Maswali yako nilishajibu hapo juu.
Kuwa na kipato tofauti na mshahara ni bora hata kama ni elfu 50 tofauti na kutokuwa nacho kabisa.
Assume huyo mwenye mshahara wa laki 4 kama asingekuwa na hizo source 8 ambazo zinamuingizia laki 6 angeishi vipi?
Hapa logic tunayozungumzia kulia lia mshahara umechelewa ,kama unapata 1.2m na inafika hadi mwihso wa mwezi mwingine na kukutana na mshahara mwingine hapo ni safi ,na watu kama hao hauwezi kukuta analilia mshahara umechelewa.
Wanaolilia maana yake mshahara umekwisha halafu hana source nyingine ya kupata kipato mpaka mshahara uingie ,hapo lazima alielie kwamba mshahara umechelewa ,kuna watu hata mshahara haangalii yeye anapiga kazi tu ,mshahara unaweza kuingia tarehe 23 yeye akaenda kutoa pesa tarehe 31 maana bado ndani ana petty cash ya kumsukuma.