Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Wakati sisi mwaka 2015 tulimuingiza madarakani muhutu ambaye badala ya kuendeleza mazungumzo ya uwekezaji wa gesi alipoyakuta kwa mtangulizi wake aliamua kuachana kabisa na mambo ya gesi leo Msumbiji ambao walitukuta nyuma yetu kwenye masuala ya Gesi wameanza kusafirisha Gesi kuelekea ulaya wakikamata fursa iliyofunguka
Kama Tanzania hatujaamua kuacha Siasa kwenye Utendaji tutazidi kuwa wa mwisho kwenye maendeleo hadi mwisho wa dunia
===
Msumbiji imeanza kusafirisha gesi asilia ya kimiminika kwa mara ya kwanza, katika hatua ambayo Rais wa nchi hiyo Filipe Nyusi ameitaja kuwa ya kihistoria.
Gesi hiyo imetolewa katika kiwanda cha kando ya pwani kinachoendeshwa na kampuni ya nishati ya Italia Eni, lakini kampuni kubwa ya mafuta ya Uingereza BP ina haki ya kuinunua.
Gesi hiyo iliachwa katika meli ya mizigo ya Uingereza kuelekea Ulaya.
Usafirishaji huo unakuja wakati Ulaya ikitafuta vyanzo mbadala vya gesi, huku ikijaribu kupunguza utegemezi wake kwa Urusi.
Msumbiji inatarajia kuwa miongoni mwa wauzaji wakubwa wa gesi asilia duniani, kufuatia ugunduzi wake kaskazini mwa jimbo la Cabo Delgado mwaka 2010.
Lakini juhudi zake zimetatizwa na uasi wa makundi ya Kiislamu yenye msimamo mkali yaliyodumu kwa muda wa miaka mitano ambayo yameua zaidi ya watu 4,000 na kuwaacha mamia kwa maelfu bila makazi katika jimbo hilo.
Serikali inaamini kuwa ugunduzi wa gesi utainua uchumi, lakini Bw Nyusi alisema Msumbiji itaendelea kuzingatia "shughuli za jadi", kama vile kilimo, uvuvi, utalii, ili kupata maendeleo.