Msumbiji yaanza kusafirisha Gesi kwenda Ulaya

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,148
25,814
Wakati sisi mwaka 2015 tulimuingiza madarakani muhutu ambaye badala ya kuendeleza mazungumzo ya uwekezaji wa gesi alipoyakuta kwa mtangulizi wake aliamua kuachana kabisa na mambo ya gesi leo Msumbiji ambao walitukuta nyuma yetu kwenye masuala ya Gesi wameanza kusafirisha Gesi kuelekea ulaya wakikamata fursa iliyofunguka

Kama Tanzania hatujaamua kuacha Siasa kwenye Utendaji tutazidi kuwa wa mwisho kwenye maendeleo hadi mwisho wa dunia
Screenshot_20221113-181331_Facebook.jpg

===
Msumbiji imeanza kusafirisha gesi asilia ya kimiminika kwa mara ya kwanza, katika hatua ambayo Rais wa nchi hiyo Filipe Nyusi ameitaja kuwa ya kihistoria.

Gesi hiyo imetolewa katika kiwanda cha kando ya pwani kinachoendeshwa na kampuni ya nishati ya Italia Eni, lakini kampuni kubwa ya mafuta ya Uingereza BP ina haki ya kuinunua.

Gesi hiyo iliachwa katika meli ya mizigo ya Uingereza kuelekea Ulaya.

Usafirishaji huo unakuja wakati Ulaya ikitafuta vyanzo mbadala vya gesi, huku ikijaribu kupunguza utegemezi wake kwa Urusi.

Msumbiji inatarajia kuwa miongoni mwa wauzaji wakubwa wa gesi asilia duniani, kufuatia ugunduzi wake kaskazini mwa jimbo la Cabo Delgado mwaka 2010.

Lakini juhudi zake zimetatizwa na uasi wa makundi ya Kiislamu yenye msimamo mkali yaliyodumu kwa muda wa miaka mitano ambayo yameua zaidi ya watu 4,000 na kuwaacha mamia kwa maelfu bila makazi katika jimbo hilo.

Serikali inaamini kuwa ugunduzi wa gesi utainua uchumi, lakini Bw Nyusi alisema Msumbiji itaendelea kuzingatia "shughuli za jadi", kama vile kilimo, uvuvi, utalii, ili kupata maendeleo.
 
Wakati sisi mwaka 2015 tulimuingiza madarakani muhutu ambaye badala ya kuendeleza mazungumzo ya uwekezaji wa gesi alipoyakuta kwa mtangulizi wake aliamua kuachana kabisa na mambo ya gesi leo Msumbiji ambao walitukuta nyuma yetu kwenye masuala ya Gesi wameanza kusafirisha Gesi kuelekea ulaya wakikamata fursa iliyofunguka

Kama Tanzania hatujaamua kuacha Siasa kwenye Utendaji tutazidi kuwa wa mwisho kwenye maendeleo hadi mwisho wa duniaView attachment 2415622
Kwa sasa kimekushinda nini?

Upatikanaji tu wa umeme umekushinda, kila siku tupo kwenye mgao usioisha, uongelee kusafirisha gas?

Kwa uwezo upi ulionao wewe Januuu--- ary?

Endeleeni kumlaumu asiyekuwepo, Mara paap, 2025, Sjui mtamsingizia Nani nyinyi wehu,!
 
Hata kwenye umeme angewekeza kwenye umeme wa Gesi leo kusingekuwa na mgao. Na uharibifu huu wa mazingira hata uwekezaji wa nyerere Dam utakuwa wa hasara tu
 
Hata kwenye umeme angewekeza kwenye umeme wa Gesi leo kusingekuwa na mgao. Na uharibifu huu wa mazingira hata uwekezaji wa nyerere Dam utakuwa wa hasara tu
Nakuulizeni, ni kipi kimekushindeni kufanya sasa,!

Au na we we ni wale vilaza wa Taifa hili, yaani wafoji vyeti, mabingwa wa kutoa lawama pasina kuleta suluhisho.?

Nyie kazaneni na umbumbu wenu!
 
Wakati sisi mwaka 2015 tulimuingiza madarakani muhutu ambaye badala ya kuendeleza mazungumzo ya uwekezaji wa gesi alipoyakuta kwa mtangulizi wake aliamua kuachana kabisa na mambo ya gesi leo Msumbiji ambao walitukuta nyuma yetu kwenye masuala ya Gesi wameanza kusafirisha Gesi kuelekea ulaya wakikamata fursa iliyofunguka

Kama Tanzania hatujaamua kuacha Siasa kwenye Utendaji tutazidi kuwa wa mwisho kwenye maendeleo hadi mwisho wa duniaView attachment 2415622
Weka in details..!!
Wanasafirisha kwa meli, ndege au mabomba?
 
We mweupe Sana kichwani,gesi itoke msumbiji Hadi ulaya kwa Bomba!?..ndege gani ilisafirisha gesi!?..picha umewekewa bado inauliza tu
Ungejua nipo kwenye industry gani usingesema..!! sometime tunauliza maswali kwa faida ya wengine..!! Anyway, ASANTE
 
Kuwa kwenye industry haijalishi,pengine unauza maandazi au kuchemaha maji huko
Unachokisema ni kweli kwamba unaweza ukawa mfagizi..!! Lakini still hujui nipo kwenye industry gani na nafanya nini..!! Ntakuuliza ya kitaalamu zaidi..!! Endelea tu
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom