Kenya 2022 Mshindi wa Urais Kenya kutangazwa saa 9:00 mchana

Kenya 2022 General Election

Mu7

JF-Expert Member
Jun 15, 2013
1,560
1,821
Stay tuned
IMG-20220815-WA0012.jpg
 
Ikiwa zimepita siku saba (07) tangu Wakenya wapige kura katika uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 09/08/2022, Muda mfupi ujao Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inatarajia kumtangaza mshindi wa kiti cha Urais.

Iwapo Rais Mteule atatangazwa leo na asipate zuio la kupingwa mahakamani, ataapishwa Agosti 30, 2022 siku 14 baada ya Matokeo kutangazwa.

Utaratibu huu ni tofauti na Tanzania ambako matokeo ya Urais hutangazwa mapema takribani siku mbili (02) baada ya kupiga kura.

WhatsApp Image 2022-08-15 at 11.29.33 AM.jpeg
 
Watangaze,Wakenya waendelee na utaratibu wa maisha kama kawaida yao,waturudishie na kwaya yetu ya Mt.Kizito pamoja JK wa pili ambaye bilashaka atakuja kuwashauri akina Nnape,Ridhiwani,Makamba jr na sr,namna ya kufanya uchaguzi huru na wa haki.
 
UPDATE:
Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) imewataka Wakenya wote “kukubali matokeo na kuruhusu masuala yoyote yatakayojitokeza kushughulikiwa na mahakama zetu”.

‘’Tangazo hili muhimu litatoa mwelekeo wa mustakabali wa nchi yetu lakini sio hali ya kufa na kupona. Kenya itasonga mbele kwa mafanikio bila kujali nani ni rais kwa hivyo watu wetu hawana haja ya kuwa na wasiwasi,’’ amesema mwenyekiti wa NCIC Samuel Kobia.
 
Watangaze,Wakenya waendelee na utaratibu wa maisha kama kawaida yao,waturudishie na kwaya yetu ya Mt.Kizito pamoja JK wa pili ambaye bilashaka atakuja kuwashauri akina Nnape,Ridhiwani,Makamba jr na sr,namna ya kufanya uchaguzi huru na wa haki.
Hapo kwenye huru na haki futa. Sio jadi yao
 
huyo JK wa pili bila Shaka atakuaa mtu kutoka sayari nyingine.
Au unamzungumzia yule aliyekuwa rais kuanzia mwaka 2005 mpaka 2015?
Kama ni huyo HANA CHA KUWAFUNDISHA WENZIE.

Back
Top Bottom