Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

uuuuuuuuwi kwa mfano tu awe ni mwanaume kapata 20ml hajui chakufanya jaman hivi mtoa mada uko serious au unawaza endapo utapata

Nadhani ingekua vema kama tungempa mawazo ya kumjenga na yeye ameona hapa ndio mahali sahihi ambapo anaweza pata msaada dada
 
1.Naunga mkono hoja ya kuhifadhi fedha kwa U.S dollar, kwa sababu shilingi yetu inayumba sana. Hivyo ukiweka ktk tsh. Itapungua thamani,
Yaani mil. 10. Ya miaka 2 iliyopita si ya leo.
Wakati dollar hata kama imehama ni kidogo sana!
(Kama ikibidi kuhifadhi fedha).
2.kama hujawahi kabisa kufanya biashara hata ya 1. Mil. Ni lazima uihifadhi kwanza ili pia saikolojia iendane na mil. 10. Vinginevyo utapiga mzinga!
3. Kuna mtaalamu wa masuala ya fedha na uwekezaji anaitwa roberty kiyosaki.
Unaweza kusachi kwa google usome kidogo madarasa yake kabla hujaaingiza hiyo pesa ktk chochote!!
Naanim utanufaika nae sana.
 
Kanunue hisa kwenye soko la hisa au UTT huku ukiendelea na kazi yako. Baada ya muda itazaa na kukupa faida bila jasho
 
Njoo Buyuni hapa Vigwaza kata pori la eka 10 kwa Tsh 4.3m, kisha zinazobaki weka akiba benki, huku ukipambanua na kuchanganua miradi kadhaa itakayojitokeza. Au njoo hapa Mkuranga, nunua shamba kando ya mto eka kumi kwa milioni saba, kisha tulia, bei inapanda sana mitaa hii ya Mkuranga. Deal nyingi zinahitaji usimamizi wa karibu sana na saa nyingine inabidi kuwa mnoko sana ili hela irudi.

Kwa real estate, inabidi mtaji uwe mzuri, japo hiyo pesa waweza anzia kwa kununua kiwanja.

nitaftie shamba na mimi mkuranga, japo acre moja
 
Mkuu inategemea mimi nna pikipiki nne nilinunua zikiwa mpya kila moja 1.8M pamoja na usajili!sasa zina miezi2,kwa wiki napokea elfu42 kwa kila pikipiki ndio mkataba nilioingia na madereva!Cha muhimu ni kupata dereva mtunzaji sababu pikipiki ikiwa mpya unaweza tembelea miezi 5-6 ukawa unabadilisha oil tu.

Mkuu kama hautamind, ntakuuliza zaidi kuhusu biashara yako hii karibuni, nafikiria kuingia huko
 
Una umri gani? Na huna familia? Ulikuwa na wazo gani la kibiashara lilikuwaga ndoto yako kabla hujapata hela?
 
Every business has ups and down so kwa 10m inategemeya na haraka yako ya kutaka kuzungusha na biashara utakayo Fanya.BT! Biashara ni ww mwenyewe.kwa mwingine only a million kwake ni mtaji tosha, tokana na mipangilio yake na malengo. So kabla sijakueleza ushauri wowote huna vitu vya kujiuliza huko juu.hela ni issue nyingine na inaweza kukuvuruga with in a sec.ukishanijibu maswali yangu nitakupa kitu kidogo coz no one knows what's on ur mind.
 
Back
Top Bottom