Mtei, Jussa watu hatari zaidi kupata kutokea Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtei, Jussa watu hatari zaidi kupata kutokea Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Apr 10, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Suala la udini ni suala ambalo muasisi wa taifa hili julius nyerere alilipigia sana kelele kipindi cha uhai wake.Leo katika hali ya kushangaza watu wawili kutoka vyama vikuu viwili vya upinzani tanzania wamenukuliwa wakitoa kauli zenye chembe chembe ya dalili za kutaka kuigawa nchi na wananchi kwa kutumia kigezo cha dini,watu hawa wawili ambao chonde chonde nawaomba watazania wenzangu tuwapuuze ni muasisi mwenye sauti kubwa ndani ya chadema bwana Mtei na kiongozi mwanadamizi na mwenye sauti kubwa ndani ya cuf ISMAIL JUSSA.

  Akiuzungumzia uteuzi wa wajumbe wa tume ya katiba bwana mtei bila haya alitoa kauli ya kilevi kwamba eti tume hiyo imejaa waislam!sina uhakika kama mzee huyu alikua na uhakika na anachokisema ama alikua anataka kusema labda tume hii ina watu wengi wenye majina ya kiislam..all in all timing ya kuitoa kauli hii ilikua ni mbovu hasa ikizingatiwa kwamba ndio kwanza tume imeteuliwa ikiwa hata haijakutana huyu mzee anaamua kuivuruga kwa makusudi ili siku ziende tukifike kwenye uchaguzi bila katiba mpya kama jk vile anataka iwe.

  Ya Jussa sina haja ya kuyarudia yote kwa kuwa kila mtu humu unajua matatizo ya jussa kwenye udini kali kuliko zote ni pale aliposema chama chake kimeshindwa uzini kutokana na jimbo hilo kujawa na wakristo!

  Hawa wawili ndio viongozi wetu wanaozitumia dini kufanikisha malengo yao,ndio mana nikaswema MTEI na JUSSA NI WATU HATARI SANA KWA TAIFA,TUWAOGOPE KAMA UKOMA,NAPENDEKEZA RAIS KIKWETE AFANYE MAAMUZI MAGUMU KWA KUWAKAMATA NA KUWATIA NGUVUNI MARA MOJA ILI IWE FUNDISHI KWA WENGINE WENYE MAWAZO YA KIJINGA KAMA HAWA WAWILI.

  Nawasilisha
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,269
  Trophy Points: 280
  Zanzibar ni nchi ya kiislamu sasa ulitaka Jusa asemaje? kura za CUF ni kutoka kwa Waislamu na siyo wakristo wala watu wabara kule nchini Zanzibar.
   
 3. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mbona walishindwa na chadema uzini?huo uislam wao haukuwasaidia?
   
 4. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Siku tarajia baba mkwe wa mwenyekiti wetu kuongea mashudu namna ile kweli wazee wasiku hizi hamna kitu
   
 5. mgashi

  mgashi JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 304
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Jussa ndo mtu hatali kupita maelezo.
   
 6. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa nini mnaficha ukweli chini ya mwamvuli wa Udini?? Sioni tofauti ya Muislamu wa Zanzibar na wa Bara!! Nachokiona ni waislamu 19 na wakristo 11... This is Maths na sio religious politics au propaganda...

  Mzee Mtei has a point!!
   
 7. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  wote tu
   
 8. Ngongoseke

  Ngongoseke JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 3,212
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  bora nibaki na ccm yangu,maana hawa wadini ni hatari sana
   
 9. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo unahisi zikipigwa kura wakristo watashindwa au
   
 10. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #10
  Apr 10, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Huenda ukaamka siku moja na kufikiri kwa upana na sio kimashudumashudu!!
   
 11. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #11
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  zitto kasema tumzomee mtei,na ile sii kauli ya chadema
   
 12. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #12
  Apr 10, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Sifikiri kwa hisia, nimesema hiyo ni hesabu sio political warfare!!
   
 13. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #13
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kweli kabisa. Na ukizingatia wakristo sisi ndio wengi ila rais, makamu, jaji mkuu na mkuu wa usalama waislamu. Yale yale ya Iraq, suni wachache wanatawala nchi imejaa washia kisa sadam ni suni
   
 14. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #14
  Apr 10, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,393
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Jussa ni mwanaCCM mwenzenu kiaina au unaweza sema "kimaridhiano" au sijui kimaridhishano. Na nyie ndo wenye dola. Mchukulieni hatua za kinidhamu mkiwa ndani, then mtoke nje mtafute namna ya kudeal na huyo mwingine.
   
 15. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #15
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  JK ndiye MDINI mkuu. Ana ajenda ya kuhakikisha mahakama ya kadhi na OIC vinaingizwa kwenye katiba mpya. Tutapambana hadi tone la mwisho la damu.
   
 16. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #16
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145

  kwa hiyo kuna impact gani kwa hiyo diff ya watu 8?hebu tuambie basi
   
 17. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #17
  Apr 10, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii thread imeshapitwa na wakati jana ilikuwepo kama hii na tume comment zaidi ya kurasa 30 sasa na wewe unaileta upya kama huna cha kupost kaa kando wewe gamba pambaf
   
 18. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #18
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wakristo hawawezi ku-give up hata siku moja. Tutapambana hadi tone la mwisho la damu.
   
 19. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #19
  Apr 10, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  CCM na JK wanadhani sisi ni wavivu wa kufikiri... na wameamua ku boycott msiba wa kanumba ili tusijadili hili...

  Tunaona, tunafuatilia na tutajadili. Hakuna suala la kuficha hapo. Interests za waislamu wa Zanzibar ni hizohizo za waislamu wa Bara, na tunatambua kuwa hata huko Zenj wapo wakrito, hata kama ni wachache je wanawakilishwa na nani??

  Vipi kuhusu population?? Hatuwezi kuwa na uwakilishi sawa kamwe!!
   
 20. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #20
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  unachanganya taarifa mzee,aliyeiweka mahakama ya kadhi kwenye ilani ya ccm ili baadae iingie kwenye katiba alikua ni mzee mkapa akiwa mwenyekiti wa ccm,jk umaarufu wake kwa waislam umepungua baada ya kushindwa kumeza tu alichokua ametafuniwa na mkapa!waislam walichukia zaidi jk alipoiondoa issue ya kadhi na oic kwenye ilani ya uchaguzi wa 2010,wanaamini angekuwepo mkapa madarkani leo kadhi angekuwepo na kilivyo chuo kikuu cha kiislam morogoro,ni kwa jitihada za mkapa,huo ndio ukweli,mengi mbadanywa jk hakuna alichowasidia waislam,yeye ni chaguo la mungu wa wakatoliki!
   
Loading...