Mkataba wa Upembuzi wa Ujenzi wa Bomba la Gesi kutoka Tanzania kwenda Uganda Wasainiwa

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,109
49,812
Mambo yameiva ,Upembuzi umalizike haraka Ili kazi ya ujenzi ianze.
---
DODOMA; Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Uganda zimetia saini mkataba mahsusi utakaowezesha kuanza kwa kazi ya upembuzi yakinifu wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Gesi kutoka Tanzania kwenda Uganda.

Mkataba huo umesainiwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Doto Biteko pamoja na Ruth Nankabirwa, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Jamhuri ya Uganda.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, kusainiwa kwa Mkataba huo kumetokana na Makubaliano ya Awali (Memorandum of Understanding - MoU) kati ya nchi hizi mbili yaliyosainiwa mwezi Agosti, mwaka 2018 kwa ajili ya ujenzi wa Bomba la kusafirisha Gesi Asilia kutoka Tanzania kwenda Uganda kutokana na Tanzania kugundua kiasi kikubwa cha gesi katika kina kirefu cha bahari na nchi kavu.

“ Nchi hizi mbili zimekubaliana kufanya kazi ya upembuzi yakinifu kwa pamoja kuwezesha tathmini ya mradi na kutoa muongozo wa uwezekano wa mradi ikiwemo muundo wa mradi, mahitaji ya gesi, ukubwa wa bomba na taarifa nyingine muhimu zinazohusu mradi huo kwa ajili ya kufanya maamuzi.” Amesema Dkt. Doto Biteko

Amesema kuwa, licha ya Tanzania kugundua kiasi kikubwa cha gesi asilia takiriban futi za ujazo trilioni 57.54, mahitaji ya rasilimali hii yanakua kwa kasi ndani na nje ya nchi na hii inapelekea Serikali kuweka nguvu zaidi katika utafutaji kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa nishati hiyo katika maeneo mbalimbali ikiwemo Eyasi Wembere, Mnazi Bay Kaskazini, Songosongo Magharibi, Ziwa Tanganyika na katika kina kirefu cha maji baharini.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini kutoka nchini Uganda Ruth Nankabirwa amesema kuwa, Uganda inatambua umuhimu wa mradi huu na kuongeza kuwa kumekuwepo na mahitaji makubwa ya matumizi ya gesi hivyo wana kila sababu ya kuhakikisha kunakuwepo na uharakishwaji wa mradi huo.

Aisha Serikali ibainishe lini Upembuzi wa Bomba La Mabomba ya kwenda Zambia na Kenya utaanza?
 
Magufuki alitudanganya???!!
 
EACOP walichotufanyia kutusomesha manotisi ya mradi wao na mavideo yao na marks tumepiga za kutosha mpaka final quiz halafu wamenichinjia baharini Mungu anawaona.
 
Mkuu

Tanzania ndio tuna gesi. Uganda kwa sasa hawahagundua gesi, bali mafuta.
ahaa! Kumbe la bomba la gesi? Mi nilijua ni bomba la mafuta la hoima uganda to chongeleani tanga Tanzania. Vipi ramani linakopita bomba hilo la gesi tayari imechorwa?
 
Iwapo kweli watafanya huo upembuzi yakinifu ndipo itapendekezwa sehemu ya kupita, kuainisha athari za kimazingira na jinsi ya kuzipoza, kukisia gharama ya ujenzi, faida za kiuchumi na mengi mengine.
 
Back
Top Bottom