Mtanzania aliyeuawa na Hamas alikuwa sehemu ya jeshi la Israel? Serikali itoe tamko Watanzania wangapi wameingizwa kwenye jeshi la Israel

kipumbwi

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
3,057
8,721
Picha tafakuri - sehemu ya wanajeshi wa Israel wakiombeoeza msiba wa mwenzao- tazama kwa umakini rangi za wanajeshi husika.
20231227_165710.jpg

Kumekua na hamaki na sitofahamu nyingi sana baada ya clip ya mauaji ya Mtanzania anaefahamika kama Molel kusambaa mitandaoni.

Katika clip husika,wauaji mwanzoni walionekana wakimhoji kwa gadhabu Mtanzania huyo na baadae aliuawa kikatili na sehemu yake ya nguo ya ndani (boxer) ilionekana ikiwa rangi ya kijeshi,well tufanye nguo tu.
20231220_085732.jpg

Gazeti moja wapo maarufu huko Israel limeripoti kua Watanzania ni miongoni mwa waafrika wanaoingizwa jeshini na kupewa mafunzo wakasaidie jeshi la Israel.
20231220_084950.jpg

Hali ya Waafrika kuingizwa kwenye jeshi la Israel nimeona hata South Africa ikionya raia wake na kua itawavua uraia kwani haiungi mkono matendo hayo.
20231220_085834.jpg

Watanzania wangapi wanakumbuka mwanzoni mwa vita ya Urusi na Ukraine kuliripotiwa Mtanzania mwanafunzi ameuawa na Ukraine kwenye mapigano?!!

Taarifa zilitoka kweli alikua Mtanzania na mwili uliletwa,je watu walihamaki kama hivi sasa?!! Hakua Mtanzania?!! Kwa nini sasa hivi watu wamehamaki sana?!!

Mtanzania alieuawa na wanajeshi wa Ukraine akiwa kwenye jeshi la Urusi alikua mkristo na mwenyeji wa Moshi pia kama huyu wa sasa wa Israel,,kwa nini watu hawakuahamaki?!! Ama kwa vile huyu ameuawa na HAMASI na alikua upande wa Israel?!
Screenshot_20231217-213440.png
20231220_084914.jpg
20231220_084759.jpg
20231220_084845.jpg

Tazama vizuri picha zifuatazo,je ni yeye ama sio yeye?!! Je alieuliwa vitani Ukraine akiwa na Urusi na huyu wa sasa kuna tofauti gani?!! Kwa nini kwa sasa hamaki ni kubwa na chuki baina yetu Watanzania?! Alieuawa Urusi serikali ilisema kwa nini alikua na jeshi la Urusi baadala ya kusema tu mwanafunzi?!! Huyu wa sasa serikali imetoa taarifa zaidi kwa nini aliangukia maeneo ya mpakani na HAMASI hadi akatekwa?!! Hamaki na kulaani ni kwingi kwakua huyu Molel ameuawa na HAMAS ambao ni kikundi cha kiislamu huku Molel akiwa sehemu ya Israel (Taifa teule?) Ili hali mwanafunzi ambae aliuawa Ukraine akiwa na jeshi la Urusi watu hawakuahamaki kwa kua ilikua mauaji baina ya wakrsito kwa wakrsito?!!

Wizara ya mambo ya nje,imetoa tamko lolote la kuwataka Watanzia wanafunzi waliopo Israel kuondoka ama taarifa za kifo tu zinatosha?!!

Ikiwa Israel inalipa mamilioni ya hela kwa waafrika ili wakafanye kazi kwenye mashamba je haiwezi kulipa mamilioni ya hela watumikie jeshi?!!

NB- video ambayo anahojiwa baada ya kukamatwa ipo. Mtu anaweza kuitazama na kutafsiri mazungumzo yao kabla hajauawa,moja ya nukuu ya mtu alieiona.
Screenshot_20231220-094835.png
 
Kumekua na hamaki na sitofahamu nyingi sana baada ya clip ya mauaji ya Mtanzania anaefahamika kama Molel kusambaa mitandaoni..
Wizara ya mambo ya nje,imetoa tamko lolote la kuwataka Watanzia wanafunzi waliopo Israel kuondoka ama taarifa za kifo tu zinatosha?

Ikiwa Israel inalipa mamilioni ya hela kwa waafrika ili wakafanye kazi kwenye mashamba je haiwezi kulipa mamilioni ya hela watumikie jeshi?!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wizara ya mambo ya nje,imetoa tamko lolote la kuwataka Watanzia wanafunzi waliopo Israel kuondoka ama taarifa za kifo tu zinatosha?!!

Ikiwa Israel inalipa mamilioni ya hela kwa waafrika ili wakafanye kazi kwenye mashamba je haiwezi kulipa mamilioni ya hela watumikie jeshi?!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Israel haina shida ya wanajeshi,
Ina wanajeshi active 169,500 na wa akiba 465,000.
 
Hii kitu inafichwa fichwa sijuwi Kwa maslahi ya nani.Kwa sababu kwenye video wale Hama wanamuhoji kuwa we Sio Muyahudi Kwa nini umekuja kuuwa ndugu zetu??Hebu tueleze ukweli .Yule alipewa visa kuwa anaenda kusomea kilimo ila tamaa ya pesa ikamfanya akaingia jeshini na kauwa raia wengi sana huko Gaza.Ila mihemko ya wabongo utadhani wanachambua mpira hawataki kutafuta ukweli.
 
Watu (Wanajeshi) kutoka nchi moja na kwenda kupata Mafunzo ya Kijeshi kwenye nchi nyingine siyo kosa Kisheria, Mataifa karibu yote hapa duniani yana utaratibu au mipango ya namna hii. Siyo kosa kufanya hivyo na wala siyo kitu kigeni au kitu cha ajabu. Hata hapa Tz hivi sasa, kuna raia wa nchi zingine mbalimbali kwenye Vyuo vya Kijeshi ambao wanapata mafunzo yao ya kijeshi.
Kosa linakuja pale ambapo Mtu anaposhiriki Operesheni Haramu za Kijeshi ktk ardhi ya nchi nyingine.
 
Hivi kumbe hili swala ni seriou
Kuna ombwe kubwa sana la taarifa, taarifa hutolewa 'kimagumashi magumashi'

Dr kwa uzoefu wako kuanzia Sakura,hadi "kwingineko" unafahamu fika sana maisha ya wanafunzi wa kigeni huishije na kwa utaratibu upi.

Tumekua Taifa la kasuku na wacheza sindimba za wapigaji,tuwaze nje ya box na always kuhitaji taarifa sahihi na zenye kujitosheleza!!
 
Israel haina shida ya wanajeshi,
Ina wanajeshi active 169,500 na wa akiba 465,000.

Ukraine ina population ya raia 45mln na Urusi ana population ya raia 145mln na bado Mtanzania alichukuliwa jeshini akapigane akiwa na Urusi yenye lukuki la wanajeshi.

Israel population yake ni 9mln na robo ya raia wake wakiwa nje ya Israel,ina Lundo la askari wenye asili ya Afrika kwa kazi maalumu.
 
Wizara ya mambo ya nje,imetoa tamko lolote la kuwataka Watanzia wanafunzi waliopo Israel kuondoka ama taarifa za kifo tu zinatosha?!!

Vurugu zilipoanza mwanzoni, kuna wanafunzi walirejeshwa Bongo na serikali, ingawa kuna wengine waliopo sehemu salama kama Tel Aviv wangali wapo huko...

CC kipumbwi
 
Hili suala tokea mwanzo nimewaambia watu wasilivae mkukumkuku limekaa kipropaganda sana.

Yawezekana huyo Joshua yupo hai mahali tu na hizo clip hata sio yeye.

Tatizo la wabongo wewe wape tu kichwa cha habari, wao wataiandika na kuisambaza habari yenyewe.

Hawawazi kufanya angalau hata kautafiti kadogo waka reason na kuunga dots ili angalau kuweza kuufahamu ukweli.

Mkaldayo Maghayo We ni mwehuuuu.
 
Hivi,huyu kijana aliwai kuwa mwanajeshi
nchini?.
Maana Sunday chanel wanasema wana footage za maafisa wa IDF wakiwafundisha Askari wa tanzania.
Na zaidi inasema ni insu ya ties za kidpromasia.
Urusi,cube,uingereza etc uja kutoa mafunzo nchini why kwa IDF iwe tofauti?.
Hata hivyo hafadhali sasa hivi yale maneno ya kuwa ile video ni fake hayapo tena.
Hammas wamekanusha uwongo wa mashabiki wao kuwa ile video ipo doctored
 
Hiyo picha ukiangalia vizuri iko edited .

Branch hiyo inaitwa Israel Border Police(Magav).

Na ukiangalia requirements za kujiunga na unit hiyo huyo bwana mdogo hakuwa anafit hata kwa asilimia 10% hana vigezo.

Pili operation za majeshi kubadilishana mbinu za kijeshi zipo sana na hazijaanza leo nakuwekea hapa bona fide evidence mjionee

Jeshi moja kubadilishana mbinu za kimedani ni kawaida

Hii ni jeshi la US na Israel
20231220_093148.jpg

Hii ilikuwa ni hapa hapa Tanzania.

Tusitafute justification kusingizia Joshua alikua mwanajeshi wakati hakuna uthibitsho hata chembe wa yeye kuwa mwanajeshi zaidi ya kuwa mwanafunzi aliyetambulika kutokea chuo cha kilimo.
 
Hii kitu inafichwa fichwa sijuwi Kwa maslahi ya nani.Kwa sababu kwenye video wale Hama wanamuhoji kuwa we Sio Muyahudi Kwa nini umekuja kuuwa ndugu zetu??Hebu tueleze ukweli .Yule alipewa visa kuwa anaenda kusomea kilimo ila tamaa ya pesa ikamfanya akaingia jeshini na kauwa raia wengi sana huko Gaza.Ila mihemko ya wabongo utadhani wanachambua mpira hawataki kutafuta ukweli.
Je, kwenye zile video wewe umeona yule Mtanzania alikuwa ameshika silaha yoyote ya Moto mikononi mwake na alikuwa anapambana na Wagamgambo wa Hamas? Je, umeona video ya namna hii??
Hata kama alikuwa Mwanajeshi au alikuwa yuko huko kwa ajili ya Kujifunza Mafunzo ya Kijeshi, bado hakustahili kuuawa na wale Wanamgambo wa Hamas, kwa sababu wakati walipomkamata mtu huyo hakuwa na silaha yoyote ya moto au kupambana na Wanamgambo wa Hamas, Sheria za Vita kote duniani zinakataza kuua raia wasio na silaha au kuua Wanajeshi ambao wamejisalimisha mateka kwa majeshi pinzani kwenye maeneo yenye mapigano ya vita.
 
Hivi,huyu kijana aliwai kuwa mwanajeshi
nchini?.
Maana Sunday chanel wanasema wana footage za maafisa wa IDF wakiwafundisha Askari wa tanzania.
Na zaidi inasema ni insu ya ties za kidpromasia.
Urusi,cube,uingereza etc uja kutoa mafunzo nchini why kwa IDF iwe tofauti?.
Hata hivyo hafadhali sasa hivi yale maneno ya kuwa ile video ni fake hayapo tena.
Hammas wamekanusha uwongo wa mashabiki wao kuwa ile video ipo doctored
Hiyo article ukiangalia footage ya wanajeshi wetu kuwa trained Israel ni ya May 4 ,2019 sasa uhusiano wa huyu kijana ameenda mwezi mmoja tu na amekuwa drafted hadi kupewa gwanda kwa kozi ya nchi ya nje , halafu inayochukua zaidi ya miezi 3 itawezekanaje?
 
Back
Top Bottom