hadi Viwanja vya Leaders Club.
  3:30 - Misa ya kumuombea na salamu mbalimbali.
  6:00 – Kuaga
  9:00 - Kuelekea Makaburi ya Kinondoni kupitia Barabara ya Tunisia


  SAHIHISHO
  Rais Jakaya Kikwete jana alilazimika kubadili ratiba yake ya safari za ndani ya nchi ili kwenda kujumuika na waombolezaji wengine katika msiba wa msanii nguli, Steven Kanumba na hakuwa na safari nje ya nchi kama ilivyoripotiwa na gazeti hili jana. Mhariri.
   
 2. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Huyu dogo hii kesi kwake haitakuwa kubwa sana kama madaktari wameshasema hivyo, ataachiwa simple kama hata kama watamfunga then hawatamfunga kwa mda mrefu na hivi alisema kwamba alimuona kanumba kaanguka tu ghafla plus madoctor na wenyewe wametoa report hiyo hiyo then dogo lulu ataachiwa ila nadhani itabidi ahamishwe bongo akaishi nchi nyingine la sivyo atauliwa huyu mtoto
   
 3. B

  Bi nyakomba JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 387
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  papizo na wee usingizi umekata lol
   
 4. CHAI CHUNGU

  CHAI CHUNGU JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 7,160
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  Ahsante kwa taarifa mkuu!
   
 5. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180

  Aiseee umekata kabisaaa ndio maana nipo hapa naperuzi najuwa utanichukua tu
   
 6. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Madaktari wa bongo hawaaminiki. Hata tiba ya babu wa Loliondo waliibariki, kumbe ilikuwa feki!
   
 7. s

  stun Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rejao, usikurupuke kijana,..nitajie daktari wa kitanzania unayemjua aliyebariki tiba ya babu wa Loliondo. Nijuavyo mimi, chama cha madaktari kilitoa tamko mapema sana. Pole sana kama huwaamini madaktari wa Tanzania.
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  At least there is a light seen far, in the tunnel
   
 9. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Sasa unataka waseme alilishwa sumu? naona bado umelewa ule ushindi mlioupata akeri
   
 10. Tai Ngwilizi

  Tai Ngwilizi JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  concussion iliyosababisha kifo cha hapo hapo...bila jeraha kichwani...

  according to J Murtagh, Principles of General practice; concussion is usually caused by significant blunt force trauma/injury to the head such as a fall, sports injury, car accident, or being hit/struck with hard object.
  bado huyu mtoto wa watu ana kesi ya kujibu...
   
 11. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Binti hana kesi ya kujibu.Ila watu watamwogopa kama ukoma
   
 12. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  taarifa ya kitaalam kawaida hueleza CHANZO au SABABU ya mtikisiko huo. Ilivyowekwa hapa imekaa upande.
   
 13. PastorPetro

  PastorPetro Senior Member

  #13
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 187
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama concussion huenda kweli alianguka mna kugonga kichwa chake au alipigwa na chupa ya pombe kichwani kama wanavyodai!
   
 14. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #14
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du hapa kuna kesi ya kujibu SK hawezi kuanguka kwa nyuma (hata mlevi yoyote) lazima Lulu alimsukuma, asante kwa taarifa ingawa Madaktari hawajazungumzia kiasi cha pombe iliyokutwa mwilini inatisha km hakulewa kuna Murder wala sio tena Manslaughter ambayo ni tricked hasa ikiwemo poison
   
 15. M

  Mpemba asilia Member

  #15
  Apr 10, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Asante kwa taarifa hii mkuu!nami nimepata mwanga sasa.
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Kama sio Lulu basi kuna mwingine mwenye kesi ya kujibu. Concussion haitokei bila kugongwa ama kujigonga. Ila ile story ya Kanumba alilegea akaanguka inaweza kumtoa (after walau 3 years). Akitoka huko atakuwa mkubwa, anaweza kugombea ubunge wa vijana ccm
   
 17. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #17
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  analipiza kisasi mtei alipomshambulia baada ya tamko lake la kuwa tayari kugombea urais fursa ikijitokeza. ila ni hatari kulumbana na waasisi.
   
 18. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #18
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Tangia Jmosi mpaka J3 uchunguzi wa sumu haujafanyika? Tanzania zaidi ya uijuavyo,dogo ataozea jela huyu its murder case mpaka hapa!
   
 19. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #19
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  ina maana hujaelewa ubongo ulitikisikate mkuu? Hapo ndipo huyu Dogo anatakiwa kueleza zaidi ilikuwaje kampigiza au kajipigiza mpaka ubongo utikisike.
   
 20. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #20
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  chanzo mbona tunakijua ni kasukumwa. Kilichobaki ni majibu ya Lulu, kweli alimsukuma? Makusudi au kujihami? Na mengine mengi. Hapo ndipo atatokea au la.
   
Loading...