Austria: Ulaya haina chaguo jingine ila kuendelea kutegemea gesi ya Mrusi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Sep 06, 2023 06:32 UTC

Kansela wa Austria amesema kuwa kuendelea kununua gesi kutoka Russia hakufurahishi, lakini gesi ya Russia ni muhimu kwa usalama wa nishati wa nchi za Ulaya.

Shirika la habari la Sputnik limemnukuu Kansela wa Austria, Karl Nehammer akisema hayo na kuongeza kuwa, kununua gesi kutoka Russia ni jambo lisilopendeza kimaadili, lakini mpaka sasa hakuna njia nyingine ya kuhakikisha usalama wa nishati nchini Austria zaidi ya kununua gesi kutoka Russia.

Kansela wa Austria aidha amesema: "Kipaumbele namba moja kwa nchi yake ni usalama wa usambazaji wa nishati. Usambazaji wa nishati ukivurugika, nchi nzima itatazika na kutazuka mgogoro mkubwa kwa wananchi wa Austria. Ndiyo maana jambo la kwanza ni kuhakikisha kuna usalama wa usambazaji wa nishati, na hatuna chaguo jingine isipokuwa kuendelea kununua gesi kutoka Russia."

Kansela wa Austria amekiri pia kuwa Russia ndiye mshirika mkuu wa kibiashara wa Austria licha ya kwamba sera za Moscow si rafiki kwa nchi za Ulaya.

Mwezi Julai mwaka huu pia, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Mafuta na Gesi la Austria, Alfred Stern alisema kuwa shirika hilo litaendelea kununua gesi yake nyingi kutoka Russia na kwamba halina nia ya kutafuta mikataba mbadala kutoka maeneo mengine kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya nishati ya Austria.

Hapo awali, Kansela wa Austria, Karl Nehmer, alitangaza kwamba haiwezekani kuiwekea vikwazo sekta ya uagizaji wa gesi kutoka Russia na kwamba vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Russia haviendelei kwa kasi kama ilivyotarajiwa na Umoja wa Ulaya.

Huko nyuma Austria ilisema kuwa inategemea gesi ya Russia kwa asilimia 80 na ndio maana haikuunga mkono marufuku ya kunua gesi kutoka Russia ingawa Vienna iliunga mkono vikwazo vya mafuta dhidi ya Moscow kwa sababu haitegemei sana mafuta ya Russia.

Umoja wa Ulaya uliifuata kibubusa Marekani katika kuiwekea vikwazo vikali Russia kwa kisingizio cha vita vya Ukraine vikiwemo vikwazo vya nishati. Lakini ni nchi za Ulaya ndizo zinazoendelea kupata hasara kubwa kiasi kwamba siku chache zilizopita serikali ya Ufaransa imeomba kuweko mkataba wa kuishi kwa amani kati ya nchi za Ulaya na Russia.

4c0v623f0ce46923wht_800C450.jpg
 
View attachment 2741838
Huyu ni kichaaa Kama vichaaa wengine tuuuu
 
Kuna kanchi tangu day one kalikataa issue ya kususia mafuta ya Urusi. Kama sikosei ni Hungary 🇭🇺
 
Back
Top Bottom